Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mungu Awalaze mahali pema peponi!

>> Monday, January 29, 2007



Hivi kwanini walazwe? Hivi peponi si sehemu ambayo mambo mengine yanaweza kufanyika?

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 6:21 pm  

Swali nzuri sana Mzee Simon,hivi peponi ni wapi?Nani anaweza kutupa ushahidi wa kweli wa peponi?naona kimya.Kwamtazamo wangu,binadamu ni kama mauwa au mmea unachanuwa na kupendezesha ipo siku lazima unyauke kisha unangolewa shambani na kutupwa mbali tofauti na binadamu tunazika na kuimba alazwe pema peponi.Kwa mtazamo wangu baada ya maisha hapa duniani banadamu anakwenda kuanza maisha mengine mapya hapo tunakutana na wale walio tutangulia tofauti na mmea unapo ngolewa shambani unatumika kama mbolea.Huu ni mtazamo wangu.

Anonymous 11:32 am  

Kwa mujibu wa Kitabu changu cha Dini, peponi ni sehemu ya pili baada ya kutoka duniani na kabla ya ufufuo. Peponi ni pale miili iliyokufa hupumzika ikisubiri kufufuliwa tena. Ndio maana huwatakia heri ya kulazwa na kupumzika vema huko peponi.

Simon Kitururu 11:51 am  

Kumbe peponi na mbinguni ni tofauti eeh!

Anonymous 4:09 pm  

Kwanza kabisa tuanze na kitendo cha kumtaka mungu awalaze watu mahali pema.

Dini hizi za kuja zinatuambia kuwa maisha yako kabla ya kufa ndio yataamua kama utakwenda kuishi maisha ya raha au moto wa milele. Hivyo kama maisha ya mtu kabla ya kufa hayakutii amri za huyo mungu anayechoma watu moto kama mishikaki, kitendo cha waliobaki hai kusema, "mungu amweke mahali pema peponi" ni sawa na kupoteza muda. Hukumu, vitabu vyao vinatuambia, itatolewa sio kutokana na waliyosema waliobaki duniani, ila jinsi marehemu alivyoishi wakati wa uhai wake.

Hivyo mtu akifa, hata sala zikitolewa na wakuu wa dini zote, kwa mujibu wa vitabu vyao, hakuna kitakachobadilika. Akifika huko ataambiwa, "nilikuwa gerezani, hukunitembelea, nilikuwa mgonjwa...." na kadhalika. Sijaona mstari unasema, "kwakuwa mashehe, mapadri, maimamu, papa, na binadamu wengine wameniomba nikuweke mahali pema, basi sitakutupa motoni."

Egidio Ndabagoye 2:32 pm  

Alikuwa mwizi twamjua muweke pema peponi.....
Bado nachanganyikiwa hapo.Peponi??

Kama unapenda pepo mbona unaogopa kufa?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP