Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Marafiki asanteni!

>> Tuesday, February 06, 2007

Tokea nianze kublogu nimebahatika kujifunza mengi lakini pia nimefanikiwa kujenga uhusiano na wanablogu kibao. Wengi wao sijawahi kukutana nao lakini huwa nasahau kuwa sijawahi kuwaona uso kwa uso. Naamini hii ni moja ya nguvu ya blogu. Wanablogu kama NDESANJO, EGDIO, DAMIJA, Luihamu...nk huwa nasahau kabisa kuwa sijawahi hata kukutana nao, kwa jinsi nilivyowazoea kifikira.Ila Rasta Luihamu wewe mdini ile mbaya! Nakutania:-). Wanablogu kama MWANDANI, JEFF , MJENGWA, nk blogu imerudisha mawasiliano ya karibu kwani ni siku nyingi hatujakutana. Na kizuri ni kwamba kila siku nakutana na kujifunza kutoka kwa watu wapya .

ASANTENI WANABLOGU WOTE!

Siwezi kusahau kuwa marafiki zangu wote hunipa tafu sana. Napenda kuchukua nafasi hii nyingine kuwashukuru wote, kwa yote. Sina picha za wote lakini nimeona niweke baadhi ya marafiki zangu ambao tumebahatika kukutana siku za karibuni na nikabahatika kuwa piga picha.

Basi baadhi ni hawa.....
Bonanza na Rummy














Halafu unajua watu wengi hawajui Rummy ni Mtanzania....hebu mcheki hapa akiwa na bendi yake ya MIGHTY 44




Haya tuendelee..




Erick
















Ronaldo












Deo


















Aliko
















Edo,-na Raymond













Gonzaga a.k.a Mr Dj













Erick the Godfather













Chriss a.k.a T.I


















Byamungu a.k.a Smooth












Chacha

















Ben a.k.a Terminator















Allen


















Mernad a.k.a Promotor












Mtimkubwa, -, na DJ Ezza





Haya jamani tuendeleze libeneke!

12 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Kibunango 5:00 pm  

Zaidi ya Kuwashukuru warafiki wa blog ambao licha ya kutoonana nao bado unahisi kama umeonana nao, nami napenda kukupongeza kwa kuniwekea marafiki ambao sijawaona kwa muda mrefu sasa. Nina matumaini ya kuwaona katika Fest Afrika (Winter Jam) kama wataweza kutembelea hapa Tampere!

Simon Kitururu 8:52 pm  

Kibunango, nafikiri wengi wao wataingia hapo katika Fest Afrika. Halafu usishau kuwa bloguni kwako mimi niko kila siku. Sijakusahau Mzee!

MTANZANIA. 5:20 am  

Hizi ndio faida za utandawizi! Japo hatufahamiani lakini tunabadilishana mawazo kwa kuheshimiana.

Mija Shija Sayi 8:18 am  

Kitururu blogu ni kitu cha ajabu sana, kama unavyosema tumekuwa tukijadiliana mambo utadhani tunajuana. Kweli hii ni njia bora ya kujenga urafiki na sipati picha siku tutakapoona wote kwa mpigo ninaamini inakuja.

Shukrani.

luihamu 2:19 pm  

Kweli Da Mija ipo siku tutakutana wote nadhani itakuwa siku ya furaha sana.Leo hii nimekutana na Maggid Mjegwa kanitembelea Ofisini na huu ndio mwanzo wa Jumuiya yetu.Mzee Simon tutakutana ndani ya ZION TRAIN.Jah live.

mwandani 2:57 pm  

Ahsante kwa picha safi kabisa. Ndio mtandao wa blogu tutaonana siku moja.

Si utani, kiwanja kina washikaji poa sana. Baada ya masiku tele nawaona wazee kina Bonanza na Ezza na wengine wengi.

Ombi: naomba uniwekee picha ya mshikaji Kijugu.

Anonymous 7:20 pm  

Umesema sawa Simon. Pengine wakati mwingine tunachukulia kuwa faida ya blogu ni kuwa na uwanja wa kujieleza, kupeana habari na elimu na kusahau kuwa blogu ni chombo cha kujenga uhusiano na watu ambao bila blogu, pengine usingejuana nao wala usingejua fikra zao kuhusu mambo mbalimbali. Nami nashukuru sana kujuana nawe kupitia mtandaoni. Na ningependa kusema kuwa blogu yako imeleta shamrashamra ya aina yake kutokana na uwezo wako wa kuweka mambo mapya na pia video mara kwa mara. Mwendo huo huo.

Luihamu: Rasta naona una hamu sana ya kukutana na Da Mija.

Da Mija: si ukutane tu na Rata kiishe?

Mija Shija Sayi 8:15 pm  

Lazima nimtafute Ras Luihamu, ninataka nihakikishe kama anaishi maisha anayoyahubiri. Hivi majuzi kule kwake ametuambia eti yeye hataki kumiliki nyumba bora(mwenyewe anaita ya kifahari)Kama nyumba mbili zikitolewa ya kifahari na duni yeye atachagua duni.

Sasa nitafanya matembezi ya ghafla nione anaishi nyumba gani? Naamini Dar kuna nyumba kama kibanda alichotuwekea.

luihamu 6:57 pm  

Ndesanjo umesema Natamani sana kukutana na wana blogu wote sana sana Da Mija.

Mzee Simon nimejifunza mengi kutoka kwako ingawa hatujawahi kukutana.Mara ya kwanza ni pale mzee wa rundugai alifunguwa blogu yako na kupenda unayoandika.

Nimejifunza kukubaliana na wewe au kupingana na wewe lakini haijawahi na haitawahi kutokea turushiane maneno machafu au matusi.

Ndoto yangu tukutane wote.
Jah Rastafarian.

Jeff Msangi 6:05 am  

Simon,
Nimechelewa kidogo kupita hapa na kusoma habari hii.Kisa,eti nina mafua!
Hongera sana kwa kazi nzuri unayoifanya.Naamini tutaonana tena siku si nyingi nitakapofanya ziara ya huko kwa "wazungu".Salamu kwa MtiMkubwa.

Anonymous 9:31 pm  

Simon nimefurahi kuona jamaa niliokuwa nao huko kwa wafinn miaka ya 90 bado wapo ndio utamu wa blog unapata taarifa ambazo saa nyingine sio rahisi kuzipata. Kazi nzuri ndugu yangu mimi huwa natembelea sana blog karibu zote siunajua tena ukiwa mwanahabari na ninasema wote nawafahamu na siku moja tutakutana uso kwa uso.

Simon Kitururu 12:42 pm  

Mzee Anonymous wa hapo juu tustue jina basi?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP