Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Vituko vya Slaa kwenye mazishi ya Mtema….”Mchumba” wake amzuia asisalimiane na JK, kisa? Italeta maneno…!

>> Friday, January 20, 2012

Mazishi ya Mbunge wa Chadema, Mheshimiwa Regia Mtema yamethibitisha kuwa vituko na vioja vya Katibu Mkuu wa Chadema, Mheshimiwa Wilbroad Slaa na “mchumba wake,” Josephine Mushumbusi havijaisha hata kama sasa wanaishi pamoja.

Kwa namna ambayo sasa imethibisha nani hasa mwenye madaraka, mamlaka na kauli ndani ya nyumba yao, Josephine Mushumbusi amemzuia “mchumba/mume” kwenda kumpa mkono Kiongozi wa nchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Mara baada ya Rais Kikwete kuingia katika makaburi ya familia ya Mtema mjini Ifakara kiasi cha saa tisa unusu mchana, Mheshimiwa Slaa ambaye alikuwa amekaa peke yake na Josephine pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema, alionyesha ishara ya kwenda kumsalimia Mheshimiwa Rais Kikwete ambaye alikuwa jukwaa kuu.
Lakini Josephine Mushumbusi alimzuia mchumba wake asiende kumsalimia Rais Kikwete akimwambia, “usiende…italeta maneno ya bure.”
Kwa namna inayothibitisha nani bosi ndani ya nyumba, Mheshimiwa Slaa alijikunja na kusalimu amri akisema, “haya bwana”.

Kila dalili za tukio hilo zimethibisha kuwa ubabe na ushujaa ambao Mheshimiwa Slaa huonyesha hadharani kwa kutukana, kukejeli na kuwashambulia wenzake katika siasa akiwamo Rais Kikwete ni nguvu za soda tu zisizotamba mbele ya Josephine ambaye alionyesha udhitibi na umwamba wake hadharani leo.

Lakini tukio la leo pia limethibitisha kwa mara nyingine kiwango cha kinyogo ambacho familia ya Slaa na mchumba wake wanayo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kikwete tokea Rais alipowabwaga na kumsambaratisha kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, 2010.

Tokea wakati huo, Mheshimiwa Slaa hajapata kumsema vizuri Rais Kikwete, hajapata hata kumtambua hadharani pamoja na kujua kuwa alishindwa kihalali, hajapata kumsalimia wala kumpa Kiongozi huyo wa nchi mkono hadharani hata fursa inapojitokeza kama leo.
Kwa ufupi, tukio la leo na mengine mengi yalimtangulia limethibitisha kuwa Mheshimiwa Slaa ni kiongozi mwenye kinyongo na asiyekuwa na heshima kabisa.

Kama ambavyo wamepata kusema wengine hana sifa za kuwa na kiongozi mkuu wa nchi yetu hii inayoongozwa kwa misingi ya maelewano na siyo kwa misingi ya chuki ambazo anazionyesha Mheshimiwa Slaa. Kwa hili Dr. Slaa Kachemsha, kadhihirisha wazi kuwa hana siyo tu ukomavu wa uongozi bali pia ukomavu wa kisiasa. Sasa naelewa pia kwa nini Slaa upadre ulimshinda.

Ni jambo la ajabu kuwa mfiwa kama alivyokuwa Slaa leo kwa sababu yeye amempoteza Mbunge anakataa vipi kwenda kumsalimia mwombolezaji ambaye amekwenda kumpa pole na kumjulia hali. Huu ni ubinadamu na uungwana kweli?

Mzee Slaa anashindwa na wadogo zake kama vile Mheshimiwa Freeman Mbowe na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ambao walipeana mikono na kukaa pamoja na Mheshimiwa Rais, kubadilishana mawazo na kuomboleza kwa pamoja.


---------------------------------------__________________________________-------------------
Nyongeza kinanihino:

HII ni habari Kikrosi kiaina  na si mie Muandishi.


Inakuja kutoka kwa MZALENDO  ajiitaye:
MTANZANIA MKWELI mwenye email:mtanzaniamkweli@gmail.com
Mie nimepiga krosi tu:-( 

Read more...

AJIRA MPYA ZA WALIMU ZATANGAZWA MAJINA YATOLEWA

>> Thursday, January 19, 2012



Kwanza Tunapenda wasalimu wakubwa wetu Shikamoo na vijana wenzetu Mambo vipi..  Tunatambua kuwa Wanavyuo wenzetu walimu walikuwa hawana kazi kwa muda mrefu Jambo ambalo liliwafanya wengi kuwa na wasi wasi na mwajiri wao. Tunapenda kuwapa tarifa kupitia mtandao wenu wa Matukio na wanavyuo (www.tzwanavyuo.blogspot.com)  kuwa, Walimu wahitimu wote  Jana usiku majira ya sa saba Nafasi hizo zilitangazwa Rasmi, Pia sisi Tunapenda kuwasilisha majina ya wanafunzi ambao wamechaguliwa Tunaomba mchukue Muda wenu kutazama kwa umakini majina yenu yote yapo hapa. Hongereni sana.


Imeandaliwa na,
Matukio na Wanavyuo Crew 

Read more...

HELMETI ya MOYO uliopenda HATA ingekuwa ni ya CHUMA,....

....LABDA bado  moyo wa APENDAYE ungeuma ,...
..... hasa kwa kuwa MOYO wa APENDAO chuma sio ngao ya kuzuia mishale ichomayo MOYO!



HELMETI ilindayo  MOYO uliopenda HATA ingekuwa ni ya DHAHABU kama sio ALMASI,...
.....bado  YA moyo THAMANI yake kipimo kizuri hakipatikani kitu kifanyacho ya MOYO kuwa na thamani kubwa kuliko chochote cha BINADAMU hapa DUNIANI halafu kwa maajabu ya MUSA  YA MOYONI MWA MTU ndio yenye  ULINZI MDOGO zaidi kuliko yote kwa kuwa ASKARI alindaye moyo ULIOPENDA ,...
... kupenda humfanya KIPOFU!.:-(

Swali nanihino kiaina:
  • Unafikiri ULINZI wa moyo wako ili  USIUMIZWE NA PENZI unauimara gani wakati labda hata kupenda kwako KWENYEWE  sio CHAGUO lako KIMAAMUZI kitu ambacho naweza kuamini UKISEMA chanzo chake PENZI LAKO chaweza kuwa ni kitu kidogo tu KILICHOWASHA BARUTI kama vile kile cha  KUCHEKEWA TU kidogo na KIJEBA MUUZA MITUMBA au tu hata kutingishiwa tako na KIGOLI- na wala sio TABIA ya MPENZI wala NINI?

Ndio,...
.....HELMET ni KOFIA,...
... na labda hata HELMET ya mwendesha PIKIPIKI hailindi kichwa kizima!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!





Hebu MAD ICE aanzishe upya kwa- Te Amo



Jamhuri Jazz Band waingilie tena kati kwa-Shingo la Upanga



Halafu Ndedi Dibango azime tena kwa -Eyo Mè





Tuko Pamoja WADAU!

... nipo na baadhi ya picha kutoka kaskazini ya dunia  ambako nako nilipita mitaa ya hivi karibu ni hizi:
























Read more...

Prawns in Coconut Sauce - Kamba wa Nazi & Cookbook from A Taste of Tanzania -Coming Soon!


Dear Friends,

Prawns in coconut sauce/ Kamba wa nazi is now uploaded on Taste of Tanzania website.

To see, just click the "Visit My Site" button in this email. Or copy and paste on your address bar http://tasteoftanzania.com/blog/2012/01/15/prawn-in-coconut-sauce-kamba-wa-nazi



Halafu :

Coming soon! Cookbook from Taste of Tanzania

Dear friends and family,

I'm excited to update you about the cookbook from Taste of Tanzania website.





I am starting self marketing early in advance. I pray this will be a year for Taste of Tanzania and Tanzania in General. I am determined to make sure this book reaches many countries, but first I need my fellow Tanzanians and Africans.

To see, just click the "Visit My Site" button in this email. Or copy and paste on your address bar http://tasteoftanzania.com/blog/2012/01/06/coming-soon-cookbook-from-taste-of-tanzania/

Mingi Love,

Miriam Rose
With TasteofTanzania.com

Read more...

Kama WANAUME ndio wangekuwa wanapata MIMBA,...

...LABDA  hiyo kitu ingegeuka kuwa KAWAIDA!:-(



Samahani nariwaindi na kuanza upya hii TARALILA.


Imetokea mara kadhaa katika michakariko hoja ikajitokeza kuwa kutokana na mfumo dume DUNIANI  wanaume  hujisahau kustukia kazi na majukumu makubwa yabebwayo na WAMAMA ikiwa ni pamoja na MIMBA kwa miezi kadhaa wa kadhaa.


Pamoja na upana wa MADA kama hii ningependa kuchokonoa kipele kidogo tu ambacho labda huchangia ni kwanini hata MWENYE NYUMBA huweza kusahau hata ya HAUSIGELI mwenye umri wa kwenda shule asipoenda shule kwa kuwa anamfanyiakazi mwenyenyumba ,...
.. na hicho ni kipele kiitwacho ``KAWAIDA´´

Na tatizo la KAWAIDA,...
.... ni kugeuza CHOCHOTE KILE kuwa ``KAWAIDA´´,....
.... kitu kifanyacho hata kunyanyasa MKE au hata kutothamini ya MKE huweza kugeuka ``KAWAIDA´´.

Swali:
  • Si unajua kuwa ukizoea kuishi pembeni ya JALALA linukalo hicho kitu hugeuka KAWAIDA kitu kifanyacho hata harufu mbaya USISIKIE kwa kuwa ishakuwa ``KAWAIDA´´?


Ndio,....
.....hata kwa baadhi ya BUIBUI  ,...
...kidume kuliwa na BUIBUI JIKE kama bonge la msosi baada  ya tendo la NDOA nalo KIBUIBUI hao  ni KAWAIDA.:-(


Tatizo/ANGALIZO ni:
  • Hufikiri moja ya TATIZO kubwa lifanyalo HATUTATUI MATATIZO YETU yawe ya NCHI zetu au hata yetu BINAFSI ni kwa kuwa yameshageuka KAWAIDA?

Ndio,...
... ``KAWAIDA´´ ikizidi,...
.... yaweza geuza usistukie kuwa USICHOSTUKIA ni kwa kuwa tu kimeshageuka ``KAWAIDA´´!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu tubadili kwa kumuangalia MIKE KALOMBO akitengeneza muziki katika- Party Everyday




Au tu hebu tubadili na kurudi miaka ya nyuma zaidi katika maswala ya Les Mangelepa katika kibao - Mimba



Halafu Don Campbell abadili mchezo na kuzima kwa - Storm Is Over Now


Read more...

ZAWADI ni TAFSIRI- na tafsiri nzuri inamchezo wa kugeuza mavi kuitwa MBOLEA!

>> Wednesday, January 18, 2012

Na kwa TAFSIRI,...
... waweza kuchukia MTU,...
.... kwa kuwa tu UMETAFSIRI kifanyacho asipendeke MTU.

Na kwa tafsiri,....
...... MTU aweza kuua MTU,....
.......kwa kuwa KITAFSIRI kifanywacho ni kupiga MWIZI au tu kuua MWIZI ,...
... kitu ambacho kwa tafsiri za wengi wapiga MWIZI swala hilo  sio LA  kuua MTU.

Na kwa TAFSIRI,....
...... Watanzania waweza MPAKA kukuapia NYERERE hakuwa DIKTETA kwa kuwa WAMETAFSIRI,...
.... na kitafsiri jamaa alikuwa MTAKATIFU ki wake UTU.

Swali:
  • Na siunakumbuka ZAWADI ni uitafsirivyo kitu kifanyacho kuna asiye na CHUPI ambaye akipewachupi atatafsiri kadharauliwa  kwa kuhisiwa hana chupi hata kama aliyenunua chupi kama Zawadi hakujua Mdada kutokana na uhaba wa chupi kavaa kaptula ya KAKA?
  • Na si unakumbuka UKITAFSIRI waweza kustukia MAFISADI nni jina tu lenye maana ileile ya MWIZI kitu kifanyacho kuwa labda NCHI na DUNIA inaongozwa na WEZI hata kama kimajina wapeanayo hutambulika kama WAHESHIMIWA?



TAFSIRIIIIIIII!

Na kwa kutafsiri ndio maana LABDA hakuna DINI moja DUNIANI,...
....kama tu ilivyokuwa hakuna ZAWADI ya aina MOJA kitu kifanyacho MAUA ni ZAWADI kwa MWINGINE jinsi ileile ilivyo ZAWADI kwa KIJEBA mwingine achukuliavyo ZAWADI ni ile kitu KIFUKO cha DHAMBARAU  TU ambacho kwa kutojiamini kimegeuka ZAWADI kisa mtoaji ni MDADA ambaye haamini ni LEVO zake aka Katika KIJIJI cha UJAMAA huyo ni Katibu KATA na kwa mkulima wa kawaida kugawiwa vyake ni ZAWADI tu kwa kuwa mgawiwa HASTAHILI kikawaida !:-(



Ndio,....
..... tafsiri ndio MSINGI na NGUZO mpaka  ya yote yadhaniwayo kuwa ni MATUSI,...
...... na ukitafsiri vizuri ,...
...LABDA chochote ni ZAWADI hata kama kinamdudu,...
...kama tu ilivyokuwa labda kuna maneno tu ambayo UKITAFSIRI yanaweza kuitwa SALA!:-(


Ni wazo tu hili MKUU!

Hebu ghafla Eduardo Paim aturudishe tena Angola kwa - Xinguila



Halafu tupitie Japan kidogo ili Marehemu NUJABE apoze kwa kurudia ndude  -Counting Stars




Halafu Jaziel Brothers wazime kwa sindimba ile - Woza


Read more...

Ya KESHO kama si MASWALA ya KESHO!

>> Tuesday, January 17, 2012

Ya kesho ,...
.....LABDA karibu kwa asilimia mia huanza kabla ya KESHO,...
.... hata kwa wafikiriao YA KESHO yako KESHO ,....
.... kama ya LEO yakumbwavyo na WATU leo.

Swali:
  • Unafikiri yako yatakayokukumba KESHO mwanzo wake hauko kabla ya KESHO?

Ndio,...
.... hata MIMBA za kesho hata za KIMAWAZO ,...
......labda  mbegu  za KIBABA WATOTO na mayai yake MAMAWATOTO wa SWALA yalishaumbwa kabla ya KESHO katika utekelezaji utakao ipasifa KESHO kwa watakao kuamini LILILOTEKELEZWA kesho lilianzia KESHO!

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na wala USIKONDE!


Hebu tena tuanzie Sierra Leone ili King Masco 
aanzishe kubadili kidogo kwa zilipendwa -Mao Mao




Tuhamie Nigeria ili King Sunny Ade aendeleze kwa zilipendwa - Ja Funmi




Halafu hapahapa Nigeria yule Fatai Rolling Dollar arudie na kuzima kwa zilipendwa-Easy Motion Tourist


Read more...

Nimerudi KIBANANGENGE kijiweni WAKUU!

>> Sunday, January 15, 2012

Na nimatumaini yangu wote WADAU wa kijiwe HII mnapata bado CHOO swafi MWKA HUU!


Madhumuni ya BARUA hii KWENU ni kuwatakia HERI YA MWAKA MPYA wote ile KIBONGE yani!

PAMOJA SANA Mwaka HUU!
-Simon




Hebu Manu Dibango & Ladysmith Black Mambazo watekenye- Wimoweh



Halafu MDADA wa KIETHIOPIA yule MEKLIT HADERO adinye pia kilainisho -Leaving Soon


Au tu  halafu Sister PHUMI asigine na kujaribu kuweka nukta kwa sindimba-AFRICA








Halafu tu The Temptations ndio waweke nukta kwa FANKY ile ya kwenye   kidude-Shakey Ground


Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP