Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Maswala ya kitu MUHIMU kwa binadamu wakati ANASUBIRIA kuwa ''MAREHEMU Alikuwa MTU MZURI!

>> Wednesday, June 25, 2008

Tafsiri ya chochote kile yaweza kusababisha mtu awe kapata au kukosa.
Ukifeli mtihani inaweza kuwa ndio somo kubwa kwako la kufaulu mtihani.

Tafsiri ya kuishi miaka mingi, inaweza kuwa ni jinsi tu ya binadamu achelewavyo kufa.

Kuna vitu kibao mtu huweza kusema ni muhimu sana maishani mwake hasa kutokana na ubahiri wake au ukarimu wake kwa binadamu mwingine au hata dunia.

Vitu kama familia, ndugu, marafiki au staili ya kumzimia MWenyezi MUNGU ,ni moja au mbili tu ya baadhi ya yale yawezayo kuwa karibu katika fikira ,ukimuuliza yule au yeye kuwa ni nini muhimu maishani mwake, ingawa inawezeka KWA KULA mlafi kasingiziwa.

Lakini.....
......INAWEZEKANA, maadui, kutofanikiwa au hata shetani atusaidiaye kukumbuka kuabudu Mungu , vyaweza kuwa na umuhimu katika dakika hizi tuishizo au tuziitazo kuwa tuko hai.

Lakini.....

....INAWEZEKANA, naogopa kuamini kuwa kitu muhimu kwangu ni cha kijinga kwako.

Kumbuka tu, tafsiri yako ya kitu inaweza tu ndio ikawa imekufanya uwe na furaha au huzuni leo.
SWALI:

  • Kwa tafsiri yako leo, wewe umefanikiwa au umeshindwa ?
  • Unafikiri tafsiri zako za maisha zinaathiriwa vipi na mtazamo wa jamii kwako?
  • Ushawahi kufikiria tofauti za mtazamo wako kuhusu wewe binafsi UKIWA CHOONI na UKIWA STESHENI ya BASI zitofautianavyo?
NAWAZA TU hapa MDAU!
SIKU njema!


Unaweza kumsikiliza kidogo Matthieu Ricard ajaribu kukupa mtazamo wake wa TABIA za kuwa na FURAHA


Au wacheki wapenzi wapendao kuishi uchi , wakisaidia kutukumbusha mapenzi ya binadamu kwa binadamu ya kibinadamu

Au msikilize tu ABETI MASIKINI kama mimi, akukumbushe kabla ya ndombolo ya SOLO

DUH !Naacha ingawa natamani kukuacha na TPok JAzz

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 7:44 am  

Leo umegusa,umenikumbusha JUMUWATA niliyojitolea lakini.........

mizimu ya babu zetu ilisema
usilolijua ni sawasawa na kiza kinene.

Rasta hapa.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP