Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NIKIKUANGALIA wakati UNA-SHAbikia, CHEkelea au ukiLIA, TIMU yako IKISHINDA!

>> Wednesday, April 30, 2008

Ukiwa na TABIA ya kumtazama binadamu, utastukia kuwa huhitaji televisheni wala kucheza bao ili ujiliwaze.

Binadamu hakosi jipya la kukustaajabisha, kama unatabia au jicho la kumchunguza.

Na....
.....ukijenga tabia ya kumtazama sana binadamu , iko siku utastukia kuwa, kama ni kubwa zima halafu halitumii kinyoleo, linaweza likawa lina nywele nywele zinakua kuanzia mashavuni kama ni janaUME, au linakua manyoya mpaka maeneo ambayo kama halijavaa kificha nyeti, linaweza kuwa na kipilipili mpaka maKWAPAni. (Na cha ajabu ni kwamba ,inaweza ikawa ngumu kwako au kwangu kufumbua fumbo la umuhimu na madhumuni ya kwanini manyoya na nywelenywele hizi nyingine humuota huyu binadamu maeneo fulani fulani bila ya faida iliyouchi ).


Binadamu kwa jina la ushabiki anaweza kulia, kupiga mtu au hata kujiua ,timu yake ikishindwa.

Binadamu hata kama ni mchezaji na achukiaye tabia za kisenge, unaweza ukakuta kampiga busu, akamkatikia kiuno na kumkumbatia mwenziye mwenye sehemu za haja ndogo zilizo fanana na zake ,KISA, amefunga goli, bila kukumbuka kuwa tabia hizo hizo alizofanya kwa kufurahia na aina ya mtu aliyemfanyia vitendo hivyo, ukijumlisha ,ndizo tabia za kisagaji ambazo yeye na jamii yake kama ungeondoa mpira na kuweka muziki wa bluzi , basi angepigwa mawe mtu na wapambe kwa kosa la USHOGA.

Inawezekana UMUANGALIAVYO mtu , unaOAnisha mahali alipo na nini kinafanyika,ili kuwa na uhakika na kitendo kuwa; ingawa anaguna, haiwezekani akawa anajisaidia haja kubwa sebuleni.
Si agunaye chooni hata kama kajikwaa huko msalani , atashukiwa tu anaguna kwa sababu anakwenda starehe kubwa?

Labda ni ka-ubinadamu kakupenda ushindani na kushinda, kamsababishiako binadamu afurahie timu yake ikishinda na ahudhunike akishindwa.
Lakini si kufurahia kushinda na kuhudhunikia kushindwa , vyote ni vitu vya muda mfupi tu?

Au labda ni kaudhaifu ka-kibinadamu kakutojua mwisho wa mchezo matokeo yatakuwaje, kamleteako binadamu tamu tamu ya kufuatilia mchezo mpaka mwisho.
Lakini si wengine huwa na uhakika wakushinda au kushindwa katikati ya mchezo au kabla mchezo kuisha?

Labda ni ka-utamu wa kushinda au uchungu wa kushindwa , kasababishako unaendelea kuwa mshabiki wa timu fulani.
Swali:

  • Unajua ushabiki , inawezekana ni aina ya ugonjwa wa akili kama lilivyo penzi?
  • Ushastukia mshabiki , nukta kadhaa baada ya kushinda au kushindwa anaweza kufanya ambacho hawezi kukiri waziwazi amewahifanya maishani?
  • Ugonjwa wa akili ni nini?

SAMAHANI nawaza tu!
Si unakumbuka hiki ni kijiwe cha Simon kitururu-MAWAZONI?
Siku njema!

Tulia na Acoustic Blues vibes kutoka kwa Eric BIBB akikupa GOOD Stuff

Au turudi tu kwenye Zouk Love ikija katika wimbo La Zouk Horay kama iletwavyo na Kaysha na kuwa remixed na DJ DUKA(samahani video inaweza kumkwaza mtu fulani au kuwa inamdhalilisha mtu fulani kwa mtazamo wa mtu fulani.Kama mtoto au mkwazika kirahisi, usiangalie .SAMAHANI!:-()

Read more...

UKINUKUU BIBLIA, KORANI au kamaSUTRA kwa MTU asiyeamini MUNGU!

Binadamu hupenda kunukuu watu, vitabu, matukio, ..... katika kujazia uzito au hata kuhalalisha kitendo au mtazamo wa mlolomo wao.


Binadamu , kirahisi, husahau wengine hawafikirii wala kuamini ukweli wao ni ukweli hata kama unaitwa sayansi wakati wanamnukuu Einstein kuwa E=mc2

Swali:

  • Unakumbuka kuna ambao E=mc2 ni= na ALbaMU mpya ya Mariah Carey na hakuna uhusiano wowote na Fizikia(Phisics)?
Nachojaribu kunong'ona ni:
....Unaponukuu mwingine asichoamini , unaweza ukawa unajipotezea muda.

Ukijikumbusha nukuu za mtoto.....
.....LImwanaMKE LAKO au LIBWANA LAKO ufikirialo kuwa ni zuri na lina roho nzuri, na ni tamutamu kama lawalawa nyama, linaweza kumliza mtoto mdogo akalia kama vile kaumwa na manyigu , kutokana na kumuogopesha MTOTO, kwa sababu kwa nukuu za mtoto, huliona hilo LImTU LAKO kuwa lina sura kama Nundu na meno kama Ngiri.


Ni rahisi kusahau kuwa kuna vitu vingi mtu umejifunza kuviogopa na hukuzaliwa unaviogopa, kitu ambacho mwenzio anaweza akawa bado hajajifunza kuviogopa na haogopi kama wewe.


Sasaaaa......

....ukimtishia asiyeamini MUNGU, maswala ya MUNGU , anaweza akamtukania Mungu wako , halafu ukajikuta umempiga ngwala, mtama au hata kuMKOLIMBA , kabla hauja MSaddam Hussein.

Lakini naamini kuwa....
......baada ya UBONGO WAKO kuamini kitu, tafsiri na wapi unanukuu viushahidi vyako au vikupovyavyo roho kuwa uko upande sahihi, HUATHIRIKA.

Inawezekana umeathiriwa na ELIMU.
Si ndio maana unanukuu vinavyotoka vitabuni ?

Inawezekana umeathiriwa na dini.
Si ndio maana karibu kila jambo utanukuu VITABU vya DINI ,mapenzi au hasira za MUNGU?

Inawezekana umeaathirika na utamaduni fulani.
Si ndio maana kuna mahali unanukuu mpaka wacheza Sindimba matiti nje, pale AIRPORT wakati Raisi wa nchi fulani ya Kiafrika kawasili,kuwa wako uchi na wafanyacho si utamaduni ASILI wa KIAFRIKA, iLA, unaamini pamba itokayo India inatengeneza nguo halisi za Kiafrika?

DUH!

Sehemu unanukuu, inaweza ikawa ni kama ujumbe uupatao kwa kuangalia sanamu.
Sentensi uitoayo kwenye sanamu ,inaweza kutowakilisha kwa mwingine ilichowasilisha kwako.

Swali:
  • Sanamu ni nini?
  • Sanamu huwakilisha nini kwako?
  • Unajua inawezekana kila mtu ANAABUDU sanamu?
  • Mwalimu asimamaye mbele yako darasani, na kuondoka bila wewe kujifunza au kuelewa kitu , hawezi tafsirika kama sanamu liwakilishalo kitu tu chenye jina MWALIMU?
Kuna atakayesema sanamu huwa alifanyi kitu, linawakilisha tu kaujumbe kawakilishwako na sanamu.


Lakini...
...wako watakao kumbuka, sanamu linaweza kukuangukia na kukuvunja nanihii!

Naacha basi kukuzingua!
Usitishike Nawaza tu hapa!

Karibu tena MAWAZONI lakini!

Pata basi TAP DANCE kutoka kwa Savion Glover

Au....

Mcheki tu Maraya Keri katika wimbo Touch my Body kutoka albamu E=mc2

Read more...

MATANGAZO ya WADAU kiduchu!

1.Filamu zinazowania tuzo ya Vinara wa Filamu Tanzania zatajwa!

Filamu zilizoingizwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2007/2008 2007/2008 (Vinara Film Awards), zimetajwa.

Katika taarifa kutoka mratibu wa One Game Promotion inayoaandaa tuzo hizo, Khadija Khalili, iliyotumwa kwenye vyombo vya habari zaidi ya filamu sabini zinawania tuzo hizo.

Taarifa hiyo ilizitaja filamu hizo kuwa ni Crying Silently (Kilio Moyoni), Kolelo, Mwanahiti, Zawadi ya Fisadi, Oloboni na Layoni, Mmera (Jando) na Nyamaume.

Nyingine ni Sumu ya Moyo, Segito, A Point of no Return I, A Point of no Return II, Dar to Lagos, Cross my Sin na Penina.

Pia zimo Habari Kubwa, Fake Pastor, Chite Ukae, Surprise, Stranger, Fungu la Kukosa, Sea Man, Mzee wa Chabo, Donda Ndugu, I Love You, Miss Bongo I, Miss Bongo II, Revenge, Behind the Scene, na My Wife.

Taarifa hiyo ilizitaja nyingine kuwa ni My Sisters I, My Sisters II, Machozi ya Nyamoma, Silent Killer, My Wife, Greena, Kiapo cha Damu, Valentine, Mwana Pango, Utata, Yolanda, Picnic, Uwanja wa Dhambi, Misukosuko II, Copy, Lugha Gongana, Mtoto wa Mjini, Nyuma ya Pazia, Macho Mekundu, Tanzia, Welcome Back, Karibu Paradiso, Swahiba, The Game of Love I, The Game of Love II na The Game of Love III.

Nyingine ni Mahabati, Security, Itunyama, The Body Guard, Agano la Urithi, Ndani ya Gereza, Simu ya Kifo, My Heart, Malipo ya Kisasi I, Malipo ya Kisasi II, Mpasuko wa Moyo I, Mpasuko wa Moyo II, Kisasi na Diversion of Love.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, majaji watakutana wiki ijayo kuanza kuziangalia tuzo hizo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa filamu zinazowania tuzo hizo ni zile zilizokamilika kutengenezwa Januari 2007 mpaka Machi 31, 2008.

Filamu zinazowania tuzo za Vinara

Vipengele vinavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo ni Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Muongozaji Sinema Bora wa Mwaka, Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu na Mtunzi Bora wa Filamu.

Vingine ni Filamu Bora ya Kutisha, Muigizaji Mwandamizi Bora wa kike (supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Bora kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa Filamu ambao wote watapata tuzo na zawadi.

Pia itatolewa tuzo ya heshima kwa wale waliotoa mchango wao kukuza sanaa nchini.

Tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Mei zimedhaminiwa na bia ya Ndovu Special Malt, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Global Publishers.


2.Kwa habari za ujerumani na historia yake tafadhali tembelea

Habari,
Ule wakati tulio usubiria sasa umefika, Website ya pekee itakayo jishughulisha
ktk kuutangaza muziki wa Tanzania ipo jikoni na ina karibia kuiva.

Unataka kusikiliza muziki wa nyumbani? Basi watembelee wajuzi wa fani hii
kupitia www.mkmusicgalaxy.com kwa miziki mipya na ya kizamani uburudike roho
yako.

4.Ushasikia.......
FotoBaraza?


--------------Mwisho wa MATANGAZO---------------------------------------

Kama una muda kidogo, jifunze WAPAGANI wanafikiria nini kutoka kwa MWANABAOLOJIA Richard Dawkins aliyezaliwa NAIROBI , KENYA

Read more...

Kama MWALIMU NYERERE angeanzisha dini kwa WATANZANIA halafu akawa HAYATi!

>> Sunday, April 27, 2008

Naogopa dini!

Dini kiboko!
Inaweza kukusababisha ukashinda njaa kwa ahadi ;utafaidi mbinguni, lakini bila kuwa na uhakika utafaidi nini AHERA , halafu ukashinda njaa.

Dini kiboko!
Inaweza kukusaidia kusamehe jamaa alivyo kunanihii.
Inaweza kukufanya uende vitani kuua kwa chuki ILI kuhakikisha kuwa MUNGU wa UPENDO na AMANI hadharauliwi.

Dini Kiboko!
Ukichacha unaweza ukaokoka ili kubana matumizi halafu ukajikuta umeokoka kikweli.
Hebu tu ANGA lie.... jinsi VOODOOO a.k.a VUDU ikimuingia MWenyEuke mdogo a.k.a.BINTI... ..


Kama wewe MTANZANIA halafu unaangalia mapungufu, utakuwa na uhakika kuwa hata wajifanyao wanafuata nyayo za NYERERE, wanaangalia TV.

Kama wewe unaangalia MAPUNGUFU,Mwalimu Julias KAMBARAGE angeanzisha dini halafu MWENYEZI ALLAH akamchukua, naamini, ungeweza ukajifunza kwanini fikira zake za MUUNGANO wa TANGANYIKA na ZANZIBAR mpaka leo tunajadili kwa kutumia hesabu kama TANZANIA =TANGANYIKA-ZANZIBAR au TANZANIA = TANGANYIKA+ZANZIBAR

Swali:

  • Hivi unakumbuka UJAMAA ni NINI?
Ukiwa MTANZANIA na unakumbuka MwALIMU KAMBARAGE aliyofanikisha, unaweza hata kukumbuka kuwa hujui jirani yako kabila gani na uliwahi kumuomba chumvi , maji, au kumchekea kwa KISWAHILI.

SWALI:
  • Kama kiswahili ni bomba, mbona ukiwa na pesa unataka kumpeleka mwanaTOTO shule ya INGRISH mediumu.
  • Hivi bado kama shule ni bomba walimu wa KIiNGRISH va INDI au wanatoka Uganda eeh?
DUH!
Hebu turudi kwenye ZE Mwalimu Nyerere akianzisha dini au kwenye dini tu....

Twende KENYA kupata DINI fulani kiduchuuu,...
Usije ukawa unaogopa MUNGIKI tu kati ya dini kadhaa milioni fulani lakini!
Kwani dini yako haija KUTISHA kumtamani au kutamani?


Naogopa DINI!

DINI inaweza ikafanya uogope tu au uogope kitu fulani wenzio wafanyacho ingawa kisiri unatamani MWENZIO alivyo BINYA au KUtomasa NYANYA fulani.

Dini nyingine unaweza kutubu lakini!:-)
AU?

Now I am depressed!:-(

Nataka kuanzisha dini lakini!

Hebu tuwasikilize WAKRISTO fulani walioKUWA na uhakika OPRAH WINFEY kaanzisha dini....

DUH!
Naogopa DINI ingawa nikianzisha moja ya dini fulani, unaweza kujikuta unaifuata kutokana na kwamba kuna KILAJI, mboga ya mchicha na NYAMA ya PaKA kwenye jumba la IBADA!:-(

USITISHIKE!
NAWAZA TU!

Hebu tumsikilize tu MANU DIBANGO atukumbushe kengele za kanisa fulani katika wimbo NEW BELL
(Hard Pulsation)

Read more...

USHUJAA wa KUKOPA!

>> Friday, April 25, 2008

Kukopa ni kazi ngumu, kwa sababu mkopo unakuja na kukutengenezea kasifa wengine wawezako kukaweka ndani ya sentensi kama:JAMAA kwa kukopa hata SERIKALI za AFRIKA hazioni ndani.

Kama si mzoefu, kijasho kitakutoka wakati unafanya maandalizi ya kukopa.

Ukizoea kukopa , unaweza kukopa kisirisiri pia au hata unaweza kukopa sehemu za siri za mwenzio.

Lakini....
....kukopa na staili yako ya kukopa , inategemea tu na ulivyoathirika kisaikolojia fulani.

Swali:

  • Hivi unakumbuka serikali ya Marekani a.k.a USA ndio miongoni mwa serikali zinazodaiwa mikopo sana duniani?
  • Unakumbuka inasemekana sasa hivi MAREKANI haiwezi kumkoromea CHINA kwa vitendo kutokana na CHINA kuwa ndio nchi inayoongoza kwa kukopesha Marekani?

Staili yako ya kukopa , hutegemea sana kuathirika kwako kisaikolojia bado kuna kuhakikishia kuwa wewe unacho au huna.

Staili ya fundi viatu nje ya duka kumkopa mwenye duka, inaweza ikawa ya upole na unyenyekevu kuliko staili ya huyo mwenye duka kumkopa fundi viatu nje ya duka lake , ingawa wote wamechacha.

Swali:
  • Unajua unabadilika sauti wakati unakopa?
  • Unajua unabadilika mwendo ukisha katashauri kumfuata umtongoze na lolote liwe a.k.a mwendo wa kumsogelea unayetaka kumkopa?

Lakini...
..inawezekana mkopaji aliye shujaa si yule aliyezoea kukopa.

Kukopa ni kitendo unaweza kukipamba kwa kusema umeazima.
Naweza kukubishia ukisema kuwa hujawahi kukopa halafu ukashindwa kunibishia ingawa kijiweni wewe ndiye usiokosa chumvi watu wakihitaji chai.

DUH!
NAACHA!

Baadaye , kesho , kesho kutwa au siku nyingine Mwenyezi Mungu akipenda iwe hivyo!
Si inasemekana hata nikifa ni mapenzi ya MUNGU?

Nakasikiliza kawimbo haka , kaitwako- To the Ceiling kalikopigwa na ISAAC BLACKMAN. Anza nako WIKIENDI ukipenda.

Read more...

NAKUPENDA!Si nilikupigia SIMU?

Ukimya unatafsiri nyingi.
Kirahisi tu , unaweza kutafsiri ukimya wa mtu kutokana na nini ulishaanza kumfikiria utakaye jibu kutoka kwake.

Unaweza mpaka kupata jibu kutoka kwa uliye jaribu kuwasiliana naye bila mafanikio, kuwa jamaa ananikwepa au ananidharau.

Wajanja husema ukiwasiliana na jamaa atakusikia au hata kukusoma.

Lakini....
...ukisikia au kusoma cha mtu, inawezekana hajawasilisha au ujumbe wake kuhusu jiko , wewe ukaelewa anazungumzia choo kichafu ambacho kina funza funza fulani WANONO.

Lakini....
...funza funza wanono watutiao kinyaa, kichefuchefu au hata hamu ya kutapika, wanaweza wakawa ni watoto wapendwa jichoni kwa mama yao NZI.

DUH!

Ningependa kuchukua nafasi hii kuomba msamaha kwa wote ambao nimeshindwa kuwasiliana nao.Najua ni watu kibao ambao wamekata tamaa nami kutokana na ka-ukimya fulani.

  • Samahani kama sijakupigia simu wala kupokea simu!
  • Samahani sijakujibu ile barua, e-mail wala labda sikugeuka uliponipigia ule mluzi!
Tuko Pamoja na WIKIENDI NJEMA!

Lakini..
.. kabla sijaondoka kabisa kwenye topiki ya kuwasiliana fulani,
nimefurahi kufanikiwa kukutana uso kwa uso na blogger wa Kitanzania ambaye tulikuwa tunajuana mtandaoni bila kuwahi kuonana uso kwa uso a.k.a EDO NDAKI

Pata baadhi ya picha zangu nilizozidaka baada ya kukutana na EDO NDAKI , pamoja na WADAU wengine.
Photobucket
Kwa wasio jua , huyu ndiyo Mzee EDO NDAKI:
Photobucket
Hapa nilijibanza naye.
Photobucket

Photobucket
MKUU wa Kikao a.k.a RAYMOND alikuwepo.

Tulia na HEAVY D akikuambia NUTTIN but LOVE

Read more...

Kuna WATU wakoKimYa lakini wameona na kusikia! UKIWAPA upenyo ,WATAKUULIZA kama USHAWAHI kuugua Ugonjwa wa akili.

Kuna topiki fulani watu hukwepa kuongelea kutokana na topiki ilivyokaa kushoto.

Ukimpa mtu nafasi au kianzio cha sentensi kuhusu topiki asiyo kuwa na uhakika inakuathiri vipi ingawa akilini mwake anaona inauhusiano sana na jambo la kutia aibu , atakuuliza .

Ukimpa nafasi au kumchekea mara baada ya kumpa tabasamu wakati anahamu na wewe, anaweza kupata nguvu ya kukutongoza.


Cha ajabu ni kwamba , asicho kuuliza uso kwa uso anaweza kuwa kasha jadili na wadau wengine mara mia kadhaa na kufikia kwenye uhakika kuwa lile gari lako umelikopa.

Kuteta, umbea au hata kumuongelea mtu kama hayuko kijiweni, ni BOMBA la SANAA kwa atakaye urahisi wa kuhakikishia ubongo wake alichosikia kwenye redio za mbao ni kweli.

Umbea na kutetana ni dalili kwamba unamuda zaidi katika maisha yako ambao huutumii kujishughulikia au kufanikisha yanayo kuhusu wewe binafsi.

Umbeya , kuteta, uzushi au hata kutungia watu vistori visivyo vya ukweli ni bomba la kazi nzuri kama una hobi ya UMBEA.
Si unaona mpaka PEREZ HILTON kawa milionea kwa kuongea umbea na uzushi?


Si umeona Tanzania kuna magazeti mangapi yanayokiri ni ya UDAKU?
Watu hupenda kuwa na taarifa zako ambazo wanahisi hutaki zijulikane.

Swali:

  • Unahisi ni kwanini humuulizi , wakati unataka kujua kama kweli ana mke mdogo pale mtaa fulani au kama bado ana kaudhaifu ka-mapenzi yake ya watoto wa sekondari ya KIFUNGIRO, kama usikiavyo?
  • Unafikiri ni kwa nini huulizi ingawa unataka kujua?
Lakini.....:
...Ukiuliza aliye ulizwa anaweza kuhisi unajua tayari ,kitu ambacho kinaweza kufanya aanze kukukwepa.
....Ukiuliza maana yake umekiri kuwa hujui.
....Ukiuliza inaweza ukawa umetoa mwaliko wa kutaka kudanganywa.

INAWEZEKANA hujauliza kwa sababu hujapewa nafasi, kianzio cha topiki au kuchekewa, USIKONDE!

Unakumbuka lakini jinsi gani mazingira, topiki iliyokuwa hewani ....vilivyochangia ujisikie huru kuulizia au kutongoza?

Unajua mara nyingi ni wewe , mimi au yule tutengenezao mazingira ya kurahisisha mpaka kutukanwa?

DUH!
Inawezekana nimeshakutengenezea mazingira ambayo utataka kuniulizia ambacho nitakwepa kujibu!:-(

Inaruhusiwa kutojibu ingawa kwa mimi kutojibu unaweza kuondoka ukifikiria ni kweli mimi bado bikira.

NAACHA basi!

Nakutakia kila la KHERI katika maisha haya ambayo yanasababisha tutake kujua mpaka visivyo tusaidia kama vile :hivi yule msichana kavaa chupi au kaptura chini ya lile gwaguro.

Tulia na Mu-Itali (ambaye usipomuona unaweza kufikiri mweusi) kwa jina la Alberto D'Ascola A.k.a. AlBorosie


Au pata ujumbe wewe kama MTU MWEUSI kutoka kwa MORGAN HERITAGE wakimkumbusha MTU mweusi hali halisi ya MTU MWEUSI,
katika songi, FALLIN RACE

Read more...

SAMAHANI! Nawakimbia tena wadau wa BLOGU HII kidogo!:-(

>> Tuesday, April 22, 2008

Samahani wadau wa blogu hii!
Nimebanwa kidogo, kwa hiyo , saundi haitoki stirio....

Lakini nafikiri kuanzia Ijumaa hii , pilau inaweza kunukia tena hapa kijiweni kama kawaida.
Au ngojea niseme.....


SASAA endelea kidogo tu na Lagbaja ambaye ndio baada ya FELA Kuti, katika AFRO BEAT, ananisaidia katika SUKUMA TWENDE wiki hiii, angalau katika wimbo FEYIN E.......akisisitiza utabasamu au kucheka hata kama nanihii ngumu:-(




DUH!
Au unaweza kujifunza kucheka au kutabasamu kitu kutoka kwa mchekaji huyu...

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP