Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKARIMU wa KUMPIGA mgeni ili MWENYEJI apone.JIFUNZE kitu fulani kutoka South AFRICA ya LEO.

>> Monday, May 19, 2008

USIJIDANGANYE!
Si kweli ukarimu wa mwenyeji wako ndio ushahidi kuwa anakukupenda au anahusudu umemtembelea chobisi.

Nadhani inawezekana umewahi kusikia kamsemo; Mgeni njoo , MWENYEJI apone!

Mgeni akija, kuna uwezekano yule jogoo wa krismas akachinjwa mapema, na pesa za kununulia nguruka wa kesho, zikanunua soda.

Lakini mgeni akiendelea kuwepo, kuna watu watapata muda wakubadili mkao , kutoka mkao wa jamaa mgeni hatuwezi kumpa jembe tukaenda naye leo kulima, mpaka mkao wa ; HIVI WEWE UTAONDOKA LINI?

Kwa walioko nchi za watu wenye rangi tofauti ni rahisi mpaka kusingizia kuwa ni ubaguzi tu wa rangi ufanyao mtu kutokukutaka kwake au hata katika choo cha jirani.

Lakini, kuna watu hawampendi tu mgeni kutokana na sababu moja kubwa kuwa,YEYE ni MGENI.

Binadamu tunaudhaifu wa kutoelewa vigeni.

Lakini...
......Kitu kigeni tusichokielewa, tunaweza tukajikuta tu.... ...

  • Tumekiabudu kama MUNGU
  • Tumekiogopa kama Shetani
  • Tuna wasiwasi nacho kama kuonja nyama ya MBWa
  • AU KAMA KAWAIDA yetu TUTAKISINGIZIA hasa kwamba ndio SABABU ya YOTE mabaya yanayotutokea.

Nakubali, umasikini, ujinga, na mengine mengi yanaweza kusababisha mgeni awe nishai!
DUH!

JIHADHARI tu kama uko SOUTH AFRICA sasa hivi na si Msauzi, unaweza kupigwa kibano.
Jihadhari kama hauko Nchini kwako, au hata mtaani kwako, unaweza kupigwa kibano.

Nimebanwa kidogo!
Labda nitaendelea na topiki hii badaye kama bado iko mawazoni!

Angalia HAPA
au soma HAPA kama unataka kujua fununu ya yawatokeayo walio SOUTH AFRICA


KAMA unanafasi....
Hebu pitia kidogo UMASAINI kama kulivyorekodiwa wakati jamiii inawakarimu Familia ya GARSON(Tahadhari:Kama hupendi kuona damu au mnyama akichinjwa usiangalie!)


Au tukatike viuno kama SOUTH AFRICA tu, ambako hatutakiwi kuwepo..katika kibao kiletwacho na TSHE-THSA BOYS

Read more...

FURAHIA maisha kwa kupata UKIMWI.:-(

Maswala ya UKIMWI si ya kutania.
Watu mamilioni wanateseka sana hivi sasa kutokana na UKIMWI.

Lakini....
...Binadamu haachi kunishangaza!

Kuna watu kibao inasemekana huwa wanatafuta kuambukizwa UKIMWI kwa makusudi ili kufurahia maisha.

Utasema utakalo sema, lakini , hawa watu kwa taaluma za kisasa za kumjua binadamu kwa vipimo vya kisasa, SI VICHAA.

Hili swala ingawa watu wengi wanasema liko kwa WASENGE tu, kuna mmoja wa watafiti wa maswala haya ambaye nimewahi kuongea naye , anasema swala hili liko hata kwa binadamu wapendao kugusanisha HASI na CHANYA (heterosexuals)katika miondoko ya mikasi a.k.a Ngono.

Tofauti kati ya Wasenge na WachezaJUMAnaROZA ni kwamba, wasenge wamefikia kuandaa pati maalumu kwa ajili ya tukio lakuwini LOTTO katika kubadili status yako kutoka negative kuwa positive, a.k.a SEROCONVERSION

Swali:

  • Unakumbuka kuna wakati UKIMWI ulidhaniwa kuwaathiri WASENGE pekee duniani?
  • Unakumbuka kutokana na jamii kutofagilia USENGE, kuna wasenge kibao ambao hawakustui tu kuwa wako katika fani?
Kwa WASENGE , ilikukusaidia upate UKIMWI kwa FURAHA, huwa wanaandaa pati ziitwazo BUG PARTIES.

Katika pati hizi kunakuwa na GIFT GIVERS na BUG CHASERS.
Hawa Gift givers ndio wenye virus tayari na BUG Chasers ndio watakao kuambukizwa.

DUH!
NAACHA HII TOPIKI!

UNaweza kupata habari zaidi mtandaoni kwa kutafuta manenoo kadhaa..

Pata basi terminology katika lugha ya KIKWERE kidogo.....

Terminology

Bugchaser
(also bug chaser) An HIV- man who actively seeks HIV infection
Conversion party
A sex party at which men attempt to seroconvert themselves or others (see also: bug party)
Fuck of death
Unprotected sex between an HIV- and an HIV+ man
Giftgiver
(also gift giver; gift-giver) An HIV+ man who infects or attempts to infect willing partners with HIV
Giftgiving
(also gift giving; gift-giving) Infecting a willing partner with HIV
The gift
HIV
Pozcum
(also pozload, poison seed) The ejaculate of an HIV+ man
Neg butt
Someone who is HIV-
"Poz my neg hole"
Give me HIV
Stealth fucking
infecting unsuspecting sex partners with HIV
Unaweza kumsoma huyu jamaa kidogo pia ,kama wewe mvivu kusaka vistori mtandaoni, akufundishe kuhusu jinsi ya kuwa MSENGE.

DUH!

Nilitaka kukukimbia, lakini...
...... nimeona nikuache tena na ELIZABETH PISANI, mtafiti wa maswala, akupe BUSARA za MALAYA ,au ajaribu tu kukushauri kuwa kama watu kwa wingi katika maeneo fulani wangefanya matusi;(samahani kwa lugha chafu!)nilitaka kusema, anadai kama WASICHANA wengi wangefanya UASHERATI a.k.a Kula Uroda a.k.a Mikasi a.k.a. Ngono kama KAKA ZAO, basi UKIMWI ungepungua duniani.

Anadai kama uko SOUTH AFRICA, moja ya njia kubwa kwako WEWE mwanaume kujilenga upate Ukimwi ,FUNGA NDOA .

CHeki kitabu chake
au
Msikilize kidogo.....


AU...

Read more...

Jifunze UFISADI- Sura ya KWANZA.

>> Friday, May 16, 2008

Mbinu moja maarufu sana ya kumshinda adui ni kumjua adui.

Si utani , ufisadi ni bomba la kitu maarufu duniani na waongeleao ufisadi mara nyingi ni wale wasiofaidika na UFISADI.

Siwezi kusema kuwa na utaalamu na somo hili ingawa nadhani kuwa, inawezekana hili somo halihitaji uende chuo chochote ili kufudhu jinsi ya KUMFISADI Mtu , Nchi au Kanisa.

Swali:

  • Ushawahi kujiuliza kwanini unaweza kuona jinsi gani MFISADI anavyofanikisha UFISADI hata bila kwenda kusomea popote wakati huoni taaluma ya PROFESA wa UCHUMI au wa KILIMO atatuavyo matatizo ya kiuchumi wa Tanzania utegemeao kilimo?
  • Unafikiri kwanini katika silabasi za shule ,hakuna kozi ya UFISADI?

Naamini UMIMI uko ndani ya binadamu tokea atokee duniani au enzi hizo binadamu walivyofikia wawili hapa duniani.

Naamini chembechembe za ufisadi zilianza kujijenga ndani ya binadamu kuanzia pale alianza kuamini uwepo wa uchache wa vitimiza mahitaji yamuwezeshayo binadamu kuishi.

Mahitaji ya binadamu na jinsi ya kuweza kuyatimiza yanaendelea kutofautiana kulingana na upeo wa akili ya binadamu ulivyo, hasa ukikumbuka enzi za KUTUMIA TREKTA na zile za KUVAA KIBWAYA , mahitaji ya RAIZONI, kunatetesi yalikuwa au bado yanatofautiana.

Kipindi cha kuishi kwa kuokota mizizi na matunda, mjanja alikuwa ni yule atakayeweza kuwa na mizizi na matunda wakati kuna uhaba wa mizizi na matunda. Lakini wakati hivi vitu(mizizi na matunda) viko vingi , ilikuwa huwezi kumtisha Mr Kidume, kwa kumnyolisha eti una mapera mengi kuliko yeye, wakati anajua kuwa hata pale apendapo kumuangushaga Binti Kitoweo jua likizama, ni chini ya mti wa mpera uliojaa matunda.

Ukiruka kutoka enzi za kupigania embeng'ong'o na mihogo mpaka kipindi hiki ambacho bado wengi hapa duniani tunaweza kupigania embeng'ong'o na mihogo ingawa wengine wanaendesha magari aina ya FERARRI na WANA VIJISENTI BILIONI kadhaa katika benki kadhaa hapa duniani, unaweza hata ukakubaliana kuwa AKILI za BINAADAMU ni UJINGA uendao na AKILI za kiBINAADAMU, hasa katika staili yake ya kusikilizia ladha ya kuridhika au MAFANIKIO.Inashangaza jinsi binadamu awezavyo kujilimbikizia wakati wengine wana njaa, kama unaweza kusahau UBINADAMU.

Unakumbuka NGAZI za MAHITAJI kwa mujibu wa Maslow (Maslow's hierarchy of needs?)

















DUH!
Naachia hapa kufundisha somo hili la UFISADI .
Unajua TENA, naweza kukudanganya bure!

Ila kumbuka kuwa chembechembe za ufisadi zipo tu hata ndani yako.

Usipoangalia , unaweza ukajikuta umeamsha chembechembe za UFISADI na ukazirutubisha pia kiaina.

Katalisti za kuamsha mshawasha wa KUFISADI ziko bwelele, zinakuzunguka hadi msalani pale ustukiapo maji hayatoki na pesa za kununulia karatasi za kujipakaza mavi sehemu zifichwazo na chupi hauna. Halafu unajua kufutia kinyesi ukutani nishai na mchanga unaweza kuwa na minyoo.

DUH!

Usitishike lakini! Labda tusipoharibu mazingira tunaweza kuwa na majani bado au mawe yafaayo kutumika kama MAKOKONEO.

LAKINI......!
Baadhi za Katalisti ziwezazo kuathiri ashki za UFISADI wako ni:
  • Utu WAKO
  • Umasikini wako au jinsi ufikiriavyo kuwa wewe ni masikini hata kama si.
  • Uelewaji wako wa staili yako ya kuridhika .
  • Udhaifu wako wa Muonekano au sehemu(status) yako katika jamii
  • Udhaifu wako ukuwezeshao kudokoa mboga ukiachwa jikoni peke yako au Ukiwekwa kwenye ofisi ishughulikiayo VITOWEO ;kwa mfano kama wewe Raisi ofisini , Mjumbe wa Nyumba kumikumi au kama VIJISENTI tu vinakatizakatiza kwenye kona yako halafu unahisi hutadakwa ukidokoa.
  • nk......kadhaaa wa kadhaaa.


JIADHARI!

DUH!
Samahani kwa simulizi chafu!

Hebu tumsikilize Ngozi Okonjo-Iweala akigusia maswala ya UFISADI au mambo ya : How to help Africa? Do business there



Au Angalia tu ujinga kama vile DUME ZIMA liwezavyo kutumia muda wake MUHIMU wa dakika kadhaa KULIA katika BIG GIRLS DONT CRY

DUH !

WIKIENDI NJEMA!

Mpate tu PAPA WEMBA au VIVA la MUSICA

Read more...

Kilema cha MAANDISHI , PICHA, TV,sinema au KUSHUHUDIA , hata katika kusaka habari za MPENZI KIBOGOYO.

Nasikitika kuwa maandishi , picha na hata ushuhuda wa macho inaweza kuwa si msaada kwa binadamu katika kukabiliana na ubinadamu au dunia hii, ingawa unawezakusema unajifunza kitu kwa kuangalia picha za nanihii au kusoma maandishi.

Ubinadamu nishai!
Karibu kila agusacho au kutumia kama binadamu, kina udhaifu.

Ndio maana hata kama huamini Mungu, ni vigumu kuwa na uhakika kuwa hakuna Mungu au angalau LIKIUMBE ambalo linasababisha binadamu huyu mwenye mapungufu, pamoja na mende, wawepo hapa duniani.

Usitishike sana!
Inawezekana nilivyovitaja vinakusaidia.
Na ni ukweli naheshimu maandishi, picha , picha zitembeazo na pia , ushuhuda wa macho.

Naandika hapa leo hii kwa sababu nimeshangaa kujikuta nabishana na watu kuhusu umuhimu wa vitu hivi, kitu ambacho sikudhani kinaubishi.

Au nisemee...

Naamini kabisa kujisomea hasa vitabu, ni bomba la ujanja katika kutekenya akili.
Ila sipingi umuhimu wa picha au picha malaya(moving pictures, TV,Videos,etc.) kwa jinsi zisaidiavyo uelewekaji wa jambo kwa kutumia kona nyingine. Pia sisahau msaada wa maswala ya shuhuda za kuona papo hapo.

Nachojaribu kusema ni.......

1. Maandishi huhifadhi taaluma vizuri sana, ingawa stori za paja la kuku, kama hujui kuku yukoje, akilini lawezakufanana na paja la kicheche uliyemzoea baada ya kumalizia kusoma stori za kuku.

Utamu wa kusoma maandishi ni pamoja na jinsi ukupavyo uhuru wa utalii wa ubongo
( imagination).
Katika maandishi na kama hujawahi kuonyeshwa michoro ya picha za shetani mwenye mapembe, basi shetani anaweza kuonekana anasura kama yule kidume au kijike umuogopaye, ambaye anaweza hata akawa ni mwalimu au mme wako.

Swali:

  • Kama usingeonyeshwa michoro ya kubunia ya shetani au YEsu , unafikiri mawazoni kwako Yesu na Mkwawa wangekuwa wanasura au wamevaa ulimbwende aina gani?
  • Tukiachana na maandishi katika barua kwa Baba:Wakati unaongea na simu na LIMTU lako , ushawahi kufikiria unayeongea naye ananukaje mdomo?


2. Maswala ya video na picha ni kiboko pia!
Usipoangalia unaweza kusahau kuwa si lazima yarahisishe kwako kuelewa kuwa hiki ni KIJIJI cha MATOMBO au hivi ndivyo jinsi BATA wafanyavyo MAPENZI.

UKiona picha au video ya kijiji ,ni mpaka uambiwe kuwa hiki ni kijiji cha MATOMBO ili uelewe kuwa hapa si kijiji cha KIABAKARI.
Ukiona picha au video za Bata wanafanya mapenzi, kama hujui kinachoendelea, unaweza kufikiria kuwa BATA wanapigana.(Kwani hujawahi kusikia waliofumaniwa na mtoto wao wakati wanafanya mchezo wa baba na mama halafu mtoto akalia kuwa BABA ANAMPIGA MAMA?)

Swali:
  • Ushastukia kuna watu duniani , picha ipigwayo Tanzania au GINI ya Ikweta(Equatorial Guinea) kwao ni sawa tu, hasa kutokana na kufikiria Afrika ni nchi moja?

3. Mwisho ....
Nakiri tuko tunaohusudu taaluma na ujinga tuufyonzao kwa kushuhudia jambo kwa macho yetu wenyewe.Lakini swala la kushuhudia jambo, ni rahisi kujidanganya kuwa utaelewa au hata kuweza kuwa mtoa ushuhuda mzuri zaidi kwasababu ulikuwepo wakati kitendo kinafanyika. Cha ajabu ni kwamba, kama hujui mchezo wa Kriketi , hata uutolee macho kama bundi, huwezi kuelewa daktari anafanya ninikatika operesheni yako ya jando, kama huna taaluma husika.

DUH!

Kuelewa ni nini kinaendelea kunahitaji tetesi za kujua unachoangalia ni nini, la sivyo ,UTABUNIA.

Katika vita zetu za kutumia SILAHA za mkuki na mapanga , hili likitu ambalo jamaa anakunyoshea bila kulirusha au kwa jina jingine BUNDUKI , mtu unaweza kulidharau kuwa si SILAHA na wala haliui kirahisi tu kama au kuliko mshale wako wenye sumu ya nyongo ya kenge, kama hujawahi kusikia duniani kuna hata kitu bomba kama GOBOLE.

Sasa cha kujiuliza tu ni kwamba.....
.....Haya yote tuyatafutayo au kuhifadhi katika maandishi , picha au ubongoni baada ya kushuhudia,si ni maswala tu yasaidiayo tu kujazia muda wa binadamu hapa duniani akiwa safarini kutoka kuzaliwa kuelekea kufa?
.......Haya mavitu tuhangaikayo kuyatafuta hata kwenye dini , pombe au moshi wa majani ya mpapai, si ni majivitu ya kujaribu kujazia tu haya maisha ladha tamutamu kunoga ili katika ujazo, yazidi kupunguza kusikia kwetu uchungu au yajaribu kurahisisha kutupatia kanjia kakuendeleza tamutamu kunoga baada ya wewe ,mimi na yule kukata roho , kufa au kuanza?


EE BWANA EEH!Naaacha basi kitopiki!
Kumbuka Mimi Nawaza tu hapa!

Hebu twende KANADA tukamsikilize tena RUSSEL PETERS akishauri WAZUNGU waanze KUPIGA WATOTO WAO.....

Au Ngojea twende NIGERIA tuangalie mambo ya KIDUNIA kama VILE ya akina DADA wakipigana....

Tulia tu na ERIC SERMON akija na kibao REACT

Read more...

KATIKA kumfuatilia MASIKINI inayedaiwa ANANOGEWA zaidi KUZAA!

>> Tuesday, May 13, 2008

Jasho laweza kukutoka wakati unajaribu kutetea utajiri wa TANZANIA katika macho na masikio yaonayo jinsi gani NCHI tajiri kama TANZANIA inavyoweza kuwa na watu maskini au kuitwa nchi MASIKINI ya dunia ya tatu.

Lakini...
....Yeyote awezaye kuona UTAJIRI ndani ya nchi iitwayo maskini na yenye maskini kama TANZANIA, ataweza kujua jinsi gani hata neno TAJIRI au MASIKINI liwezavyo kuwakilisha mtazamo tu fulani wa watu kutokana na jinsi tulivyofundishwa kuangalia mambo.

Lakini...
....Wengi huweza kukuapia kuwa wanajua kipimo cha utajiri na umasikini hapa duniani.

Na hata ukijifanya unatumia vipimo vya furaha au kuishi na uvitakavyo tu , bado unaweza kujikuta unachekesha katika jamii ambayo tokea unazaliwa inajaribu kukujenga kimawazo kufikiri walionavyo zaidi wamekuzidi ujanja.

Tatizo ni kwamba,.....
...... jamii ina staili ya kuangalia ulivyonavyo utake usitake, na hujaribu kukutafsiri kuwa wewe kiboko au panya.

Cha kusikitisha ni kwamba,.......
......ingawa umaarufu wa tajiri mara nyingi ni umaskini wake kama unachagua kumuangalia huyo tajiri bila kutishika na nyumba, magari au suruali yake ya kodrai, bado kwetu wengi tajiri ni mjanja hata akifa kwa BP au utajiri wake wa kifikira ukiwa ni KUBWA jinga.

Swali:

  • Hivi ni kweli MASIKINI huongoza kwa kuwa na watoto wengi?
  • Nani kasema MASIKINI wananogewa ZAIDI kujifungua ZE TOTOS?
Kati ya jambo nililoulizwa mara kadhaa hivi karibuni, ni kwanini masikini hawajifunzi kuwa ni ghali kuzaa watoto wengi.

Ukiacha CHINA ambako kisheria huruhusiwi kuwa na watoto wengi, utastukia nchi nyingi zilivyozidi kutajirika, ndivyo asilimia kubwa zaidi ya raia wake walivyopunguza namba ya watoto katika familia.

Kama unafikiria zaidi ughali wa kulea mtoto, unaweza kushangaa kwanini matajiri wawe na watoto wachache halafu masikini wawe na watoto wengi.
Swali:
  • Unafikiri maana na vigezo uitavyo ni utajiri , vingekuwa na tafsiri gani kama ungelelewa katika jamii ya ujanja ni kuwa na kidogo?
  • Unauhakika utajiri si jambo liishio mawazoni tu?
  • Kisaikolojia unafikiri ni mpaka uwe na walivyonavyo matajiri ilikupata ladha tamutamu ya tamu ya kuwanavyo?


Si mshauri masikini aige tajiri katika uvivu wa kuzaa!


KWANI Inasemekana ni rahisi zaidi kwa maskini kufa kuliko tajiri kukata roho katika mazingira ya dunia hii ya leo ambayo ujanja ni jinsi gani unaweza kununua madawa, kujilipia hospitalini au hata kuweza kujinunulia dagaa na mchicha .



Ila.....
...Tafsiri nzima ya utajiri , inaweza isiongee lugha moja ukimuuliza tajiri wa Kiafrika afuataye UAFRIKA ndani ya AFRIKA na tajiri wa KIJERUMANI, afuataye UINGEREZA aishiye ndani ya MAREKANI kuwa ;UTAJIRI ni nini?

DUH!

NACHOJUA......
Umasikini noma!Hasa kutokana na kumaanisha masikini ni mtu anayeshindwa kupata atakacho.

LAkini......
Swali:
  • Tajiri umjuaye unafikiri anapata vyote atakavyo?
  • Unauhakika kama huvifikirii sana ulivyokosa; wewe si tajiri?
DUH!

UFIKIRIAYE ni masikini , si lazima kuwa kweli ni masikini, kama utajiri kwako ni jinsi mtu alivyojilimbikizia asivyohitaji.

Halafu tukumbuke kuwa katika maswala ya vipimo, familia yenye watoto wawili ni wengi, kama walitaka kuwa na mtoto mmoja.

PIA....
...Pamoja na sifa zote mbaya za umasikini, kama ushawahi kumsikiliza Mother TERESA, watu husahau ukaribu wa masikini na MUNGU.

LAKINI kama ....
......kwa masikini watoto ni MTAJI , BIMA, TREKTA na hata UTAJIRI, kwanini wasizae sana?

BASI bwana topiki imenishinda!
Samahani hapa NAWAZA tu !

Hebu twende KENYA tukatembelee CRIB ya OMONDI....


Ngoja niache tusikilize utundu wa COURTNEY PINE akiwa na MANU DIBANGO katika midomo ya BATA na...au..... DUH! ..... LION OF AFRICA.

Read more...

Nataka , HATAKI!Akiwa TAYARI au akitaka, MIE nimechoka!:-(

Katika maswala ya" NATAKA, HATAKI , akiwa TAYARI nimechoka", najaribu kuangalia Mahusiano ya muda, watu na tukio litokealo , hata kama tunaweza kusingizia kuwa haya maswala ni moja ya sababu zifanyazo kuwa wewe umepata na sisi wengine tumekosa.

Udhaifu wa kibinadamu, hauruhusu tuwepo sehemu zote au tuwepo katika nyumba wahitajiyo hausiboi au hausigeli mwenye sifa kama zetu wakati au siku wenye nyumba wasubiriyo mtu agonge hodi, akitafuta kazi.

Ni kweli inasemekana kuwa udhaifu wa binadamu unatofautiana ukiuchungulia katika mida tofauti au maeneo tofauti.

Kwa hiyo ,...
....inaweza kuwa ni kweli, ndani ya muda au siku fulani, kumtongoza HIDAYA ,anawezakukubali kirahisi kuliko wengi wahisivyo kutokana na wamjuavyo kwa sifa zake za kununia wanaume.

Kwa hiyo,...
.... kuna muda unaweza kujikuta umefanya dhambi kirahisi zaidi kuliko jana.

Kwa hiyo ,....
......inawezekana ndani ya muda fulani, ni rahisi kuliliza jibaba zima hata bila KULIPIGA roba ,kwa kulitukana kuwa ni ;KUBWA zima jinga!

Swali:
  • Unakumbuka kuwa labda ungecheza LOTTO sasa hivi wakati unanisoma hapa, labda ndio muda wako wa kushinda?
  • Hujawahi kushindwa kitu watu wakisifiacho kwa urahisi wake?
Inasemekana kila mtu ana nafasi yake yakuwa milionea au kupata , kama atacheza mchezo sahihi katika dakika, sekunde au muda sahihi.


Uhusiano wa kitu kiitwacho BAHATI NASIBU na ashindaye bahati nasibu, ni uhusiano wa mcheza sahihi katika muda sahihi na ndani ya mchezo sahihi.

LAKINI ...
...Kama kila mtu angeweza kugundua siri ya kucheza sahihi , muda sahihi , ndani ya mchezo sahihi, inawezekana WATU WOTE uwajuao, WANGEKUWA WANALIA sasa hivi, na hii DUNIA yetu yenye mapungufu isingeweza kuwepo tena , kutoka na mtu kufanya kitendo sahihi kama cha kulipua mabomu ya nyukilia.

Tukumbuke kuwa, kucheza kwako sahihi iliumpate Hidaya au Hamisi, kucheza kwako sahihi ili upate kazi fulani au mshahara fulani, kuna ambaye mchezo wake sahihi atakao kuucheza sahihi, ni kujaribu KUKUUA WEWE kutokana na rangi au sura yako, au kukuliza kutokana na afurahiavyo staili yako ya kulia.


Sidhani kama ni kwa bahati mbaya tu DUNIA HII tuishiyo iko kama ilivyo.
Sidhani hata binadamu wajaribu vipi ,wanaweza kuondoa mapungufu ya binadamu na dunia hii.

Kwahiyo nafikiri....
.. bado kuna ambao tutawaita kuwa wana bahati kutokana nakufikiri kila wakijaribu kitu fulani , wao hupata wakati siye tukimngoja HIDAYA uchochoroni, hapiti njia hiyo siku hiyo.

SWALI:
  • Unakumbuka umpendaye anaweza akawa anampenda yule ambaye anampenda yule akupendaye ambaye humpendi?
  • Unakumbuka kuwa hapo hapo katika barabara uivukayo, KUNA MTU atagongwa au alishagongwa muda fulani?

Katika maswala ya kukosea TIMING au kamuda, unaweza kujikuta unawaza...
....Ningependa kuonja sasa hivi , lakini dhambarau hazijaiva.
...Ningependa kuonyesha penzi, lakini mbona sina mpenzi zaidi ya hili limtu niishilonalo kwa kuogopa nini jamii itasema ndoa ikivunjika.


Lakini.....
...Mpenzi wako achekaye ukimtekenya, sikushauri umtekenye ilikujaribu kumpoza au kumuondolea maumivu ya kichwa au msiba.

Na kuna wakati kama hutaki kushindwa, ni afadhali usimpe kauli ya kutaka mkacheze MCHEZO wa BABA na MAMA au wa KUIBA yule atokaye MSIKITINI au KANISANI, wakati utaalamu wako wa kauli unashindana na wa PADRI au SHEKHE, ambaye ashamuingiza akilini umlengaye, mahusiano ya tamaa zako mbaya za kibinadamu na DHAMBI au AHERA.



LAkini.....
.....Nafikiri pamoja na udhaifu wa binadamu, ni rahisi kugundua kuwa ukirudiarudia mara nyingi kitendo kwa kutumia njia ujuayo ni sahihi, unaweza kujikuta UMEPATA kazi uitakayo, umepata MIMBA au umefanikiwa kufanya kitendo sahihi ndani ya muda sahihi na kweli jiwe ulilorusha jikoni kwa mtu , limempiga BABA mwenye nyumba aliyekwenda kuonja mboga kisiri jikoni wakati MAMAA anasukwa nywele kibarazani.

Naamini kama tunajitahidi kufukuzia kitu, sekunde ijayo inaweza ikaoanisha kitendo sahihi , mahali sahihi na muda sahihi na kutuwezesha kufanikiwa lile jambo au kufa.

AU?
DUH!
Samahani niko tu MAWAZONI kidogo!
NAACHA basi!

Mpate LUPE FIASCO katika FIGHTERS


AUtwende tu na PEPE KALLE kumtafuta kipenzi HIDAYA

Read more...

Napenda WANAWAKE!Samahani kwa udhaifu!:

>> Sunday, May 11, 2008

HAPI MAZAsDEI!
Ingekuwa ni chaguo langu, kila siku ingekuwa ni siku ya KUMSHUKURU MAMA!


Pamoja na matatizo ya mama wa kambo na mama aliyemtupa mtoto jalalani,au kumuacha tu pale hospitali au sehemu sehemu,NAWEzakukiri kuwa asiyekiri kuwa mama KIBOKO, kwangu yeye SI KIBOKO.
MIMI MDHAIFU!

Kwangu MAMA KIBOKO!

Lakini.....
Nashangaa kuwa kwa watu fulani hasa waitwao wanaume, waweza kumuelewa binadamu aliyezaliwa kutoka kwa mwanamke , kumdharau mwanamke,hata kama wameshuhudia au wameliangalia dume zima likililia mwanamke.

Mwanamke , dada, msichana au tu wewe MWANAMKE mwenye mtoto;HESHIMA YAKO!

HERI ya SIKU ya MAMA!

Pata wimbo maalumu KWA MAMA...


NI vigumu kuutoka mkao wa kumshukuru MAMA.

Lakini pata baadhi ya picha zangu kadhaa na wadau bila kusahau ISRAEL VIBRATION walionisaidia kuipitisha wiki ile ilioisha ijumaa hii.



Photobucket
Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket




Au wasikilize tu ISRAEL VIBRATION kiduchu...

Read more...

KATIKA mwendo WA MARINGO, kuna WATIKISAO matako!

>> Friday, May 09, 2008

Anayeringa MJANJA!

ANAYERINGA , amekuzidi kwa kufanikiwa KUJIDANGANYA kuwa, kuna kitu amekuzidi.

Ukitaka kujua kuwa anayeringa ni mtundu, fikiria yote uyajuayo tokea uzaliwe kuhusu binadamu, yakuhakikishiavyo kuwa, hakuna binadamu asiye na kasoro, na jinsi gani akufungaye katika mchezo wa karata, uwezavyo kumshinda katika mchezo wa kuruka kamba au kumshinda kwa ulafi.


DUH!
Sitanii!

Binadamu katika ujazo , wote ni sawasawa, kutokana na mapungufu yao na waliyobarikiwa ambayo hutofautiana kutoka mtu mmoja mpaka binadamu mwingine.
Swali:

  • Ushawahi kufananisha vitendo vya anayeringa na yule binadamu watu wamuitaye TAAHIRA?
  • Unauhakika na vigezo vyako vikuhakikishiavyo kuwa binadamu huyuhuyu aendaye msalani kama wewe , anakuringia?

Lakini....
... anayetembea kwa maringo , hukimbia kama mimi na wewe tu , kipepe kasingiziwa, ukimsakizia MBWA.

Lakini....
......Unauhakika huringi?

Nisikufiche!
Sidharau waringao ingawa siwaelewi.
Nahisi kuna kitu wanapata ndio maana wanaringa.

AU?

Lakini...

..Mringaji ndio atumiaye nguvu na achoshaye ubongo katika kujiandaa na kufanikisha kukuringia.

Anayeringiwa ana bahati!
Anaweza akaamua kutomwangalia anayeringa na kupumzisha macho na kidubwana wengine wakiitacho ROHO.

Swali:
  • Kama unanyanyasika kwa kuringiwa , unafikiri AKUringiaye alitarajia nini?

DUH!
NAACHA!
WIKIENDI NJEMA!

Twende GABON utulie na OLIVER Ng'oma akija na Muetse

Au mpate tu Yasmine JET akija na Detachement

Read more...

SAMAHANI, nakojoa!Si ni KITENDO tu cha Kibinadamu?

Si siri!

Binadamu huridhika kufanya kitendo kwa muda fulani mfupi tu.
Ukimzidishia muda katika kitendo, anaweza kukiita kitendo ADHABU.

Swali:

  • Unakumbuka kitendo binadamu ajinomacho, kama kula maparachichi, mafenesi, migagi au kukuna kipele, ukikiongezea urefu wa muda, BINADAMU anaweza kusema; utamu wake umeyeyuka au kugeuka na akaugawia jina ;UCHUNGU?
  • Unafikiri ni muda gani kitendo chako cha kujua na kufaulu mtihani kinadumu KABLA HUJAHITAJI tena kufanya kitendo cha kujisomea na KIJIFUNZA upya, iliubakie na sifa ya kuwa;WEWE UNAJUA?


Vitendo vya kibinadamu NISHAI!

Hata kama huvipendi , unawezalazimika kuvirudiarudia tu ili uishi au uendelee kuwa MJUAJI:-(

Hata kama umekula sasa hivi, lazima tu itabidi ule tena baadaye au kesho, kwa sababu ya njaa ikupendavyo na kutokukuachia uingie uvivu wa matumizi ya baadhi ya MATUNDu ya mwili yakufanikishiayo hata KUCHIMBA mzizi.

SIna uhakika!

Lakini...,
......
nahisi nataka kujaribu kuongelea vitendo binadamu afanyavyo duniani hapa,
kwa kutumia mfano wa kitendo binadamu afanyiacho mazoezi kila siku, ingawa bado siku mojamoja anaweza bado kujisaidia pembeni kidogo ya tundu la kidaka haja , KWA BAHATI mbaya.

Sasaaa....
......Kukojoa ni moja ya vitendo mamilioni , VIFUPI, binadamu afanyavyo na awezavyo kudai amemaliza au kabla hajamaliza akakujibu kutoka chumba cha kujisitiri kuwa ;ANAKUJA sasa HIVI!


NArudiA....
....Tatizo la vitendo afanyavyo binadamu, ni ulazimikaji wake wa kuvirudiarudia kabla hajafika kwenye
ZE KABURI.

Lakini......
......Tatizo au uzuri wa binadamu, .....

.....ni jinsi anavyoweza kushindwa kustukia kuwa kitendo hicho hicho cha KULA UGALI , anakifanya tofauti kila akirudiapo na kuwa, utamu wa ugali huohuo aulao ,unatofautiana ladha katika tamutamu ya TONGE la kwanza na TONGE alibwialo akishashiba.

Tatizo mojawapo la ubinadamu , .....
......ni ugumu wake kwetu sisi bin-ADAMU, kukubaliana naye MTU, kuwa amemaliza kitendo na HAWEZI kufanya ZAIDI, hasa tukikumbuka kuwa INGAWa KITENDO kimefaNYIKA, baada ya muda fulani mfupi ; nyumba itabidi kupakwa tena rangi, na labda itabidi MTU arudi tu tena jikoni, ilikujihakikishia uwezekano wa kurudi msalani.

DUH!

Lakini haishangazi,.....
.... mjanja anaweza kutamba kuwa ashafanya yote na kumaliza, kama atafumbia macho ufupi wa maisha ya kitendo kilichofanyika.

Na...
....Labda ni kweli vitendo hufanya zaidi ya maneno.
SI ndio maana kunawapatao UKIMWI au mimba kutokana na kitendo?

Swali:
  • Unamjua binadamu yoyote aliyemaliza kutenda ?
  • Hudhani kuwa kitendo binaadamu akifanyacho na kukimalizia vizuri ni kitendo cha kufa kwake mwenyewe?
Kabla sijaendelea kukunong'oneza.......

Samahani kwa kutamka neno KUKOJOA hadharani , hasa kama neno kukojoa linakukumbusha aina maradufu za KUKOJOA!

DUH!

Nakukubalia kuwa kuna vitendo ambavyo si lazima uvitamke au umwambie mtu kuwa unafanya au ulifanya KWA sauti.

Lakini.......
... uzuri au ubaya wa kitendo chochote afanyacho binadamu, ni ufupi wake katika kipimo cha muda ambacho binadamu anaweza kukiri ladha ya utamu wake.
Unaweza kubisha...
.......lakini binadamu hachukui muda mrefu kukinaishwa na kitu , kufa au kufanya kitendo kiwezacho kumjaza mimba asiyeficha maeneo.(Samahani kwa lugha chafu, namaanisha , asiyeficha sehemu nyeti au za siri)


Katika swala la vitendo sisi binadamu tufanyavyo....
...ingefurahisha kama ingewezekana kuwa ; kama umetubu leo au umeomba masamaha jana, maana yake hutamkosea tena yule kidume, kidosho, MWENYEZI Mungu, au yule binadamu,katika vitendo au mnong'ono, kesho.

....ingefurahisha; kama ingewezekana binadamu kumaliza ulichoanza kabla ya kulala , hasa kutokana na kutokuwa na uhakika na uwezo wa binadamu wa kufanya kitendo cha kuamka, baada ya kulala.

Swali:
  • Unafikiri YESU , Mtume Mohamedi, au Muheshimiwa DItopile walimaliza?
  • Kwa nini ukianza kitendo unafikiri ni lazima umalizie?
Samahani kama nakukwaza au unafikiri nakufuru!

Lakini...
...Labda kuna kitendo umeanza au ulianza , ambacho inabidi umalizie kibinadamu au inabidi ufanye tu!

Fanya tu basi hicho kitendo!
Inawezekana MARA hii kitendo chako kikalipa OOHOO!
Nakutakia kila la kheri!

Naacha HII topiki nisije nikamalizia kitendo bure halafu ukadharau ubinadamu wangu!

Kabla sijakuacha, hebu tuangalie kitendo cha binadamu ambacho wengi wangependa kukifanya KWA SIRI.Namaanisha kitendo cha KUJAMBA, ambacho unaweza kushangaa kushuhudia kuwa kinawachekesha binadamu kadhaa kiduchu, kama sio mimi na wewe!

Unajua, labda umeangalia kitendo cha kiJINGA?

Tumuachie tu BOB Marley atukumbushe hali halisi katika wimbo CONCRETE JUNGLE

Read more...

UTUuzuri WAKO , labda ni WOGA!

>> Wednesday, May 07, 2008

Hakuna uhakika akufanyiaye mazuri , anakufanyia mazuri kwa sababu anafurahia kukufanyia mazuri.

Lakini...
...yule mtu mzuri amepata umaarufu huo kwako na kwa jamii yako kutokana na tafsiri yako na ya jamii katika kutathmini aliyofanya hata zaidi ya ambayo hajafanya.

Inawezekana kabisa hata mimi na wewe tunafanya mazuri kwa sababu tunaogopa matokeo ya kumfanyia mtu mabaya.

Swali:

  • Ungekuwa una uhakika na kesho , kesho kutwa yako,mtondogoo au ....., una uhakika hakuna ambaye ungempiga konzi ?
  • Unauhakika unapima uzito wa UTU UZURi wa mtu zaidi kwa aliyokufanyia au asiyokufanyia ambayo ndio msaada?

Unaweza kubisha!

Lakini wapo wengi wanaogopa kukufanyia mabaya kwa kuogopa maswala ya wakishadedi.
Wangekuwa na uhakika na nanihii za baada ya kifo labda wangesha kubaka!:-(

DUH!
Naacha!
Siku njema!
Tulia na Sade akija na Smooth Operator (Jazz version)

Read more...

UDONGO uukanyagao Inawezekana ni MABAKI ya MAITI ya mtu au HAYATI Mjusi !

Kwa wengine ni mwiko kucheza makaburini !

Lakini...
.......binadamu wengine wanafanya pikiniki makaburini.
Swali:

  • Makaburini ni wapi?

Binadamu bingwa wa kuoanisha mboga za majani na chakula ,lakini sio mabingwa wakuoanisha kabichi au maharage na mavi ya kuku, mavi ya ng'ombe au mbolea fulani ambazo hunukia manukato ya choo.

Ukifikiria kidogo, utagundua kuwa MAJI YOyoTE utumiayo ni maji ambayo inawezekana yalishawahi kuwa mkojo wa tembo, mcheuo wa bata , kamasi la nguruwe au pia jasho la mmea kama unafualilia MZUNGUKO wa MAJI (water cycle)hapa duniani.

Kwa mtazamo mwingine, maji yoyote utumiayo, ni machafu!

Nampenda binadamu kwa uwezo wake wa kufumbia macho baadhi ya mambo na kuyatolea macho yale mengine kwa visingizio vya ajabu kama vile dini,utu au hata elimu.
Ukweli ni kwamba uyatoleayo macho ni kwasababu unaweza tu kuyatolea macho.
AU?

Kuna watu wana uhakika kuwa binadamu asipoelewa kitu atamsingizia Mungu au Miungu, lakini mimi nadhani mara nyingi binadamu asipoelewa kitu hulifungia macho na masikio hilo LIKITU.

Swali:
  • Unajua ukibanwa sana na kiu utakunywa mkojo?

Nafurahia mitazamo ya binadamu!
Maiti ya mbuzi , anaweza kuisifia kuwa ni bomba la Ndafu lakini hayati mjusi anaweza asimuite mshikaki.
Si vyakula vingine tunajifunza kuviondoa sumu au uchungu lakini tunaweza kutamka neno TAMU tukizungumzia bia na chai?

DUH!

Tafsiri za binadamu ni ngumu kuzielewa kutokana na ubinamu wake unavyocheza zigzag.

Chura, konokono, mbwa na popo , binadamu mwingine atasifia ni chakula kizuri, wakati binadamu mwingine atakushangaa ukila nyama ya ng'ombe, nguruwe au matako ya sungura.

Binadamu fulani ataamini kuwa binadamu wote ni watoto wa Adamu na Hawa ,lakini ataku-Saddam Hussein au kukuKOLIMBA ukimstua kuwa kaoa dada yake au kamchumbia kaka yake kinamna.

Swali:
  • Hivi kama binadamu wote ni ndugu, unashangaa nini ukisikia kuna vita duniani?
  • Kwani hujawahi kukorofishana na ndugu yako?

Binadamu eeh!

Najua wewe binadamu unajua kuwa tokea binadamu aanze kuwepo hapa duniani kuna kaburi fulani la Adamu na Hawa halijulikani lilipo.

Na nafikiri unajua ni virutubisho gani viko mwilini mwa mwili wa binadamu ambavyo mimea na samaki huvigida.

Usifikiri nakutukana......
....... nikijaribu kuhisi kuwa kuna uwezekano kuwa binadamu wote washakula Watu.

Usifikiri nakutukana .......
.......nikijaribu kuhisi inawezekana nyumba yako imejengwa kwa kutumia mabaki ya maiti za watu na chakula ulacho kinaweza kikawa na chembe chembe za Adamu na Hawa.


Lakini....
Hakuna noma!
Najua ni ujanja kuogopa MAITI!

Labda mimi na wewe ni binadamu tu, ndio maana mimi mwenzio nikiona mchele nafikiria maswala ya ubwabwa .

DUH!
Kwangu fikira za ubwabwa ni ubwabwa tu .
Tofauti za ubwabwa ni maswala ya ubwabwa unaulia nyumbani, msibani au ni Darling ,kishtobe au zee la nyeti limepika.

DUH!
Naacha!

Hebu tuangalie mapenzi ya BABA na MWANA kidogo....


Mpate Neneh Cherry akupe kibao WOMAN

Read more...

Kwa mara nyingine, ASANTENI WADAU!

Sitachoka kushukuru kwa wote na yote !

Katika dunia hii kichaa, unaweza kuwehuka kama hauna timu ya watu ambao wanakupatafu kimawazo ,kikukushusha presha au hata kukubadili tu mawazo kwa kukuelimisha au kukupa jinsi mpya ya ya madoido ya kufuatilia madoido yaletayo ugali mezani, na labda kukufikisha mbinguni.

AU niseme....


Narudia!
Asanteni ndugu ,jamaa, marafiki na maadui!

Nilifanikiwa kudaka picha mchanganyiko kidogo za baadhi ya marafiki walonipa tafu hivi karibuni....


Tulia na hiki kibao basi.....

Read more...

MATANGAZO kiduchu!

>> Monday, May 05, 2008

1.AFRICAN NIGHT -HELSINKI


PLACE: Ravintola Kaisaniemi(Kaisaniementie 6, Helsinki)

DATE: Saturday 10.05.08

Entrance:10Euro + 2Euro Coat check

Stori zaidi: www.africannight.org




















2.Majaji tuzo za Vinara wameanza kazi !


Na Mwandishi Wetu

Jopo la majaji wa Tuzo za Vinara wa filamu nchini (Vinara Film Award) leo Jumamosi ya Mei 3, 2008 linatarajiwa kuanza rasmi kazi ya kuziangalia filamu za Kitanzania zinazowania tuzo hizo kabla ya kuzitolea maamuzi.

Mratibu wa One Game Promotion inayoaandaa utolewaji wa tuzo hizo, Khadija Khalili amesema kuwa, majaji hao watatanguliwa na semina ya siku moja kabla ya kuanza zoezi la kuziangalia filamu hizo chini ya usimamizi wa maafisa wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Jopo hilo linaloundwa na wataalamu wa mambo ya filamu nchini wanakutana leo katika hoteli ya Regency ya Mikocheni jijini Dar es Salaam na kuendelea na kazi hiyo kwa siku kadhaa kabla ya kuibuka na majina ya filamu na wasanii walioingia katika makundi ya kuwania tuzo hizo.

"Kikubwa ni kwamba jopo la majaji linategemea kukutana Jumamosi ya Mei 3 (leo) katika hoteli ya Regency Mikocheni kwa ajili ya semina na kuanza kazi ya kuzipitia filamu zilizowasilishwa kwa ajili ya kuwania tuzo za Vinara," alisema Khalili.

Vipengele vinavyoangaliwa ni Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Muongozaji Sinema Bora wa Mwaka, Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu na Mtunzi Bora wa Filamu.

Vingine ni Filamu Bora ya Kutisha, Muigizaji Mwandamizi Bora wa kike), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kiume, Adui Bora kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa Filamu ambao wote watapata tuzo. Pia itatolewa tuzo ya heshima kwa wale waliotoa mchango wao kukuza sanaa nchini.

Wiki iliyopita, Khalili alisema kuwa, zaidi ya filamu sabini zimeingizwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo hizo.

Filamu zinazowania tuzo hizo ni zile zilizokamilika kutengenezwa Januari 2007 mpaka Machi 31, 2008.

Tuzo hizo zitakazotolewa Mei 30, zimedhaminiwa na Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia ya Ndovu Special Malt, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Global Publishers.

-----------Mwisho Wa Matangazo--------------------------------------------------

Kama unamuda, pata baadhi ya salamu kutoka MAREKANI....

Read more...

NAOMBA UFUNGUO wa MOYO wako ili UJIDANGANYE kuwa sitaUMIZA roho YAKO.

>> Sunday, May 04, 2008

Unaporuhusu mtu akujue, unampa huyo mtu ufunguo wa kiboksi cha UJUZI wa wewe ni nani.

Akujuaye halafu atake kukuumiza, huwa habahatishi madoido au staili ya kukutomasa kidonda.
Akujuaye ndio anaweza akawa anajua mpaka staili yako ya kulia, kupiga mayowe au hata ya kulamba kamasi lilengalo mdomo ukilia.

Lakini...
.. ni vigumu kukiri kuwa kama ufurahiavyo kumuona achekaye, kuna wachekeshwao na muonekano wako wa sura wakati unalia.
SI unajua unaweza ukawa unakunja sura kama unanusa kimavimavi wakati unalia?

DUH!

Kama watu waogopavyo ngurumo ya radi wakati wanajua ukisikia ngurumo maana yake radi imekukosa, ndio wengine wahudhunikavyo kumuona anayelia bila kugundua kuwa tatizo ni kile kimlizacho mliaji na sio aliavyo.

Kulia humsababisha mliaji asikie ahueni.
AU?

Tatizo ni kwamba, binadamu hapendi upweke kama anaishi maisha ya kawaida ya kibinadamu.
Utajikuta umelazimika kumpa mtu fulani funguo ya moyo wako ili achokonoe roho yako.

Nakutakia kila la kheri katika kusubiria uliempa ufunguo wa kiboksi cha ujuzi wa WEWE NANI afanye ubinadamu na kukuumiza kiduchu kabla haja pulizia.
Ndio maisha!
Kwani bila maumivu tungejua utamu ni nini?

Kwa kherini kiduchu wadau wa blogu hii!
Tutaonana tena kijiweni baada ya siku kadhaa wa kadhaa!
Nakuacha na Patrice akupe EVERYDAY GOOD

Au ngojea tu aseme HOW DO U CALL IT

Read more...

SIKUPENDI kwa sababu WEWE MZURI!

Msichana mzuri kumzidi Khadija, inaweza ikawa ndio sababu ya Khadija kumchukia Zubeda.
Kuna wengi ambao watakubali kuwa......
....... akisifika kwa mazuri kuliko wewe, na kama huoni hata jinsi yakukaribia mafanikio yake, anaweza akawa TISHIO KWAKO na sio faraja.

Kuna ambao watakubali kuwa.....
.....Uzuri wa unayefikiri mko sawa au umemzidi kakitu, ni jinsi asivyokutishia maisha na kukufanya ujihami na kujikuta unaanza kupiga mswaki, kuchana nywele, kubadilisha chupi au kuficha kile kitu uvunguni kabla hajatokea.

Kuna wengi ambao ukifanana fanana nao wanaweza kukualika kirahisi UGAli ukiiva bila kujali njegere hazina vitunguu.

Lakini....
....Tajiri na masikini ingawa wote ni watu wazuri , wanaweza kujisikia huru zaidi kula mbatata katika sebule au hoteli tofauti.
DUH!

Kuna watu husahau kuwa hata pendo huweza kuwa ni maumivu kwa umpendaye.
Kuna watu wanaweza wakawa hawakupendi kwa vitndo vyao wafanyavyo kwa mapenzi yao ya dhati.

Swali:

  • Hujawahi kumzimia mtu mpaka ukashindwa hata kuongeanaye akikuchekea?
  • Hujawahi kustukia karoho ka-kwanini yule na sio mimi baada ya kushuhudia na kuhisi labda yule umpendaye kila kitu utakacho kununua yeye anapewa bure?

Kumbuka tu kwamba kipimo cha nani mzuri kubwa kuliko akilini mwako na katika jamii yako hutokana na mlivyoathirika kisaikolojia.

Kumbuka.....
..... Mungu inawezekana ni mzuri kwako, lakini ni mbaya kwa jamii ya KISHETANI.
......Demokrasi ni nzuri kwa viongozi wa Marekani wenye pesa za kugombea Uraisi, lakini Ukomunisti mzuri kwa viongozi wa China.

......Wali mzuri kwa watu fulani, lakini wengine hawashibi bila ugali.


Lakini...
....Kuna mtu anaweza kukupenda kwa sababu ya ubaya wako ambao unaweza ukawa unafaida zaidi kuliko uzuri wako kama mabepari walivyostukia.
Swali:
  • Unakumbuka asilimia kubwa ya uvionavyo katika maduka fulani, viko dukani kujaribu kukukumbusha kuwa HUJAPENDEZA na wewe MBAYA ili ununue mafuta ya mgando,chupi fulani au raizoni ?
DUH!
Naacha topiki hii!
Mpate Mighty Shadow akupe kibao WHATS WRONG WITH ME


Au tulia na Arrow wakikupa HOT HOT HOT

Read more...

WAKATI unamkana NDUGU yako aliyedakwa UCHAWI.

Kukana kitu ni jitihada za kutaka kuhakikishia wengine kuwa huhusiki kwa sababu kwa kisiri na kama wewe ni mkweli kwa wewe, ulichofanya kisha kuathiri na hata ukaneje ushaathirika nacho.

Ukishaonja ukwaju , unaweza kushindwa kuelezea tofauti ya utamu wake na embe bolibo, lakini hata ukane kwa wengine hujui utamu wa ukwaju, unajua chini ya dhamira yako kuwa ukwaju na asali vinautamu tofauti.

Nikikuudhi au kukutia aibu, unaweza kukana uhusiano wetu , undugu wetu , hata kama watu wanauhakika mimi fundi koroboi wako.

Nikisifika, unaweza kusimulia mpaka jinsi babu yako mzaa babu na shangazi ya babu yangu walivyokuwa marafiki shule ya vidudu, ilikuonyesha ukaribu wako kwangu.

DUH!

Lakini....
......Hata ukikana, UKWELI uko palepale.

Gari la zamani hata ulipake rangi bado ni baiskeli ya zamani.

Kukana inawezekana , na watu wanaweza wasijue ukweli kwa muda fulani kwa sababu binadamu ni mvivu wa kufuatilia ahisiyo ugumu na ambayo hayamsaidii kupata utamu HATA AKIJUA sasa hivi.

Unaweza ukawa unataka kujua kivipi BALOZI wa NYUMBA kumi kumi wako katajirika haraka haraka alipochukua ofisi kwa sababu zako binafsi za kuhisi KUTAJIRIKA KWAKE ni KUNYONYWA au kuibiwa kwako, la sivyo inawezekana usingejali kwanini ghafla tu, RAIS wako MTUKUFU kawa bilionea wakati nchi ina madeni.

LAkini....
.....jina lako likiwa linatajwa mara kwa mara likihusianishwa na uchawi, MCHAWI au Mama Ntilie, kuna watu kutokana na uvivu wa kufuatilia na urahisi wa kuhitimisha , watakua wanadhani wana uhakika kuwa wewe mchawi, ulilogwa au ni MAMA NTILIE.

Mchezo wakuhitimisha bila ya kuwa na vigezo vithibitishavyo nani alimpa kuku mimba lililo rutubisha yai la kwanza, ningependa libakie tu katika sentensi; kati ya yai na kuku sijui nini kilitangulia kuwepo duniani.

NAKUBALI unaweza kudai ni yai lilitangulia bila ushahidi zaidi ya kwamba katika kundi wewe ndio UNASAUTI KUBWA na wengine wameathiriwa na jamii kiasi kwamba katika mambo mengi kiduchu ya jamii, WAMEFIKIA kukubali tu kutokana na kutojiamini kama wewe ujiaminivyo katika hata mambo usiyojua.

NAKUBALI unaweza kukana!
Kana tu, hakuna noma!
Swali:

  • Ushawahi kukana wewe sio wewe?
  • Unajua unaweza kukana kile kitu lakini ukaendelea kuona aibu kutokana na kitu hicho hicho ulichokuwa shupavu kukana?

Usisahau kuwa, mara nyingi unakana kutokana na kujihami kuwa ukikubali utajiweka katika mazingira mabaya zaidi.

Usisahau kuwa, hata usiyo yaelewa lakini ukahisi ukikubali utaenda paradiso, hukawii kukiri kuwa wewe Msabato au MUNGIKI.


Naacha basi topiki hii usije ukanikana bure!
Samahani lakini kwa kukutia aibu!

LAkini....
WHO wrote the BIBLE pt1?(msikilize basi Robert Beckford)


Kuna mdau kanistua kuwa nagusia sana dini .Napenda kukiri naguswa sana na dini na ni mifumo yake tu inayonizingua....
Lakini nasikiliza ya ulimwengu tu kama ya Timbaland na Magoo wakikiri INGAWA hawamuelewi......(samahani wanatumia lugha chafu!)

Read more...

KUKATA TAMAA ni UJANJA

>> Saturday, May 03, 2008

Kuna atakaye sema kukata TAMAA ni kitu kibaya!

Lakini...
...ukikata tamaa, utajipa nafasi kuwa HURU kujitoa katika MNASO.
Kukata tamaa ni SANAA kali, si kila MTU ni stadi katika kukata tamaa kinadhifu katika swala ambalo anahisi kukata tamaa na KUCHEKESHA ni saresare maua.

Ukikata tamaa, unaweza kujikuta umeacha kuhangaikia kitu.

Ukikata tamaa , unaweza kuacha kuchamba kwa sababu tishu, maji, mchanga, majani au jiwe utumialo kama MAKOKONEO pale msalani ,vinakosa umuhimu sana kwako kutokana na mnuko wa mvundo wa chooni na MANUKATO ya UTULI, hukosa tofauti kubwa.

Ukiweza kuishi UKIWA na MATUMAINI wakati unaweza kufanya afanyacho aliyekata TAMAA, wewe unaFURAHA maishani na jirani hakutishi.

Swali:

  • Unakumbuka kama ushawahi kutamani inawezekana huhesabu tu ni mara ngapi ulikata tamaa?
  • Unajua inawezekana kuwa kama tamaa zote si mbaya basi kukata tamaa kwingine ndio ushindi?
Naamini kuna ngazi za kukata TAMAA.
Wewe kama ni mtu wa dini lakini umefikia kwenda kwa mganga wa kienyeji kutafuta dawa ya MKUYATI, basi kuna maeneo unahisi kuna MATUMAINI na umekatia tamaa dini lakini bado unatafuta kuendeleza TAMAA ya KITU na sio KUIKATA.


NAAMINi....
...kila kitu kinaMPITO!
Kama unasikia UTAMU sasa hivi, USIKATE tamaa, UCHUNGU uko kwenye kona , utakudaka tu hata kama sio leo.

Kama uko kwenye MACHUNGU leo hii, kumbuka UTAMU ni kifo.Utakudaka tu, hata kama sio leo.
USIKATE TAMAA!

Swali:
  • Hivi inawezekana kuna UTAMU kwenye UCHUNGU?

Basi bwana NAACHA!
WIKIENDI NJEMA!
Nakuacha na KY-MANI MARLEY akikupa kibao COUNTRY JOURNEY

Read more...

KUPAMBA maumivu kwa KUKIRI!

Ukikiri, unatua MZIGO wa siri na UNAANZA kutibu ugonjwa wa nyuma YA KWANINI.
Nyuma ya Kwanini kuna ile kitu yenye jina fulani lakini inawakilisha NINI kimefanyika au hakikutendeka.

DUH!

Watu hupenda kusikia kutoka kwako mwenyewe umekiri walichosikia kuwa UMETENDA.
Kusikia kutoka kwa mwingine ni CHAKULA kisichoungwa, kuna ladha fulani MTU fulani anaweza kuhisi chai imekosa chumvi .

Lakini....
...IKIWEZEKANA ,usikiri JAMBO kama unaweza.

UKikiri , unawaondolea watu fulani faida za kubunia jambo(benefit of the doubt).

Ukikiri inasemekana kuwa unatatua jambo, ingawa inawezekana unasambaza maumivu kwa mwingine kama sio wengine kwa kuwasababisha kuishi wakijua ni kweli ulijinyea kwenye harusi ya jirani.

Binadamu anajaribu sana kuondoa kero maishani mwake na ni rahisi mtu kujisahau kuwa hata ufanyeje, wewe kama binadamu, basi wewe si malaika na kwahiyo utakereka tu sehemu fulani ingawa hutaki.

Kukiri ni moja ya njia tu binadamu hujaribu kutumia kukwepa KERO moja kabla hajadakwa na KERO jingine kwa sababu umekiri.

NIsikutishe, KIRI tu kama unapata AUHENI.
Swali:

  • Ushastukia kila siku kuna kitu unakiri hadharani ila huiti kitendo;KUKIRI?
  • Unafikiri ukikiri, UNATATUA au unabadili mchezo na kukabiliana na tatizo kwa kutumia kona nyingine?

Lakini....
......Ukifumaniwa unakula denda hata bila kukiri kuwa ulipata uroda, kuna watu watataka kujua na UKIRI kama ilikuwa chuma mboga au ulisomea umishenarini.

Lakini....
....watakao UKIRI hata wakijua, haikusaidii sana wala haiwasaidii sana kama unakumbuka dunia ilikuwepo tu kabla hujazaliwa na kufanya watakacho UKIRI .
Wanaodadisi jambo, hawataishiwa jambo la kufanya usipokiri kama bado wanataka kuwa katika uwezo wa kula na kunya(samahani, kwenda haja kubwa) kesho na kesho kutwa.

Basi bwana!
Kiri tu kama INATATUA!
Baadaye basi!


Pata tu swala kutoka kwa IMAM mtoto......akikuuliza DO YOU KNOW ALLAH?

Au pata tu Mahubiri kutoka kwa Mchungaji mtoto....


Au mshangae mpiga ngoma mtoto Kanisani......


AU msikilize tu MTOTO katika fani fulani za siku hizi.....

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP