Ndio,...
.....labda HARUFU ya ANUKAYE ni dalili za tatizo la ANUKAYE,...
......au tu na ni TATIZO sumbufu kwa wanukiwao na hiyo MIHARUFU,....
.... lakini ngoma iko palepale kuwa HARUFU sio tatizo kwa HARUFU.
Swali:
- AU?
- SI unakumbuka HARUFU yenyewe KIYENYEWE huwa haina PUA ya kunusia harufu -na ni MIJIVIUMBE tu mingine tu yenye mchezo wakunusanusa hata UVUNDO kisa inaMIPUA ndio imegeuza HARUFU kuwa DILI?
Na WEWE labda sio tatizo kwa WEWE,...
.... ingawa bado LAKO labda ni chanzo cha tatizo LAKO,....
...... na lako ni TATIZO sumbufu kwa wanukiwao wengine na hilo LITATIZO lako,...
....... ingawa ngoma bado iko palepale kuwa WEWE ni WEWE na WEWE sio TATIZO.
Swali:
- AU?
- Una uhakika WEWE na yako WEWE huwa UNAYATOFAUTISHA hasa ukizingatia labda WEWE na YAKO WEWE ni vitu viwili TOFAUTI?
- Na si HARUFU inaweza kuwa ni ile ya KUNUKIA na sio tu ile ya KUNUKA?
Na kama unafikiri MIMI au MTU mwingine ndiye tatizo LAKO,...
....labda ngoma iko palepale kuwa UMEJIONGEZEA tu MWENYEWE yasiyo TATIZO LAKO,...
... na sasa WEYE MWENYEWE unaelekea kuwa TATIZO la wengine!:-(
Swali:
AU?
Kwani ni kweli HARUFU ni tatizo la HARUFU?
Ndio,...
..... labda siri igeuzayo HARUFU kuwa tatizo ni pua za WENGINE tu,...
.... kwa kuwa kama JALALA ni LAKO,....
..... harufu ya jalala lako lazoeleka,...
.... na hilo sio tatizo LAKO bali la WENGINE.
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA,..
...kutolinyaka KIMAANA RUKSA!
Nakutakia SIKU KABAMBE MKUU!
Hebu tena Tony! Toni! Tone! waingilie kwa kuriwaindi - Whatever You Want
Au hebu tubaki na Raphael Saadiq katika -Good Man
Halafu
Raphael Saadiq ajaribu kuzima kwa
- It's a shame
Halafu D'angelo ndio azime kwa - She's always in my hair
Read more...