Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda AAMINIYE dini ya KIPEPE ,ni kutokana na ANUKUAVYO na KUKARII MISTARI badala ya kusoma HADITHI NZIMA!:-(

>> Wednesday, January 07, 2009

Chakushangaza ni kwamba, .......
.......MWENYE BUSARA na AKILI na mwenye dini,LABDA atakunukulia mpaka ZUBEDA SITA mstari wa NANE sura ya ishirini na kumi, Zubeda asemavyo; '''AKUCHEKEAYE ANATAKA'', katika kukushawishi katika JAMBO MUHIMU kuwa JAMAA LINAKUTAKA, kwa sababu kuna mstari huo kwenye kitabu cha NABII ZUBEDA aongeleacho hadithi ya jinsi FISI hawatakani.

Staili hii ya kunukuu mistari inatusaidia sana kuwa na Wakristo wenye makanisa bwelele, Waislamu wagombanao, Dini ya Mbuyu isiyoaminika,........... na hata BINTI MAIMUNA na KIJEBA kupata MDUDU.

Swali:

  • Unafikiri MTU WAKAWAIDA umjuaye ukimnukuu mstari kwa mstari, sentensi zake zote ni za KIJINGA na hazina busara za KIMBINGUNI?

Ndio!...,
....LABDA busara za aaminiye HADITHI za kwenye kitabu cha JUMA na ROZA, Biblia, Korani, au Bwiti, kwa wengi ni BUSARA iliyodakwa katika MISTARI iliyonukuliwa, SURA zilizo nukuliwa, MAFUNGU yaliyonukuliwa, kama sio kwa KIBABA au KILO zilizonukuliwa , NA SIO kwa FULU HADITHI hasa katika mahubiri au katika kujazia TU hoja ya MTAALAMU AKUSHINDE kama sio KUKUOKOA wewe au mimi mwana MPOTEVU.

Lakini....
...Hadithi ya KIPUMBAVU ya Simon Kitururu itakumbukwa kuwa yote ni ya kipumbavu tu hata kama kulikuwa na fungu la busara katikati ya hadithi lizungumzialo NYAMA YA BATA NI TAMU.

Na upumbavu wa Simon Kitururu utaeleweka NA KUKUBALIKA TU KUWA ni UPUMBAVU TU, kwa sababu yeye sio nabii na wala sio GURU wa Hare KRISHNA ingawa Simon asiye nabii, sheik ,au padre wa DINI YA ROHO YA KOROSHO na Manabii wenye uhusiano na MWENYEZI MUNGU ,wote wakila hunya.:-(

DUH!

NAACHA kuu!
Ngojea tu nikuache na: Simon Kitururu SITA ,sura YA ishirini na kumi, MSTARI WA SABA ,usemao;
''NAKUTAKIA KILA LA HERI WEWE Mwenye busara NA IMANI, na ni BINGWA wa KUNUKUU mistari bila KUJUA HADITHI NZIMA!''

Swali:

  • Si una IMANI?


Tupumzike kwa kuangalia trailer ya SINEMA ihusuyo mambo ya AKINA MAMA kujifungua katika Orgasmic CHILDbirth...[Usiangalie kama MTOTO, Mtoto kiakili, au utakwazika!:-(]



Au tu Aaron Neville anisaidie katika kusema...Tell it like IT IS..

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MARKUS MPANGALA 5:45 pm  

nikampatia ngumi ya jicho..halafu nikampiga kichwa meno matano yakang'oka, mdomo ukavuja damu. Nikamrushia ngumi kali sana akapotea nikaona hapa ni kama santuri ya kwaito ya MANDOZA ya Nkalakatha, si unajua navyosifia kwao, nami nasifia ngumi zangu ni za moto kama siyo cheche kama Lennox Lewis au Matumla. zinawasha kama upupu na zinafikirisha kama Falsafa za Kitururu AJABU eti hawaelewi, uwongo wao hawataki kufikiri mmmmm.
Topiki imenishinda. Lakini kweli mwanampotevu atajisfia kwa kumng'oa mwenzio meno? ana ngumi kali kama Lewis? Duh kumbe tuwe na IMANI hata ya kusadikishwa lahaula! NAWAZA TU JAMANI nami nitazaliwa kwenye zizi la ng'ombe halafu niwe maarufu kuliko OSAMA BIN LADEN.
MAWAZONI MWANAWANE

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP