Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Marehemu Alikuwa Mtu Mzuri!

>> Friday, October 06, 2006

Marehemu Simon..

Mtu wa Kwanza: Kwa heri Simon! Upumzike mahali pema peponi.
Mtu wa Pili: Alikuwa rafiki yangu sana!Nakumbuka alikuwa ananisaidia kuchuma kisamvu.

Mtu wa tatu:Duh !Sasa sijui nitafanyaje maana ana madeni yangu! Alikuwa hajali watu! Lakini afadhali kaanza tu!
Mtu wa nne:Duh !Msiba huu bomba! Msosi na vinywaji kibao!

Marehemu IDD AMIN

Mtu wa kwanza:
Alikuwa bomba la mnyama afadhali kafa.

Mtu wa pili:
DUh! Aliwanyosha Wahindi na Wazungu alikuwa bomba sana.


Marehemu kwa ujumla.


Watu asilimia kubwa kuliko:
Marehemu alikuwa mtu safi sana.

Hivi marehemu wanasikia? Kwa nini usimshukuru na kumsifia mtu wakati yuko hai? Hivi yale maua na vitu vinginevyo umleteavyo katika mazishi au kaburini vinamaana kwa mrehemu?

Au unajifariji mwenyewe katika kifo cha mwenzio?

Oho! Naona unajisikia vibaya kwa sababu unataka kucheka kilioni baada ya kushuhudia mtu analia mlioa dizaini!

Samahani nabunia tu. Usijali!

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 8:06 pm  

Greetings I AND I.Peace.its true why do we wait until someone is dead that is the time we cry.i think we are hypocrates(wanafki)sasa mzee wa Zion Train itakuwaje nini chakufanya ili AFRIKA IBADILIKE?pili wale ndugu zetu kama wakina NDESANJO, kwanini wasirudi AFRIKA,hebu nipemawazo yako.I WANT TO SEE THE UNITED STATES OF AFRICA BEFORE I DIE.(COME RAIN COME SUNSHINE IT HAS TO BE ONE).

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP