Nilifurahi kukutana na washikaji kutoka mabara yote duniani jana. Naombea siku moja dunia hii iwe kijiji ambacho mtu mweusi hateseki kwa sababu ya rangi yake. Naweka baadhi ya picha za washikaji niliobadili nao mwaka wa kirumi jana.Lakini kabla ya hilo unawakumbuka Arrested Development?Unakumbuka sisi ni binadamu tu! Uwe mjanja usiwe siku moja uta ....... tu!
Kutoka Marekani Eugene Darby ....
Hapa chini Bobby Culture akiwa kazini....
Bobby kutoka Jamaika na mimi... Msichana Ninja ajulikanaye kwa jina SASA...
Dj Natty Fruit akiwa kazini...
Mzee Abdulkarim na Aliko wakiwasilisha Afrika Mashariki...
Raymond au kwa jina jingine Mkuu wa Kikao, mimi na Biyamungu Mzee Mago akiwa na Mzee Watts Mzee Ben akiwa na Mkuu wa Kikao.....
Mzee Aliko akiwa amezungukwa na mataifa.....
Kutoka Afrika Magharibi Mzee Mudu na Mbaye... Haya tena tufurahi !Baadaye!
Katika vitabu ninavyovipenda kimoja wapo ni biblia. Leo naendelea kusoma historia ya kitabu hiki kama nilivyosema kwenye video hapo juu.Nitaandika zaidi siku nyingine lakini kwa kifupi historia ya kitabu hiki huwa inanizingua sana .Najaribu kukisoma na kuendelea kujifunza kutoka kwa watu wengine wengi . Na kila mara nakutana na watu wengi wenye maelezo tofautitofauti wakiwamo hawa hapa chini...
na mwingine huyu hapa..
Pia ningeomba mtu mwenye data nzuri za kuaminika kuhusu historia ya Kuran zaidi ya hii hapa anisaidie dondoo za vitabu au sehemu nayoweza kujenga picha zaidi ya jinsi kilivyoandikwa na kutunzwa mpaka sasa.Ningependa zaidi kujua histori ya jinsi maandishi yalivyokuwa yanaandikwa au kukaririwa katika kipindi Quran ilipoandikwa. Nakuacha na Injili ya Yuda hapo chini, wakati nikiendelea kutafakari kasoro na upungufu wa kiubinadamu unaotukabili sisi wanadamu.
Kabla sijasema sana ningependa kuachia The Last Poetswamwage shairi....
Watu weusi bado tumegawanyika sana.Moja ya mgawanyiko ni ule wa Weusi wa Afrika na weusi wenye asili ya Afrika ambao kuwako kwao mbali na Afrika ni matunda ya utumwa, na wengine ambao walihama wenyewe. Waafrika ndani ya Afrika bado tumegawanyika sana pia, kimakabila , kidini,kiutajiri au umaskini na mambo mengine kemukemu ikiwa mpaka rangi.Unakumbuka katika kundi la watu weusi bado tunabaguana kwa rangi , nani mweupe na nani mweusi? Watu weusi waishio mabara mengine nao wamegawanyika kwa hali ya mali,elimu na hata jinsi ya toni za mwonekano wa rangi ya weusi wao . Marekani na sehemu nyingi bado ile hali iliofanya watumwa weupeweupe kupewa kazi za ndani na wale weusi kabisa kazi za nje bado upo.Hivyo bado wale weupe weupe mara nyingi huonekana wazuri kuliko weusi kabisa. Hiki kitu ndio kile kile kinachofanya akina dada kujichubua Afrika katika kutafuta kuwa weupe weupe kwa imani ya kuwa ndio uzuri. Hivi uzuri ndio nini?Haya mambo ambayo binadamu anajitengenezea akilini na kutengeneza mazingira ya kuhalalisha mtazamo yanazingua sana.
Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana! Kila wakati na kila siku yuko shuleni. Anajifunza ladha na anajifunza kuishi katika mazingira yake. Ndio maana kila siku utasikia, alah! Hiyo fasheni imepitwa na wakati! Halafu ghafla atakuambia nilipoonja bia kwa mara ya kwanza sikupenda ladha yake.Wakati yeye ndiye ajulikanaye kwa unywaji wa bia. Binadamu huyo huyo katika kutafuta kujiridhisha huwa anapenda kujifananisha na wenzake na kujipima kupitia wenzake. Hii pamoja na kujipatia furaha pia huleta mikwaruzo ndani ya jamii.Mikwazuzo hii hutugawa lakini pia kutujenga.Tatizo letu watu weusi bado tumeshindwa kuunganisha nguvu zetu na mikwaruzo yetu inatubomoa zaidi yakutuletea changa moto zakutujenga.
