Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Chachandu ya TUNACHOJUA sasa!

>> Sunday, February 13, 2011

MOJA ya kisababishacho yoyote ya BAADAYE ya BINADAMU,...
....kama yale ya hivi ni kweli hivi mpaka  MWAKANI bado ntakuwa naendelea kumpenda bado mpenzi KAPECHO , bado nitakuwa na kazi ,hivi  nitafanikisha tungo la MIMBA...
.... au kwa UJUMLA yale yote ambayo yanapangwa tu na BINADAMU  yafanyike baadaye na sio SASA HIVI ,...



.....ni KITENDAWILI na hayana UHAKIKA,...
.... kwa kuwa hupangwa kwa BINADAMU ajuayo SASA,...
.... na karibu wote tunajua AJUAYO binadamu SASA HIVI  labda hayana chachandu yakutosha kukabili MTU asiyoyajua ya BAADAYE!.:-(


Swali:
  • SI inajulikana labda wote hatuna hata uhakika wa ni saa ngapi  kwa uhakika angalau tutabanwa mkojo kisawasawa kesho?




Ndio,...
....labda YAJAYO kama watu HATUYAJUI kwa uhakika na labda hicho ndio kilema cha UBINADAMU!

Ndio,...
...na kwa bahati mbaya TUNACHOJUA  SASA na mapungufu yake ni MOJA ya KITU muhimu kama sio  PEKEE  kitusaidiacho kuamua mengi  kuhusu YAJAYO na ndio maana yeyote aongeleaye ya BAADAYE kwa kiasi kikubwa tu ANABAHATISHA TU kwa kuwa bado  anatumia ayajuayo SASA HIVI yenye mapungufu tu  ya KIBINADAMU!:-(


Swali:

  • Lakini umeshastukia kama sasa hivi BINADAMU wangekuwa na uhakika na ya BAADAYE katika dipatimenti ya KUJUA si kuna watu wangepaniki kila siku kwa kuwa watu labda wangejua kabisa kuwa ni lini kitarehe na dakika hapo baadaye ndio watabakwa uchochoroni au tu watafanya  mchezo wa KUFA kwa hiyo labda  hata kujisomea au kuendelea kwenda kazini wakati unajua siku zako zimeisha isingeleta maana?

Ndio,...
.... labda tushukuru hatujui sana kila kitu  SASA HIVI  wakati tunapanga ya BAADAYE,...
.... kwa kuwa tungekuwa tunajua sana kuna chachandu ingepungua ya kuendelea KUJITUMA katika ya maisha SASA kama vile tunauhakika vile na ya BAADAYE!:-(


Ndio,...
.....ukifikiria sana jinsi binadamu wapangavyo ya BAADAYE,...
... kwa mfano hata jinsi wajiwekeavyo akiba hata za fedha kwa matumaini watazitumia kesho, wajitunziavyo  bikira eti kumsubiria THE ONE, mpaka tu  waendavyo kuhenya mashule  kusoma MASOMO ambayo labda hawatayatumia MAISHANI hapo baadaye labda ni kauwendawazimu fulani au kifungo tu  kama JELA ambacho kinaondoa uhuru wa binadamu kisa tu ni kwa kuwa hajui kwa uhakika ya BAADAYE!:-(

Ndio,...
...NAWAZA tu hapa MHESHIMIWA!:-(




Hebu chapuchapu TAMISHA NICHOLLS aanzishe mshawasha tofauti kwa kutingisha kidogo makalio tena katika kutusaidia kuachana na wazo hilo hapo juu katika ndude-Bounce





Au tu Tamisha NICHOLLS asisitizie tu kitu kilekile nyomi  tu na -Badder dan DAT

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP