Kuchamba kwa aina yeyote ni staili tu mojawapo yakushika mavi.
>> Tuesday, February 13, 2007
Kwetu wengi ni ujanja kukimbia baadhi ya kazi ziletazo masilahi katika maisha.
Tunachagua kazi kutokana na sifa au tafsiri ambayo kwa vigezo fulani inaleta aina fulani ya heshima ikubalikayo katika jamii ilengwayo.
Wakati nafuatilia maswala ya ni nini taaluma au kazi yenye heshima nikastukia kuwa jambo hili si rahisi kama nilivyokuwa nafikiria.
Nikakuta kuna jamii marubani ndio wenye heshima zaidi.Jamii nyingine ni madaktari.Nyingine wanasiasa , wafanyabiashara nakadhalika.
Halafu nikastukia pia jinsia huchangia pia katika kuchagua hadhi ya taaluma fulani fulanni. Nasikia siku hizi mitaa ya Brazil ,ukiwa daktari uliyebobea katika operesheni plastiki zenye kulenga urembo, basi wewe ndio kiboko.Wakati wasichana wengi Russia inasemekana wanakuheshimu sana ukiwa mfanyabiashara.
Sasa ukisikia jinsi maswala ya kubeba maboksi na ufagizi yanavyozungumziwa na baadhi yetu utaweza kufikiri hiyo ni kazi ya ajabu sana.Unaweza kufikiri kuwa wafanyao kazi hiyo si muhimu. Lakini ukweli ni kwamba kazi ni kazi.Na kazi yoyote inayo kupatia maslahi mimi naamini ni kazi bomba. Na mara nyingi hizi hughuli ambazo hata hatuzitaji kwenye umuhimu , ndizo zitusaidiazo sana kila siku.
Swali:
Umuhimu wa kazi ni nini basi kama si kukupatia maslahi?
Halafu je, unafikiria ni kitu bomba kama watu wote watabobea kwenye shughuli zile ambazo jamii fulani imechagua tafsiri ya kwamba zina hadhi ndogo?
Hivi hadhi yako si kitu cha kufikirika tu kwako na hata katika jamii?
Au unafikiri kuna ukweli wa zaidi ya kifikira?
Ndio, madaktari ni muhimu, lakini unafikiri waosha maiti wakikosekana nini kitatokea?
Unakumbuka moja ya kitu kitufanyacho kuwa binadamu baada ya kula ni ile haja ya kwenda haja kubwa. Baada ya kumaliza haja ,kuchamba kunafuatia.
Hapo kila mtu sasa huonyesha maringo yake dingiri dingiri mpaka chini!
Wengine hutumia maji ,
Wengine makaratasi,
Mawe,
Majani,
Mchanga,nk.
Kila mtu hutetea staili yake ya kushika mavi inamafanikio zaidi.Au wengine husema ni ya usafi zaidi.
Lakini lengo la wote ni moja. Kuweka moja ya sehemu nyeti katika mwili wa binadamu iwe safi.
Lakini mimi naamini hiki kitendo wote tunakifanya na hatukionei kinyaa.
Hivyo kama wote tunaweza kufanya kitendo hiki mara kwa mara, sioni sababu ya sisi walewale kuanza kufikiria eti kuna baadhi ya shughuli haitufai au ina hadhi ya chini.
Kwamaana naamini kitendo cha kuchamba ni shughuli ya hadhi ya chini ambayo wote huishughulikia kwa makini na mafanikio bila kulalamika.
Duh! Hivi kitendo hiki cha kuchamba ni cha hadhi ya chini kweli?
Halafu ushastukia kuwa vyote tuvitumiavyo kufanikisha shughuli hii ukiviangalia katika kona nyingine vyote ni uchafu?
Hapa nazungumzia maji,makaratasi, mawe majani na vingine vyote vitumikavyo kama makokoneo.
Maji yaweke yasipotakiwa, makaratasi ,nk. yote yanafanikisha tafsiri ya uchafu.
Pia yanaweza kuitwa uchafu kama hayalengi ufumbuzi wa jambo lilengwalo.
Sasa sikatai kuwa taaluma yako ni muhimu kwako.Sikatai kuwa jamii inatafsiri na kuzipa hadhi taaluma fulani fulani kutokana na mahitaji yake katika jamiii. Sikatai kuwa taaluma yako inaweza ikawa ndio inaumuhimu katika jisi utafsirivyo hadhi yako.
Lakini kama unaenda haja kubwa na unachamba , mimi nahisi tuko katika hadhi moja.
Unaweza kunibishia na kunikatalia lakini!
Swali:
Hivi kwanini kinyesi cha mtu mwingine kinatutia kinyaa kuliko cha kwetu wenyewe?
Au ndio kinanuka zaidi?
Duh!Sijui kwanini kitendo hiki kinaitwa kujisaidia.Lakini tusisahau kushukuru kama tunapata choo.Kwa maana inamaanisha tumekula chakula.Na tusisahau kuwa kunawatu wanakufa njaa sasa hivi.
Haya tufanyeni tu hizo kazi zitupatiazo maslahi.
Siku njema!
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Umeniacha hoi na Ndingili ndingili mpaka chini. Ila uliyosema yote ni kweli tupu.
doh!
"WEngi wanataka Jina Mimi nataka heshima" kunha msanii mmoja aliimba hivyo.Nyumbani sasa hivi moja ya kigezo kinachofanya wasiokuwa na kazi kuongezeka ni kitendo cha kutafuta "heshima" yaani wanaita heshima katika kazi.
Wote ya wasomi wetui wanataka zile zinazoitwa White Collar Jobs na sio Blue Collar jobs.Kila mtu anataka kufunga tai na kiyoyozi kikubwa.
Ukienda sasa hivi kuwauliza watahiniwa wa B.com pale mlimani wantaka kufanya kazi wapi wakimaliza masomo yao basi wengi watakuambia CRDB,BOT na sehemu kama hizo.
Simon,
nimekushtukia kuwa wewe ni mchokozi sana. Tena sana. Huwa nacheka sana nikisoma maswali yako. Changamoto nzuri sana na kama usemavyo, ni chakula cha fikra.
@Ndesanjo:Duh!
[url=http://firgonbares.net/][img]http://firgonbares.net/img-add/euro2.jpg[/img][/url]
[b]autocad mep 2009 sheet set list problems, [url=http://firgonbares.net/]top educational software[/url]
[url=http://firgonbares.net/][/url] shop 2.0 by software site to buy software
where to buy adobe photoshop [url=http://firgonbares.net/]adobe creative suite 4 production premium crack[/url] i sell oem software
[url=http://firgonbares.net/]buy the photoshop[/url] egghead discount software
[url=http://firgonbares.net/]university software discount[/url] buy software license
buy open source software [url=http://firgonbares.net/]downloadable software[/b]
Post a Comment