....ingawa STORI NYINGI zaidi zitakazo kuwepo ni za kutungwa.:-(
NA ALIYEJUUakianguka CHINI KABISAA ambako ni chini zaidi ya ile CHINI KIDOGO,...
....kikubwa WALA SIO stori ZITAKUWEPO,...
.... bali ni jinsi gani ALIYEANGUKA anakubali kwa haraka KAANGUKA ili ajifute mavumbi kwa haraka na KUANZA UPYA HARAKA kabla hajageuzwa kuwa wa KILE KITENDO CHA KUANGUKA mtumwa.:-(
Swali:
Si ukianguka umeshaanguka na hata ufanyenini hauwezi kubadili ukweli kuwa umeanguka?
Na ukianguka kifuatiacho ni kuinuka tu?
Ndio,....
.....UKIANGUAKA stori zitakuwepo mpaka kwa wasiohusika,....
......lakini KIKUBWA kumbuka KUWA hizo ni stori tu na labda ni mpaka uziruhusu zikuingie MUKICHWA ndio zinaweza kukufanya ujisikie MPAKA kama umevaa chupi chafu halafu watu WASAFI wanajua siri YAKO ujaribuyo kuitunza kwa makini HIYO.:-(
NI WAZO TU hili MHESHIMIWA! SIKU NJEMA!
Hebu The Blackstones warudie kitu - Sentimental Reasons
Au tu BLACKSTONES warudie tu tena na ndude - SWEET FEELINGS
Labda ni tabia MBAYA kujisikia vibaya kwa kuwa tu humuelewi KHAMIS,...
....kwa kuwa kutomuelewa huko kwaweza kuwa ndiko KUSAIDIAKO kufarijika kwako wakati unamuelewa KADALA kirahisi.:-(
Na labda PIA hata kutokuuelewa kwako UHANISI,...
...ndiko kusaidiako mpaka FARAJA za kudhani kwa kuwa kuna viagra basi tatizo la bamia-nyama tepwetepwe si tatizo kwako kwa kuwa bila maringo LINATIBIKA kirahisi.:-(
Swali:
Lakini hufikirii kutomuelewa kwako MUNGU husaidia kutomuelewa kwako SHETANI?
SI kuna uwezekano UNANIELEWA hapa?
Ndio ,...
.... hata KUTONIELEWA KWAKO kunaweza kuwa NDIKO kunakusaidia sana kufarijika wakati UNAMUELEWA paka au hata tu BLOGU YA MTU mwingine.:-(
NIMEACHA!
Kumbuka ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
SIKU NJEMA MKUU!
Basi ngojea GREGORY ISAACS arudie -IF I don't HAVE U
Oliver Ngoma arudie ndude-Bane
Au tu Oliver Ngoma arudie tena mdinyo- Julie
Halafu sijui kwanini lakini ngojea tu na SEAL abandue kwa-Kiss From A Rose
[Tahadhari: Taralila hii inawazo lililokaa uchi!:-(]
ASEMAYE,...
...anaweza kuwa ASEMACHO ni kwa MTAZAMO wa waliomsemesha!:-(
Na kwa kuamini wakusemeshao unaweza mpaka kuamini wavuta bangi WOTE wamechanganyikiwa hata kabla huja kutana na mvuta bangi kama Barack Obama au Bob Marley na kusikiliza wakati wamevuta bangi wanaongea nini.:-(
Swali:
Si KUNA MWENYE UHAKIKA KWA KUSIKILIZA TU MTU KUWA mvuta bangi na asiyevuta bangi wanaguna tofauti wakati wanazini ingawa hajachunguza wasiovuta bangi wawili wanaweza wakawa wanagunia shughuli kitofauti wakati wanafanya shughuli KAMA WEWE ile ya mtindo kavukavu?
Na wamseshao mtu AKASIKILIZA kwa bahati mbaya ni wengi,...
..... na kwa kusikiliza tu watu unaweza mpaka KUSTUKIA NA kufikia hitimisho asemaye mtazamo wake ni kwamba NYAMA YA BATA NI TAMU ANAPATIA kuliko ya KUKU hata kabla hujamshikilia kiuno njiwa au hata huyo binamu ya KUKU ambaye ni njiwa.:-(
Swali:
Si wewe kama MUISLAMU hustukia mapungufu ya aongeaye KATIKA KUATHIRIWA ki MTAZAMO aongeacho kirahisi kinatoa siri umsikilizaye walio muathiri ni wakristo na KIMUATHIRICHO HATA KATIKA KUFIKIRIA kwa kutumia akili kuwa kwa nini kuingiza na kuchomoa BANANGENGE anakuita ni uzinzi kwakua fikira yake ya mzalisho imekaa KIKRISTO kama aliyemsikiliza kuwa MKE WA NNE DHAMBI ?
WEWE kama MSABATO si unastukia staili ya asemaye YESU kama huyo ni MROMANI KATOLIKI hata kabla hajamgusia BIKIRA MARIA aliye BIKIRA ambaye AMUITAYE BIKIRA Maria anakiri alimzaa kwa kugunia mzao kama kawaida YESU?
NDIO,....
....labda UNACHOSIKIA labda jaribu kumjua ANAYESEMA NI NANI kwa kuwa kama unasikiliza tu NAKUFUATA bila kujua asemaye,...
...unaweza kuchanganyikiwa bila sababu HATA ukinunua CHUPI isiyoruhusu KIPENGELE CHAKO KIPUMUE WAKATI KIMEBANWA NA KIFICHA NYETI kwa kuwa umsikilizaye katika stori za chupi anaweza kuwa ni yule ambaye HAJAWAHI KUVAA chupi mpya.:-(
Swali:
Unachosikia huwa unachunguza nani anasema hata asemaye AKISEMA hakuna ajenda ya siri katika hilo ASEMALO hata kama limeegemea kukufanya upende KAROTI ZAIDI wakati wewe ni mpenda MAPERA?
NIMEACHA
Usikonde lakini hasa kama weye ni miongoni mwa wamsikilizao POPE BENEDIKITI katika maswala ya husuyo ladha ya KONDOMU kuliko MALAYA aliye wahi kupata mpaka gono wakati anacheza na kivalishwacho kondomu!:-(
Tupate KWA KUBADILI USTAARABU angalau tukunyema kidogo ya UKIMWI kutoka kwa FRANCO akinyambulisha kiua nyege katika ndude-ATTENTION na SIDA
Au tu VYBZ KARTELna SPICE walainishe swala tena kwa mkito - RAMPING SHOP
[Tahadhari: Tararila ina wazo lililokaa vibaya!:-(]
Yasemekana PENZI halina mipaka,....
.... na ili penzi lako la MAANDAZI LIDUMU wakati kila siku unaona vitumbua na keki INADAIWA utumie juhudi za kushika breki usije tu kujikuta umerukia mpaka viazi vitamu kwa muonekano tu na ukavuka MPAKA.
Swali:
Hivi una uhakika kuwa kama wewe ni MPENDA VIAZI VITAMU kwa CHAI huwa mapenzi yako ya VIAZI VITAMU kwa chai yanashushwa makali kisa kwa adoado asubuhi nyingine unagida CHAI kwa maandazi au UJI wa mihogo kwa VITUMBUA?
Ngoja turudi kwenye hoja kuhusu huyu MDUDE aitwaye MDADA;......
Kwa kuwindwa MWANAMKE anajulikana,...
... ingawa kwa KUWINDA ni mahiri mpaka adakwaye anaweza katika mawindo anaweza kwa kutostukia ni yeye aikuwa anawindwa na wala hakua mwindaji ndilo laweza kujulikana.
Kwa VISASI mwanamke ni risasi,...
... na kwa bahati mbaya kwa kulipiza VISASI anaweza akawa mpaka ni BUNDUKI na RISASI.
Na kwa huruma yasemekana MWANAMKE anaweza kuzaa mpaka na mwenye UKOMA,...
... na kama weye ni fundi wa kutia huruma kwa huruma kuna MDADA anaweza mpaka kukupa mbele na nyuma wakati kwa huruma anakumegea UKOMA.
Swali:
Hivi kwa ujuavyo MDADA awindwavyo si unaweza kusahau MKAKA akipata mawindo kuwa katika mchezo huo kufanikiwa ni MDADA ndiye mara karibu zote huwa MARADONA?
Unathamini JUHUDI za mpenzi wako adaiye ni wako tu kubakia wako tu ?
NIMEACHA,... unajua ni PASAKA!
NA usitishike kwa wazo ligusialo MDADA zaidi ya NJEMBA hasa ukikumbuka hili ni WAZO TU MHESHIMIWA!:-(
AU?
Tubadilishwe wazo na NINA SIMONE katika -Young Gifted and Black
Nina Simone aingie ndani zaidi katika kuongelea ya roho katika-If U knew
Au tu NINA SIMONE alete pia ndude ambayo maneno yake hunitekenya sana tu katika- Ain't Got No...I've Got Life
DUNIANI kuna mengi ,...
....na hayo mengi kwa bahati MBAYA hutokea kona zote za DUNIA.
KWA Bahati mbaya MAMBO mengi ya AJABU kirahisi husakiziwa WAAFRIKA au AFRIKA siku hizi zidaiwazo zina mengi,...
.... lakini hali halisi inaonyesha kuwa YA AJABU yako DUNIA NZIMA na cha ajabu kwako chaweza kuwa ni kawaida mahali pengine SASA HIVI ingawa kuna kipindi LABDA yalikuwa ni kawaida HATA hapohapo ulipo katika upande huohuo wako wa DUNIA.
Swali:
Unabisha?
Ukikuta STORI ya ajabu kutoka NCHI ZIITWAZO ZIMEENDELEA inakuwa kama ni kitu cha ajabu ,...
.....na chaajabu ZAIDI ni kwamba ni wale watokao NCHI ZIITWAZO HAZIJAENDELEA ndio wanakuwa wa kwanza KUSHANGAA na kuona ajabu kuwa imekuwaje MFARANSA mstaarabu ndiye anakula KONOKONO halafu ananiona miye wa ajabu kwa kuwa nagida KUMBIKUMBI na kwa kuwa kwa mchoma mishikaki napenda kuagizia pumbu za mbuzi .[samahani katika neno pumbu nilikuwa natakutumia neno LA KIHESHIMA ; ``makende´´:-(]
Stori kama ya juzijuzi ya JINSI YA KUMUANDAA PAKA MTAMU ya mpishi maarufu wa KIITALIANO ilyosababisha sangambingo kwenye TV katika kipindi cha La Prova del Cuoco iliwakera WAITALIANO lakini katika wote nilioongea nao ,- watokeao KUNAKO BARA LA GIZA ndio nilishuhudia WAKITOA BONGE la mshangao zaidi kuwa hawa jamaa wanavyopenda Paka na MBWA kistaarabu sikutegemea kuwa walikuwa wanagida PAKA wala sio muda mrefu kwa kuwa bado kizazi cha wagida paka bado kipo- hasa kwa jinsi wajulikanavyo kwa kushangaa wengine wa pande nyingine za dunia wakati wanafaidi POPO wa kukaanga au tu pale mitaa ya CHINA paka huyohuyo akibanikwa poa.:-(
OK!
Stori ya HISTORIA ya kula PAKA ITALI sio lengo muhimu la taralila hii ya leo ingawa KAMA UMEINGIWA MDADI WA STORI ngojea niianzishie upya stori utamu ..
Basi MUTU MUKUBWA ndani ya MAPISHI ITALY kwa jina Beppe Bigazzi alikasirisha WAITALIANO kwa kutoa siri kuwa PAKA alikuwa KITOWEO MURUA TU Italy. Watu walikasirika kwa kuwa wanaona hilo ni jambo ni shai kwa zaidi ya mtu kujamba makusudi mbele za WASTAARABU.:-(
...au pata tu dondoo ya utamu wa NYAMA YA PAKA kwa maneno yake mwenyewe BEPPE BIGAZZI hasa kama umeshawahi kumdeku paka anakatiza halafu ukafikiria kwa maringo yake inaweza kuwa KUMGIDA NI sumu.
BEPPE anadai:
“I’ve eaten it myself and it’s a lot better than many other animals,” he told viewers. “Better than chicken, rabbit or pigeon.” He said that for optimum flavour the meat should be “soaked in spring water for three days” before being stewed.....
Ila kama nilivyosema LEO tujikumbushe BIASHARA ya MAITI UINGEREZA katika enzi za ma-BODY SNATCHERS
STORI yenyewe ni ...
Kuna kipindi kufukua maiti na kuziuza Uingereza ilikuwa bonge la ujasiriamali ......
AAAAHG! Hebu endelea mwenyewe HAPA na taralila ianzayo.....
``During the 17th and early 18th centuries, a grim profession emerged. A growing number of anatomists, keen to improve their medical knowledge, needed corpses on which to conduct dissections, which were often done in ‘theatres’, where members of the public could pay to watch............
Swali:
Si unakumbuka KUKUMBUKA idaiwapo AFRIKA hatuachi vita kuwa ULAYA , Asia ,...na mpaka AMERICAS wana historia ndefu sana na ILIYOANDIKWA ya vita vya wao kwa wao ambayo imefanikiwa kuua vya kutosha tu labda hata zaidi ya AFRIKA ambayo hata jiografia yenyewe ilikuwa inafanya iwevigumu siye WAPARE kuwakong'ota vizuri WACHAGA mitaa ya Kilimanjaro?:-(