Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kijiwe kiko PUMZIKONI,...

>> Monday, November 28, 2011

...tutaonana hapa MWAKANI,....
.... kama MUNGU akipenda!


















Read more...

TANZIA

>> Sunday, November 27, 2011




FAMILIA YA MWAKIPUNDA WA NGAMANGA IPINDA KYELA MKOANI MBEYA WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MPENDWA WAO ANNEL MWAKIPUNDA MWAISUMO KILICHOTOKEA TAREHE 26/11/2011 DAR ES SALAAM. MAZIKO YATAFANYIKA MOROGORO TAREHE 28/11/2011.

HABARI ZIWAFIKIE FAMILIA YA MWAKIPUNDA,FAMILIA YA MWAISUMO,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI POPOTE WALIPO.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE MILELE NA MILELE

AMEN

Read more...

Haya tena:Jesus was a Buddhist Monk( BBC Documentary )

>> Saturday, November 26, 2011


Read more...

VIVA KAMANDA LOWASSA




 LOWASSA KUANZA KUANIKA UKWELI KUHUSU RICHMOND KWA KWELI NAONA ANAFANYA KILE NILICHOWAHI KUTABIRI KWENYE MAKALA YANGU YA "LOWASSA SEMA NENO MOJA TU"

...NIMEAMUA KUMTUNGIA SHAIRI HILO HAPO CHINI...





Kalamu yangu nashika, shairi nakutungia
Kamanda umeongea, kiwingu umeondoa
Hukutaka kusinzia,makosa kuyarudia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa



Mwananchi nimesoma, la jana nilinunua
Machoya yakatuama, dukuduku umetoa
Uliyosema Dodoma, Kwakweli yanavutia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa



Richmond kupasua, mapema uligundua
Kikwete ukamwambia, mkataba kuondoa
Rais akakataa, nini alitegemea?
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa



Nape akashikilia, lile asilolijua
Mikoani kaambaa, uzushi kang’ang’ania
Jinalo kulichafua, wewe ukavumilia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa



Mapema nilitabiri, falsafa nikapinga
Magamba sikukariri, kuvuana sikuunga
Ukweli niliukiri, mantiki iso kunga
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa



Beti sita nakomea, kalamu naweka chini
Mengi nimeongelea, soma tena kwa makini
Yatazidi kutokea,kusini kaskazini
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa.


Shairi limetungwa na Nova Kambota Mwanaharakati,
Tanzania, East Africa
Jumamosi, November 26, 2011

Nimetumiwa hii nanihii na:
Nova Kambota

Read more...

Kama NCHI iumwayo inahitaji TIBA ya haraka , labda DEMOKRASIA sio DAWA .

Mifumo ya KIDEMOKRASIA inakamchezo ka KUCHELEWESHA mgonjwa kupewa DAWA hata ijulikanayo kuwa inatibu GONJWA,...

... kisa DEMOKRASIA inafanya WATU hata WASIOJUA KINACHOENDELEA kuruhusiwa KULUMBANA hata kuhusu dawa wasizozijua  wakati mgonjwa anaendelea kuugua ,...
...kisa KIDEMOKRASIA kila KIMBULUKUTU inabidi KISIKILIZWE ili iaminike hata dawa sahihi aijuaye ni MTU MMOJA imeamuliwa na WENGI.

Swali:
  • SI unakumbuka WENGI WAPE lakini kama wengi watakacho kupewa kinavimavimavi bado MMOJA ajuaye hao wengi wanakosea bado ndio MWENYE dawa sahihi hasa kama vimavimavi sio sahihi hata kwa hao wengi waliochagua bila KUJUA wanachagua nini?


NI wazo tu hili MKUU!
Hebu tupumzike kiwazo zaidi kwa kudeku...



China's Capitalist Revolution - BBC (6.2009)


http://www.bbc.co.uk/programmes/b00lfcz6
Producer: Robert Coldstream
Executive Producer: Nick Fraser.
Aired: June 20, 2009, July 25, 2009

Read more...

Twanga Pepeta wavamia jiji la London


Bendi ya Twanga Pepeta imewasili leo mjini london tayari kwa makamuzi katika
ukumbi wa Silver Spoon London kwa ajili ya Kuadhimisha miaka 50 ya
uhuru wa wa Tanganyika. Usikose show hii ya Ukweli

Asanteni,

Urban Pulse Creative



Nimetumiwa na:
Frank Eyembe wa Urban Pulse

Read more...

Leo katika Mtonesho: CHINA ndani ya Bongo / AFRIKA/The Chinese Are Coming

China's Investments in Africa









BBC Documentary - The Chinese Are Coming




Hebu tudeku mahali pengine ambako sio AFRIKA kwa kina WAZUNGU OBAMA  katika kidude:
The CHINESE are not COMING, They are ALREADY here




Ni MTONESHO tu huu MKUU!

Read more...

Ya DUNIA: Mwanamke ampika MUMEWAKE!

>> Friday, November 25, 2011

Haya DEKU mwenyewe stori,...

Read more...

Kikuchekeshacho chakuchekesha kwa kuwa kuna kitu katika hicho unajua Mshikaji!

Na vichekesho kwa kawaida havina maana ,...
.... kama havibebi  unalojua Mshikaji!

Swali:
  • Mshikaji  si unakumbuka lakini  kuwa huhitaji  kujua kikulizacho  ili ulie?

Ni hilo tu MSHIKAJI!
Na Ijumaa na WIKIENDI njema MSHIKAJI!


Hebu BARON aturudishe Trinidad & Tobago katika-Somebody





Eddy Grant aturudishe Guyana tena kwa SUGAR BUM BUM



Halafu azime tena kwa -Hello AFRIKA



Read more...

Watanzania wawili kucheza ligi daraja la pili Sweden


William John

Joseph Kaniki (Golota)



Wachezaji wawili wa kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) na William John wamefanikiwa kujiunga na timu ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio( Trials). Majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya thelathini ambapo wachezaji watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF)

Habari hii imeletwa kwenu na:http://www.africa4life.com/


Nimetumiwa na:
Nancy Mtunga

Read more...

Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone Awarusha Wakaazi wa DMV

Mwana muziki wa kizazi kimpya ndani ya Washington DC, AJ Ubao wa kwanza (kushoto) pamoja mzee wa kuwachanganya Dmk global Dickson Mkama. wa kwanza( kulia) wakiwanyumba ya jukwa na mwana muzingi aliekuwa anasubiriwa kwa hamu siku ya jana Jumatano Nov23, 2011 katika sherehe za Thanksgiving Muimba Jose Chameleone katikatia, akisubiriwa kwa hamu na wapenzi wake
Nyuma ya jukwa mwana dada Luren akipata flash ya pikee kabla ya unyesho kuanzaa
Muimbaji Ana Lov akipata flash ya pamoja na rafiki yake kwenye onesho hilo la  Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone.
Cheif wa swahilivilla Abou Shatry akipata picha ya pamoja na kundi zima la muimbaji kutoka Uganda  Jose Chameleone.
Aj Ubao alikuwa ni mumbaji wa pili kuimba katika onyesho hilo waliosherikiana na mwanamuziki wa kutoka Uganda Jose Chameleone, wakiwa nyuma ya jukwa  akipata flash ya pamoja na mdhamin wake wapendo
Wapenzi wa tazamaji wakisubiri kwa hamu onyesho hilo kuazarasmi ndani ya ukumbi wa Rendezvous mitaa ya Parklawn Dr, Rockville Maryland U.S
Mwana muziki wa kizazi kimpya kwa muziki wa R&B ndani ya Washington DC, AJ Ubao akiwarusha vibaya sana wapenzi wa muziki wa nyumbani wanaoishi hapa DMV Jana jumatano Nov 23, 2011 Nchini Marekani.
 
 
Wapenzi wa muziki wakinyumbani wakiwa wanamshangaa Msanii wa hapa Washington DC, AJ Ubao
Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone akifanya vituz vyake ndani ya Rendezvous Hall mitaa ya Parklawn Dr, Rockville Maryland U.S
Mamia ya watu jana walifurika kuja kumuangali Msanii kutoka Nchini Uganda  kwa jina maarufu la Jose Chameleone, ana nyimba zake, ikiwemo mama roda, Jamalila analia, na nyingi nyenginezo.
Mamia ya warembo waliohudhuria kwenye Show hiyo ya Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone
Warembo mikono juu wakiwa wamevudiwa na uwimbaji wa mwanamuziki huyo ndani ya ukumbi uliofurika warembo wa Kiafrica.
Juu na chini full warembo wakipata hisia za muziki wa muimbaji maarefu kutoka nchini Uganda Jose Chameleone.
 
  
Sauti ya muimbaji Jose Chameleone inayofurahisha warembo wamuziki wa kinyumbani
Kama kawaida yake akiwa na kundizima ndani ya Washington DC Jana Jumatano Nov 23,2011
Wakati mwengine warembo hupandwa na jazbaba wale wanaposhindwa kujizuwia na kuomba mic ili kuchombeza wimbo uliokuwa unaimbwa hewani wa kipepo
  
 
Mambo ya jana hayo cheza ni kucheze ndani ya Rendezvous Hall
Mapozi na wewe: mrembo akipata picha kutoka kwa mpiga picha wetu
Hivyo ndiovyo ilivyoo hakuna fitina
Cheza nikucheze juu na chini warembo wa Kiganda ndani ya Nyumba
 Mrembo aleehudhuria ndani ya unyesho hilo kabambe la Muimbaji Kutoka Nchini Uganda  Jose Chameleone
Kwakweli ilikuwa sho ya aina yake wapenzi wengi ambao ni Waganda aliofurika na kumuunga mkono jamaa yao
Mwana mitindo wa Uganda jina lake hatujaweza kulipata vyema lakini ni Mwanamitindo wa Uganda!
Cheza ni kuche hiyo huku warembo wakipata flashi ya pamoja kwenye show hiyo ya Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone Alivyo warusha Wakaazi wa DMV Jana Nov 23, 2011 kwenye siku kuu ya Thanksgiving Nchini Marekani. Picha zote na http://swahilivilla.blogspot.com/


Nimetumiwa hii na:
Juma Issa

Read more...

Twanga Pepeta Wakamata Pipa

Bendi ya Twanga Pepeta wakijiandaa kuingia kwenye Pipa

Chalz baba akiwa tayari kuingia kwenye Pipa

Full Mzuka

kikosi cha Twanga kikijiaandaa kuingia Katika Uwanja wa Julius Nyerere

Kutoka Kulia Amigolous akiwapa Mikoba Jojoo, Jumanne, Baby Tall na Luiza

kutoka kushoto Shalapova, Charles Baba na Shakashia

Maria Soloma akiwaaga mashabiki wake Nyumbani

Victor Mkambi mpiga kinanda wa Twanga akiwa na Maria Soloma ambae ni dancer wa twanga




Salam,

Twanga Pepeta ''KISIMA CHA BURUDANI''  wameondoka leo asubuhi kutoka uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea  kuvinjari katika Jiji la London ili kusugua kisigino na wapenzi wao walioko nchini Uingereza na nchi jirani ikiwa ni katika kusherehekea maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.  Kundi hilo lililokamilika katika safu zake za waimbaji, wapiga vyombo na wacheza show linatarajiwa kuwasha moto wa burudani yao siku ya Jumamosi, tarehe 26 Novemba 2011 katika Ukumbi wa Club 2000 Savoir Banqueting Suite, Popin Building Southway, Wembley HA9 0HB kuanzia saa Tatu Kamili Usiku mpaka alfajiri (9pm  til late).
Mheshimiwa Balozi Peter Kalaghe atakuwa mgeni rasmi. CD za album mpya na za zamani zitauzwa na vinywaji pamoja na vyakula vya kitanzania vitakuwepo vya kumwaga. Viingilio vitakuwa £20 (singles)  na £35 (couples) kabla ya saa sita (mid night) na £25 (singles) na £40 (couples) baada ya saa sita usiku.

Njoo tujumuike, njoo usugue kisigino, njoo usherehekee uhuru wa nchi yako, njoo ule na kunywa kitanzania. Burudani ni watu na watu ni pamoja na wewe. Tanzania itajengwa na watu wenye moyo kama wewe. Karibuni sana.

Shughuli hii imeandaliwa na Urban Pulse Creative wakishirikiana na Miss Jestina Blog, chini ya maelekezo thabiti ya Ubalozi wa Tanzania, London. 
Tumethubutu, Tumeweza na Tunaendelea Mbele


Nimetumiwa na :
Frank Eyembe

Read more...

Katika KUMBUKUMBU:George Washington Carver

>> Thursday, November 24, 2011

George Washington Carver
SIO SIRI
.....jamaa NAHISI ni mmoja ya MTUZ,...
.....ambaye naamini WATU weusi wanahitaji KUJIVUNIA!





Hebu tekenya....
.....An Introduction to Dr George Washington Carver




Endeleza kipengele....



Mdake kwenye HABARI...




Habari zake zaidi jaribu kubinyabinya HAPA

.... au hata  HAPA

Read more...

ASANTE KOTOKO in DAR



TIMU ya soka ya KUMASI  Asante kotoko ya Ghana inatarajiwa kuwasili nchini Desemba 9 tayari kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya kombaini ya timu za Yanga na Simba siku ya Desemba 11 kwenye uwanja wa Taifa.Mchezo huo ni sehemu ya kukamilisha maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Future Century Limited, Helen Masanja.Masanja alisema kuwa timu hiyo itafikia Zanzibar na baadaye kuja jijini Dar es Salaam kwenye hotel ya Lamada tayari kwa mchezo huo ambao umedhaminiwa na PPF, Kenya Airways, Vanedrick Tanzania Limited, Lamada Hotel na Vanne Fashion Tabata. Alisema kuwa wanatarajia kuwa na burudani ya aina yake kwani tayari kombaini ya timu ya Yanga na Simba itaundwa na wachezaji nyota wanaocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.Aliongeza kuwa   makocha wawili, mkongwe, Abdallah “King  Mputa” Kibaden na Fred “ Minziro” Felix ndiyo watakuwa wakuu wa benchi la ufundi la timu hiyo ambayo itaundwa na wachezaji 20 watakaotangazwa hapo baadaye. Wengine katika benchi la ufundi na meneja, Boniface Pawasa na daktari wa timu, Juma Sufiani.Alifafanua kuwa uteuzi wa timu hiyo hautajali uraia wa wachezaji hivyo kama wachezaji kutoka nchi za nje ambao wanachezea timu hizo watateuliwa, basi watacheza mchezo huo.Masanja alisema kuwa Yanga na Simba zimekubaliana na kuweka historia kwa mara ya kwanza tangu timu hizo zitengane mwaka 1935. Alisema kuwa historia inaonyesha kuwa timu hizo zilikuwa pamoja kuanzia mwa 1922.Mwenyekiti wa Yanga Lyod Nchunga alisema kuwa mechi hiyo itaondoa tofauti iliyopo baina ya mashabiki wa Simba na wale wa Yanga hasa zinapotokea timu hizo zinacheza mechi za kimataifa ambapo imekuwa ni kawaida mashabiki wa timu hizo kushangilia timu pinzania.Wakati Nchunga akisema hayo, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kuwa muungano huo utaleta tija kwa timu hizo ambapo mashabiki wa Simba na Yanga siku hiyo watakuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuishangilia timu yao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.Alisema kuwa huu ndiyo mwanzo wa kuanza kushirikiana katika mechi za kimataifa na kuwataka mashabiki kufika kwa wingi na kutoa sapoti kubwa kwao.


Nimetumiwa taarifa na:
Shaffi Dauda

Read more...

Kwani MTANDAONI unastukiaje ANONYMOUS ni MWANAMKE au MWANAUME kimaandishi yake TU?

Najiuliza tu  baada ya kukutana  na baadhi ya WADAU WAWILI JANA  ambao mtandaoni nilikuwa nadhani ni WANAUME  ,....

.... na kumbe ni vigoli bomba tu!(Msinitusi  kama mwanisomalakini leo)

Na katika kuongeanao  tukatofautiana  kidogo kuhusu EMU THREE ,...

... wao wanadai ni demu na mimi tokea enzi hana BLOGU yake na nakutana na comment zake kwa DINAHICIOUS wa MAHABA  HUKU,...
... kuwa huyu NGULI ambaye nakiri simjui jina lake halisi ni DUME.


Kwa M3:

Ambiere M3 EEEH!,..
...jana  kuna katopiki  ambako  kamefanya nipende zaidi staili yako kwani mpaka leo niwafahamuo kila mtu  anauhakika kivyake TOFAUTI kuwa wewe ni JINSIA GANI.

Ila mie niko pale pale kuwa weye ni (kwa kipare)MGHOTHI aithee!

Tukiachana na hilo:
  • Wewe unastukiaje JINSIA ya mwandishi asiye jitambulisha mtandaoni?
  • Na kwani ni lazima  kujua MWANDISHI KIJINSIA ni yule akojoaye kirahisi  kasimama  au ni yule achuchumaye  kiusataarabu ili kukojoa kirahisi  ili kulenga shimo  la choo cha shimo wakati MADA iongelewayo  labda haina uhusiano na jinsi ya kukaa kistaarabu  kwa aliyevaa sketi fupi kwa kuwa ni ile ya  hivi DAR -ES- SALAAM ile posta mpya itaitwa POSTA mpya mpaka LINI wakati labda wala sio MPYA tena siku hizi?


Ni MTONESHO tu huu MHESHIMIWA na usikonde!

Hebu Kleptomaniacs watunishe- Tuendelee




Mashifta warudishe - System ya Majambazi





Mashifta waongezee-Pesa ,Pombe, SIASA  na Wanawake


Halafu LONGOMBAS wazime kwa kukumbusha-Vuta pumzi

Read more...

Labda wenzetu WAZURI na wale wenye MIAKILI SANA watuachie kwanza siye wengine NDIO tuwastukie kwanza kuwa wao ni WAZURI au ndio WENYE MIAKILI sana!

YATUMIAYO AKILI SANA ,......
.....labda ni YA KAWAIDA kwa  MWENYE akili,...
....a.k.a  yatumiayo akili sana KWAKE ni kawaida !

Na kwa isemekanaye ni  MZURI SANA,...
... labda yatakiwa UZURI wake uwe kwake ni KAWAIDA  kwa kuwa umemng'ang'ania  na kwake huo sio kitu cha kutia akili,...
....a.k.a UZURI  kaumbwanao kwa hiyo huo  kwake ni KAWAIDA.

 Swali:
  • AU?

NDIO,...
... labda kustukia yatumiayo sana AKILI,...
... labda hiyo ni shughuli ya WENGINE ambao hustukia nani ni mwenye AKILI,...
... kama labda kama MTU  ni MZURI  labda hiyo  ni shughuli ya wengine  wastukio kwanza !

LAKINI:
  • Si labda mtu akisubiria WENGINE   , wengine wanaweza wasistukie anamiakili  na pia haki yanani  labda ni kweli  yeye ni mzuri kweli  hata bila nguo kitu ambacho JAMII  kwa jamii IJIFUNDISHAYO  miakili na UZURI wake unaweza USITAMBULIWE?:-(

Ndio,..
... kuna WENYE akili wajijuao wanamiakili WASIOTAMBULIKA na JAMII kwa kuwa jamii  inakipimo tofauti cha nini AKILI SANA na usipopasi  mtihani wa jamii  basi weye hutambuliki,...
... kama tu ijulikanavyo kuwa JAMII ikijifunza kupenda wenye tako lililopigwa pasi  WAZURI  wenye tako kubwa huondoka kwenye kipimo cha wazuri katika jamii kisa tako kubwa na matege kwa mbaaaaali!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(


Hebu DIDO aingilie kati na kulainisha kwa-THANK YOU





Ghafla Youssou Ndour aingilie kati kwa-Medina



Halafu Youssou N'dour azime kwa -Africa, Dream Again

Read more...

Kuna wadhaniao UJINGA KISIRI CHOBISI unanafuu kuliko UJINGA HADHARANI kwenye UMMA!

Lakini,....
.... labda MJINGA,...
.... ni MJINGA tu kama kitafsiri za wadaio kuna BINADAMU mwenye pumba za KIJINGA,...
... hata kama ujinga wake MHESHIMIWA kafanya SIRI.

Swali:
  • Kwani KUHUSU YA SIRI-unafikiri HATA kwa kuficha HATA nyege KISIRI inamaana mwenye nyege hana NYEGE kisa anazificha na hiyo nni SIRI?

Na ndio ,...
..... hata kwa KISIRI,...
....... labda kifanyacho MTU hufanya hicho ni SIRI,....
... ni kwa kuwa UKWELI NI KWAMBA jambo lifanywalo siri hilo SIO SIRI na  lipo PALEPALE na ndio maana mwangalifu katika kumdeku mficha SIRI ,...
...yasemekana  jinsi MTU afichavyo siri ndio KIFICHUA SIRI.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


Hebu MCHUNGAJI Solomon MUKUBWA abadili wazo na kurudisha hali ya hewa laini kwa watu baadhi kwa kudinya pini la kikristo lile-Mfalme Wa Amani



Halafu Zain Bhikha aingilie kati  mchezo kwa - Give Thanks to Allah


Read more...

...ndio HERUFI hujenga NENO na MANENO hujenga SENTENSI....

>> Wednesday, November 23, 2011

 ...... ila  maswala ya  UJUMBE,....
........ hata sentensi iwe ni ipi LABDA hilo ni swala JINGINE!:-(

 Swali:
  • Na  si  unakumbuka maswala ya UJUMBE umuhimu wake labda UNATEGEMEA apataye UJUMBE anastukia au tu anahitaji UJUMBE GANI?


Ndio,....
.....na SENTENSI zozote zile  labda zina UJUMBE,....
.... kama tu KWAKO  katika hizo unastukia UJUMBE,....
.....ingawa bado  swala la UMUHIMU wa UJUMBE HUO kwako,...
.... hilo nalo ni SWALA JINGINE.:-(
 NI wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu Zap Mama, Talib Kweli, Common wabadili kwa  - Yelling Away





Au tu Talib Kweli azime kwa-Move Somethin'

Read more...

Swala la kuwa na ``UHAKIKA NA KITU´´ labda ni jambo la kufanyia kazi KILA SIKU....

 ....kwa kuwa  SWALA la UHAKIKA,...

.... laweza kuwa lahitaji IMANI......
....na  kwa bahati mbaya labda IMANI,...
.... moja ya misingi yake ni KUTOKUWA na UHAKIKA baadhi ya nyakati.:-(

Swali:
  • Si unajua ulichonauhakika nacho LEO sio LAZIMA kila siku zijazo/KILA WAKATI  utakuwa na UHAKIKA nacho kwa KIPIMO HIKIHIKI cha LEO?

Na  USICHO na UHAKIKA wala IMANI nacho LEO,...
... labda ni swala la kukipa MUDA tu HICHO.


Ni wazo tu HILI MHESHIMIWA!:-(



Hebu Asa arudie - Jailer



Halafu Seu Jorge aturudishe kidogo brazil kwa - Pretinha ao Vivo



Halafu CEU hapahapa Brazil azime kwa- Malemolencia

Read more...

Wakati kuna SARESARE MAUA -Weye UNAOGOPA nini na WENZAKO wanaogopa NINI?

 Na labda  huhitaji hata HISTORIA kujua,...
.... labda wengine  hawaogopi hata KUFIA wanachokiamini ,...
... kiwe ni  SIASA au hata DINI.

Na wajua wengine HAWAOGOPI   MTU  wasiyemjua au hata kufia  NCHI  ambayo  kwa walivyo nyong'onyea labda ni nchi isiyo wajua angalau hata  KWA kuwaunga mkono angalau nao  wafaidike angalau na yake MADINI.

Swali tena:
  • Je wewe UNAOGOPA nini?

Na ni  ndio ,...
.....kuna ambao waogopacho sana ni  VIBOKO,mitihanin, mende  au tu kuparuriwa na KUKU.


Na ndio,...
.... kuna waogopao vifo  ingawa wanapoteza muda kwa kuogopa visivyoua kama  vile vya majungu  rasharasha aka ``JE WATU WENGINE  WANAWAWAZAJE TU ´´ kitu ambacho  HAKIUI MTU  labda.:-(


Je waogopa NINI?
Ni wazo tu hili NGULI!




Hebu Nneka Egbuna aanzishe tena kwa-Beautiful



Nneka aongezee- Lost Souls



Halafu Nneka ,Ziggy Marley na Eeday wazime kwa-Express Yourself


Read more...

LABDA hakuna MTOTO awazaye akikuwa atakuwa mfanyakazi wa MOCHWARI kuosha MAITI!

Swali:

  • Au unafikiri kuna MTOTO atamaniye akikuwa ofisini kwake kuwe kunalazwa WAHESHIMIWA MAREHEMU?

Ndio kuna ya UTOTO,...
.... na ya UTOTO ya mpenda UDEREVA ,....
..... mara nyingi sio  yale ya UKUBWANI ambayo huweza geuza MTOTO aliyependa kuendesha apende KUENDESHWA!:-(
Swali:
  • SI umestukia UKUBWA nuksi  hasa pale  kama MTU ni mwenzangu na mimi asiye na MIURITHI ya KITAJIRI astukiapo inabidi afanyie kazi MSHAHARA na ofisi labda ni popote?
  • Na kazi si  ni KAZI tu  ingawa bado ukweli uko palepale  kuwa kazi nyingine MUHIMU   ni zile za kupima wingi wa minyoo kwenye kinyesi cha Mheshimiwa MAABARA ili kuhakikisha kama kweli MHESHIMIWA ana MINYOO?

NDIO,....
... na MAITI wanahitaji WATAALAMU husika ambao ni muhimu tu,...
.... ndio maana MOCHWARI ni ofisi tu za kawaida za WATU  tena labda wale waliokuwa wanaogopa stori za vifo UTOTONI.:-(

NI WAZO TU HILI MKUU!




Hebu AKON aanzishe upya kwa-Mama Africa



Halafu Céu azime  kwa - Roda


Read more...

Amigolous na Saleh Kupaza walonga.

Salam,


Wanamuziki Amigous na Saleh Kupaza kutoka  bendi ya Dansi Twanga Pepeta "KISIMA CHA BURUDANI" wakiongelea kuhusu maandalizi ya ziara yao Nchini Uingereza Katika Kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania yatakayofanyika tarehe 26 Novemba 2011 katika ukumbi Club Club 2000 Banqueting Suite(Former Silver Spoon) Popin Building Southway. Wembley HA9 0HB kuanzia saa 9pm- 4am. Kiingilio ni £20.00 kwa single na couple £35.00 kabla ya saa sita Usiku
Asanteni

URBAN PULSE CREATIVE wakishirikiana na MISS JESTINA BLOG





Nimetumiwa hii na:
Frank Eyembe

Read more...

Afrika KUSINI na vyombo vya HABARI!

Ya: ``STATE SECRETS´´ law....
...na dalili za WANAHABARI kufungwa midomo.....

Read more...

Na ni mstari mwembamba kati ya KUFAULU na KUFELI!

>> Tuesday, November 22, 2011

Na  kama UMEFAULU,...
.....labda  kumbuka kufeli kupo tu  ,...

.... na kuna uwezekano  ALIYEFAULU  hajisikii kafeli kwa kuwa kaegemeza mitazamo yake mbali na YALE  aliyofeli.


Na kama  MTU anajisikia KAFELI,...
.... akumbuke tu  KUFAULU kupo tu,...
.... .... na kiendeleacho  ni labda kabobea katika kuangalia zaidi ayatambuayo kama KUFELI.

Swali:

  • Si  katika  MTU alilofaulu  akijichunguza bado MAISHANI anaweza kustukia nini alichofeli na ndio maana hata mtu ajulikanaye kwa kufaulu KISIASA kama NELSON MANDELA  bado anakiri wakati anafanikiwa KISIASA , kifamilia ALIKUWA anafeli  kitu kilichofanya ndoa zake mbili kufa na watoto kulelewa bila BABA?


  • Na si unakumbuka hata MOTHER TERESA yasemekana alikuwa anaona wale WALIOONEKANA na JAMII kuwa ndio waliofeli kimaisha  na kuwa masiki kupindukia ndio ambao KIIMANI  walionyesha kufaulu zaidi kuwa karibu na MUNGU?
  • Na si nasikia hata katika LIFAULIWALO/Lifaulwuo moja ya siri ya wafauluo HILO  ni kufeli katika hilo  bila kukata tamaa nakulifanyia kazi  hata kama ni  kimazoezi mara kwa mara  kitu kisahauliwacho na washabikiao  KUFAULU tu ?

Ndio,...
... labda tukumbuke  hakuna AFELIYE au KUFAULU  kila kitu,...
.... na  ni tabia tu zawatu  kuruka baadhi ya mambo kufanyacho  hapa DUNIANI kuna wenye lebo za kuwa wao WAMEFAULU,...
.... autu ni wale WALIOFELI:-(



Ni wazo tu hili MKUU!


Hebu BONEY M warudie-MALAIKA



Au tu Anjelique KIDJO naye arudie-MALAIKA


Halafu tu tena BONEY M wazime kwa-JAMBO BWANA/Hakuna MATATA


Read more...

Anayenipa motisha fulani leo ni: HELEN OYEYEMI!

Kama unahusudu kusoma au unahamu yakuandika,...

... cheki kazi za huyu mdada Helen Oyeyemi....
...ambazo kiaina zimenianzishia wiki kisababu mbalimbali:

Msikie kidogo akiongea....








Habari zake zaidi HUKU


Kwa kifupi:




Helen Oyeyemi

Helen Oyeyemi was born in Nigeria in 1984 and has lived in London since the age of four.

She completed her book The Icarus Girl just before her 19th birthday while studying for her A-level exams. She is now a student of social and political sciences at Cambridge University.










AU:

Helen Olajumoke Oyeyemi (born 10 December 1984) is a British novelist. She was born in Nigeria and raised in London.

She wrote her first novel, The Icarus Girl, while still at school studying for her A levels at Cardinal Vaughan Memorial School.

Oyeyemi studied Social and Political Sciences at Corpus Christi College, Cambridge, graduating in 2006. Whilst at Cambridge, two of her plays, Juniper's Whitening and Victimese, were performed by fellow students to critical acclaim and subsequently published by Methuen.

In 2007 Bloomsbury published her second novel, The Opposite House which is inspired by Cuban mythology.

Oyeyemi is a lifelong Catholic who has done voluntary work for CAFOD in Kenya[1].

In 2009 Oyeyemi was recognised as one of the women on Venus Zine’s “25 under 25” list. [2]

Her third novel, White is for Witching, described as having "roots in Henry James and Edgar Allan Poe" was published by Picador in May 2009. It was a 2009 Shirley Jackson Award finalist and won a 2010 Somerset Maugham Award.

Her fourth novel, Mr Fox, was published by Picador in June 2011.

Read more...

YA PAKISTANI:Kutuma meseji ZA SIMU zenye matusi mwiko kuanzia hivi karibuni !

PAKISTANI yataka kampuni za simu kuzuia meseji zenye maneno ya matusi.

... na maneno kama ,Jesus Christ, Satan, TAXI, Idiot, yakiwa ni miongoni mwa ambayo itakuwa mwiko kumtumia meseji rafikiyo  ukitumia sentensi yenye maneno hayo.....
DEKU ndude,...






Read more...

ASHA BARAKA na AMOSI wazungumzia kuhusu 50th Independence Tour

Salam,

http://www.youtube.com/watch?v=xQQx2A59kMw&feature=channel_video_title


Mkurugenzi wa African Stars ASHA BARAKA pamoja ofisa wa Ubalozi nchini Uingereza AMOSI MSANJILA wanazungumzia kuhusu maandalizi na matayarisho kwa ajili ya ziara ya Twanga Pepeta "KISIMA CHA BURUNDANI'' nchini Uingereza katika Kuazimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Show hii itafanyika jumamosi Tarehe 26 November 2011 katika Ukumbi wa Club 2000(Silver Spoon)Savoir Banqueting Suite, Popin Building Southway, Wembley HA9 0HB.

Asante,

Urban Pulse Creative



Read more...

Ngumi kupigwa Desemba 18,MZALENDO PUB

>> Monday, November 21, 2011




Na MWANDISHI WETU

WASANII mbali mbali hapa nchini wanatarajiwa kutoa burudani katika pambano la mchezo wa ngumi lisilo na ubingwa litakalowakutanisha bondia, Mada Maugo na mpinzani wake Suleimani Saidi 'Toll' Desemba 18 mwaka huu katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama JIjini Dar es Salaam.

Akizungumza na kona hii ya burudani Raisi wa shirikisho la ngumi za kulipwa hapa nchini (PST) Emanuel Mlundwa alisema, maandalizi kwa ajili ya pambano hilo yamekamilika.


Aliwataja wasanii watakaotoa burudani siku hiyo kuwa ni Kundi la mapacha watatu Khalid Chokoraa (Halidi Chuma)pamoja na msanii wa mziki wa bongo fleva Mwana FA (Hamisi Mwinjuma).

Alisema licha ya kuwepo kwa burudani hizo vile vile atakuwepo kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila Super D kwa ajili ya kutoa mafunzo kupitia Dvd pamoja na kuzisambaza.

Aliwataka mashabiki wao wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani hiyo, licha ya kuwa mchezo huo haupewi kipaombele watahakikisha wanasonga mbele katika kuazimisha miaka 50 ya uhuru.

aidha katika mapambano ya ngumi ya utangulizi mabondia Yohana Miyayusho na Shadrack Juma, Doto Kipacha atazidunda na Saidi Muhidini na kwa upande wa mchezo wa Kick Boxing ambao utatuwakilisha kimataifa Tanzania Muaythai Academy of Combat watawaletea mpambano kwa mara ya kwanza nchini kati ya bondia Emanuel Shija kutoka Tanzania na Munyeshyaka Vincent kutoka Rwanda Mpambano huo utakuwa wa kimataifa kutokana na ushiriki wake wa nchi hizo mbili nchini zitakuwa zikipeperusha bendera zao.
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania



Nimetumiwa hii na:
Super D

Read more...

Mahojiano Maalum na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda Part 3

Salam,


Urban Pulse Creative inakuletea sehemu ya tatu katika Mahojiano maalum kutoka kwa Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
.
Asanteni,

Urban Pulse Creative







Nimetumiwa hii na :
Frank Eyembe wa Urban PULSE

Read more...

Ngumi kupigwa Desemba 9 DDC Keko Dar es Salaam

Ramadhan Nassib kulia



BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Ramadhan Nassib, anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na mpinzani wake Antony Kariuki wa Kenya, katika pambano la maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru litakalopigwa kwenye Ukumbi wa DDC Keko Dar es Salaam, Desemba 9 mwaka huu.

Akizungumza  Mratibu wa pambano hilo, Pius Aghaton, alisema kuwa pambano hilo linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na rekodi zilizopo kwa mabondia wote.

Alisema kuwa pambano hilo litakuwa la uzito wa Fly ambalo litapigwa katika raundi 10.

“Tumeandaa pambano la aina yake kwa ajili ya kusherekea miaka 50 ya Uhuru na pia kuweza kuwajengea mabondia wetu uwezo wa kucheza mapambano ya kimataifa” alisema.

Mratibu huyo alisema kuwa katika pambano hilo, kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo bondia Juma Fundi atazichapa na Juma Seleman katika pambano la uzito wa Fly la raundi sita, Fred Sayuni atazipiga na Bakari Dunda katika pambano la uzito wa Feather la rfaundi sita.

Pambano jingine litawakutanisha mabondia Rashid Ally pamoja na Daud Mhunzi katika pambano la uzito wa Feather la raundi sita na Faraji Sayuni atazichapa na Alpha George katika pambano la uzito wa Fly la raundi nne.

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
Mob;+255787 406930
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
--
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania



Nimetumiwa hii na:
SUPER D

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP