Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KATIKA kumfuatilia MASIKINI inayedaiwa ANANOGEWA zaidi KUZAA!

>> Tuesday, May 13, 2008

Jasho laweza kukutoka wakati unajaribu kutetea utajiri wa TANZANIA katika macho na masikio yaonayo jinsi gani NCHI tajiri kama TANZANIA inavyoweza kuwa na watu maskini au kuitwa nchi MASIKINI ya dunia ya tatu.

Lakini...
....Yeyote awezaye kuona UTAJIRI ndani ya nchi iitwayo maskini na yenye maskini kama TANZANIA, ataweza kujua jinsi gani hata neno TAJIRI au MASIKINI liwezavyo kuwakilisha mtazamo tu fulani wa watu kutokana na jinsi tulivyofundishwa kuangalia mambo.

Lakini...
....Wengi huweza kukuapia kuwa wanajua kipimo cha utajiri na umasikini hapa duniani.

Na hata ukijifanya unatumia vipimo vya furaha au kuishi na uvitakavyo tu , bado unaweza kujikuta unachekesha katika jamii ambayo tokea unazaliwa inajaribu kukujenga kimawazo kufikiri walionavyo zaidi wamekuzidi ujanja.

Tatizo ni kwamba,.....
...... jamii ina staili ya kuangalia ulivyonavyo utake usitake, na hujaribu kukutafsiri kuwa wewe kiboko au panya.

Cha kusikitisha ni kwamba,.......
......ingawa umaarufu wa tajiri mara nyingi ni umaskini wake kama unachagua kumuangalia huyo tajiri bila kutishika na nyumba, magari au suruali yake ya kodrai, bado kwetu wengi tajiri ni mjanja hata akifa kwa BP au utajiri wake wa kifikira ukiwa ni KUBWA jinga.

Swali:

  • Hivi ni kweli MASIKINI huongoza kwa kuwa na watoto wengi?
  • Nani kasema MASIKINI wananogewa ZAIDI kujifungua ZE TOTOS?
Kati ya jambo nililoulizwa mara kadhaa hivi karibuni, ni kwanini masikini hawajifunzi kuwa ni ghali kuzaa watoto wengi.

Ukiacha CHINA ambako kisheria huruhusiwi kuwa na watoto wengi, utastukia nchi nyingi zilivyozidi kutajirika, ndivyo asilimia kubwa zaidi ya raia wake walivyopunguza namba ya watoto katika familia.

Kama unafikiria zaidi ughali wa kulea mtoto, unaweza kushangaa kwanini matajiri wawe na watoto wachache halafu masikini wawe na watoto wengi.
Swali:
  • Unafikiri maana na vigezo uitavyo ni utajiri , vingekuwa na tafsiri gani kama ungelelewa katika jamii ya ujanja ni kuwa na kidogo?
  • Unauhakika utajiri si jambo liishio mawazoni tu?
  • Kisaikolojia unafikiri ni mpaka uwe na walivyonavyo matajiri ilikupata ladha tamutamu ya tamu ya kuwanavyo?


Si mshauri masikini aige tajiri katika uvivu wa kuzaa!


KWANI Inasemekana ni rahisi zaidi kwa maskini kufa kuliko tajiri kukata roho katika mazingira ya dunia hii ya leo ambayo ujanja ni jinsi gani unaweza kununua madawa, kujilipia hospitalini au hata kuweza kujinunulia dagaa na mchicha .



Ila.....
...Tafsiri nzima ya utajiri , inaweza isiongee lugha moja ukimuuliza tajiri wa Kiafrika afuataye UAFRIKA ndani ya AFRIKA na tajiri wa KIJERUMANI, afuataye UINGEREZA aishiye ndani ya MAREKANI kuwa ;UTAJIRI ni nini?

DUH!

NACHOJUA......
Umasikini noma!Hasa kutokana na kumaanisha masikini ni mtu anayeshindwa kupata atakacho.

LAkini......
Swali:
  • Tajiri umjuaye unafikiri anapata vyote atakavyo?
  • Unauhakika kama huvifikirii sana ulivyokosa; wewe si tajiri?
DUH!

UFIKIRIAYE ni masikini , si lazima kuwa kweli ni masikini, kama utajiri kwako ni jinsi mtu alivyojilimbikizia asivyohitaji.

Halafu tukumbuke kuwa katika maswala ya vipimo, familia yenye watoto wawili ni wengi, kama walitaka kuwa na mtoto mmoja.

PIA....
...Pamoja na sifa zote mbaya za umasikini, kama ushawahi kumsikiliza Mother TERESA, watu husahau ukaribu wa masikini na MUNGU.

LAKINI kama ....
......kwa masikini watoto ni MTAJI , BIMA, TREKTA na hata UTAJIRI, kwanini wasizae sana?

BASI bwana topiki imenishinda!
Samahani hapa NAWAZA tu !

Hebu twende KENYA tukatembelee CRIB ya OMONDI....


Ngoja niache tusikilize utundu wa COURTNEY PINE akiwa na MANU DIBANGO katika midomo ya BATA na...au..... DUH! ..... LION OF AFRICA.

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 8:47 pm  

Hiyo crib ya Omondi lazima ifikishwe kule MTV...umasikini ni jambo la kujiwekea...usiporidhika wabaki masikini...ni hali ya kibinafsi...wacha wapiga hesabu!

Simon Kitururu 5:38 pm  

@Serina:Muhimu kujivunia ulichonacho.Crib ya Omondi na jinsi anavyoitambulisha lazima ugundue kuwa huwezi kumnyanyasa OMONDI.

Frankie 3:52 pm  

nitatafuta websaiti ya kiingereza ili niweze kusoma haraka. nimehamia http://jkuattalkshop.wordpress.com

Simon Kitururu 7:36 am  

@Frankie:Asante kwa kunifahamisha:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP