Kwa kuwa MAISHANI kuna ASIKIAYE atakacho kusikia, AONAYE atakacho KUONA na atafsiriye ATAKAVYO kutafsiri,.....
>> Friday, April 01, 2011
..... labda hata WASUKUMA wabisheje kuwa WALI sio chakula kama ilivyo UGALI,...
.... kuna watakao amini UBWABWA sio chakula cha ndege na ni bonge la MGIDO kichakula kama NGUNA tu,...
..... na HAKI YA NANI hata UBISHE ,...
....kuna atakaye ona NYONYO wakati wengine wameng'ang'ania kuangalia matako,...
.... kama ilivyokuwa LABDA kuna atakaye tafsiri salamu zako na uongeayo ni MATUSI wakati wewe unafikiri unatongoza kwa nidhamu TU na ustaarabu.:-(Swali:
- Kwani si unakumbuka wakati unaangalia au unasikia kitu na watu wengine- uwazavyo akilini wakati huo na wawazavyo wengine waangaliao kidude hichohicho na wewe WAKATI HUO MMOJA- mnaweza kuwa mnatofautiana MUWAZAVYO ndio maana MALAYA yuleyule udhaniaye ananuka naye bado ana wateja?
- Si unakumbuka stori hiyohiyo moja YA kutia watu MOTISHA na yenye madhumuni ya kupandisha watu MORI kijazba ile IKUKASIRISHAYO - inaweza kufanya watu wengine WACHEKE kwa kudhania STORI HIYOHIYO inachekesha na ndio maana PILIPILI ikuwashayo kunawadhaniao ni TAMU?
- SI pia UNAKUMBUKA maishani kuna wastukiao BUSARA katika yale wewe udhaniayo ni UJINGA?
Ndio,...
.... kwa kuwa MAISHANI kuna ASIKIAYE atakacho KUSIKIA,...
....AONAYE atakacho KUONA,...
... na ATAFSIRIYE atakacho KUTAFSIRI,...
.... lakini bado MTU akitaka KUELEWESHWA wengine waelewavyo ,...
....na KUELEWA wengine labda inawezekana pia!:-(
Swali:
- Si inasemekana maishani kuna mpaka wapotezwao na WENGINE?
Ndio,...
... labda tukumbuke tu kuwa,...
.... kabla ya kufikia HITIMISHO kuwa wakati tunaangalia KITU mitazamo yetu ndio jinsi KARIBU watu wote ya KITU kitazamwavyo,........ tukumbuke tu kuna wafikiriao chupi wakati wanatazama KITU na si kila aliyefumbua MACHO na kuyaelekezea kwenye KITU ni kweli anaangalia KITU hasa ukizingatia labda ni YALE TULIYO YAELEKEZEA FIKIRA ZETU na wala sio MACHO ,...
.....ndio labda TUYAONAYO, tuyasikiayo na TUYATAFSIRIYO.:-(
Ni wazo tu hili MKUU!:-(
Ijumaa naWIKIENDI njema MHESHIMIWA!
Hebu Barrington Levy abadili kwa kuanzisha upya kwa-She's mine
Barrington Levy aendeleze kwa - Shine eye girl
Adinye pia -Black Roses/Here I Come
Sijui kwanini -ila ghafla hebu tu D'Angelo abadili tena kwa kurudia -Brown Sugar
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Ndivyo ilika katika ulimwengu huu. nimepita tu kusalimia na kupoteza mawazo kidogo bado sijatengamaa...
Ndio kwa ufupi maisha ni demokrasia ya nafsi...TUPO MKUU, ANGALAU KUPITISHA MACHO MAANA WENYE NACHO HAWATUPI NAFASI!
Ni maluweluwe tupu! Hakuna uhalisia!
@Yasinta: karibu sana Mtoto mzuri!
@M3:Tuko Pamoja!
@Mkuu MMN:
Sina uhakika kama nimekuelewa!:-(
Post a Comment