Leo tokea niamke nahamu ya MAHINDI ya KUCHOMA ,..
....halafu yale yachomwayo BARABARANI.:-(
Halafu mahindi ya kuchoma ,...
....niyatamaniyo ni yale yachomwayo pembeni ya barabara kwa kuwa kwangu sijui kwanini huwa napenda ZAIDI mahindi ya kununua pembeni ya barabara kuliko ya kuchoma mwenyewe nyumbani!:-(
DUH! Halafu leo ningepata na MAFENESI nayo baada ya kumalizana na MAHINDI ya kuchoma,...
....halafu yawe ni yale ambayo YAMESHA POKOCHOLEWA kutoka kwenye TUNDA MAMA ili nisihangaike nayo kuyatoa kwenye FENESI mwenyewe ingekuwa BABU KUBWA yani!:-(
DUH au angalau basi nimgepata CHIPSI DUME kwa kachumbari , Juisi ya UKWAJU, madhambaru au angalau MAHINDI ya KUCHEMSHA kama sio yale ya KUCHOMA,...
..... au angalau nipate TU mua uliokatwakatwa kabisa vipande ingekuwa MURUA kweli yani.:-(
Kwa kifupi :
....Niko hapa
TALLIN -
Estonia nikiwa na bonge la
Homesickness na kungekuwa na angalau KIMWANA wa KIBONGO hata wakulipia a.k.a MALAYA wa KIBONGO - hapa nahisi ningeingia dhambi ya angalau kufikiria au kufanya kabisa kitu KIMHONGO angalau tufanikishe kufanya dhambi za KUDANGANYANA au hata za MATUSI KABISA angalau kwa kiswahili tu katika kujaribu kujisahaulisha nje kuna baridi FRIJI halioni ndani na halihalisi inachangia kutojisikia hatuko HOMU yani :-(
Ee BWANA eeh!
JUMAPILI NJEMA na samahani kama nimekukwaza kwa kuwaza KWANGU NYOKO hapa KIJIWENI kwa SAUTI!:-(
Na moja kwa moja wakati nawaza TOTOZ za KIBONGO ambazo natarajia hapo mbeleni maishani KUCHUKUA MMOJA wotewote kama MKE - ambao hapa nilipo ni hadimu KWELI kama manyoyanyoya YA KIKUBWA kwenye kwapa la mtoto - ngojea niendelee kujituliza kwa kusikiliza
Jamhuri Jazz Band wakati wanamuongelea mtoto mzuri mwenye
-SHINGO ya UPANGA
Jamhuri Jazz Band wanifikirishe maswala ya kuangalia uwezekano wa kurudi SHAMBA katika
-Nafikiria Kurudi Shamba
Au tu
PATRICK BALISIDYA na
AFRO 70 Band waingilie kati tu TENA mwisho wa wikiendi yetu hii kwa wimbo
-WIKIENDI
Bado nipo hata kama kwa mtu mwingine anaweza kufikiri niko kipumbavu! !:-(
Read more...