Nipo zaidi BONGO!
>> Wednesday, April 07, 2010
Nachezea vipengele zaidi MOROGORO, Dar ES salaam , ARUSHA na NAIROBI!
Na kwa kuwa niko njiani sana UNAWEZA kunikosa kwa muda HAPA kijiweni.:-(
Lakini kama unataka kuninong'oneza kitu,....
...waweza kufanikisha kwa kutungua namba:
+255756295664
SIKU NJEMA MKUU!
11 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kila la kheri. Na uwe na wakati mzuri sana ila ingependeza kama ungeaga kabla hujaingia Bongo labda ungepata maagizo:-(
nakutafuta kwa udi na uvumba tufunge ndoa haraka tuishie zetu majuu....LOL, duh! bahati ya mtende hii jamani.......
Uje na dagaa wa kigoma wakati wa kurudi.
bado unakula ndezi???
Safari njema Mwanafalsafa Mtakatifu...
Ahaaaaaaaaaa.!!
Basi ingia "mawazoni" mwa wananchi kisha utueleze "namna waonavyo tatizo" lao maana wasipo-"vukani"ka kuna uwezekano wakafuata taswira ya uso (ambayo si mara zote huwa sahihi) watakaposhindwa kutambua kuwa "chakula kitamu na kichungu vyote vyaweza kumfanya mlaji akakunja uso". Utakuwa chachu ya "maisha na mafanikio" yao ukiwaeleza ukweli wa maisha na kuwawezesha "kujitamgua" na kufanya kazi na sio kung'ang'ania "kijiweni" kusiko na uzalishaji.
Pia ukirejea tueleze namna ambavyo "wavuti" zetu zatumika kuelimisha na kukomboa jamii za huko.
Kila la kheri Kaka
Tuonane NEXT IJAYO hapa hapa kwenye your "little world"
njoo Bukoba au Musoma pia
Nadhani sasa utakuwa wakati muafaka wa kutukutanisha wanablogu tuishio Bongo.
Mwananchi mimi nina hamu ya kukutana nawe ili tu jielewe na kuambizana kulikoni ughaibuni kabla hatujaambiwa karibuni nyasa.
Kila mtu na kipaji chake, kaka Mubelwa ndo fundi wa kuunganisha blogs zikaleta maana.
Mtakatifu, Askofu anaomba uhakikishe mnakutana ili wazo la kaka Bwaya lifanyiwe kazi.
Asanteni Wote!Na ntajaribu kufanyia kazi yote mliyodokezea!
Post a Comment