Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MH. JOHN MNYIKA TAARIFA ZA VITENDO HIVI VINAVYOENDELEA KATIKA SHULE ZA MSINGI JIMBONI KWAKO UNAZO?

>> Thursday, October 06, 2011

Mh. John Mnyika Mbunge wa Jimbo la Ubungo Dar es salaam.

Kuna taarifa saa hizi zimetufikia kupitia kipindi cha Redio ya Clouds FM cha Leo tena, kuhusu shule moja ya Msingi Jimbo la Ubungo.

Shule ya Msingi Tuliani iliyopo katika Kata ya Kilungule Wilaya ya Kinondoni kuna vitendo vichafu vinaendelea kufanywa na Vijana wahuni wa maeneo hayo vya kuwalawiti wanafunzi wa Shule hiyo ya Tuliani.

Vitendo hivyo mpaka walimu wanavijua na wanashindwa la kufanya kwa sababu nao Walimu wa kike wanaogopa wanaweza kubakwa. Vitendo hivyo hufanywa na vijana hao katika vyoo vya shule hiyo, kutokana na hali ilivyo mbaya mpaka walimu pia wakienda Chooni ni lazima wasindikizane kwa kuwaogopa Wabakaji hao. Kwa taarifa pia kupitia Leo tena, Polisi wa kituo cha jirani wanalijua hili lakini hawalifanyii kazi.

KAPINGAZ Blog kwa kutambua utendaji wako wa kazi tunakuomba ulifanyie kazi haraka sana, ili kuweza kuokoa vizazi vyetu visije vikaangamizwa na Wabakaji hawa. Vitendo hivi vimekuwa vikikua kwa kasi sana hasa katika Shule nyingi za Dar es salaam. Tunaomba Serikali kupitia Wizara husika nao walifanyie Kazi haraka sana.



Nimetumiwa na:
Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP