MAITI haiachii ushuzi. Kama hupendi harufu mbaya , inawezekana UNAUWEZO TU wa KUNUSA na sio kweli unapenda harufu nzuri.
Tunaweza tukajifanya hatukusikia ingawa unajua tunajua umejamba.
Kumbuka lakini....
Mara nyingine tusikiacho si kijambo ingawa tunabana pua wakati unajua uliburuza kiti tu. Ukidhani tunadhani umeachia ushuzi, unaweza ukawa unajisikia kama tu ulivyojamba.
UKIKAA KIMYA si lazima maana yake HUBISHI na hutumii nguvu kwa kukaa kimya. Swali:
Unafikiri hujajaribu kukibishia kijambo leo?
Bado hunibishii tu? LOOH!
Unauhakika hutumii nguvu kujaribu kunielewa kama niandikacho ni ujinga au ushuzi?
Ukijamba , kumbuka kuwa ulikuwa na cha kujamba.
BASI NAACHA MKUU!
Twende tena kiduchu basi KAMERUNI kwa RICHARD BONA aseme EYANDO
AU twende tu na South Afrika kwa SOUL BROTHERS waseme INTOKAZI Read more...
Naamini unaweza ukadhani unajua sura ya KITUMBUA ingawa UKWELI ni kwamba unajua kitumbua ni utamu tu wa kitumbua na sio umbo la kitafunio kiitwacho KITUMBUA.
Lakini unaweza kukibadili umbo kitumbua na kukiita jina SIKUJUA , kama unahisi ndio jina kitakachoitika.
Unaweza kusahau! Ukionyeshwa picha ya KAKOBE mara kwa mara na kuambiwa huyo ni KAKOBE, hukawii kuanza kuamini kuwa umuangaliaye ni KAKOBE.
KUMBUKA TU kuwa ukiendelea kuitwa NGURUWE kila mara na watu au PUSI wadhaniao unaitwa NGURUWE, hutakawia kuanza kugeuka au kuitikia jina NGURUWE.
Swali:
Unaitwa nani vile?
Unauhakika hilo jina lako ni wewe?
SIKU NJEMA!
Tulia tuangalie ujinga kama vile ujinga ni kuzaa
Au ngojea Wasalu Muhammad Jaco aka LUPE FIASCO aseme DUMB IT DOWN
ASANTE SANA kwa wadau wote na pia ambao hamkunitenga juzi ya jana ambao baadhi ni .....
Au endeleza kuangalia kiwezacho kuwa ni busara kutokana na kona ya mtazamo wako sasa hivi kutoka kwa BUSTA RHYMES katika Lyte ya ass on FIRE Read more...
Unaweza kubisha! Ukiwaangalia wote bila sauti wafanyayo kwenye nyumba yao ya kilevi ingawa inaweza kuitwa KANISA au MSIKITI kama sio CHOO, wafanyayo katika kusujudu yaweza kukukumbusha mcheza mziki achezaye mziki vizuri wakati hakuna mziki .
Staili za kainama kainuka, kapiga magoti kabinuka, zinavalishwa heshima tu jamaa watafsirivyokuwa unamsujudia MUNGU wao wakweli ambaye ukweli wake kwako unauhakika kwa sababu wewe MSABATO na sio MLUGALUGA kama wale wajambao katika kuita MBINGU au kujaribu kukwepa JEHANAMU .
Kumbuka hata ubinuke vipi , kama humbinukii MUNGU au ZUBEDA aaminikaye analipa katika jicho laafikiriaye anajua nani ana tamutamu kunoga, wenye kuona waweza kutaka kukuokoa kwa kuzani unambinukia MIUNGU na sio MUNGU. Swali:
Wakati natafakari ushindi wa BARRACK OBAMA.............
Labda ni kweli sio sisi wote wenye ujasiri wa kufanya. Labda ni kweli sisi sote TUNA uwezo wa kufanya. Labda tofauti ya wafanyao na wasiofanya pamoja na mafanikio ya utengenezaji wa mimba au ugali iko nyuma ya kujiamini na kujua halihalisi au kujijua.
Waweza kujisahau na kuishi kutokana na muonekano na sio halihalisi. Hata kama hali halisi ni ukweli kuwa wewe ni uwezaye ,waweza kujikuta unaishi kama jamii ilivyokufunza kujiona au hata baba , mama na ndugu kama sio marafiki, walivyokupiga makonzi kwa kufanya wadhaniacho hakitakiwi kufanya hata kama kinaleta firigisi mezani.
Ukifuatilia jinsi watu wapatavyo moyo na matumaini ya uwezekano wa jambo kutokana nakushuhudia awezavyo mtu mwingine, waweza kustukia kushamiri kwa kutokuwa na uhakika chini ya sura za kishujaa za watu bwelele katika kuweza jambo.
Labda kwa watu weusi tunahitaji kuhakikishiwa na Ushindi wa Barrack Obama kuwa tunaweza kutokana na halihalisi ilioshamiri duniani kuwa mtu mweusi hawezi na Obama kama mtu mweusi aliyeweza ni nguvu yetu katika kutuletea imani yetu kuhusu sisi kwetu wenyewe.
Tatizo ni kwamba ....... ....matumaini kama moto wa kuni , huhitaji kuni zaidi na zaidi na wachochea moto pia ili moto uendelee kuwaka.
Halafu....... Histori sio shule nzuri, kamatu unakumbuka kuwa, kwa watu weusi , baada ya uhuru wa nchi nyingi za kiafrika , kulikuwa na mfumuko wa matumaini kuwa tunapiga hatua kujikomboa kwa kila aina ikiwepo muonekano na sifa za mtu mweusi, kitu ambacho mpaka sasa hivi kinasumbua.
Mpaka sasa......
Tunaendelea kupigana Congo , na sio muda mrefu hata Kenya ambako tumaini jipya kupitia Obama linaamsha hali ya kujisifia mtu mweusi, hakukua na amani.
Mtu mweusi katika tamaduni nyingi duniani inaaminika ana rangi isiyofaaa.
Sasaa tukumbuke tu kuwa ... .. ukifurahishwa sana na kitu labda cha muhimu ni kujiuliza kwanini umefurahishwa na hicho kitu. ....ukifurahia sana kuvaa nguo , jaribu kukumbuka kwa nini unavaa nguo.
Labda kuna pengo ndio maana unataka kuziba. Kuna pengo labda ndio maana tunafarijika. Lakini..... ...kwa nini kuna pengo ? Swali:
Unafikiri kwenye pengo nilazima pazibwe?
Unafikiri unaweza?
TUSIUE matumaini, chochea moto. TUSIUE matumaini, ongezea kuni moto usizimike. TUSIUE matumaini, FANYA. Siku njema!
Ni nini kweli itofautishayo upigavyo kura na apigavyo kura akitaka na ukataapo ?
Unajua nini na anajua nini kiwatofautishacho katika maamuzi yahusuyo hata juisi ya ukwaju?
Inasemekana ni busara kuwa wengi wape.
....Lakini labda wengi wakiamua wanaweza kuchukua hata kinguvu, kwani wachache hata kama ndio wenye nguvu, labda waamue tu kuwa hawatalala kamwe ilikuweza kuziba kona zote za walio wengi kuja kutungua mapera wakati wote.
Labda hakuna mjinga wala muerevu kutokana na kwamba ujinga na uerevu ni mambo yakubunia tu na cha maana ni kwamba umechagua na unataka kuwa ushinde na walioshindwa wakubali na kuishi na ushindi wako wa ubwabwa , wakihisi au kutumaini angalau hata ukoko watapata kama sio utandu. DUH!
Nawaza tu Mkuu,USITISHIKE!
Pumzika na Mganga wa kienyeji atabiri ushindi wa Obama
Au ngojea tuwasikilize Wabongo akiwemo Mwenyekiti Maggid Mjengwa
DUH Asante pia wadau wote ikiwamo hawa ambao hamkunitupa hivi majuzi
Bila kuwasahau Bitty Maclean na Peter Hunnigale
Bitty.. Kama alivyonisaidia kwa kupiga wimbo wake huu.. It Keeps Rainin'
Au Peter Hunningale
kwa kunikumbusha wimbo wake huu- Roots & Culture Read more...
UNACHOSHA saa nyingine kama MIMI na YEYE, usijidanganye!
Labda mimi na yeye tumepungukiwa na uwakilishacho au utugawiacho, ingawa unagawa kinyemela, ndio maana hujastukia.
Ukinipa au kumpa, labda nimepata au amepata. Nikipata, labda sikuhitaji ,ingawa sina uhakika na yeye kama anakuhitaji baada ya kumpa namna vile bila hata aibu.
LOH!
Kumbuka lakini.....
......Labda unanipa mbele wakati nataka nyuma.
Kumbuka lakini.... .....Mara nyingi wa mbele ndio wa kwanza kugonga ukuta ,na wa nyuma ndio chaguo la chui.
Nikikataa, bado labda hujazidisha! Ukikataa, kumbuka nilitaka kukupa. Swali:
Unafikiri hujamchoka?
Unauhakika dakika ijayo hutaanza kufikiria kuwa labda umemchoka?
Naacha basi! BAADAYE basi kama hujafa! Labda nitakuwa nimekufa baadaye lakini! Si baadaye wote tutakufa? AU? USITISHIKE! SIKU NJEMA!
Tulia na DELLA MANLEY akiwa na MUTABARUKAwakisema I KNOW
Au labda turudi tu TANZANIA kwa mwanadada ambaye na udhaifu naye, aitwaye NURU, akikiri anampenda MSELA
Kuna vitu viko tu , ukichomoa labda haikuchomekwa. Kama tu ulivyozaliwa na makengeza, haukuchagua kuzaliwa kujikuta mkristo halafu kunajisi dhambi.
Ujanja ni kuishi tu na ukweli . Hata kama si mjanja, hali halisi ndio ukweli wenyewe hata kama hali halisi ni kwamba hupendi bamia.
Kujilaumu kwa ukweli kuwa una matege, kwaweza kukusaidia kujisikia vibaya wakati asiye na matege, ana miguu kama njiti.
Chomoa tu ukitaka. Si iliingia?
Kujilaumu hata kama kunaundugu na kitu kibaya , labda ndio kitu kinachokusaidia kujisikia kuwa uko hai. Kutojilaumu kwaweza kuwa kunakusaidia tu maeneo fulani katika wewe ambayo yana kaukweli kuwa hunampango na wewe ni boaring.
AU?
Jifinye basi usikie maumivu, kama huna uwezo wa kunywa sumu. Na kama unanguvu ya kutafuta sumu uvunguni, labda unaweza bado kucheza nguti mkekani. Ishi basi!
Swali:
Una uhakika uko hai kama hujui waliokufa wanajisikiaje?
Nani kakuambia kucheza bao sio kazi?
DUH! Tulia na DJ FATBOY SLIM awarushe watu UFUKWENI pale Brighton