Wakati NJEMBA inahangaikia KUJUA ambayo hayatamsaidia KITU !
>> Friday, November 02, 2012
Wakati MTU anahangaikia KUJUA yasiyomsaidia ,...
.... kuna uwezekano,...
...yahangaikiwayo sana ndiyo YASIYO na MSAADA sana kwa MTU!
Swali:
- AU?
- SI kuna UWEZEKANO kwa kuangaikia kujua sana BAADHI ya vitu ndio sababu kubwa ya MTU kuruka kujua MENGINE hata ki ni kiainagani kwake ni MSAADA?
- Na si KUNA UWEZEKANO asilimia KUBWA ya usiyoyahangaikia NDIO yakuwekayo sawa leo hii hata weye bila KUJUA?
Ndio,...
.... LABDA mengi yakuvutiayo kama tu UTAKAYO SANA kuyajua,...
.....kama tu yale yapewayo umuhimu kama UZURI wa MAPAJA kwa mpenda mapaja ambaye ahitajicho KIMALENGO ni mtu apate UJAUZITO,...
....labda MICHANGO yake ni DHAIFU kiumuhimu wa ili MALENGO ya mimba yatimilike,...
... na hapa siongelei tu yale malengo ya ili mtu apate mimba ambapo labda paja halihusiki kihivyo kuliko sehemu za siri na viungo vyake vya uzazi ambavyo si makalio wala paja,....
..... au tu KAMA nguo za mtu safi akiwa na BIBLIA au KORANI yake KANISANI au MSKITINI vilivyo DHAIFU kama roho na ya kiroho HAYAJAANDALIWA kupokea ufunuo wa ya yakiroho ili ya KIROHO yatimilike.
Swali:
- SI unajua labda kuipa kipaumbele BIBLIA au KORANI hata kwa MKRISTO au MUISLAMU bila kuandaa ukunjufu wa MOYO labda ni kujiangaisha kujua ambayo mwisho wa siku hayatamsaidia muungwana katika swala zima la kuweza kuifikia MBINGUNI kwa kuikodolea macho ?
Ndio,...
.... labda kuna vigezo vitusababishavyo kujikuta kuna mambo twayapa KIPAUMBELE katika kutaka kuyajua,...
... na hapa siongelei tu yale ambayo hayatusaidii KITU kama YALE ya kutaka kujua :
- Hivi sijui SIMON KITURURU katukana tena hadharani LEO kimaandishi?
- Hivi sijui ni kweli MKE wa Mheshimiwa matako yake ni ya fulu Mchina kama NYONYO zilivyo?
- Hivi sijui Rais Kikwete ananunuliaga wapi chupi?
- Hivi fulani kala nini?
... au tu yale MENGINE mengi ambayo kwa kweli HAYATUSAIDII zaidi ya kutupotezea MUDA.
Ila swali:
- Hivi unadhani MTU anaweza kupoteza MUDA kweli?
- Si asiyepoteza Muda SASA hivi ,huyo atapoteza tu MUDA BAAADAYE wakati wake ukifika?
- Kwani unafikiri asiyepoteza MUDA anafanya nini la maana ambalo lamfanya kila MUDA afanyalo LIWE ni la MAANA TU na halipotezi muda wa huyohuyo kufanya jambo jingine MUHIMU zaidi?
Ndio,...
.... labda wakati jamaa linahangaika KUJUA,...
.....lapoteza MUDA wa kulala au hata NGONO ambayo kwa wakati huo ingekuwa na UMUHIMU wake zaidi kuliko KUSOLVU mahesabu ambayo kwa BIASHARA yake ya NGURUKA hayatamsaidia kitu katika KUUJAZA ulimwengu ,...
..au hata wala haitamtuliza mawazo kipumziko liletwalo na KULALA.:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na ni RUKSA kutolielewa!!
Nakutakia SIKU MWANANA sana tu AISEE!
Hebu Arrested Development warudishe-Everyday People
Arrested Development waongeze kidogo dozi kwa- Mr. Wendal
Ghafla Mark Morrison aingilie kati kwa - Return of the Mack
Planet Digable wajaribu kuzima kwa-Rebirth Of Slick (Cool Like Dat)
Halafu Genuwine ndio azime kwa- PONY
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Bonge la ujumbe!!Ahsante Kadoda na uwe na ijumaa njema pia wikiendi kwa ujumla..
Post a Comment