Kwa JUUJUU!
>> Thursday, June 11, 2009
Kwa JUUJUU,...
.... amuonaye anayecheka hudhania achekaye moyoni anafuraha!
Kwa JUU JUU ,....
.....aliaye anaweza dhaniwa halii kwa furaha!
Kwa JUUJUU ni ngozi ,...
......na kuna BINADAMU weupe na weusi wasahauo kuwa wote WAFANANA kwa ndani!:-(
Kwa JUUJUU ,....
.....akaaye kimya wanadhani KASAHAU!
Kwa JUUJUU,....
..... unaweza kutomstukia atakaye hata kukupiga JUJU!
Kama unajua JUU JUU ,...
.....weye hujui undani wa KITU au MTU na ujuacho ni kwa JUUJUU na labda ni kweli udhaniaye mlevi hajalewa!
Na,...
... kwa JUUJUU labda nilichoandika ni UJINGA!:-(
----------------------------------------------------_______________----------------
NI wazo tu MKUU na NIMEACHA!
Swali:
- Unadhani kuna umjuaye kiundani?
- Unadhani ni mara ngapi unajaji kitu bilakukijua kiundani?
Namuacha Mr FOX adai-Yo No Tengo La Voz
Au tu YONDO SISTER alete-Mbuta Mutu
Read more...