Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUSIKILIZA likiwa kama SOMO JIPYA kwa ASIKILIZAYE angalau MGUNO!

>> Wednesday, May 11, 2011

Hata palipo KIMYA ,...

.... kuna vya kusikiliza ingawa vingine labda asikiaye ni TEMBO kwa kuwa SIKIO la BINADAMU lishadhani hapo pako KIMYA!

Na hata katika mkao wa kusikiliza walioko KIMYA,...
.... ukichunguza unaweza kustukia  labda wanahitaji nao KUJIFUNZA UPYA  kusikiliza wasemayo WENGINE,...
.... kwa kuwa katika kusikiliza  hata kwa waliko kimya WENGI  wafanyacho ni KUSIKIA watakavyo KUSIKIA kitu na sio kusikia jinsi KIMAANISHWAVYO  au hata kisemwavyo kitu na MSEMAJI   huku WAKATI HUOHUO wakijiandaa kukabiliana na wanachokisikia hata kama ni kwa kujiandaa kubisha tu bila mpango   au kukidharau  hata kwa kukaa kwao tu KIMYA.:-(


Swali:
  • SI unajua kuna WAKUSIKILIZAO ingawa wanasikia tu kile watakacho KUSIKIA?
  • Na si unakumbuka KUSIKILIZA hudhoofishwa na uliyojifunza kabla ya KUSIKILIZA KITU kitu kifanyacho kama ulishajifunza KUDHARAU UISLAMU  katika kusikiliza mtu  akikuhubiria UISLAMU  kumsikiliza kwako kwa makini huharibiwa na jinsi gani wakati huo unamsikiliza ANAYEBWABWAJA UISLAMU na jinsi gani unadhani anachemka kutokana na uliyojifunza kabla ya kumsikiliza  muhusika ambaye anaweza kuwa anaongea kweli tupu?
  • Unafikiri huhitaji kujifunza kusikiliza vizuri?
  • Unafikiri USHAWAHI kusikiliza kitu kwa makini?

Ndio,...
... inasemekana kwa mpenda MATITI ni vigumu kumsikiliza kimwana MZURI mwenye MATITI mwanana akiongelea MWIDU na MCHICHA,...
... bila kusikilizwa kwake kudhoofishwa na wazo la  MSIKILIZAJI mpenda NYONYO kuwaza angejisikiaje kama angetomasatomasa TITI  katikati ya aendeleavyo kusikiliza stori za MWIDU na MCHICHA!:-(

Ndio,...
...na kutokana na kuwa watu hatujifunzi  KUSIKILIZA vizuri hata kwenye stori za MCHICHA,....
... kuna uwezekano MSIMULIAJI alikuwa naongelea UGALI ambao ndio KIINI cha simulizi ingawa kwa kuwa KATIKA KUSIKILIZA tumechagua kusikia na kukumbuka  tu KIPENGELE cha mboga ilikuwa MCHICHA.:-(


Swali:
  • Na sikama unasikiliza kwa makini si inasemekana  MGUNO  ni sentensi tosha kwa binadamu kwa kuwa kwa MGUNO tu BINADAMU huweza kuongea sentensi maelfu kuanzia kuwa anaumia, anasikia utamu , kaelewa au HATAKI tena mambo zako ya kifirauni?
  • Na si eti hata WASOMAJI nao wanamchezo wa kuelewa watakacho tu kuelewa na kukumbuka tu watakacho kukumbuka na ndio MAANA  unaweza kukuta katika stori nzima  niliyoandika hapa labda kuna ambaye atakumbuka tu kuna mahali niliandika neno MATITI?


Ndio,...
... kama mzaa vile,...
... lakini labda hata kwako wewe UNAYENISOMA unahitaji kujifunza upya KUSIKILIZA.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na JUMATANO NJEMA!


Au tu ABETI MASIKINI atukumbushe wapenda wali na wajuao KISWAHILI  katika - LIKAYABO


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP