Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UMUHIMU wa kutokuwanacho KIDUDE!

>> Friday, August 13, 2010

Kama huna jiulize;...
.... HIVI wenye NAVYO wana nini  IKIWA  hulka ya BINADAMU hufanya wenye navyo kusahau au hata KUTOSTUKIA umuhimu wa walicho NACHO na hapo ni kama wanakumbuka  kidude WANACHO?

....HIVI hata  WENYE amani  maishani mwao YOTE kwani ni kweli wana AMANI kama  hawajawahi kustukia  ni nini kutokuwa na  amani MAISHANI?




KUTOKUWA nacho KITU,...
....yaweza kuwa ndio changamoto  imfanyayo MTU kustukia thamani  ya  KIDUDE.


Na  wengi waliozaliwa na kukikuta KITU,....
..... yaweza kuwa hawapati hata motisha ya kujifunza ni nini thamani ya KIDUDE.


Swali:
  • Au?
  • SI inasemekana hata thamani ya pesa ni tofauti kwa aliyezaliwa na kujikuta yuko kwenye familia ya wenye pesa  kitu kiwezacho kusumbua kujifunza kwake kubana matumizi?

  • Unafikiri mwenye tako analithamini tako kama asiye natako alithaminivyo tako ?

Ndio,...
..... labda mpaka hata MSOSI huthaminiwa zaidi na wasio na chakula.:-(

Ndio,....
..... labda moja ya tatizo la TANZANIA ni jinsi ilivyopata uhuru kirahisi  KWA POROJO ZAIDI  kitu ambacho LABDA kinaathiri UTANZANIA wa WATANZANIA hata katika kufikiria ni jinsi gani maendeleo ya TANZANIA yapiganiwe kwa vitendo  zaidi ya POROJO.:-(


Swali:
  • Unafikiri WATANZANIA kwa kutokuwa nacho KITU wanajifunza kitu kweli kama haliyenyewe miaka yote tokea uhuru ndio hii?

NI WAZO TU HILI lisilotimilifu MHESHIMIWA!

IJUMAA NJEMA na WIKIENDI NJEMA NJEMBA!

Katika kubadili hali ya hewa kijiweni labda USIANGALIE kideo hiki-Make Sure The Kiddies Are Sleeping Before .....usije kwazika.:-(






Au turudi tena Kameruni -Sally Nyolo arudie -Tam TAM



Tubakie hapa hapa Kameruni Bébé Manga arudie ngoma-Mota Benamaa



Au tu Bébé Manga arudie tu na kitu -Amio


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 11:17 am  

Wanasema kuwa ukiwa nacho ndio utalalamika kuwa hakitoshi, lakini kama huna utaishia kutamani.
Mwenye kutamani, anaweza akatamani hata kile kisichowezekana, kwasababu hana, akizidisha au akipunguza haitamuathiri, ndio maana sisi hatujifunzi kitu kwasababu hatuna, zaidi ni kutamani kwa wenzetu kuwa na sisi kama tungelikuwa vile!

Fadhy Mtanga 1:41 pm  

duh mtakatifu!

Yasinta Ngonyani 2:12 pm  

Kaka Simon! Kaazi kwelikweli!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP