Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Shikamoo Mwalimu!

>> Friday, July 07, 2006

Nilivyokuwa mtoto niliamini Watu wazima wanajua kila kitu. Niliamini hata hawaanguki. Watu wazima kama wazazi niliamini ndio kila kitu duniani wanajua.Ni mambo mengi wanatufundisha lakini tukifikia kuamini kila kitu wanajua basi tumepotea. Sasa baada ya kukua na kuingia duniani kisawasawa nashangaa kukutana na watu bado wanaamini mtu akiitwa profesa anajua kila kitu. Watu wanasahau kuwa kila binadamu ana mipaka yake. Au una fikiri Profesa Lipumba anaweza kutibu mifupa kama profesa Sarungi?

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Christian Bwaya 5:38 pm  

Kitururu,
Hapa unaongelea hasara za elimu yetu inayothibitishwa eti na wingi wa makaratasi yaitwayo cheti.
Mwenye makaratasi mengi hata akiongea pumba waungwana wanatikisa vichwa "pointi!". Ole wako ukiwa na nusu karatasi! Hakuna anayekusikiliza "Ana nini huyu hata aseme?"
Umefika wakati tuseme basi. Mimi nasema hizi zote ni athari za ukoloni na nashangaa tunazing'ang'ania.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP