Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa, INGAWA, , halafu,....LABDA!

>> Sunday, April 03, 2011

Kwa kuwa ,...
.... inaaminika,...
...halafu UKAAMINI,...
... na kuaanza kufikiria ,...
...LABDA ,...
... ni kweli,...

.....

Swali:
  • Si unajua ukikwama hapo ndio unaweza kuzidiwa NA udhaifu wa KUJIAMINI mpaka yale yote ambayo ulikuwa unauhakika sio sahihi MWANZONI  yanaweza anza kuonekana labda ni kweli kwa kuwa yako tu wakati unaudhaifu unafikiri labda kimfikirio ULIKOSEA kitu?


Kwa kuwa ,....
.....INGAWA....
..... halafu......

.....LABDA,...
.... bado si kweli majibu ya ATAPATAPAYE kwa kuwa maji yamemfika SHINGONI bado ni KIGEZO kuwa NI  kweli yake ni ndio MAJIBU sahihi hata kama ni KIIMANI tu kwa waaminio!:-(


Ni wazo tu hili BINGWA na NI ruksa kutolielewa!:-(



Hebu I Wayne aanzishe UPYA kwa -Need Her In My Arms



I-Wayne adinye tu na- Living In Love




Aingie ndani zaidi ya nanihii kwa-Life Seeds




Au tu Richie Spice aingilie kati na kuzima manyanga kwa - More Life


Read more...

Bado ukweli uko pale pale kuwa SIGARA , bangi, kidude, mbirimbi , POMBE mpaka NYANYA zilizokolezwa madawa ya kuua wadudu LABDA si nzuri kwa AFYA yako!:-(

>> Saturday, April 02, 2011

CHA kusikitisha ni kwamba,....

.... labda karibu kila kitu si kizuri kwa afya yako,....
.... ukitazama maswala kwa kuzingatia kuwa ,....
.... karibu  MAZAO yote sehemu nyingi kutokana na madawa na mambolea yachumvichumvi  NA MADUDE MENGINE yatumikayo ,...
... tukiachilia jinsi WATAALAMU WA SAYANSI  tuwaaminio kuliko WAGANGA WA KIENYEJI wazidivyo kuchezea mazao  kwa KUYAKOROFISHA KIJENETIKS aka Ki- genetic modification ukiyachunguza,...
... labda hakuna lililosalama kihivyo hata kama unatumia kondomu.:-(



Kwa hiyo labda wakati unanyooshea watu kidole,....
... kumbuka LABDA ufanyacho kinamadhara yaleyele.:-(

Swali:
  • SI kuchambia maji labda kuna madhara yaleyale ya kuchambia TISHU ingawa mchambia mchanga  labda ndiye aonaye tofauti?
  • Unafikiri afanyaye kitu makusudi huku akijua madhara yake na afanyaye bila kujua kama akimbiliaye KULA kula mboga za majani  ambazo HAJUI  tu kuwa zimekolezwa madawa GANI kisawasawa YAFANYAYE mtoto mzuri wakike awe TASA kama tu RIJALI awe na udhaifu wa KUDINDISHA MTALIMBO na ni afadhali tu angejilia NGURUWE ki nyama ya kitimoto-  nani ni  anaafadhali?

Nawaza tu!:-(


Hebu Carlos Santana arudie - Oye Como Va



Au tu Carlos Santana aje na Rob Thomas warudie - Smooth

Read more...

R.I. P . ADAM LUSEKELO!:-(




Katika waaandishi  na MABLOGA wa BONGO ambao tokea enzi FULANI za ENZI zangu walininasa ni:
....ADAM LUSEKELO!



Rest in Peace BROTHER!

Habari hii nimesita sana hasa kwa kuwa ilinifikia katika tarehe 01.04. ijulikanayo kama siku ya WAJINGA.

Na mpaka sasa hivi ni watu kadhaa niwaaminio wasititizao kuwa ni KWELi na  sio MZAHA hii habari ,...
......
...kwa MARA nyingine,...
...Rest in PEACE  Adam L. Mwakang'ata!




Habari nyingine kuhusu hii habari pata  HUKU

Au  HUKU


...hata HAPA

... ambako kuna waliodaka habari na kuiamini nakuianika mapema zaidi wakati mie bado SIAMINI kitu hii.:-(






Kwa kumbukumbu angalau ya BLOGU YAKE  mtembelee kwenye iliyokuwa BLUGU yake HAPA




I still want to BELIEVE this is not TRUE!:-(




Habari zaidi:

By DAILY NEWS Reporter, 1st April 2011

SEASONED and veteran journalist, Adam Lusekelo (54) passed away while being rushed to Muhimbili National Hospital (MNH) on Thursday night, his wife Scolastica Lusekelo, said. Ms Lusekelo said the deceased’s health deteriorated on Thursday night when relatives rushed him to MNH.

“He didn’t even reach the hospital, he breathed his last on the way at around 11pm,” Ms Lusekelo said. The 'Sunday News' columnist has been battling diabetes for a long time and was surviving on medication.

“Oh, no! We have lost a 'Sunday News' readers’ favourite,” lamented the newspaper’s Editor, Ichikaeli Maro upon receiving news of Mr Lusekelo’s death. His column, a unique blend of writing serious issues of national importance with a soft touch, won many hearts and souls.

“My husband will miss him badly, he was his favourite columnist,” said Joyce Sabuni, Tanzania Standard Newspapers employee in the circulation section.

TSN Acting Managing Editor, Mkumbwa Ally also mourned the death of one of journalism’s most gifted writers.

Burial arrangements are being made at his home at Ubungo Maziwa, but the body is likely to be transported to his home region of Rungwe in Mbeya, his wife said. The late Lusekelo is survived by a wife and three children, two daughters and a son.

He worked with TSN briefly in the 1980s before joining BBC as a correspondent based in Dar es Salaam.

Read more...

MONOGAMY aka siasa za mapenzi kiubahiri za CHANGU ni changu tu kama hicho KILICHO changu ni MPENZI WANGU!

 Maswala ya :

  • Hivi ni kweli BINADAMU anatakiwa awe na Mpenzi mmoja tu?





.... yaliyosababishwa  na kamjadala  MTAANI nilikokuwa nagida MOJA moto moja BARIDI kabla ya kuelekea nyumbani LEO HII ulioletwa na ATIKO  ya Leanne Bell iongeleayo MONOGAMY ,...
.....  nakiri nimeyaachia katikati  YA MJADALA wakati  WADAU  wakiendelea kupambanua swala.

Paka nikimbie mjadala kutokana na MUDA na STIMU  vilevile ya KILAJI kuistukia inaanza kufanya ushirikiano wa miguu kuanza kuwa dhaifu  na kauli kistaili kuanza kugeuka  kimvuto na kunistua ninywacho ni POMBE na  sio CHAI  ,...
...mambo yalikuwa ngoma droo kati ya wale waaminio BINADAMU hakuumbwa awe na MKE au Mpenzi mmoja tu  na haya maswala ya MPENZI mmoja BINADAMU kajifunza juzijuzi tu na wale ambao wanadai BINADAMU sio MNYAMA na  kidude kimoja ndio astahilicho ,....



.... hapo mifano kibao iliingiziwa mpaka ya akina KING Solomon wapenzi wa MUNGU kuachiwa waoe mpaka wake Mia nane, King David mpaka kuua askari wake ili achukue mke  wa HUYO askari wake, mpaka tetesi kuwa kuna makabila ukichoma mkuki nje ya nyumba ya mtu  mke wake mali yako kwa hiyo siku ki kwenda mbele, BILA kusahau waaminio kuwa mazingira yakiruhusu kila mtu mpaka Papa Benedict anaweza kujikuta kafanya mashambulizi ya URODA kwa kuwa si kila siku binadamu ni SHUJAA wa kubania nanihiii....



....bila kusahau walioingizia maswala ya NI DHAMBI  kupewa tamutamu na zaidi ya mtu mmoja,...
.....na hata  UKIWA NA MTU MMOJA  ni mpaka MCHUNGAJI au SHEKHE aamrishe kuwa sasa kagidaneni.....


 ENIWEI,....

 Leanne Bell alichokoza mjadala HUU  kwa kuanza hivi ndude:

The same person...the same face, the same body, the same lips, the same everything, from this day forward for the rest of your life.

Can you handle it?

According to some people, it's like hell on earth.


Endelea HUKU

....kwa Leanne Bell
....http://www.andtheylivedhappilyeverafter.com



Swali:
  • Wewe unafikiriaje? 
  • Kidude kimoja hata kama ni ANDAZI  chakutosha kiasi  kwamba Mkate , KEKI na vitumbua NO matamanio angalau ki ktutaka KUONJA tu?


Mie naendelea KUWAZA! :-(
Nisikudanganye ! Mie naenda zangu kulala ingawa ni saa sita tu na dakika sita usiku kitu ambacho ni mapema sana kwangu kwa kawaida kwenda KUMBONJI!:-(
JUMAMOSI njema MHESHIMIWA!

Hebu  Angélique Kidjo ambaye nimekuwa namsikiliza tokea niingie homu aje na Carlos Santana waanzishe upya kwa - Adouma



Au hebu Angelique Kidjo aongezee dozi kwa -Babalao



Angelique Kidjo adinye-WEWE



Au amalizie tu kwa -Agolo


Read more...

STORI yangu, STORI YAKE na ukweli wenyewe IKIWA ni vitu VITATU tofauti!

>> Friday, April 01, 2011

STORI za GADDAFI stori za WAPINZANI wa GADDAFI na ukweli wenyewe LABDA ni vitu vitatu TOFAUTI!:-(

Washabiki wa OBAMA wamsifiavyo, WAPINZANI wa OBAMA wamkandiavyo na UKWELI wenyewe wa astahilivyo OBAMA kusifiwa labda ni vitu vitatu TOFAUTI.:-(

Wapinzani TANZANIA waongeayo, Washabiki wa CCM waongeayo na ukweli wenyewe labda ni VITU vitatu tofauti.

Swali:
  • AU?

Binadamu ni MPENDELEAJI,....
..... na kama unaangalia TAARIFA za HABARI au tu unamsikiliza MTU,...
.... kumbuka kuna uwezekano usikilizacho ni UPANDE mmoja tu wa HABARI na ukweli wenyewe LABDA  ni KITU tofauti.:-(




Swali:
  • SI unajua ni vigumu sana kwa WAZIRI MKUU wa UINGEREZA kumsifia GADDAFI hata kwa GADDAFI astahiliyo kusifiwa kwa kuwa habari kwa mtazamo wa KIMAGHARIBI kumsifia adui sio kitu kifagiliwacho?
  • Si unajua muwamba ngoma huvutia kwake?




Tatizo ni kwamba,...
...... kuna wadhaniao kwa kuwa KUNA upande una hoja nyingi za kutetea mitazamo yao ,...
... basi kwa hiyo huo UPANDE ndio uwakilishao UKWELI wa jambo kitu ambacho yawezekana sio KWELI.:-(

NI wazo tu!



Hebu tusikilize kiletacho maana....

Read more...

Kwa kuwa MAISHANI kuna ASIKIAYE atakacho kusikia, AONAYE atakacho KUONA na atafsiriye ATAKAVYO kutafsiri,.....

..... labda  hata WASUKUMA wabisheje kuwa  WALI  sio chakula kama  ilivyo UGALI,...
.... kuna watakao amini UBWABWA sio chakula cha ndege na ni bonge la MGIDO kichakula kama NGUNA tu,...


..... na HAKI YA NANI hata UBISHE ,...
....kuna  atakaye ona NYONYO  wakati wengine wameng'ang'ania kuangalia matako,...
 .... kama ilivyokuwa LABDA kuna atakaye tafsiri salamu zako na uongeayo ni MATUSI wakati  wewe unafikiri unatongoza kwa nidhamu  TU na ustaarabu.:-(

Swali:
  • Kwani si unakumbuka wakati unaangalia  au unasikia kitu na watu wengine-  uwazavyo akilini wakati huo na wawazavyo wengine waangaliao kidude hichohicho  na wewe WAKATI HUO MMOJA-  mnaweza kuwa mnatofautiana MUWAZAVYO ndio maana  MALAYA yuleyule udhaniaye ananuka naye bado ana wateja?

  • Si unakumbuka  stori hiyohiyo moja YA kutia watu MOTISHA na yenye madhumuni ya kupandisha watu MORI  kijazba ile IKUKASIRISHAYO -  inaweza kufanya watu wengine WACHEKE kwa kudhania STORI HIYOHIYO inachekesha na ndio maana PILIPILI ikuwashayo kunawadhaniao ni TAMU?

  • SI  pia UNAKUMBUKA maishani  kuna wastukiao BUSARA katika yale wewe udhaniayo ni UJINGA?


Ndio,...
.... kwa kuwa MAISHANI  kuna ASIKIAYE atakacho KUSIKIA,...
....AONAYE atakacho KUONA,...
... na ATAFSIRIYE atakacho KUTAFSIRI,...
.... lakini bado  MTU akitaka KUELEWESHWA wengine waelewavyo ,...
....na KUELEWA wengine labda inawezekana pia!:-(

Swali:
  • Si inasemekana maishani kuna mpaka wapotezwao na WENGINE?
Ndio,...
... labda tukumbuke tu kuwa,...
.... kabla ya kufikia HITIMISHO kuwa wakati tunaangalia KITU  mitazamo yetu  ndio jinsi KARIBU watu wote ya KITU  kitazamwavyo,...
..... tukumbuke tu kuna wafikiriao chupi wakati wanatazama KITU  na si kila aliyefumbua MACHO na kuyaelekezea kwenye KITU ni kweli anaangalia KITU hasa ukizingatia  labda ni YALE TULIYO YAELEKEZEA FIKIRA ZETU na wala sio MACHO ,...
.....ndio labda TUYAONAYO, tuyasikiayo na TUYATAFSIRIYO.:-(

Ni wazo tu hili MKUU!:-(
Ijumaa naWIKIENDI njema MHESHIMIWA!


Hebu Barrington Levy abadili kwa kuanzisha upya kwa-She's mine




Barrington Levy aendeleze kwa - Shine eye girl





Adinye pia -Black Roses/Here I Come



Sijui kwanini -ila ghafla hebu tu D'Angelo abadili tena kwa kurudia -Brown Sugar


Read more...

Watoto wa Abrahamu (Waislamu ,WAYAHUDI na Wakristo) katika -Reuniting the Children of Abraham

Inasemekana KUTOFAHAMU KITU aka kutokuwa na KNOWLEDGE ya kitu ,....

....ndio moja ya NDUDE ifanyayo Waislamu na Wayahudi/Wakristo na Waislamu /Wayahudi na Wakristo wanabwengana aka wanapeana mkong'oto na fulu kuchukiana aisee!:-(




Wakati kuna fununu UDINI hasa wa WAKRISTO na WAISLAMU unachokochoko zake ambazo zina chokochoko zake TANZANIA,....
.... deku hii DOCU. kama unamuda,.........
... ifuatiliayo Wajaribuo kitu kujaribu kulainisha kitu kwa KUUNGANISHA vijana kwa KUWAFAHAMISHA kitu ,.....

....katika -The Children of Abraham Project














Kitu DINI na IMANI na mavituz yake yana noma zake na si rahisi sana kwa watu kuelewana hasa ukizingatia wanaongozwa zaidi na IMANI ambayo inamchezo wa kutoruhusu KNOWLEDGE kufurukuta.


Lakini,...
.... nikiona ndude kama DOCUMENTARY hii NAFARIJIKA kuwa angalau kuna WATU ambao BADO hawajakata tamaa na wanajaribu KUELEWANA ingawa DINI zao zinasuguana katika kugombania roho za MTUZ!

Read more...

Watoto wa Abrahamu/ Children of Abraham

Wakati tunajikumbusha bado kuwa ukiachilia DINI na IMANI,...
..... Wakristo , Waislamu na Wayahudi wote wanaunganishwa kitu na ABRAHAMU .:-(



Katika ndude hii:
A three part story about Israel and Palestine ..brothers seperated by war and the wall..

Original story and Paintings by POTENZA na Bret Martin ,...
....about two brothers' one raised as Palestinian one as an Israeli..











Stori zaidi kiaina:

Children stories of the prophets of god according to the quran and the authentic hadith:




Abraham and Sarah

A puppet sketch we did at a dedication service at out church - the story of Abraham and Sarah




Haya tena na mabishano yaanze upya:

Sacrificed son: Isaac or Ishmael?



MIE nimeacha!

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP