Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UNAUHAKIKA unafikiria JIPYA leo AKILINI lililo TOFAUTI sana na Ulivyofikiria JUZI ?

>> Saturday, June 28, 2008

INAWEZEKANA hakuna JIPYA!:-(

Kuna mambo , ni staili yako ya kuyafikiria leo itofautishayo ULIVYOFIKiRI mwaka juzi!
Kwa ujumla inawezekana kila siku tokea uzaliwe kuna mambo yajirudiayo ambayo siku nyingine eti utanikuta nimenuna kana kwamba ni jambo jipya!

Sasaaa.....
Kutokana na taarifa bwelele kuhusu NANIHII zote watu wajuazo ,nikichezea moto nikaungua, na maswala ya ukicheza peku si lazima upate au umgawie mimba yule nanihii , SI ni jambo lijulikanalo na KWA HIYO nikipata UKIMWI au kwenda MOTONI au akipata mimba, pale nikifanikiwa kufa, si nisi- AU asi-shangae?

AU?

INAWEZEKANA tokea asubuhi mpaka jioni , ni chaguo lako tu la nini au nani UNATAKA kiuumize roho au kiangalie mnato katika makalio yako ili ustukie LEO ambacho KILIKUWEPO jana au walikuwepo tu tokea msimu wa UKWAJU.

Swali:

  • Unafikiri ni mangapi uyapitayo njiani bila kuyaona lakini unamstukia nanihii?
Samahani narudia mcheuo...
Nahisi labda fikira zako za jana zinaweza kuwa ndio hizo hizo zikuzinguazo leo ila staili tu ndio ya leo inaweza ikatofautisha MAPENZI yako kwa NYERERE , KIGOLi au RAis MUGABE.
Kwa mfano:

  • Kama una njaa leo , utafikiria kuhusu maswala ya kula kama juzi tu, labda staili ya kupata CHAKULA ndio itafanana na ya mtondogoo.
  • Kama wewe muhusika huna uhakika na wewe mwenyewe , watu wakicheka leo utahisi wana kucheka kama juzi tu ulivyofikiria.
  • Kama wewe mwanaumume , kuna kamuda kwa siku, fikira za UASHERATI ukiona au ukikosa nanihii zitakuja kama juzi tu , hasa kama mazingira ni ya kawaida na hufukuzwi na kicheche ndani ya muda .(Si ndio maana wenye busara wanashauri tuondokane na UKAPERA?)

Sasaa....
Ni mangapi umefikiria leo ni sawasawa na MWAKA JUZI?
  • Na ni kwanini leo au juzi ya wiki iliopita inawezekana ukawa unahisi UMEFIKIRIA ZAIDI na unakumbuka zaidi UBWABWA wakati jana katika yote uyakumbukayo ukipewa karatasi itachukua muda kuyaweka yote ndani ya kibwagizo?

  • Hivi si Ubongo wa binadamu unafanyiakazi mambo bilioni kwa sekunde?Sasa kwanini unakumbuka unachokumbuka na hukumbuki usichokumbuka?


DUH!
NAWaZA tu hapa na NAACHA topiki!
JUMA fulani NJEMA!

Mpate kidogo Youssou N'Dour na Neneh Cherry wa kupe maswala ya "7 Seconds"


AU ngoja Murray Gell-Mann achokonoe kiduchu hamu yako na yangu ya kudadisi kuhusu swala la:Do all languages have a common ancestor?

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Egidio Ndabagoye 11:20 pm  

Mkuu nimekuandikia barua pepe kwa anuani ya Gmail,sijui nimekosea

Simon Kitururu 12:03 am  

@Egdio:Sijaipata.nitumie kwenye: skitururu@gmail.com

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP