Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

STIGMA na DOGMA!

>> Thursday, March 05, 2009

Unaweza kuogopa kuanguka hadharani kwa kuogopa STIGMA iambatanayo na KIFAFA ukianguka badala ya kuogopa MAUMIVU ya kuanguka , wakati kuanguka ni kawaida hasa kama umewahi kusimama au kutembea, ingawa kama WEWE ni mjanja , inawezekana ulishawahi kuanguka wakati umelala.

DOGMA zaweza kukusababishia usijiulize uwezekano wa uwepo wa MUNGU WENGI au SHETANI WENGI kutokana na kuaminishwa kuwa kuna ukweli mmoja na ukweli wenyewe ni kwamba kuna MUNGU MMOJA mzuri na SHETANI MMOJA mwenye sura mbaya.



Labda,...

  • kuna ambaye hafanyi kitu ingawa kinafanyika kwa kuogopa STIGMA.

  • HAKIPINGIKI kitu ingawa kinapingika kwa sababu ya DOGMA.


Labda,...
  • DOGMA ni kukana MACHALE yako!
  • STIGMA ni kuogopa yako TAFSIRI ya machale yako , kwa sababu jamii inatafsiri na kuoanisha tafsiri na kitu .Kitu uofiacho kinakuathiri!


Dosari za stigma ni pale wewe mwenyewe utakapofikia kuamini waaminiyo kuwa ni dosari hata visivyo na dosari kwa sababu kuna stigma iliyojengeka katika jamii hata kama ni ya kuoanisha kula sana na ulafi hata kama kazi yako ni mgonga kokoto na umbo lako ni kubwa kuliko, na sahani kubwa inakuja na hali halisi na si kwa ulafi kwako .

Dosari za DOGMA ni ukweli kuwa ni mtu mwingine yalimshinda kuelewa na kuelezea KWA NINI, na kaamua kuwa HIYO iwe ndio kweli tupu kwa wengine wote na USIBISHE.

Labda,...
.... katika kulainisha mambo ya STIGMA unaweza kuunganisha na ya jamii ya KiTZ ya kama labda :

  • Ukibana matumizi na kama wewe ni MPARE kama mimi, watu wataendelea kufikiri wewe ni BAHIRI kwa sababu Wapare wana STIGMA ya ubahiri.

  • Hata kama wewe tajiri , ukiomba halafu ikajulikana wewe ni MGOGO, watu wataamini kuomba kwako kuko kwenye damu kwa sababu kuna waaminio ombaomba ni Wagogo.

  • Ukiiba kama wewe MCHAGA kama watani zangu, kuna watakaodhani unatunza na kudumisha MILA na DESTURI kutokana na STIGMA iwalengeshayo Wachaga na wizi.

  • Tukipenda ngono kama WEWE halafu ikawa sisi ni Wahaya , LABDA kuna....
  • Nakadhalika tatu katika stigma na....


Na maswala ya DOGMA yanaweza yakakuchanganya hasa katika mambo ya dini ambapo usipoangalia utashindwa kuelewa akusimuliaye kuna MUNGU MMOJA lakini hapo hapo kuna Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu roho Mtakatifu , wakati unamsikiliza adaiye yeye kapatia kwa kuamini kuna MUNGU MMOJA na SHETANI MMOJA katika ya Mungu mengi na ya Shetani lukuki.

Swali:

  • AU?
  • Kwani STIGMA ni mpaka iwe ya UKIMWI au UKOMA mtaani na DOGMA aamue PAPA wa Kiroma VATICAN?

Katika STIGMA labda kunamchango wako kama unasaidia kuamini kuwa kuna dosari ambazo zinamng'ang'ania mtu daima na kwa mahesabu yaleyale uliosimuliwa ni MAHESABU ambayo ukitekenya lazima yazae DOSARI.

Katika DOGMA , sema unataka tu kurahisisha ili kujisaidia usijishughulishe kuelewa tofauti.

Swali:
  • AU?


STIGMA na DOGMA
DOGMA na STIGMA
......na labda vyote ni UJINGA.:-(

NAACHA!
KUMBUKA NINAWAZA tu hapa!
Nakutakia mafanikio MEMA NA MAKUBWA chooni leo!


Tutulie na Dave Chappelle alete busara za kukojoa katika- Piss On You


Au DAVE Chapelle aendelee katika- NIGGAR FAMILLY


AU tu Burning Spear a kumbuke katika -Days of Slavery

Read more...

TUKANA katika staili ya kujaribu KUEPUSHA usistukiwe huna HOJA!:-(

Kama unajulia , kuna ambao HAWATASTUKIA!

Na,..
... kama unajua kutoa HOJA wakati UNAHASIRA, basi wewe BINGWA.



UKIKASIRIKA usipoangalia BADALA ya kueleza unaweza kujikuta UNAJIELEZEA.

Swali:

  • Ushawahi KUJISIKIA kutukana kwa kukosa NGUVU ya hoja?
  • Hivi tusi sio HOJA?


HONGERA!


Naacha!
Nipo lakini!:-(
Photobucket
Au ngojea nijaribu tena kusema....


Au tu Eddy Grant azungumzie - Killer On The Rampage

Read more...

Labda UNAONJEKA!

>> Tuesday, March 03, 2009

Kuna watakaodai ukila si lazima uonje kama ladha hakuna, kama tu watakaodai shughuli ya leo muhimu ya viumbe ni kubugia ili kuishi hata kama kiumbe KINA kionjea ladha.

SIKUBISHII!!

NA,..
... wakati unajiandaa kujitetea kuwa huonjeki, WAULIZE minyoo na mafinyofinyo makaburini ni watu wangapi wameshawaONJA!:-(

Katika safari ya kumalizia safari ya umeumbwa kwa udongo na utarudi kwa udongoni , LABDA ni lazima uonjeke ili ugeuke udongo.:-(

Swali:

  • Hivi busara za majeneza ya chuma kama sio almasi kwenye kaburi la sementi si nikumuingilia Mungu na vipingamizi katika kuhakikisha alivyokuumba kwa udongo usirudi kuwa udongo?
  • Unakumbuka kama huna dhambi na ukafa bila kuwahi kufanya dhambi na kwenda mbinguni ,labda si utaanza kujiuliza utamu wa dhambi ulikuwa ni nini?

Wakati unadai huonjwi , usiende kwa daktari asije akahakikisha uogopacho kwa kusema kuna virusi na bakiteria vinavyokuonja sasa hivi hata kama hujisikii kuumwa leo kama jana!:-(

SAMAHANI KAMA ninakukwaza ingawa naamini kama unadini fulani kuna uwezekano ukatubu na kujisikia vizuri.
Swali:
AU?
Si dini ni za kuwasikilizisha watu VIBAYA au VIZURI kutokana na mahitaji ya mfuata dini?

SIku njeMA!


Namuachia Nusrat Fateh Ali Khan atupe muziki aina ya QAWWALI katika - Improvisation..

Au tu NIN na mshairi SAUL WILLIAMS wazungumzie- List of Demands

Read more...

MKE mmoja, MME mmoja NA matamanio MAWILI na nusu!

Mke mmoja, Mume mmoja MTAMU!

.....Wakati ananoga,....
kikunogeacho hakiongezeki utamu UKINOGEWA.



Mume mmoja, Mke mmoja MTAMU!
.... Akiacha kunoga,....
kikunogeacho bado kitamu ingawa MWANABIBI kaacha kuonja na chakulambia,
......kama alivyokuwa akionja wakati tamu AKINOGEWA.



Mke mmoja, Mume mmoja hakuna UTAMU!
---Hakikuwepo kinachonoga...
hakikuwepo katika mhusika tokea mwanzo, ingawa MABURUKI adai
......kilikuwepo na utamu ALINOGEWA.



Mume mmoja, Mke mmoja vuguvugu UTAMU!
.....Mapungufu ya kunoga ....
ingawa Mme yupo na Mke yupo na bado mawazoni ni KITU- FANTASI ya mhusika wa tatu,
....kitu kikusogezeacho utamu UKINOGEWA.



Mke mmoja , Mme mmoja.
Mme mmoja , Mke mmoja.
.... Mawazoni una watu wangapi?



Mtu mmoja na Limchumba moja ndani ya UTAMU!
... Utamu wa wawili ukinoga,....
jumla ya utamu bado ni elfu tano
,
... na LABDA ndoa bado zipo hata mmoja USIPONOGEWA.

-------------------------------------------------------------------------------------

NAACHA!
Kumbuka nawaza tu na usitishike usiponielewa ingawa labda kuna watakao nielewa naongea nini kinamna!:-(

Swali
  • Hivi mpenzi wako UBWABWA ni mzuri na anakaribia kufanana na yule umpendaye AKILINI-MUKICHWA au katika fantasi za WALI?
  • Hivi unauhakika ndoa ni zaidi ya neno ndoa wakati bado MWILI WAKO uko kwenye ndoa na MAWAZO YAKO yameacha MWILI na YANAJARIBU ndoa IENDELEE kufanana na uaminicho ni ndoa?
  • Mke mmoja Wanaume sita si ni NDOA kama ilivyo kwa Mume mmoja Wanawake ishirini na nusu?
  • Hivi mchumba ni mtu?

Samahani naenda kukojoa!:-(
Baadaye!
Ngojea Teddy Pendergrass azungumzie - My Greatest Inspiration


Au turudi tu tena Ethiopia kukutana na TEDDY AFRO atulize mshawasha akisema- JAH

Read more...

Watu WEUSI wadhaniapo MWENYE ROHO MBAYA ana ROHO NYEUSI!

>> Monday, March 02, 2009

Kuna WATU WEUSI wafikiriao na KUAMINI rangi nyeusi ni ishara ya kitu kibaya kama tu wabaguzi wa watu weusi wajaribuvyo kuwaaminisha watu kuwa MTU MWEUSI ana kasoro na ni MTU MBAYA.
Swali:

  • Si umecheki walivyofanikiwa eeh?

Unaweza mpaka kuwasikitikia WATU WEUSI ambao wanadiriki mpaka kutamka kuwa RANGI NYEUSI nishai na ni rangi ya mavi kwa mapungufu yao ya kugundua kuwa mavi yana utajiri wa rangi nyingi.


RANGI na MAANA ZAKE hutofautiana karibu kila mahali.Kuna nchi rangi nyekundu ni mbaya na inaashiria maovu wakati katika jamii nyingine rangi hiyohiyo ina ashiria MAFANIKIO.
Swali :
  • Samahani kwakukuuliza; lakini hivi unafikiri tokea uzaliwe mpaka leo umefanikisha vinyesi vya rangi aina ngapi?

Tukirudi kwenye hoja........,

Kuna watakao sifia suti NYEUSI kama tu Benzi JEUSI kuwa zina rangi ya heshima na mafanikio, wakati wakikataa kuitwa WEUSI kwa sababu za;

  • Weusi
  • Giza, Usiku, -Maana yake huoni vizuri.
  • Mtu mweusi ,-maana yake si mweupe.
  • Nguvu za giza, nyeusi ,- maana yake ni za shetani.

na..
...nakadhalika tatu na nusu, ya kitu kilichowatoa kujiamini kwa kuwa WEUSI .

Swali:
  • Umeshastukia KIDUME mpenda ngono hupenda kuiingiza kitu sehemu za giza asizoziona vizuri kwa furaha na hahitaji tochi?

  • Hujawahi kugundua nguvu waziitazo za GIZA hufanyika zaidi MCHANA kwenye mwanga?

  • Bado unaamini shetani ni mweusi na JINI ni mweupe?

Kumbuka SIRI ya DUA la KUKU kutompata MWEWE ni ukweli Mwewe hana imani na hajui kalaaniwa na KUKU.

WAKATI Mtu MWEUSI.....
.... anaamini UWEUSI ni LAANA , labda kwa AAMINIYE inakuwa kweli LAANA.

Cha kufurahisha,...
.... tupo ambao tunajua kuwa kuna ulaini pia uletwao na kuwa MWEUSI.

Cha kusikitisha ni,...
.... WAPO waaminio kuwa kwa kuwa WEUSI wamelaaniwa na watakao tumia mpaka vitabu kama BIBLIA kuhalalisha.:-(
Swali:
  • Kama hakuna aliyewahi kuona ROHO, WEWE kakuambia nani kuna WENYE roho NYEUPE au ya RANGI ya MAVI?

NAACHA!
Siku Njema!

Tubakie Mozambique kwa André Cabaço ...



Au twende tena Cape Verde tukapate- Music Mix...

Read more...

TULIA!

Kuna UWEZEKANO kabisa......
...... ukitulia kisaikolojia UTASIKILIZIA vizuri.

UKITULIA utakuwa na uwezo zaidi wa kufuatilia hatua za utamu ZIKUSOGELEAVYO kabla ya KUSIKILIZIA ingawa unajua unaonja nini.

Kama hujui uonjacho,...
....UKIKUZA sana TEGEMEO la UKUBWA wa paja la utamu wakati hujui utamu wa bata na hukuona BATA aliyechinjwa, unaweza usiridhike na KAPAJA ka kuku utakakopata ingawa bado kuku ni MTAMU.

Labda Kisaikolojia,...
... ukiamini itauma au itaumiza kunauwezekano ikawa CHUNGU au usifaidi utamu wakati uonjacho ni kitamu kwa kuwa unahofia labda ni kona ya pili yenye UCHUNGU ingawa MASAJI upewayo ni FULU UTAMU kona hii.
Swali:

  • AU?

Naacha!
Twende Mozambique ukutane na GITO....

Read more...

Wakati tunaendelea KUKATAZA wanawake WASITAHIRIWE au KU-ze-KUKEKETWA!

>> Sunday, March 01, 2009

Nashauri,...
..... tuendelee kupinga mkeketo wa NANIHII kutokana na madhara ya KIAFYA, Kisaikolojia na hata ya KIKUJINOMA.

Tukumbuke tu!
......Ukichomoa uwe na CHA kuingiza kama hutaki kishimo kibakie kitupu.

Kumbuka,...
...hata kama unataka kuacha POMBE, jiandae kuwa na KITU kingine kitakacho CHUCHUMAA pale ULEVI ulipokuwa unachuchumaa , la sivyo utarudia POMBE a.k.a KILAJI tu, kama umeacha tu na KIU ipo tu na haina tiba tofauti ijaziayo palipoachwa na KILAJI.

Kumbuka pia moja ya kiwafanyacho watu waende KISIMANI ni kwa sababu za kuishi katika mazingira yenye KISIMA la sivyo kama katika mazingira kungekua hakuna KISIMA , labda tungeweza kwenda NAO kuvizia mademu bombani.
Swali:

  • AU?
Kwa hiyo wakati unaacha au kuachisha, jiandae au ANDAA vilevile MAZINGIRA yasaidiayo ari mpya na nguvu mpya ya MUACHO . Na kama nia yako ni KUOKOKA na KUACHA POMBE , labda kwepa walevi na jichanganye na WALOKOLE, ingawa labda kama unajiamini , unaweza kuwa Mlokole wa Kikristu ujichanganyaye na waislamu na kuzawadiwa KUJUA zaidi ulokole na UISLAMU.
Swali:

  • AU?
  • Si sehemu watumiayo kisima , watu wanaweza kuridhika na bomba la maji kama tatizo ni MAJI?
Kuna waliofanikiwa kuondoa JANDO na UNYAGO bila kuwa na elimu nyingine imfunzayo KIGOLI shughuli na KIDUME aliye balehe KUSHUGHULIKA , matokeo yake SHUGHULI NA NDOA zinashindikana na tunalaumu TV na MAISHA MAGUMU , ingawa pia siku hizi KUNA wajanja wanafikiri somo litolewalo na SOMO linatosha kufunzwa kwa siku moja kwenye KICHENI PATI .

Somo lililohitaji MKUFUNZI ahakikishe MWANAWANI anapitia UCHUNGU na UTAMU, siku hizi lina WAKUFUNZI wasisitiziao UTAMU TU na ni kwa siku moja, kwa kuandaa LIMTU kwenye maisha yenye MACHUNGU labda zaidi ya utamu.

NI muhimu UKISHACHOMOA , ingiza kama unataka mchezo uendelee.
Swali:
  • Unafikiri madhumuni ya maumivu ya Kidume kukatwa jando bila ganzi yanatimizwa na Kidume akikatwa maeneo na ganzi hospitalini?
  • Hivi madhumuni ya JKT ilikuwa nikuwatesa vijana Tanzania?

NA ,..
..... ni muhimu kabla HUJATOA na unajua kuna madhara ya KISHIMO kubakia kitupu, UJUE utaingiza nini katika kujazia.

SI lazima kama ukitoa SEMENTI , ukijazia UDONGO utakuwa umedhoofisha UMADHUBUTI wa KISHIMO. Labda SEMENTI ilikuwa inaumiza tu KISHIMO na kujazia kishimo KWA unga wa ULEZI ndio ilikuwa na NI dawa ya NYUFA.

Swali:
  • AU?


Kumbuka,...
.... wakeketaji walikuwa na sababu zao na jaribu kuzijua kabla ya KUTOA na kujikuta hauna cha KUINGIZA, au tu kujikuta kuwa kutokana na kutokujua PICHA NZIMA unashindwa kutetea hoja zako za KUCHOMOA hata kama una cha KUINGIZA.
Swali:
  • Hivi ukijua ni lazima uchomoe na hujui cha kuingiza, uiachie MUMOMUMO nini?
  • Kwani ukiacha ya SHETANI ni lazima ufuate ya MUNGU?

Naacha!
Topiki IMENISHINDA:-(
Tuendelee kuwepo South Africa kwa Busi Mhlongo katika- Urbanzulu


Au tu twende PANAMA kukutana na KAFU BANTON enzi hizo kabla watu hawajastukia Reggaeton katika - EL MAD MAN

Read more...

Wakati KUNA vitu JAMII INAENDELEA kuamua ni MWIKO KUVIONGELEA kama tu KUCHEZEA mavi!

Ni kweli,...
.....CHA AJABU ni kwamba jamiii imeamua kukataa mambo fulani yasiongelewe.

Lakini,.....
......MAMBO yanaendelea KUFANYIKA katika jamii ingawa hatutakiwi KUYAONGELEA.

Tatizo ni,....
.... jamii na JAMII hutofautiana na MIIKO ya jamii moja ni ruksa katika jamii nyingine.

Wakati jamii moja ni mwiko adhabu ya KIFO, nyingine kifo ni jambo la kawaida na KAMA WEWE MWANAFUNZI ukiandamana, hukawii kupigwa virungu na ukifa poa tu.

Na,...
....kuna JAMII ziaminizo ni mwiko kula kwa mkono kama tu waaminio kula kunahitaji KIJIKO, UMMA na KISU.

Swali:

  • Hivi JAMII ndio akina nani kama wewe hauhusiki?
  • Si labda KUTAWAZA msalani ni kuchezea mavi ingawa ni mwiko kuwa na huo MTAZAMO katika JAMII?

Miiko NI KIBOKO na inaweza kumfanya MUISLAMU ajifanye MLOKOLE kama jamii ni ya KILOKOLE.

Na,....
..... MWANAKIJIJI anaweza kufikiri ni lazima ajifanye ni MTOTO wa MJINI kama anahisi kuna MIIKO inayomkumbusha kuwa hayuko KIJIJINI kama tu Msenge ajaribuvyo kujifanya basha maeneo mengine.

WAKATI katika jamii MIIKO inaweza kumfanya MKATOLIKI ASIKIRI kaokoka, MLOKOLE anaweza akamkana YESU katika kusawazisha ya KIDUNIA kama ya KUOPOA NGOMA.

Labda,...
.... sababu za MENGI kutoongelewa ni fikra kuwa:
  • SI heshima KUNONG'ONEZA
  • SI busara KUONGELEA
  • NI aibu KUSEMA
  • NI matusi KUSIKIKA

AU
....LABDA hatuna uhakika na MAANA ya UYASEMAYO nayanachangiaje katika MUONEKANO WAO katika JAMII hata zaidi ya MUONEKANO WAKO.


Tatizo ni,....
...... ukichukua muda kufikiria ni kwa nini jamii INAMTISHA mwanaJAMII , unaweza kugundua ni kwa sababu MWANAJAMII HUTISHIKA.

Swali:
  • Unakumbuka lakini kuwa hata ukianguka sokoni kwenye UMATI wa watu , ni asilimia ndogo sana tu ya watu inayoweza kushuhudia UMEANGUKA au hata kukumbuka ULIPIGA chini?

  • Ushawahi kusikia AIBU kwa afanyayo MTU mwingine wakati hakuhusu na afanyayo HAYAKUHUSU?
  • Kwanini?

  • Ushawahi KUJIPENDEKEZA kwenye sifa za MWINGINE hata kwa kudai unauhusiano naye au mnatoka kijiji kimoja wakati HAKUHUSU na yake HAYAKUHUSU?

NAJUA baadhi ya niandikayo hapa kijiweni KUNA waaminiyo hayafai kwa kubwa zima KUONGELEA.

Lakini narudia,....
.... JAMII zina TOFAUTIANA kutokana na wanajamii KUTOFAUTIANA.
......JAMIII zinaendelea KUTOFAUTIANA kutokana na WANAJAMII kuendelea kutofautiana.


Na,....
......JAMII zilizotofauti ZINAENDELEA kuungana hasa kwa jinsi DUNIA inavyozidi kugeuka KIJIJI.

Usishangae kupigwa BUTWAA kila kukicha kwa kushuhudia MIIKO ikivunjwa kuanzia kwenye TV yako sebuleni mpaka kwenye uchochoro wa pembeni ya KANISA lako , MSIKITI wako , SINAGOGI lako au PALE uchochoroni, pale kati ya BAFU na CHOO chako.

Lakini,...
.... MIIKO ni gundi ya jamii na kama unavunja MIIKO kaa katika mkao wakujua kuwa BINADAMU ni king'ang'anizi wa MIIKO aliyoizoea imfanyayo aamini ANAELEWA na KUJIELEWA.

UKIVUNJA miiko unaweza ukawa ni tishio katika JAMII na BINADAMU kama MBWA KOKO , si kila mara ukimtisha anakimbia.

Mara nyingine BINADAMU kama MBWAKOKO ukimtisha akajisikia unamuweka kwenye KONA , anaweza kukung'ata MAENEO kama MJUSI tu.

Swali:

  • LEO umekwepa KUONGELEA mangapi kwa kuhofia JAMII itakuelewaje?
  • SI unakumbuka JAMII inaweza kuwa MAMA, Baba, DADA, Kaka, Mchumba, Kimada, Rafiki wa Mpenzi wako utamaniye KUMKONYEZA,.....na WEWE?


Tukumbuke tu LABDA,...
.....katika JAMII kuna wakwepao NYAMA YA NGURUWE na kula YA MBWA, kama tu ambavyo wapo wakwepao NYAMA YA MBWA na kula YA POPO . Na hata kama mambo yote ni MCHICHA , mwiko wako wa kula PEREGE labda haumuhusu mwenye mwiko wa kula SATO kwa CHUNGA.

SHIKILIA yako yenye MAANA kwako, YA wengine kama hayakuathiri wewe WAACHIE wenyewe WAHUSIKA hata kama yaletayo maana kwa WAHUSIKA ni KUCHEZEA mikojo.

Swali:
  • Miiko ya Mkatoliki Itali unafikiri inafanana na MIIKO ya Mkatoliki TANGA?
  • Miiko ya MUISLAMU Yemeni unafikiri inafanana na MIIKO ya Muislamu KAGERA?
  • HIVI miiko yako SEBULENI inafanana na ya CHUMBANI?
  • Hivi DINI yako sio KIONGEZO cha mkusanyiko wa MIIKO yako na labda SI lazima wengine IWAHUSU?


NAACHA MAHUBIRI!
Topiki imenishinda!:-(

Twende South Africa kuangalia somo katika -Music and apartheid in South Africa


Au tu huko huko South Afrika , Black Mambazo & PJ Powers wazungumzie -Knocking on Heaven's Door

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP