..... ndio maana hata kuruka KICHURA CHURA kukitazamwa kwa mtazamo wa kuwa KICHURACHURA NI MAZOEZI huwa ni MAZOEZI ,....
.... wakati ukirushwa KICHURA CHURA ukiwa na mtazamo ni ADHABU hicho hicho KICHURA hugeuka kuwa ni ADHABU.:-(
Swali:
SI umewahi kuona watu katika mazoezi wanapigishwa PUSHAPU na wanaitikia wito wa KOCHA WA ZOEZI kwa FURAHA?
MTAZAMO ni kitu cha ajabu,.....
.... kwa kuwa unaweza kukufanya URIDHIKE hata na UMASIKINI kwa kuwa kwa mtazamom wako hicho ni kitu cha kawaida kwa kuwa jamii yenyewe yote uishinayo ni MASIKINI na kuona ombaomba ni KAWAIDA.
MTAZAMO ni kitu cha ajabu,....
.... kwa kuwa kwa MTAZAMO wako kama wewe unajihisi ni MBAYA hata uwe MZURI VIPI unaweza usijiamini KIUZURI kitu kiwezacho kukufanya upende kusifiwa mara kwa mara ni MZURI ili tu angalau ujiamini kuwa labda wewe sio MBAYA SANA kitu ambacho kinaweza kuhasiri hata ni NANI UNAFIKIRI NI MARAFIKI WA KWELI kwako kisa wanakusifia tako kitu ambacho kinafanya udhanie wasio kusifia kalio hao sio MARAFIKI WA KWELI na kwa kidhungu aka LUGHA YA KITAALAMU YA KIBISHOO ukawaita MA- HATER kama tu vile kutokusifiwa sio KAWAIDA.:-(
MTAZAMO ni kitu cha ajabu,....
.... unaweza ukakufanya usistukie MUHESHIMIWA ni MALAYA ingawa afanyacho ndicho ukiiitacho UMALAYA kwa kawaida.:-(
SAMAHANI NALIKATIZA WAZO HAPA kabla ya kuongelea kwa kina ,....
....``MTAZAMO kama SILAHA uwezavyo kumsaidia MALAYA kuvumilia maumivu ya biashara ya KUJIUZA!´´
Swali:
Kwani kwa MTAZAMO wako hujanielewa naongelea nini katika kudai MTAZAMO wako unaweza kuwa ndio ukuponzao kusikia maumivu wakati ungegeuza mtazamo CHUNGU ingekuwa TAMU?
Hebu LOPANGO YA BANKA wadinye ndude kubwa KATIKA KUBADILISHA HALI YA HEWA KIJIWENI kwa kitu-MPO NA KONGO
Bisso Na Bisso nao wanyokolishe kwa kitu - Le Reve Africain
AU tu hebu tu BISSO na BISSO wamalizie na ndude-Bisso na BISSO
[Tahadhari: Wazo limepinda na linakonakona kimtiririko kwa hiyo shauri yako kama unanisoma halafu huelewi, Miye SIMO!:-(]
Kabla sijakupotezea muda;
KWA KIFUPInachokilenga mjeledi KINUNDU katika TARALILA hii ni kuwa:
´´Rais yeyote yule atakayechaguliwa TANZANIA awe kutoka UPINZANI au CCM hataweza kutimiza malengo ya WAMPIGIAO KURA kwa kuwa MIUNDO ya TAASISI za BONGO na UKIRITIMBA WAKE haufanyi kazi ipasavyo......
Na kiongozi ambaye hataweza kulenga PAMOJA NA YOTE , miundo ya TAASISI ZA SERIKALI na ufanyakazi wa TAASISI kwa kuziboresha au kuzipamburua ili kuondoa ukiritimba - na ambaye hata lenga kujenga Taasisi MPYA ambazo zinalenga matatizo ya WATANZANIA na TANZANIA sasa, .....
.....hata weza kuondoa RUSHWA, umasikini, UJINGA, na kwa kifupi ataendelea kurudia yaliyomshinda NYERERE ambayo yanamshinda Rais KIKWETE.´´ - Mwisho wa KINUNDU.
HEBU tuliangalie swala aka KINUNDU kwa kuangalia jinsi KUTOKA WAZO la kitu mpaka MAFANIKIO YA KITU yahitajivyo ufanisi wa MIUNDO ya TAASISI kwa kuangalia dondoo za miundo ya taasisi za SEHEMU ZA SIRI aka uchi wa MNYAMA ziwezavyo KURAHISISHA uelewaji hasa UKIZINGATIA;....
......mfano wa JINSI mfikiria kupata mtoto awezavyo kufanikiwa kupata mtoto IKIWA TU miundo mbinu na miundo ya taasisi HUSIKA zinamuunganiko usababishao KIFIKIRIWACHO kizae mimba.ukikumbuka tu hapa KILENGWACHO KATIKA MFAN ULIOPINDA ni kuangalia jinsi MKUU wa SERIKALI na WAFIKIRIAJI WENZAKE wahitajivyo miundo mbinu bora na MIUNDO YA TAASISI BORA ili WAZO lizae MATUNDA.:-(
Mwanzo wa mtazamo:
MFIKIRIA kuzaa mtoto ili kiutekelezaji azae mtoto ,....
..... miundo mbinu ya taasisi za sehemu za siri hufanikisha tu anachofikiria- hapa na maanisha kumpa mimba au kupata mimba- kwa kuwa miundo ya taasisi za sehemu za siri ipo na inafanyakazi bila ukiritimba ,....
....kitu kifanyacho WEWE KAMA MWANAUME kinakuwezeshaKUFANYA UFIKIRIACHO kiamshe hisia , HISIA ZIAMISHIAZO MAJUKUMU katika MIUNDO YA taasisi ZA CHINI YA KITOVU ambazo zina mfanyakazi mwenye support system aka miundo mbinu na shehena ambayo ingawa kuna ladha kama motisha kusaidia kazi ifanyike na kimiminika kisafirishwe mpaka katika mdomo wa KIFAA cha fani.
....kitu kifanyacho wewe kama MWANAMKE kisaidie unachofikiria na kama muda ni sahihi KITAIMINGI miundo ya TAASISI zako za sehemu sehemu itumie MIUNDO MBINU BORA ya taasisi za sehemu zako za siri ILI ziwezeshe malighafi YAI iliyotengenezwa katika moja ya TAASISI MWILINI ifikishwe kwenye uchochoro WA MAKUTANIO ya yai na mbegu hasa kama miundo mbinu ya upelekwaji wa YAI lisilodariziwa na LILILODARIZIWA TAYARI mahali maalumu yote ikiwa ni katika kuwezesha mchezo wa baba na mama uzae matunda.
..... kitu KITUKUMBUSHACHO PIA umuhimu wa mahusiano ya watu- IKIWA KATIKA MFANO ni mwanamme na mwanamke wajuao mchezo - ingawa KISEREKALI ni WAFANYAKAZI BORA WAJUAO KAZI hata kama kuna TAASISI BORA KIMIUNDO ili matunda yatokee.
KWA KIFUPI,....
....inahitaji ushirikiano wa MWANAMKE na MWANAUME hata kama TAASISI ZAO ZA SEHEMU ZA UZAZI ziko bomba ili kusababisha matunda ya dunia kujazwa yafanikiwe kama tu ihitajikavyo TAASISI bomba ki miundo kitu ambacho TANZANIA HATUNA ili kufanikisha MAWAZO YA RAISI kufikia utekelezwaji murua hasa ukikumbuka umuhimu wa TAASISI HIZO ZENYE MIUNDO MZUKA ihitajivyo wafanyakazi BOMBA..:-(
SAMAHANI ngojea nilainishe lugha:
Sasaaa....
Tanzania kwa MIAKA NENDA RUDI imesifiwa hasa na WATANZANIA WENYEWE kuwa ni nchi ya amani. Cha kushangaza ni kwamba pamoja na amani yake maendeleo yake yanautapiamlo kiasi kwamba utakuta NCHI ZISEMEKANAZO kukosa amani huwa wala hazitishwi kimaendeleo na TANZANIA ambayo hata kwenye MPIRA wa miguu wenye washabiki wenye munkari au kwenye POMBE ambako kuna washabiki wenye motisha tumeshindwa kuwakilisha katika dunia kwenye fani.:-(
Na wakati huu wa uchaguzi TANZANIA ni rahisi kushabikia KIONGOZI MGOMBEA mmoja au MWINGINE bila kujiuliza ni kwanini viongozi lukuki waliotangulia kuanzia Rais NYERERE mpaka Rais KIKWETE ,....
.....siye na amani zetu bado hatuchezi mbali na UMASIKINI, ujinga, CHUPI ZA MTUMBA ,.. ...nk
Na tunajua kuwa WATANZANIA wanaweza wakiamua hasa ukifuatilia jinsi tuwezavyo kufanikisha KICHENI PATI , harusi za ajabu, kushangilia timu za mpira wa ULAYA, mazoezi ya kupata na kumpa mtu mimba, kupata kilaji ,nk
SWALI:
Umenielewa nalenga nini?
Umesikiliza ni hoja gani za MGOMBEA ambazo zinatekelezeka na umefikiria ni kwanini KILIMO kwanza haimfanyi BISHOO ajisikie kushika jembe KIUTEKELEZAJI?
Ndio,....
...... labda TATIZO SIO NANI NI RAIS Tanzania kwa kuwa LABDA hata UMRUDISHE Moringe SOKOINE hakuna atakachofanya kama MIUNDO ya TAASISI zenyewe ambazo ni muhimu katika utekelezaji WA LILILOKUWA WAZO mambo yake ni kama tako la Mzee aliyejisaidia kaba ya kuchambwa.:-(
Ndio,...
....na LABDA hata kukiwa na TAASISI zenye MIUNDO bora, kama hazina WAFANYAKAZI wajuao kazi na wenye munkari wa kazi ni BURE kama tu Mbwa jike ALIYE KWENYE SIKU ZAKE mwenye taasisi zenye miundo bora ifanyayo kazi sawasawa lakini hajuikumgawia mbwa dume KISHUGHULI au tu Mbwa dume hapatii MSHUGHULIKO wawezavyo kusababisha TAASISI KUTOTIMIZA lengwa ya duninani kujae zaidi MBWA.:-(
Swali:
SI unakumbuka ni KWANINI Waziri MREMA alifanikiwa kusababisha UJAMBAZI upungue kwa kustukia TAASISI katika miundo unahitaji vituo vya polisi vidogo karibu zaidi na WANANCHI?
NIMEACHA!
USITISHIKE MHESHIMIWA hili ni wazo tu NA SAMAHANI kiduchu KWA KURAHISISHA hoja ngumu na NZITO kwa kuiingilia kimtindo wa taralila za UJINGAbusara MKUU !:-(
Hebu Don Carlos arudie mkuno-Time
Au tu DON Carlos arudie ndude-Just a passing glance
Hebu nimuachie tu Tenor Saw enzi za 1985 arudie-Ring the Alarm na pia Fever
Au tu turudi SenegalDAARA J wadunge tena kitu- ALLAH
... mara nyingi KINAWEZA KUELEZEWA kwa kutumia mfano WA JINSI mtu afikiriavyo NI KWELI hana hajakubwa wakati anatembea kwa maringo ,.....
..... kwa kuwa tu ETI hajabanwa hajakubwa.:-(
Swali:
SI unakumbuka labda kwa MTU labda mavi yapo hata kama ni kweli HAJABANWA choo?
Uongo si ni kweli ni UONGO kwa hiyo UONGO labda ni UKWELI?
Ukweli ,....
......labda ni UKWELI pale tu kabla hujastukia uongo wake na ndio MAANA MPAKA hata imani ziko nyingi na zote ni za kweli kwa aaminiye kwa kuwa kwa KUAMINI KITU labda ni kukiri KWA MTU kuwa bado hajastukia DANGANYATOTO kitu.:-(
Na labda UONGO ni KWELI,....
..... kama ni kweli ni UONGO.:-(
NI WAZO TU HILI MKUU na RUKSA kulitemea koozi kama halipandi mukichwa!:-(
Hebu turudi HAITI tena ili Sweet Micky arudie ndude -Ou lala
Au tu tubaki tu hapahapa HaitiMichel Martellyaka Sweet Micky adunge na ndude -Cocorico
Na labda tupitie tu tena CongoTabu LEY alete ya kishtobe - Jolie Elie
Kuna kitu WATU wengi hawajui kuhusu MIE Simon KITURURU,...
... ila ukweli ni kwamba mkono wangu wa kulia haufanyi kazi vizuri kama inavyotakiwa ,...
... kwa KIFUPI hata UKIWA sio mbali sana siwezi nikakurushia jiwe kama nataka kukubwenga JIWE kirahisi na MKONO WA KULIA.
Na tatizo lilianza kisa nilikuwa naficha siri eti kwa kumuogopa BABA.:-(
STORI fupi laini na YA KWELI :
Tulikuwa tunaishi SONGEA na moja ya vitu MDINGI alikuwa hapendi ikiwa pamoja na KUWA MCHAFU , kufeli mtihani enzi hizo nikisoma SHULE ya MSINGI MFARANYAKI (kitu ambacho nilikuwa sifeli) ,....
..... nilikatazwa kupanda juu ya MITI aka kuparamia miti kimichezo.
Siku moja mie na marafiki zangu tukaenda kuiba maembe aka KUTUNGUA MAEMBE yasiyo yetu shambani kwa WANAFUNZI WA SONGEA GIRLS. Enzi hizo shamba la songea GIRLS lilikuwa kubwa na sisi tulikuwa tunaingilia upande wa UWANJA WA MEDICAL karibu na nyumba za mwisho mwisho za walimu enzi hizo za miaka ya NAINTINI EITEZ( (Kumbuka ni miaka mingi sijafika Ruvuma sijui maeneo hayo yakoje siku hizi)
Basi BWANA katika kuwinda maembe bolibo na embe sindano tukaupata mti ambao mbivu zilikuwa zimenona juu kabisa. Na mie ambaye hukatazwa kupanda miti nilikuwa kiongozi kuparamia juu kabisa kutikisa mti.
Kilichotokea ni kwamba,...
.... katika kutikisa tawi ili kudondosha maembe tawi likakatika na kilichofuata nilijikuta chini nikijiuliza niko HAI au NIMEKUFA,.....
.....na chaajabu hata marafiki zangu wakinisemesha nilikuwa siamini kama niko hai kwa KUWASIKIA kwa kuwa nilikuwa nahisi kuwa labda hata MFU akisemeshwa huwa anasikia.:-)
Katika kufupisha stori hii ya kweli;...
....nilivyoanguka nilitegua mkono wa kulia na baadaye nikaja stukia labda na kitu kingine mkononi kiliharibika.:-(
KIKUBWA:
Kwa kuwa kwanza nilikatazwa kupanda miti na PILI miye na marafiki zangu tulikuwa tunaiba maembe ya wana SONGEA GIRLS nilifikiri sio busara kusimulia hicho kitu nyumbani. NILIFICHA maumivu na ugonjwa kisa NAMUOGOPA BABA....
.....na kwa bahati nzuri ilikuwa ni kipindi cha baridi SONGEA na maswala ya SWETA na JACKETI pamoja na MAIGIZO kuwa NIKO BOMBA yaliniwezesha kuficha nimeumia mpaka mkono ukapona kinamna.
TATIZO ni kwamba mkono ulivyopona mpaka leo hauwezi kumlenga MBAJUWAYU bila msaada wa mkono wa kushoto.
Kwa kifupi :
Nilijitia udhaifu wa mwili KWA KUFICHA UGONJWA kisa NAOGOPA KUCHAPWA. na BABA:-(
Unajua tena AKILI ZA KITOTO!:-(
NI moja tu ya stori ndogo ya KUJARIBU kukufanya MHESHIMIWA ufikirie kabla hujamfanya mwanao AKUOGOPE mpaka ashindwe kukutaarifu hana pesa za kutoa mimba kwa hiyo atajikorokochoa mwenyewe kisiri bafuni.:-(
Na ni HILO TU MKUU!
Hebu OCHESTRA MAKASSY wadunge ndude-MKE WANGU
Hebu NDALA KASHEBA arudishe ndude-MARASHI YA PEMBA
AU hebu tu DDC OCHESTRA Mlimani PARK wakite kwa -MTOTO AKILILIA WEMBE
Na mbu JIKE ndiye aumaye watu kisa anatafuta VIRUTUBISHO vya wanawe.
Na jitihada za MBU JIKE aitwaye na wazungumzao ung'eng'e{ Anopheles} za kutafuta PROTINI kwa kuwa ni mjamzito ndizo zimfanyazo apigwe vita na BINADAMU kwa kuambukiza watu MALARIA,....
Swali:
Unafikiri ni wangapi wanawahurumia MBU NA KUACHA KUWA BWENGA kwa kuwa WANAJUA ni kweli MBU JIKE ambao ndio wanyonyao damu za watu WANANYONYA tu katika kutaka angalau watoto wao wapate virutubisho vilivyopo kwa watu damu?
Si unajua nia ya MBU sio kuambukiza mtu MALARIA?
Unafikiri ni mangapi ukiruka mimba kuna mtu angepigwa BONGE LA MBATA kama kitendo kingejulikana pamoja na tamu ni kile kimuambukizacho BINADAMU MWINGINE bonge la gonjwa kuliko malaria?
Ndio,...
.... labda MAISHA hata ya BINADAMU ni lazima yawe magumu tu kama huyo BINADAMU anaishi.
Swali:
SI Binadamu tuna mchezo wa kuamini MAREHEMU ni mtu mzuri kwa hiyo akifanikisha umarehemu kapumzika kama hakuwa mzinzi , mdokoa mboga au tu zile zambi mhusika adhaniazo ni bonge za dhambi zenye tako kubwa?
NAACHA wazo MKUU, na ni wazo tu hili BINGWA wala sio BIBLIA !:-(
Hebu Mbaraka Mwishehe aulize - MATUSI YA NINI?
Kwa kubaraguza ngojea tudeku baadhi za MOVIE nilizo zirudia kwenye maktaba yangu ndogo ya nyumbani kama:---- Samuel L Jackson katika diner ndani ya movie - Pulp FIction
Samuel L Jackson katika Pulp Fiction - Ezekiel 25:17 ndani ya kazi ya Quentin Tarantino
GoodfellasJOE Pesci arudie kitu katika kazi ya Martin Scorsese
... kuliko BINADAMU astukiavyo hata BINADAMU mwenzio mwenye kikohozi anaweza wakati wowowte KUBANJA.:-(
Swali:
AU?
Katika kunusa ,....
.... tunajua NGURUWE na MBWA wana pua kali kuliko BINADAMU.:-(
Ndio,...
... kuhusu kusikia ,...
... tunajua hata TEMBO na PWEZA wanasikia kuliko awezavyo kusikia BINADAMU.:-(
Na sikubishii MHESHIMIWA ambaye unaweza kustukia mbwa kajamba kwakuwa unanusa,....
.....HASA KAMA wakati unamuona BINADAMU ni kiboko kwa kuwa wewe ni BINADAMU unashindwa kustukia KUNGUNI na chawa wana janja zao hata katika kujificha katika MAVUZI ya MHESHIMIWA MCHAFU HATA SIO SANA ambaye ni binadamu.:-(
Swali:
UNauhakika BINADAMU ni mjanja KULIKO MINYOO kwa kuwa kuna BINADAMU mwenye BENZI halafu aligundua tumizi la chupi?
Unauhakika MENDE wajuao JIKO lako MREMBO ni chafu hawana busara za utafutaji maisha kuliko WATANI zangu WACHAGA pale MOSHI stendi?
LAKINI BINADAMU huyohuyo ukimsikiliza ,...
.... kwa kudai yeye ni mtu apendaye amani kwa JINA hata la yesu anaweza kukubwenga kisawasawa ili uelewe AMANI ni nini hutu akimtukania mama yako.:-(
NI wazo tu hili MHESHIMIWA lililokaa KI-MAMA KISEBENGO!:-(
Usitishike BISHOOO MHESHIMIWA ni wazo tu hili!:-(
Hebu Tabou Combo adinye kitu - Pi Gro Pi Long
Au tu Jean Philippe Marthely adunge ndude - Bèl kréati
Au tu Patrick Saint Eloi akung'ute mkito -Chiré
Na labda tu Jean Claude NAIMRO amalizie KWA ngoma - Ave'w Doudou
AU niache tu baadhi ya picha za juzi ya jana....:-(