Tukirudi kwenye KWANZAA, mimi naona ni moja ya jambo ambalo pamoja na mengine linajaribu kuunganisha watu weusi. Na nafikiri jambo lolote liunganishalo watu weusi wenye asili ya Afrika ni jambo muhimu kwa sababu umoja tuna uhitaji sana sisi kama watu weusi.Vizazi vijavyo vya watu weusi vitashindwa kutuelewa ni namna gani Afrika pamoja na mali zetu bado tumefanikiwa kuwa masikini na wanyonge hivi.Kizazi chetu hiki tu bado tuna maswali ilikuwaje wakoloni wachache waliweza kututawala .Unakumbuka tulikuwa tunawabeba kuwasafirisha maporini? Unakumbuka mara nyingi ilikuwa waafrika wanne wanambeba mzungu mmoja na anatoa amri hata huko msituni, huku watu wakitii?Sasa fikiria baada ya miaka kadhaa sisi ndio tutakuwa somo.Vizazi vijavyo watajiuliza, hivi hawajamaa vipi? Kila siku kugombana tu huku wakijua maugomvi yao yananufaisha wengine.
Sasa hivi kuna Wamarekani weusi watambuao umuhimu wa Afrika katika maisha yao lakini wapo wengi wachukiao Afrika na waafrika.Wao kwa wao hawana umoja , wamegawanyika hadi kwenye maadili.Waangalie wengine hawa hapa wakijielezea....
Nasi Afrika hatujakuwa mfano mzuri wakujivunia. Na katika hili na kubaliana na wale wanaoenzi nguzo saba za kwanzaa ambao wanatafuta maadili kutoka Afrika ilikujisikia kamili.Kwani hata kwa hili kuna kaumoja kanajengeka. Kumbukeni kama watu weusi ni miaka mingi imepita bila kula raha na kufurahia uweusi wetu.Ngoja Mighty Diamond wakukumbushe hapa chini...
Sasa mimi na wewe tunafanyanini katika kuleta mikwaruzo yetu na tofauti zetu kama watu weusi iwe inatujenga zaidi ya kutubomoa?
Samahani nilisahau kuwa bado tuko katika shamra shamra za KWANZAA, kusubiri mwaka mpya na kadhalika nyingi!Haya basi tuendelee kufurahi. Nakuacha na Lagbaja hapa chini.
Leo nasikiliza sana Zouk, kama za Kassav hawa hapa chini.....
lakini pia mdundiko na nyimbo mbalimbali nazipitia pia ingawa wimbo huu hapa chini uitwao Kiuno Viuno unanifikirisha kidogo!Hii sio kutiana majaribuni?
Nafikiri binadamu mara nyingi hutafuta sababu ya kusherehekea.Hii ni kawaida.Tanzania katika mila zetu utakuta sherehe hizi nyingi tu. Kuhusu Krismaskama siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa yesu ni tarehe iliyo buniwa tu. Tafiti nyingi zinadai kuwa kwa kufuata kalenda tuitumiayo na mambo mengi yaliotokea kipindi cha kuzaliwa kwa yesu inawezekana kabisa ikawa Aprili ndio kipindi.Hata hivyo hakuna uhakika asilimia mia wa siku hiyo.Na nukuu nyingi hizi zilizoko kwenye biblia ziliandikwa miaka mingi baada ya kufariki kwa yesu.
Kuhusu mwaka mpya ndio hivyo tena ukifuatilia historia ya kalenda na ukajiuliza kwanini watu wengi walikuwa na kalenda tofautitofauti, na bado wana kalenda tofautitofauti utapata jibu.
Kuhusu Santa Klaus au Saint Nicholaus- askofu wa mji wa Myra,Uturuki na kuibiwa na Waitaliano waliomhamishia mji wa Bari na kuingia dili na kanisa ilikukuza utalii kwa kumtangaza. NAfikiri unajua nafikiria nini. Lakini Cocacola Kampani ilimtafutia vazi zuri ilikupendeza akitangaza Coca cola.
Tukiachana na hilo, nadhani asilimia kubwa yetu tunapenda sherehe na tunapenda zawadi.Nafikiri hakuna haja ya kufuatilia sana mambo haya maana utaondoa utamu wa sherehe yako. Heri ya Krismas na Mwaka Mpya, lakini kumbuka siku ya krismas na mwaka mpya zaweza kuwa ni siku yoyote ile uamkapo, na hizi siku tusheherekeazo ni binadamu kama mimi na wewe waliozitunga.