Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Atekenyaye wazo leo ni - FELA KUTI!

>> Sunday, March 20, 2011

Hebu tukae kitako na kumsikiliza,...

....FELA ....





Hebu chapchap Fela adinye-ZOMBIE



Baada ya somo hebu Billy Paul abadilishe nadharia na kuzungumzia mapenzi yake na mke wa mtu katika ndude-Me and MRS Jones



Ni mtekenyo wa wazo tu huu MKUU uheshimiwaye!:-(

Read more...

Kuna MAMBO labda YAFANYE matusi au YASEME tu SASA hivi wakati UMRI unaruhusu!:-(

>> Saturday, March 19, 2011


Ndio,...
... kwa kuwa UKINGOJEA ili  uyafanye BAADAYE  ,...
... au UYASEME baadaye,....
... hasa katika JAMII HII  ambayo kwa kawaida  ina MAMBO  ambayo imeshajiwekea kuwa  hata kitendo cha kumvumilia  MTOTO ALAMBAYE kamasi hutegemea MTOTO alambaye malighafi HIZO za pua ana UMRI GANI,...
....inaweza kukuona hufai KUHESHIMIKA  ukingojangoja kufanya mengine baadaye ambayo labda inatakiwa UYAFANYE SASA HIVI.:-(

Swali:

  • SI unajua kuna uwezekano hata UVAAVYO  baadaye ukikuwa kidogo  KIMINI chako SKETI au KIBWAYA - kitakuwa hakifai kuonwa katika JAMII ya siku hizi ambayo paja kidogo tu kuonekana ASHKI KIBAO hupanda WATU WAZIMA na VIJANA -hata kama bado unamapaja mazuri kwa kuwa ushakuwa LIMAMA na jamii inaamini LIMAMA ni nishai kuvaa kama kigoli wa miaka kumi na tano?


  • Au?
  • SI inasemekana MICHAEL JACKSON kwa kuanza ukubwani kuchezea midoli amabyo labda angetakiwa kuichezea UTOTONI wakati anafanya ya KIKUBWA  ile  JAMII  HIIHII ilishindwa kumuelewa?

Ndio,...
....labda KUNA MAMBO  ni ruksa  kwa mtoto au KIGOLI  ambaye jamii inaamini bado hajajua kustukia maswala ya kiutu UZIMA,...

..... na kuna ambayo usipofanya SASA hivi  au kusema sasa hivi  KIDUME aka NJEMBA,...

.... labda ndio imetoka hiyo  kuyafanya KIUHURU kwa kuwa UMRI UKIENDA unawezashindwa kuyakatikia kiuno vizuri  pia bila kustukia MADHARA ya kuwa UMRI umekwenda na mifupa haina OIL KIUJANA  na utundu MAFANIKIO YAKE  unabakia ni kwa kushughulikia tu vitu kwa taaluma na uzoefu tu ujao na UUTU UZIMA na sio madoido ya UJANA na nguvu za UJANA.:-(

Ndio,..
...hili ni WAZO TU Nguli!:-(



Hebu Hypnotic Brass Ensemble katika kubadili wazo waingizie-WAR



Bassekou Kouyate na Ngoni Ba wabadili mchezo kidogo ingawa aimbaye ni Amy Sacko mke wa Bassekou ambaye kwa KIAFRIKA zaidi alawalawishe kwa-Jonkoloni



Bassekou Kouyate aendeleze zaidi mdindo kwa - Ngoni Fola


Bassekou Kouyate na Ngoni Ba waguseguse chini kidogo zaidi karibu na nanihii kwa- Segu Blue


Au tu Hypnotic Brass Ensemble wazime ndude kwa-Brass in AFRICA

Read more...

Kwani unafikiri WANAOKUHUBIRIA DINI wanakupenda sana ndio maana wanajali kwanini wewe hufuati DINI yao?

 .... ni swali  ambalo anayemaindi nani ni MUISLAMU au nani MKRISTO anaweza kujiuliza wakati anahangaikia  kukosoa kwa kuwa kuna wamuaminio BUDDHA  TANZANIA na basi hao kuna kitu wanakosea.


Wakati tunatafakari  pia kuwa  BADO wapo wengi wenye dini zao wasizouzia wengine kama tu   WAKRISTO na WAISLAMU  kama wachawi watunzavyo uchawi usijulikane na kila mtu au WAYAHUDI na dini yao ya KIYAHUDI wasivyoiuza kirahisi kwa wengine  ,...

..ndio wakati tunafikiria hata WAYAHUDI ni miongoni mwa wenye dini zao ambao hawana mcheche wakutaka watu wengine BWELELE wajiunge na dini yao ya KIYAHUDI ili waokoke;....

Swali zaidi:
  • Unafikiria wajalio wengine wanafuata dini gani huwa ni kweli wanafanya hivyo ili kutaka kuwaokoa au kujiokoa wenyewe hasa huku wakijaribbu kujiaminisha kuwa WAAMINIYO ndio sahihi?
  • Kwani hujawahi kustukia wahubirio kuokoa wengine ambao ukikutana na wafanyiayo wengine mtaani  yaonyeshacho ni CHUKI tu juu ya BINADAMU wengine hao hao ambao KIDINI hujifanya wanawapenda na kutaka kuwaokoa?

Ndio ,...
... kuna uwezekano ajaribuye kukuokoa kiimani,..
... hana mpango nawe kihivyo kama tukichunguza anavyo KUJALI kikweli kimengine katika MAISHA mtaani!:-(



Ni wazo tu ANDUNJE hili MKUU na wala usikonde!:-(




Hebu Apache Indian alainishe tena kwa -Boom Shak a lak



Apache Indian aingilie ishu kwa - The Israelites



Au tu Apache Indian arudishe tu anachojua zaidi tena katika -Arranged Marriage



Apache indian alainishe zaidi kwa-Dil luteya



Au tu aje na Maxi Priest warudie-Fe real

Read more...

Matatizo ya KUSHIBA yakifanya mtu ARIDHIKE na kujisikia mvivu kutafuta tena MLO kama kupata kwake MUME kulivyomuondoa MREMBO juhudi za kuendelea kupata HAMU kwa ajili ya MUMEWE!:-(

 Inasemekana aliyeshiba ,...
 ......ni rahisi KURIDHIKA hata bila kula  ,...

... kama tu ilivyo kwa ajuaye anacho kama tu MUME au MKE awezavyo kuingia uvivu kukihudumia kwa kuwa ANAAMINI TU  anacho na kiko  BWELELE na akitaka tu,....
...ni maji mara moja kama MAHARAGE ya MBEYA !:-(

Swali:

  • Si inasemekana  juhudi nyingi za hata WASOMI   huishia wakisha pata vyeti kwa kuwa ushahidi upo kwa JAMII walifaulu na kuwa waliwahi kwenda shule na kiendeleacho baada ya hapo ni  ujinga tu ulindwao na  kuwa wana VYETI vikumbushao JAMII  kuwa hapo mwanzo walikuwa na juhudi ya kujua kitu kifanyacho watu wadanganyike kuwa LABDA WASOMI HAO WALIOSOMA ZAMANI bado wanajua?
  • SI unajua unaweza ukaridhika UNAJUA kitabu kwa kuwa uliwahi kukisoma miaka fulani iliyopita ingawa ukweli ni kwamba UKIPIGWA maswali  ukumbukacho kuhusu hicho kitabu  ni hiyo tu KUMBUKUMBU kuwa uliwahi KUKISOMA?

Ndio,...
... kuna wengi ubunifu wa hata kutibu nyege huisha tu pale wajuapo tu matibabu ya nyege wanayo,...
... ingawa wanasahau kuwa  kwa  kuua juhudi BADO HAKUBADILI KUWA wenza wao bado wanahitaji TIBA kama ileile yenye juhudi za  MWANZO,...
...kitu kiwezacho kusababisha KWA APUNGUZAYE JUHUDI  kutostukia MWENZIE inabidi ahudumiwe na wengine MTAANI!:-(


Ndio,..
... inasemekana kuridhika ni chanzo cha uzembe,...
.....na UZEMBE  pamoja na kwamba nao una FARAJA ZAKE,...
... lakini kabla HUJARIDHIKA na kuwa MZEMBE labda pima kama unafarijika zaidi na FARAJA ZA UZEMBE wakuridhika au LA!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na ni ruksa kulitemea koozi!:-(


General levy aanzishe mshawasha tofauti upya  kwa -Incredible




Achezecheze nayo  kwa -Shake





General Levy adodose zaidi mbirimbi kwa-Champagne Body



Generali LIVI aendelee kumwaga njugu kwenye bata wengi kwa -Heat



General arudishe dalili za kueleweka kwa -The Wig




Au tu General Levy alainishe zaidi tu NDUDE kivyake kwa nyundo-Right Thing



Sijui kwanini ngojea Apache Indian aanzishe upya kwa-Original Nuttah

Read more...

Tuangalie safari MOJA ya MHESHIMIWA MSAFI ya kuelekea kwenye CHOO kichafu!

>> Friday, March 18, 2011

Tahadhari MHESHIMIWA : Wazo  Limepinda!:-(



STORI  ya kiaina TAIMU:

 ------------------------------___________-----------------------------__________-------------


 Kikao kilianza salama tu ofisini kwa bosi,...
.... ingawa kila mmoja alihisi bosi hayuko kama kawaida yake hasa kwa kuwa safari hii bosi alikuwa anaonyesha dhahiri kutojiamini  kitu ambacho wafanyakazi wote hawajawahi kukiona,...
... kutoka na ukweli kuwa bosi huyu ni aina ya wale MABOSI ambao hata kama hawajui KITU hujifanya wanajua na wanaamini kwa kujifanya wanajiamini mbele ya wafanyakazi ndio moja ya kitu kifanyacho walete picha ya wao kuwa  ni viongozi bora mbele ya wawaongozao.

HALIMA alimfinya  pajani  AGNESS ambaye ni mfanyakazi mwenzie waliokaa naye karibu kwenye meza ya mkutano  huku wote wawili wakijizuia kucheka na kuendelea kujikausha kama vile hawajastukia tofauti ya hali ya hewa ofisini hapo,...
.... kwa kuwa ukweli ofisi  nzima ghafla ilianza kunuka kama KINYESI aka MAVI   ingawa kama kawaida ya watu wazima hasa wajiheshimuo na wasiotaka kudhalilisha mtu wote ofisini  ilibidi wajifanye hawajui kinachoendelea na kujitahidi sana kutofikiria ni nani katika mkutano ule hapo ofisini ndiye mhusika aliyechafua hali  ya hewa kwa silaha ya nyuklia aina ya ``USHUZI tepwetepwe ule usiotoa sauti´´.:-(

Na baada ya uvumilivu wa mabomu kadhaa  yenye harufu zisizo kifani , kila mtu aliyehudhuria alifarijika kwa kuwa mkutano uliahirishwa. Na wakati  wafanyakazi wamepozi koridoni kidogo kujadiliana maswala yaliyoongelewa ofisini kwa bosi wakati wanaelekea makazini kwao ,...
... ghafla ndio wakashuhudia bosi akitoka kule ofisini  na kuwapita kwa mwendo wa ajabu kidogo kihatua za kunyata hata USITAJI wa kutingisha tako ,... 
...hasa kwa kuwa walijua mwendo wake wa kawaida ni upi  kwa kuwa  waliozoea kumkodolea macho akitembea hata tu wakati walichokuwa wakifanya ilikuwa ni  kutathmini tu ughali wa nguo zake mwanana.

Ila SAFARI hii bosi alichofanya ndicho kiliongezea watu kumuangalia kwa kuwa ALIWACHEKEA PIA wakati anawapita,....
... hasa ukizingatia huyu MHESHIMIWA  ni aina ya mabosi ambao wako siriasi sana  na huwa hawachekicheki hovyo hasa mbele za wafanyakazi,...
... ingawa baadhi ya wafanyakazi waliowahi kugongana naye BAA  akiwa na marafiki zakewakipata MA-COCKTAILS aka KILAJI SHORORO  wanadai alionekana yeye ndiye mchekeshaji wa mashoga zake na wakati wote ni fulu kukenua menu hasa kwa staili ile maarufu ya KUTABASAMU.


``Leo mbona BOSI  anatembea kiajabu?´´ -ni moja ya sauti moja ya mfanyakazi mmoja wapo ilisikika ikidadisi.

``Vipi tena mbona bosi anaelekea kwenye choo cha wafanyakazi  wa kawaida na hivi kuna maji kule kweli?´´- sauti nyingine ilisikika ikinong'ona.

Halafu karibu wafanyakazi wote hata bila kutamka neno walionekana kuunganisha safari hiyo ya bosi, MWENDO WAKE WA KUSUASUA  na makombora ya kemikali ya aina ya USHUZI  walioyahimili kwa muda mrefu MKUTANONI kwa kujibaraguza hawayastukii kule ofisini kwa bosi,..
...ingawa ilionyesha dhahiri karibu kila mmoja wao hakuwa kastukia kuwa yale makombora aliyekuwa anayatungua kimya kimya kwa staili ya KUYAPOROMOSHA  KIMYAKIMYA alikuwa ni bosi yule ambaye ni mwanamama mwanana ambaye  kwa wengi pale kazini hata kwa mvuto wake tu ilikuwa tosha kufuta hisia za kumuhusisha yeye KIBOSI mzuri kama MALAIKA na matumizi ya choo kwa staili ya KUSHUSHA kilo za timba aka kunya  au tu hata  katika lile swala laini lijulikanalo kwa lugha ya kitaalamu kama KUKOJOA.

------------------------------_________________________------------------------------

Safari ya MHESHIMIWA  ya kwenda chooni ilianzia ofisini.

Siku hiyo ilikuwa ni ya pili katika ukarabati wa choo chake cha ofisi ambacho alitaka kiwe cha kukaa na sio  cha kihindi kwa kuwa alidai  maswala ya kuchuchumaa hapendelei na yanamchezo wa kufanya baadhi ya sketi zake  kukunjika kunjika asivyotaka hasa ukizingatia yeye anamaindi sana muonekano wa nguo zake ambazo huziagizia Ufaransa tu  ambako ndiko alisomea na kuishi miaka mingi kabla ya kuamua kurudi Tanzania.


Na siku hizi mbili za ukarabati wa choo chake binafsi alipanga asiwe kazini ingawa kutokana na dharura akajikuta analazimika kuwepo na pia kuitisha mkutano wa dharura ofisini mwake ili kuhakikisha mambo yanaenda mswano katika KAMPUNI.

Wakati bado anajiuliza maswali yaliyoegemea kwenye kujilaumu ni kwanini itokee siku ambayo ofisi yake yenye  kila kitu mpaka bafu  ndani iwe na choo kisichotumika siku ile -ndio itokee ana matatizo ya tumbo lenye gesi na sasa anahisi linapiga hatua ya pili na kuashiria  uwezekano wa  mharo  pia,...

.... alijitahidi  kutembea kwa madoido  AWEZAVYO  katika kujaribu  kutoweka wazi  kuwa kabanwa bonge la haja.Na katika hatua hizo za kujibaraguza alijikuta anachekeachekea wafanyakazi njiani kitu ambacho kilizidi kumstua alipostukia kuchekea kwake watu kunafanya watu wanapigwa na butwaa.


Na baada ya kufika CHOONI pamoja kuwa kabanwa sana na labda hata chupi yake ya mauamaua imeshapigwa kamstari kidogo KANJANONJANO  KIUJIUJI  ambako hakakuwepo hapo mwanzonin wakati  anavalishwa mwili wake MWANANA  kificha nyeti hicho cha bei ya GHALI -alihakikisha ana fungua maji   mpaka mwisho yajae kwenye ndoo itumikayo kukusanyia maji ya kuchambia na ya kuflashi  bidhaa zikisha fanikiwa. Ingawa nia ilikuwa ni maji YAPIGE KELELE TU  ili kuua sauti mbalimbali ambazo anajua tayari ndizo atakazo tengeneza wakati anajisaidia haja zote MBILI kuu kwa msukumo na juhudi zote ,...
... ili kama kuna mtu atakaye kuwa nje ya mlango wa choo asiwe na uhakika MHESHIMIWA anaenda choo namba ngapi na kwa staili ipi kwa kuwa alikuwa anaombea makelele ya maji  yameze sauti mbalimbali za kitarumbeta mbovu zitakazo tokana na Mheshimiwa kupumua kwa juhudi au tu katika ushushaji tu wa kilo kadhaa TEPWETEPWE  huku akijizuia kustukia ni jinsi gani kalazimika kwenda kwenye choo kichafu ,...
... ingawa pia akijisikia UAHUENI a.ka FARAJA kuwa angalau choo cha kujisitiri kakipata kabla ya mambo kuharibika kabisa ,...

....ingawa bado kitu kimtishacho ni fikira zilizomjia ghafla KWA MUDA MFUPI na kumfanya ajiulize kimoyomoyo kama bado anaweza  kuchambia maji  kwa kuwa yeye ni mtu wa TISHU na kuchambia maji anakuhusianisha na kuchezea mavi kwa kuyashikashika   ,.....

....ingawa WAZO hilo lilimpotea tena haraka sana  KWA FARAJA ALIYOIPATA baada ya raundi moja na nusu aliyoitekeleza kwa uhuru kabisa  yenye mchanganyiko wa vijambo na shehena tepwetepwe ya aina ya uharisho huku bado kidogo AKIRI kwa SAUTI ``Leo ningejinyea kama choo hiki hakikuwepo hapa karibu kwa jinsi nilivyobanwa.:-(´´




Na hiyo ndio ilikuwa moja ya safari ya mheshimiwa mmoja ya kwenda  kwenye choo kichafu akidharaucho kwa kuwa hakimuhusu na kwa kawaida hata hakifikirii uchafu au UBORA wake  kwa kuwa ni cha mahohehahe wafanyakazi tu ambao kwake hawako  sawa naye !:-(



Ndio stori hii imeruka jinsi MHESHIMIWA baada ya kuingia chooni alivyovua chupi ya MAUAMAUA na kufungulia maji yameze kelele za shughuli kwa spidi na nguvu ambazo hata MENDE waliokuwepo hapo chooni walionekana kupigwa butwaa kwa kuwa katika chabo zao hii ya SHUGHULIKO la MHESHIMIWA  ilivunja rekodi.


Na ni kweli iliruka PIA hata kipengele cha  kuwa  MHESHIMIWA kibosile wakati anatoka  chooni na huku katika kuwaza anafikia uamuzi wa kurudi NYUMBANI  ili kuepuka kujidhalilisha zaidi HAPO kazini  - kwa bahati mbaya alijamba kidogo tena  safari hii kwa SAUTI mbele za wafanyakazi aliowapita akielekea ofisini  ambao nao walimezea tena na kujifanya hawajastukia hata safari hii  bomu lile la kemikali!:-( 

------------------_____________________________------------------------------------------



Katika kurudisha taralila upande wa BUSARA zaidi  na kuliondoa kwenye Ujinga katika UjingaBUSARA
huu:

Ndio,...
..... MTU ukidharaucho kama BOSI alivyokuwa anadharau choo ambacho alifikiri hakihitaji ,...
.... kuna siku hicho ukidharaucho huweza geuka MWOKOZI!:-(


Ndio,...
.....kunauwezekano hata mtu ajifanyeje kazoea kutumia UMA, KISU  na VIJIKO katika kudadavua NGUNA   na kula kwa mkono hawezi,...
... ikibidi chakula kwa mkono kinalika tu  kwa YEYOTE YULE  kama BOSI alivyogundua  kuwa KUCHAMBIA maji kunakuja automatiki tu hata kwa ajifanyaye sio mtaalamu kisa kazoea MAKOKONEO ya aina ya TISHU ,...
...na  hata bosi mwenye anaweza kukiri kama chooni kulikuwa hakuna maji angebunia TU kitu katika kushughulikia kuchamba na katika ubunifu hata chupi yake ya ghali ya mauamaua  ingeweza kufaa tu katika shughuli ingawa ingesaidia pia  kuziba choo kama angeiacha kwenye tundu la choo katika staili ya kujaribu kuziba shehena aliyoitengeneza isionekane na watu kirahisi atakaye kuja baada yake CHOONI  ingawa bado  haitazuia vizuri shughuli za INZI.:-(


Swali:

  • Si unajua karibu kila mtu kuna safari fulani hata kama ni mara moja moja humpeleka ajifanyako hakumuhusu kwa kuwa ukweli bado uko palepale hata mtu ajifikirie ni spesho vipi ila kama ni MTU  basi kama MTU yawakumbayo watu yatamkuta tu siku moja?

  • Na si unajua  hakuna la KIBINADAMU lenye uhakika na hata upange vipi kama tu FUKUSHIMA JAPANI kuna kiwezacho kutokea ukagundua ni zaidi ya mipango ujiandaayo nayo na kwa hilo ukahitaji msaada hata wa udhaniacho sio msaada kwako?



Uliotakiwa kuwa ni utangulizi wa Taralila hii:

IKIBIDI na kama nin lazima ,....
... haki ya nani utalazimika KUFANYA mbele za watu uwafichao kitu !

- ni moja ya hoja ya msafiri kafiri aliyeonekana akitokea vichakani kujisaidia.


Njaa ikiuma vizuri UHARAMU wa nyama ya NGURUWE huisha -ni hoja ya MUUMINI mmoja



Choo kichafu hutembelewa na yeyote ahitajiye USITIRI wa choo,...
... na ni pale tu kama MAHITAJI ya choo sio ya lazima sana ndio SISTA DUU  au BRAZA MENI  Mheshimiwa  anaweza kukwepa choo kisa anahisi choo KICHAFU!


-ni hoja ya  Mheshimiwa kibogoyo Wakufikirika.


Kwa hiyo,...
.....kama unachagua CHOO MKUU,...
.... wewe hujabanwa vizuri bado!:-(

Ni wazo tu hili KAMANDA Mheshimiwa hata kama limepinda!:-(








Na hebu Phil Colins abadili kwa-Drums na Take Me Home



Phil Collins adungunyue-True Colors




Phil Collins apapasepapase maeneo kwa - In the air tonight




Au tu Phil ajaribu kuzima tu manyanga kwa -Do U remember?



Ingawa sijui kwanini Bryan Adams  ngojea aingilie kati tu na kudai- The Only Thing That Looks Good On Me Is You


Read more...

Mtekenyo wa leo - MAREKANI bila MUNGU na Madalyn Murray O'Hair

Wakati kuna waaminio kuna MUNGU,..
...na wakati TANZANIA siku hizi ni fasheni kushabikia udini.
....hebu tudodose swala kinamna ingine kiduchu,...
...kwa kudeku ndude-Godless In America

Stori ipapasayo maisha ya The most hated woman in America -Madalyn Murray O'Hair





Tuanze....



Tuendelee.....


Tuendelee....



Tudodose....



Mmmmh....



Au tumalizie tu kidude....



MADHUMUNI ya NDUDE HII ni kujifunza tu kitu  MKUU kutoka kwa WENGINE kinamna na wala usikonde!:-(


IJUMAA na WIKIENDI  njema MHESHIMIWA!:-(

Read more...

Katika WOGA wa waogopao zaidi huo `` WOGA´´ kuliko kitu kingine- LABDA hata bila kustukia !

>> Thursday, March 17, 2011

Woga kwa KUJITEGEMEA unavigezo vyote vya kutisha,...
...na ,....

....kuna watishikao na WOGA huohuo wenyewe,...
..... na UKICHUNGUZA utastukia wala wakihofiacho katika WOGA huo  sio KITU HATARI zaidi ya  KILE ambacho kimetengeneza  , kinauwezo zaidi wa kutengeneza au kiko nyuma ya woga ambao wanauogopa!:-(



Swali:
  • Unabisha?


Ndio,...
... inasemekana MTU anaweza kuwa ni MUOGA wa kuogopa tu  ,...
.... mpaka WOGA wa kuogopa ukawa ndio uwaogopeshao kuliko kitu kilicho tengeneza WOGA wauogopao.

Swali:
  • SI inasemekana kuna waogopao  mpaka woga wa kupata mimba  kutokana na woga wa matatizo ya mimba waliyoushuhudia kwa aogopaye  ambao labda woga huo ni woga  zaidi ya waogopavyo matatizo yenyewe ya kikweli ya Mimba?
  • Umeshawahi kusikia usemi wa Kindengereko wa``There is nothing to FEAR but FEAR itself´´?

Ndio,....
... labda kuna woga wa WOGA tu pia,...
....na katika KUOGOPA ,...
.....kiogopwacho kinaweza kuwa wala sio kistahilicho WOGA  wa MTU  aisee!:-(



Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(



Mighty Shadow aingilie kati tena kwa - Yuh Lookin Fuh Horn





Denyse Plummer atawanye swala kwa - Nah Leaving




Sugar Aloes ashikeshike swala katika - Reflections




Baron amwage tu naye tena -Mother Earth Crying

Read more...

Wakati nimerudi tena KIJIWENI kutoka kwa BABU pale LOLIONDO,...

>> Wednesday, March 16, 2011

... ingawa labda wala sikuondoka KIJIWENI,...
.... kama KUTOKUWEPO na  uwepo wa mtu MAHALI ukiangaliwa vizuri !:-(




Swali:
  • Si unajua kuwepo MAHALI  sio lazima uwe MAHALI hasa ukizingatia uwepo wa mtu ndani ya mtu unaweza kuwepo tu vizuri KIMAWAZO TU kama tu uwepo wa mtu CHOONI labda   hauashirii KIUHAKIKA kimawazo mtu huyo yuko CHOONI?

  • Na si unajua kuna mtu UNAYEFIKIRIA NDIYE uongeaye naye ambaye wala hayuko na wewe hapo umuongeleshapo kwa kuwa hata awazacho wakati upo naye  UKIMUONGELESHA sio wewe wala uongeayo-hata kama hapa sizungumzii UWEZEKANO  kuwa PIA kunauwezekano mpaka hata mtu unayengonoka naye labda kimawazo hangonoki nawe kwa kuwa MAWAZONI ANAMUWAZA MTU MWINGINE na  akitaja au kupayuka jina kwa bahati mbaya wakati wewe unashughulika kumpa tamutamu inaweza kustukiwa na mpaka majirani WAPENDAO KUWASIKILIZA mkiwa kwenye yenu ya UNYUMBA  kuwa atamkalo jina kitandani, MKEKANI, kwenye meza chafu jikoni, kwenye sofa  au tu migombani sio jina  lako ?
  • Unauhakika ni WATANZANIA wangapi hawakuwepo LOLIONDO angalau kiduchu hivi karibuni hata kama ni kimawazo tu? 
  • Kwani unauhakika mie MTAKATIFU Simoni MKODO Heriel Kitururu nimerudi kutoka LOLIONDO  kwa BABU kikweli ?



Ndio,...
... labda kuna  HATA  kingunge ambaye anafikiri kuwa anaushahidi yuko na mume wake chumbani,...
... ambaye ukweli ni kwamba MMEWE wakati huo bado yuko ofisini na MREMBO sekretari anatomasatomasa!:-(



Swali:
  • Si unajua  haya maswala ya UWEPO na KUTOKUWEPO kunibishia RUKSA?
Ndio,...
....nimerudi KIJIWENI hapa ,...
......na hili ni wazo tu MHESHIMIWA !



Hebu Mighty Shadow aanzishe upya mkuno  tofauti  KIWAZO  kwa - Bassman



Mighty Shadow ATEKENYE tena na -Feeling the feeling




Mighty Shadow aendelee na -Tan Tan



Shadow asisitizie-Swing de ting



Amalizie tu tena na -Whats wrong with me?

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP