Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati tunawafikiria WATU ambao MTOTO MZURI hajakutananao KIMWILI bado!

>> Saturday, February 12, 2011

Ukifuatilia maisha ya MTU tokea azaliwe mpaka UTU UZIMA wake,...

.... unaweza kugundua umuhimu wa WATU ambao mtu hajakutananao BADO.

Kwa kuwa karibu kila mtu muhimu MAISHANI mwa mtu hata tukiondoa MAMA yake,...
.... labda BABA, ndugu , MCHUMBA ,mwalimu  mpaka MAADUI ni miongoni tu mwa BINADAMU mtoto atakaokutatananao baadaye  NA UMUHIMU WAO ATAKUTANANAO BAADAYE  hata kama leo labda makutano BADO.:-(


Swali:
  • AU?

Basi labda asilimia kubwa ya WOTE ambao ni muhimu leo,...
... ni  wale ambao MTU alikutananao BAADAYE katika safari tu ya MAISHA  na bila kusahau mpaka wale ambao hata  LEO mtu hajakutananao BADO !:-(


Na chakukumbuka ni kwamba LABDA mpaka leo,....
....kuna watu muhimu ambao MTU atakutananao BAADAYE  ndani ya LEO HIIHII ambao leo bado hajakumbananao BADO!


Swali:
  • Unakumbuka kuwa kuna umuhimu labda MAISHANI  mwetu hata wa wale ambao HATUJAKUTANANAO bado?
  • SI unastukia tunakumbushana tu hapa kuwa labda ni KESHO ndio utakutana na ambaye humjui ambaye ndiye jibu la MASWALI yako?


Ndio,....
....pamoja na KWAMBA  umuhimu wa MTU sio mpaka ukutane naye,...
..... bado kuna mambo huwa MPWITO TU KWA SANA  pale tu ukutanapo na  ambaye NI MUHIMU kwako kama vile lile lililowahi kugeuka muhimu kwa  MTU  UMJUAYE baada ya kukutananalo mbele ya SAFARI YAKE ya maisha nakuligeuza kuwa LIMCHUMBA lake ili liwe LAKE  kitamu za maisha mpaka wakati yuko UCHI lotelote!:-(


Ndio,...
..... labda tukifikiria ambao hatujakutananao na kuwazua yaliyofichika HATA NDANI YETU ambayo  labda YATABUMBULUKA TU pale tutakapo kutananao wastuao mioyoni au akilini mwetu yategemeayo  MTU mwingine tukutanenaye,....
... labda kwa ambao HATUJAKUTANANAO tutegemee lolote!:-(



NI wazo tu hili mkweche MHESHIMIWA!:-(
Jumamosi NJEMA Kingunge!


Na hebu TABIA asawazishe mudi kijiweni kwa-They LIE


BOMANI aingilie kati shughuli kwa -La BUSH



Au tu na LUTA achanganye manyanga kwa - TIGHT spot

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

nyahbingi worrior. 9:23 am  

mkuu Simon,habari zasiku,nimepita kibarazani kwako kukujulia hali.

amani mkuu.

Yasinta Ngonyani 10:28 am  

jumamosi njema nawe pia!!

Goodman Manyanya Phiri 3:06 pm  

Kitururu Mkuu!

Asante sana kwa kutuweka kiakili MAXHAPESHU ("pilikapilika", kwa lugha yetu ya Kixhosa, Afrika Kusini).

Ya umuhimu ni kwamba wale tunawowajua tuwafanyie bila kukosea haki na majukumu yao kama inavyostahili.

Haohao ndio daraja ya kutufikisha kwa wale tusiyewajua.


Kwa mfano. Inawezekana hujawoa na unataka kwanza mchumba na kumbe Mwenyezi-Mungu amepanga umpate huyo mchumba pitia binamu yake mama yako.


Sasa kama hukuonyesha pendo na heshima kwa huyo unayemjua (binamu yake mama yako) utafanikiwa kweli kumchumbia usiyemjua (mtoto wa rafiki yake binamu yake mama)?

Simon Kitururu 9:13 am  

@Rasta LUIHAMU: Asante Mkuu kwa kunitembelea! Vipi MTWARA hakujambo? Na shemeji vipi? HAJAMBO?

@Mtoto mzuri YASINTA: Asante Kimwana!

@Mkuu GOODMAN:Nakunukuu katika baadhi ya mahubiri yako: ``Ya umuhimu ni kwamba wale tunawowajua tuwafanyie bila kukosea haki na majukumu yao kama inavyostahili.´´- mwisho wa nukuu.


Naendelea kuwaza comment yako NGULI ambayo inaendelea kunifunza na kuniwazisha!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP