Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SHENZI mimi au YULE!!

>> Tuesday, June 24, 2008

Mapenzi ya kutukana yako kichwani mwangu na kwako tu.
Lakini kuna maneno ambayo hutambulika kama matusi ambayo sijui yanatokea wapi mpaka mimi na yule tunaamini kuwa tumetukanwa.
AU?
Swali:

  • Unafikiri kutukana ni nini?
  • Ushawahi kukasirika baada ya kuamini umetukanwa?
  • Hivi matusi ni nini?

Samahani blogu yangu imezubaa siku hizi kutokana na ukweli kuwa niko kushoto.
Samahani kiduchu kuna haka kawimbo ka KASSAV kako kichwani kidogo:-(

Niko kushoto kidogo a.k.a nchi fulani ambayo kupata internet connection ni ujanja kidogo ndio maana blogu iko nanihii.

LAKINI Unaweza ku -search chochote kwenye blogu hii wakati unanisubiri niandike ujinga mpya tena ukipenda au kama wewe mdau wa kijiwe hiki.
Cheki baadhi ya picha zangu za Vilnius LITHUENIA na......
Photobucket

Photobucket
Photobucket

Photobucket

Photobucket
Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket






SAMAHANI kwa ambaye anaweza kuzinguka!
Kama una nafasi unaweza kusikiliza mziki naoendelea kusikiliza sasa hivi ingawa usiniulize muziki huu unafundisha nini:-(
Mpate basi Snoop DOGGKatika wimbo GO Girl


Usimuangalie hapa kama unamchezo wa kuogopa majini, shetani au mambo yawezayokuwa mbele KIDOGO ya kinyesi kwa KUCHEFUA..... katika wimbo KUUA ni KESI niliyoPEWA.


Pata busara au msikilize Michael Shermer akukumbushe kwa nini nikijaribu kukudanganya unastukia na......

Read more...

Kama BADO unataka kuanzisha KANISA, dini AU kutongoza ili ufaidi nanihii ,JIFUNZE saikolojia ya kitu fulani kiduchu!

>> Thursday, June 19, 2008

Udhaifu wa binadamu kichwani , unakautamukake katika swala zima la kuuchezea.
Tatizo ni kwamba , inawezekana anayechezewa MUKICHWA ni mimi na wewe , na ni yule mpendwa NANIHINO ndio anafanikiwa kutuchezea.

Utamu wa kuchezewa akili ni jinsi unavyopunguziwa mahangaiko ya kufikiria mwenyewe katika kufikia hatima ya kustukia kuwa inawezekana ni kweli Maisha ya amani na upendo yanakuwa rahisi zaidi kama katika UHUSIANO wenu na liMPENZI lako , mmoja wenu ni MJINGA .

Swali:

  • Si inasemekana mafahari wawili hawaishi zizi moja?
  • Si ni kweli kama ushaambiwa njia ya kwenda mbinguni ni nyembamba,huna haja ya kufuata njia pana ya ahera ingawa ushastukia njia pana imejaa nanii za kidunia tamutamu sana ingawa nyingine zinaweza zikawa zinanuka?

Sasaa....

Ngoja tujifunze kitu kidogo kutoka kwa James RANDI hasa kuhusu lile swala la kucheza na akili za watu hasa kama wewe unania kama yangu ya KUANZISHA dini....
cheki basi....


Tuendelee..


Nazimia kweli staili ya Peter Popoff ya kuwafisadi wafuasi fulani ambao kwa sababu za kisaikolojia fulani ukiwaelewa,nahisi wanaweza kukusaidia sana katika kupata wafuasi wa dini yako mpya mdau.
AU?

Hebu mcheki kazini....


Pata kidogo dondoo kuhusu BENNY HINN

Basi Mkuu, NAACHA hii topiki...
Lakini....

Swali:
  • Nani kakudanganya kuwa hupendi kudanganywa?
  • Unafikiri huchagui ukweli usiotaka kuusikia; kama ule wa labda umfikiriaye ni baba yako , ukweli ni kaka yako kutokana na kamchezo alikocheza babu?

DUH!
SAMAHANI!
Hebu tumsikilize huyu MVULANA tena akimsimulia mwenyeuke hali halisi...



Kwa wapenzi wa REGGAE MUSIC , jifunzeni ufanisi wa WAIMBA REGGAE kutoka kwa Clint THE DRUNK:-)

Read more...

Kama wewe ni MSHABIKI wa MCHEZO au timu ya MATOMBO STARS!

Napenda saikolojia ya washabiki au wanadini.

Unaweza kusahau!
Lakini....

Mshabiki wa timu fulani anauwezo mkubwa wa kufumbia macho mambo kibao katika kuendekeza tamutamu au chachu imnasishayo yeye na Litimu lake.

Mkristo akisha amini, HISTORIA nyingine nishai ambazo zinazunguka Ulutherani wake, zinafumbiwa macho ili kuendekeza mtazamo wa yale mazuri au yale yamtekenyao kwa mkao wa kukimbia kwenda motoni!
Nafikiri kamchezo haka , KISAIKOLOJIA, kanapatikana hata kwa wafuatao dini za kuabudu chooni.

Swali:

  • Wengi si tunajifanya hatukumbuki kuwa mpenzi huwa anajamba?
  • Unafikiri ni kwanini watu husimulia ushindi zaidi kuliko shule ya kushindwa?
SITANIIII !
Kama wewe mshabiki wa CHELSEA , Matombo stars,Mshabiki wa timu ya RUGBY afrika KUSINI......au mshabiki wa timu fulani tu na si lazima iwe kusini kwa mwili wa mtu,
UNAJUA HISTORIA YA TIMU UISHANGILIAYO?

Hebu tujikumbushe kakitu kidogo kutokana na vipengele viduchu kutoka katika historia za timu zifuatazo .....




DUH!
NAACHA naacha basi topiki!

Samahani natoka nje kidogo ya topiki , nikichukua nafasi kumshukuru MZEE MANENTO!
MANENTO eeh!
Asante kwa kutonitenga na sijasahau!
Hizi picha kali MKUU!
Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

DUH!
SAMAHANI kwa wawezao KUZINGUKA!

Tulia na Montell Jordan akija na Get it on tonight

Read more...

NGUVU ya KICHWA kimoja KATIKA kuchokonoa NANIHII!

>> Wednesday, June 11, 2008

Katika dunia hii ambayo inaweza kukukatisha tamaa kila siku, ni vizuri tu kukumbuka kuwa ingawa KIDOLE kimoja hakiui chawa, lakini kichwa kimoja chaweza kugeuza mitazamo ya mamilioni au hata kusababisha idadi kadhaa ya watoto kibao mtaani!

Katika historia , ni vizuri kukumbuka kuwa kuna majina fulani unayajua na si vikundi ambavyo vilifanikisha mambo kugeuka.
Nahisi unafahamu mchango wa baadhi ya watu nyuma ya majina fulani katika dunia hii ya mamilioni ukoje.

Kuna majina kama...

  • YESU(samahani hapa namchukulia kama binadamu , nisameheni)
  • Martin Luther na ishu zake na UKATOLIKI
  • GANDHI
  • Nyerere
  • Baba yako
  • Nk....
Mchango wa mtu mmoja unaweza ukawa mara kumi ya mchango wa mamia kama unagusa swala katika kipele.
Tatizo ni pale mchango wangu au wako unapomtegemea Kikwete au RAY C


Inawezekana ni wewe , mimi au yeye ambaye atabadili staili ya Watanzania ya KUCHEKELEA kanyau!


Topiki inaendelea........Nisubiri kiduchu!

Mpate Chris de Burgh akija na LAdy in RED


SAMAHANI naweka tena Picha zangu na wadau za mchanganyiko! Naendelea kuwashukuru wadau wangu kwa yote niliyojifunza kwenu na mliyonisaidia, Wadau ambao tumekutana , Wadau niliowaweka picha hapa na pia wadau wote popote duniani!
ASANTE!

(Zinaweza zikawa zinajirudia kutokana na kuzipandisha haraka haraka)

Samahani kwa wawezao kuzinguka!

Photobucket
Photobucket
Photobucket


Photobucket
Photobucket
Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket



Photobucket
Photobucket
Powered by beta.joggle.com


Nakuacha na Queen Latifah akiwa na Al GREEN

Read more...

Inawezekana Unataka kushindana UKIHISI tu kuwa Unayeshindana naye KIBONDE!

Labda binadamu hata wakati anakuhurumia ni kwa sababu anahisi wewe kibonde!

Kuna watakaokubali kuwa binadamu hukwepa kuvamia anachoamini hakiwezekani .

Ni rahisi kumuonea KIBONDE kirahisi tu, hata kama hukiri au hukustukia ni kwanini nirahisi kwako kumpiga kibaka akikuibia pochi kwa kukutishia na kisu kuliko jambazi ambaye anaweza akapora nyumba yako nzima kwa bunduki isiyo na risasi na hata kunajisi kuku wako.


Swali:

  • Hukiri kuwa BARACK OBAMA kwa Watu weusi , amesaidia kutoa ka mwanga kuwa kale KAKIJEBA labda kanapigika ukikaa mkao wa ngwala?




Naacha Basi kwa sasa!

Topiki Inaendelea.. nipe muda kidogo!
Mpate JHIKOMAN kidogo....akikuambia SET ME FREE

SAMAHANI naweka tena Picha zangu na wadau za mchanganyiko! Naendelea kuwashukuru wadau wangu kwa yote niliyojifunza kwenu na mliyonisaidia, Wadau ambao tumekutana , Wadau niliowaweka picha hapa na pia wadau wote popote duniani!
ASANTE!

(Zinaweza zikawa zinajirudia kutokana na kuzipandisha haraka haraka)

Samahani kwa wawezao kuzinguka!



Photobucket

Photobucket
Photobucket
Photobucket

Photobucket

Photobucket
Photobucket

Photobucket

Powered by beta.joggle.com

Tulia na Tina Turner akisema BE GOOD TO ME

Read more...

UAFRIKA wako ni UARABU kama Asili yenu ni WAZUNGU!Unafikiri WaaFRIKA walijua lini kuwa pamoja nakuwa WAGOGO bado wanahitaji kutambulika kama WAAFRIKA?

Nafurahia sana kusikiliza mijadala ihusuyo UAFRIKA hasa pale Mpare au Mgogo aliyevaa JEANS afikiriapo MYAO achezaye sindimba Hoteli NYONYO nje, au Mmasai ambaye hajazoea chupi kuwa hachezi Uafrika.

Kuna wenye busara wanaodai kuwa wenye uke wavaao nguo fupi, hawafuati maadili ya Kiafrika.

Kuna Waafrika watumiao vitabu kama Biblia , au VITABU tu kwa ujumla ,kuhakikishia umati kuwa maadili yao ni kiboko na kuwa Uafrika wao hauna dosari kama ukilinganisha na wale Waafrika ambao kwao Uafrika ni neno la kujifunza tu na UCHAGA ndio asili waijuayo


Swali:

  • Uafrika ni nini?
  • Unafikiri ni lini ulistukia kuwa wewe si Mzungu au kwakua sehemu zako za siri tofauti , basi , unatambulika kama MwenyeUUME zaidi ya toto jinga katika jamii?
  • Unafikiri ni UAFRIKA kwa watu wenye asili ya Kiafrika kuongoza katika kuamini dini zisizo za asili ya Afrika ?




Naacha!Unajua niko mawazoni tu MKUU!

Nitaongelea zaidi topiki baadaye.......

Pata basi haka kawimbo ka Mighty Sparrow
ambako kalinisaidia kucheza muziki wakukumbatia(Dansi ya kushika kiuno kwa mwenye sehemu za siri hasi) na niliyekuwa na udhaifu naye kwa mara ya kwanza maishani, enzi hizo za karibu na kufikia umri wakuwezesha kumpa mimba asiyeficha nanihii!


SAMAHANI naweka tena Picha zangu na wadau za mchanganyiko! Naendelea kuwashukuru wadau wangu kwa yote niliyojifunza kwenu na mliyonisaidia, Wadau ambao tumekutana , Wadau niliowaweka picha hapa na pia wadau wote popote duniani!
ASANTE!

(Zinaweza zikawa zinajirudia kutokana na kuzipandisha haraka haraka)

Samahani kwa wawezao kuzinguka!

Photobucket
Photobucket
Photobucket

Photobucket


Photobucket
Photobucket
Photobucket
Photobucket

Powered by beta.joggle.com


DUH!
Tulia basi na CRAZY ataBIRI miaka ijayo itakuaje katika kibao IN TIME TO COME

Read more...

Samahani kwa Kupotea kiduchu!

Katika mtafuto wa kuweka maisha katika uzani ambao hauangaishi sana, nikajikuta niko uchochoroni kiasi kwamba, kuna maeneo hasa ya mawasiliano na ndugu, jamaa,maadui na marafiki , yakakaa kushoto kidogo.

Kwa wadau wa BLOGU hii, ..
Samahani kwa kutokuwepo hapa kijiweni kwa muda!:-(
Tuko Pamoja!
Au niseme......

Kabla sijasema zaidi, msikilize kidogo MOS DEF



SAMAHANI naweka tena Picha zangu na wadau za mchanganyiko! Naendelea kuwashukuru wadau wangu kwa yote niliyojifunza kwenu na mliyonisaidia, Wadau ambao tumekutana , Wadau niliowaweka picha hapa na pia wadau wote popote duniani!
ASANTE!

(Zinaweza zikawa zinajirudia kutokana na kuzipandisha haraka haraka)

Samahani kwa wawezao kuzinguka!


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket
Photobucket

Powered by beta.joggle.com

Basi Bwana!
Mpate tu Talib Kweli akikukumbusha KUSIKILIZA

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP