Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nani Hapendi kuwa BWANA MKUBWA kama Robert Mugabe?

>> Friday, March 28, 2008

Sikatai ukweli kuwa wapo binadamu ambao hawapendi kuwa mabwana mkubwa kinamna!

Lakini...
...ukifuatilia vitu fulani, utastukia kuwa asilimia kubwa ya binadamu wote wakiwa katika ulaji , ni vigumu kuwatoa mezani.

Ubwana mkubwa una ulaji wake.
Ubwana mkubwa hauko tu katika vitu au taito za ofisi zilizo waziwazi.

Mtu anaweza akakutawala kisaikolojia , ukatawalika bila hata kujua ukurupuke vipi.
Mabwana mkubwa wako kisaikolojia pia hawataki kuachia kiti hicho.

Swali:

  • Ushawahi kusikia Mwalimu wako , hata baada ya wewe kumzidi madarasa akakataa kiti cha ukweli kwamba ni mwalimu wako?

  • Ushawahi kumstukia aliyekufundisha ukafaulu , awezavyo kutumia kisa hicho kutengeneza ubwana mkubwa sehemu nyingine ? Namaana ,hujawahi kusikia jamaa akisema kitu kama ;`` nilimfundisha Nyerere mimi! ´´, kwa sababu Nyerere baabu kubwa?


UKIFIKIRIA SANA, HAKUNA ALIYEWAHI KUWA KATIKA ULAJI AKAUACHIA KIRAHISI .

Katika Ubwana Mkubwa naamini :
  • Mwalimu Nyerere alifikia kiwango ambacho hakuhitaji awe ofisini ili awe Bwana Mkubwa,bado alikuwa Bwana Mkubwa. Angenyanyua simu wewe kama Rais ungejibu na kusema; ndio Mzee!
  • Bill Clinton bado anauhusudu ubwana mkubwa na ndio moja ya motisha yake ya kufanya kila njia Mrs Clinton awe ofisini.
  • Putin wa Russia , kuachia Uraisi na kuchukua Uwaziri Mkuu ni dalili hizo hizo za kutotaka kuondoka jikoni.
  • Fidel Castro , kumuachia mdogo wake Urais na kuwa mshauri Mkuu wa serikali, ni dalili za kutotaka kucheza mbali.

  • Wanasiasa Tanzania ambao tokea tuzaliwe mpaka leo hii ni waheshimiwa wabunge, ambao wameacha kulala bungeni kutokana na televisheni............ni katika swala hilohilo la ugumu wa kuachia kakitu ulikozoea.

Naweza kuendelea milele........


Lakini watu wanasahau kuwa...........
....Ubwana mkubwa unakuweka katika sehemu ambayo mahitaji yako husikilizwa kirahisi.

Kisaikolojia, ubwana mkubwa unaleta utiifu kwa walengwa iwe kwa nguvu za mabavu au vinginevyo.
  • Mtoto anaweza akasababisha utii amri zake za kununuliwa pipi kwa kuililia hadharani na wewe ukatii amri.
  • Kama unapenda michezo ya ubaba na mama chumbani, unaweza ukajikuta unatii amri ya kununua ile zawadi ambayo ulikuwa unafikiria ni kupoteza fedha , ili usinuniwe chumbani.

Nachojaribu kusema ni:

Robert Mugabe na miaka yake themanini na ushe, hataki kuachia Urais na baadhi ya watu wanashangaa sana, lakini si kitu cha kushangaza.Wengi wangependa kufanya kama yeye kama mazingira yange ruhusu.

Jamaa kanogewa!

Lakini pia....
....
tusisahau kuwa kuna watu kama hawa akina Robert Mugabe ambao wanaonekana wabovu, wakiachia maeneo, yanakuwa kama Iraki. (Siumecheki jinsi hata upinzani ulivyogawanyika Zimbabwe?)

Unakumbuka mambo yakumtoa Saddam Hussein katika uongozi Iraki kwasababu alikuwa mtu mbaya anaye ua watu wengi, yamesababisha watu wazuri walioingia kurekebisha nchi, kutengeneza mazingira ambayo yanaua watu wengi kwa siku kuliko hata mtu mbaya Saddam Hussein . (Lakini nafikiri unajua kisa cha kumtoa Saddam hakikua kwasababu muuaji.)

Sasa nachojaribu tena kusema ni;

Asilimia kubwa ya watu wakiustukia Ubwana Mkubwa katika anga yoyote ya maisha ,ni vigumu kuiachia.

  • Mtoto akijua akilialia anapewa atakacho, hawezi kuacha kulialia.
  • Mwanadada akigundua akikunyima nanihii inakusababisha usikilize matakwa yake ya kumuachia akacheze mdundiko, atakunyima nanihii.
  • Dume zima likistukia likinuna lifikapo nyumbani haliulizwi kwanini limechelewa kurudi nyumbani, litanuna halafu na maji ya kuoga litachemshiwa.

Wakati unangalia wikiendi hii Robert Mugabe anavyogombania ubwana Mkubwa, kumbuka kuwa inawezekana hata mimi na wewe kila siku tunagombania kubakia na ubwana mkubwa kinamna , ubwana mkubwa ambao kama unatimiza angalau kupata nanihii, hatutaki kuuachia kirahisi.

Swali:
  • Ushawahi kuona mzee anakubali kirahisi kuwa kaishiwa nguvu na anahitaji msaada wako kumpeleka chooni na kumchamba?
WIKIENDI NJEMA!
Hebu twende SENEGAL kidogo kuwasikiliza hawa jamaa DAARA J wakikupa kibao ALLAH

Au endeleza tena na DAARA J live

Baadaye!

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP