JINSI WABONGO TURUDIVYO NYUMBANI BAADA YA KUBEBA MABOKSI UGHAIBUNI!
>> Thursday, October 04, 2007
Staili za kurudi bongo, kama uko nchi nyingine ni nyingi.
Na sababu za wabongo kuwepo nje ya Bongo ni nyingi.
Swali:
Hivi ushawahi kuona tangazo la kazi , wakitafuta mbeba maboksi?
DUH!
Sasaa...
Baadhi ya dondoo ya jinsi Wabongo warudivyo bongo:
Mara nyingi ni kimawazo,
...unarudi kimawazo , unajitengenezea ugali na mbilimbi, makande, kisamvu au chakula chochote kikukumbushacho bongo, huku kwa mbali unasikiliza kimasomaso au miziki fulani ikukumbushayo ulivyokuwa pale bongo kwenye kioski fulani.
Duh!
Naacha!:-)
Lakini kabla sijaacha....
- Unaweza ukajiandaa na kurudi na vyeti vyako au kale kamtaji. (si unajua siku hizi si ujanja kurudi na friji?)
- Unaweza usijiandae na ukarudi au kurudishwa tu Bongo(si unajua yote mbele kwa mbele?)
UKWELI ni KWAMBA, wote tunajua BONGO inahitaji MINYOO , samahani, MICHANGO ya Wabongo wote(walio ndani ya nchi na pembeni)
Inahitaji michango ya hata wasio Wabongo pia.
Kitu hiki, wengi tunakikumbuka ingawa tunakumbushwa kila siku na wadau na hata halihalisi ya kuwa pembeni ya mipaka ya Bongo.
Ukiwa nje ya Bongo, kitendo hicho tu cha kutokuwepo Bongo, hukukumbusha bongo. Na kama wewe ni mkereketwa, kila siku utatafuta jinsi ya kubadili jambo bongo.
SWALI:
- USHAWAHI kukutana na Mbongo HATA mmoja, AMBAYE chini na hata JUU ya moyo wake, HAJALI BONGO?
- NI nini maana ya kujali BONGO?
Nakuacha na TALINA akija na Pour te Revoir
Kumbe haimbi Kibongo ,DUH! Read more...