Unaweza ukajikuta umehakikishia UMATI upumbavu kwa kitendo chako cha KUONGELEA KITU au hata SENENE.
Tatizo la kukaa KIMYA, ni udhaifu wake katika kusaidia watu kujua NANIHII au UPUMBAVU.
Ukitaka kuongea kama unaAKILI kuhusu jambo la KIPUMBAVU, kuna watakaofikiri jambo la KIPUMBAVU ni la MAANA au ni la akili.
Lakini... ...inawezekana kwamba ni kweli kila mtu anaAKILI na ni ujazo tu katika MATUMIZI ya AKILI utofautishao UJINGA wa yule na yeye kama sio MIMI.
Natishika na JINSI wenye BUSARA na AKILI wafanikishavyo KUFANYA UJINGA kwa kutumia AKILI!
SWALI:
Ushafanikiwa kufanya UJINGA mara ngapi tokea JANA?
SIKU NJEMA!
------------------------------------------------------------------------------------ Kama una nafasi mcheki Joshua Klein: azungumzie maswala ya AKILI ZA KUNGURU katika :The amazing intelligence of crows
Mike Myers akughanie malalamiko yake kidogo kuhusu MWANAMKE katika Woman Beat Poem
LAKINI................. ..utamu wa KUMTEGEMEA ni pale UHISIVYO anaKUNYIMA.
SWALI:
Ushawahi kutegemea kuna KESHO kwa sababu leo umeAMKA?
Unakumbuka SIASA ni neno tu liwakilishalo NANIHINO isababishayo uhisi KIGOMA ni pazuri kuliko NJOMBE?
SAMAHANI tu kwa KUKUZINGUA kwa kuongea UJINGA!
:-( ------------------------------------------------------------------------------------------------- Tumsikilize kidogo NELSON MANDELA kabla hajawa MPOLE.
Staili yako yakuvutiwa kugida UKOKO anaijua aliyepembeni yako wakati unajifanya unaonja UTANDU. Asiyejua jinsi uchuchumavyo MSALANI ,wakati unatafuta KUSIGINA, anaweza akadhani kuwa anajua unavyo KUNYA kwa sababu anajua kilaMTU baada ya muda fulani KIDUCHU, ana kunya.
(SAMAHANI kwa kutamka neno KUNYA. Nilikuwa na maanisha kwenda haja KUBWA!):-(
Wakati unamtamani KIKWETE au KHADIJA, inamaanisha USHAKULA chaKULA.
Ukiwa na njaa........., HAUSIgeli,hausiBOI,au hata MWALIMU wa KEMISTRI, haTAMANIKI.
HATAZUBEDA au SAIDI, kama unatumia afichasho SAIDI na MWAJUMA,hatamaniki kama tu KISAMVU wakati unahisi unataka kula CHIPSI mjusi.
LAKINI..... .....wakati unafikiria kutamani kufanya UASHERATI na nanihinoo, inamaana ungetaka tu kufanya UASHERATI na nanihino kwa sababu nanihii IMEPIGA MAGOTI au imelowa kutokana na shahuku ya JEMEDARI HAMU. Tendo hilo lingekufanya UWE TUBINADAMU haLISI.
Kuna vitu wewe kama binadamu , lazima uvipitie au vikuPITIE tu.
AU?
SWALI:
USHAWAHI kutamani KUWA MKUBWA?
Naacha hii TOPIKI MDAU! NAACHA kabla ujaanza kuwa na uhakika kama namtamani HAUSIGELi wako kama TIGER WOODS alivyo mpata MKEwake kpitia kwa .........
DUH! ------------------------------------------------------------------------------------ PATA kidogo TOUCH and GO wakiuliza UTAFANYA uasherati na MIMI?
Jaribu kucheka kama HAWA JAMAA watakuchekesha
AU tuende tu kumsikiliza ISPECTA akiwa na wadau zake wa BONGO NYOSO katika dawa iitwayo JELA Read more...
Ushawahi kukutana na UAMINIYE kuwa ni MVIVU wakati ana NJAA?
Uaminiye ni Mvivu, anaweza kukushinda kwa bidii ya KUOMBA!
Mvivu kwenda KAZINI, anaweza akawa ni JEMADARI kwa kwenda MADUKANI kununua ANASA , kama unampatia au anajipatia ile PESA AMBAYO ingekuwa yakununulia Bata wa KRISMASI au ya kujipendekeza tu kwa MAMA MKWE au JIRANI
Mvivu wa kusoma KAMASUTRA aweza kuwa anajuhudi ya kupika KASHATA:
Saaaaasaaaaaaaaaaaa!
NISikuzingue MDAU!
SIna stori kama kawaida zaidi ya ujinga wangu!
WIKIENDI NJEMA!
------------------------------------------------------------------------------------------------- SAMAHANI kwa HERUFI KUBWA!
HEBU kama si muoga wa mashetani au muoga lakini unataka kujua stori za ATOLEWAYE SHETANI , twende UFILIPINO Kidogo tukasikilize kitu....
HALAFU Kama MUOGA , usiangalie kideo hiki cha SHEKHE amtoavyo shetani pale BRUNEI
MIMI NAOGOPA kufanya dhambi kutokana na kufunzwa na kujifunza ubaya wa dhambi hasa katika kusababisha kuwezesha kwenda kwangu JEHANAMU!
:-(
Tatizo la uoga wa kufanya dhambi ni uwezo wetu binadamu kuzoea vitu hasa kama matokeo ya kucheza na moto huyastukii hapahapo kuwa UMEUNGUA .
UZOEFU wa kuzoea KIPORO cha wali na MAHARAGE ya nazi ya jana, hutufanya kudhani kuwa kwa sababu hatuumwi tumbo, basi KIPORO hakina vijidudu au , bakteria wakichezeacho MDAKO wakati unakigida.
Swali:
Kama unapenda maziwa , ushastukia kuwa maziwa yamgando, mtindi au..... ni maziwa yaliyoharibika?
Ushawahi kumuogopa MZAZI , au NDUGU akutakiaye mema kwa staili zake za kukufikishia ujumbe?
Ushawahi kuogopa kumuambia umpendaye kuwa UMEMZIMIA na kila ukichukua sabuni yako ya MBUNJU kwenda KUOGA ,unamuona kwenye beseni?
Ukifikiria sana, unaweza kukumbuka kuwa kama wewe ni mshirikina, LIBINTI au LIMVULANA zuri MAKABURINI waweza kulikimbia kwa kudhani ni JINI wakati pale maeneo UNGELIMEZEA mate.
Kuna watu HUSAHAU ubingwa wa binadamu kuogopa kufanya jambo fulani hata kama JAMII linaita hilo jambo kuwa ni ZURI au limevaa ulimbwende.
Binadamu kwa ujumla huogopa kufanya chochote kile ukimtengenezea mazingira au akiwa katika mazingira ambayo kisaikolojia au ki AKILI ZA KIBINADAMU anaanza kustukia kuwa labda ni kweli pale MAKABURINI , kuna BINTI mchawi na HAWALA yake watakaoKULOGA ukienda kuchuma KISAMVU.
SAMAHANI labda ninakuogopa wewe kwa sababu wewe....:
....... ni PADRE au Shekhe, hukawii kunikumbusha miye ni mwenye dhambi .
....ni mzuri kupita kiasi na naogopa utaninyima nikikuomba kwa staili za ; HALO DADA ULE MPANGO VIPI?
......unamiakili sana na kila nikiongea na wewe najisikia MJINGA!
......mkarimu sana kiasi kwamba najiona mimi mtu mbaya nikiwa nawe kwa sababu sijasaidia kama nitegemewavyo wale NDUGU, JAMAA, MARAFIKI na MAADUI kama wewe usaidiavyo!
......unamiguvu na hukawii kuwa na KISIRANI ukikosa nanihii pale nanihii.
AU nakuogopa tu kwa sababu wewe si ndio yule?
Swali:
Ushawahi kuogopa kulala ukupendako kwa kuogopa hutaamka?
Ushawahi KUTOOGOPA kufanya dhambi kabla hujajua kufanya nanihii ni DHAMBI?
Pamoja na uzuri wa KONDOMU , ikitumika hutupwa!:-(
SAMAHANI ! Ngojea nikusalimie kwa sauti!
KONDOMU kiboko!
Ikishabeba ujauzito, hutupwa! Inawezekana kuwa marafiki wengi uwaitao MARAFIKI ni kwasababu UNAWAITA marafiki na wanakupenda kama chakula kabla hujakistukia KIMECHACHA.
CHAKULA kilicho chacha kina harufu fulani ambayo unaweza usiistukie mpaka UONJE:
Labda RAFIKI yako mpenzi umuitaye RAFIKI mpenzi ni kwa sababu unaamini ni RAFIKI mpenzi.
LABDA...
...RAFIKI wa kweli ni yule umuitaye ADUI YAKO ambaye anakusaidia KUSTUKIA unacheza na moto wakati unacheza na MOTO:
DUH!
NAACHA TOPIKI HII!
ENDELEZA lakini PENZI na YULE , yeye au RAFIKI kwa furaha hata kama UTATAFUTA jalala kutupa mafanikio yatokanayo na kufanikisha ambayo hayakusitishi kutupa KONDOMU uisifiayo !:-( -------------------------------------------------------------------------------------------------- Mpate tu RAY C akupe dawa iitwayo SOGEA SOGEA
AU pata baadhi ya PICHA zangu na baadhi ya WADAU ambao hawakunitenga maeneo fulani.
AU wapate tu
Professor Jay & MwanaFalsaFA katika dawa iitwayo JUKUMU LETU
Hukawii kusikia mtu anamfananisha mtoto mwenye kitumbo kikubwa kutokana na KWASHAKOO kuwa anafanana na BABU yake mwenye kitumbo kikubwa kutokana na POMBE ya ULANZI.
Kirahisi tu, waweza kuogopwa au kupendwa kutokana na staili yako ya nywele kama MADENGE .
Watu kirahisi wataamini kuwa ULIFANYA kama unafanana na waaminiye ANAFANYA!
Ukifanana fanana na MWIZI au MALAYA pale maeneo, kama hawajui kuwa wewe swala tano au 24, watakutendea kwanza kama wamtendeavyo MWIZI au MALAYA .
Staili ya jamii kukushuku kutokana na KIMINI SKETI chako, PARA LAKO kama mvuta bange au MARASTA YAKO kama kichaa, INAWEZA KUKUSAIDIA KUPATA au KUKOSA.
Na staili ya jamii kutengeneza tuaminivyo kuwa PADRE au SHEKHE ni mwaminifu kuliko MFYEKA MAJANI au MUUZA KIGENGE pale kona, imesaidia sana kuwasababisha WAHALIFU wakubwa kutostukiwa na watenda wema kuonekana MAFALA .Na labda inasaidia wake na wanaume wa watu fulani KUONJA KITUMBUA wakikinai MAANDAZI kila siku,hasa pale watu wafikiriapo kuwa kwa sababu wewe WINNIE MANDELA basi huwezi kumfikiria CHAKUBANGA katika kutimiza kukuna NAZI.
INASIKITISHA sana kuwa BINADAMU WENYE AKILI bado tunadhani kuwa KIBAKA , MHUNI , MALAYA au MSWALIHINA ana sura fulani au anavaa kitu fulani na sio USHANGA ULE kiunoni.
DUH ! NAACHA topiki!
SAMAHANI! Swali:
Unafikiri wewe si MHUNI?
Wikiendi Njema basi Mdau!
------------------------------------------------------------------------------------------------- Twende shuleni kidogo tukaangalie wanafunzi wanafikiria nini, katika ...A Vision of Students Today
Halafu twende KENYA tukapewe MUZIKI na Wyre & Prezzo katika Gimme the music
Lakini... Kama wewe MWEUSI hata kama staili fulani ya MUZIKI haipandi, jaribu kumsikiliza BUNNY WAILER katika kibao RISE and SHINE Read more...