Thamani ya HESHIMA ya kijambo!
>> Thursday, July 03, 2008
Kama unaishi inamaana unathaminisha vitu.
Kama unathaminisha vitu inawezekana unadharau kitu au kuna kitu unafikiri kinathamani zaidi ya kile , hiki au hata nywelenywele za kikwapa cha nanihiii.
Lakini ....
Labda thamani ni kama noti ya pesa ambayo ni karatasi tu, wengi mkiwa na machale nayo, inageuka kuwa kama pesa ya Zimbabwe mwaka 2008, ambayo hata uwe na noti ngapi, unawezapata tatizo lakukusaidia kununua vikusaidiavyo kukuwezesha kwenda choo.
Labda hata thamani hata ya maneno inafanya tuamini kuwa maneno fulani ni machafu na mengine ni ya kuimbia kwaya KANISANI au pale chini ya MBUYU.
AU
Labda kweli kuna uchafu na usafi, hasa kama kwako vipodozi ni usafi ingawa huvilambi, mate kwako ni uchafu ukitemewa lakini si ukipigwa busu, au ukioga unaamini ngozi ishakuwa safi kama tu uaminivyo ukipiga deki, sakafu ni safi.
Angalau bado inasemekana;
HESHIMA ni kitu cha BURE.
NA....
Labda ni kweli kuna kitu umewahi kufanya kwa thamani iitwayo bure!
Lakini ni kweli inasemekana ,
.... kuna vitu baadhi ya watu wanaweza wakakiri kutoweza kuthaminisha, kama vile, mapenzi yao kwa wazazi , ndugu ,jamaa au limpezi nanihino.
Swali:
- Kitu cha bure ni nini?
- Unafikiri thamani ya kitu ukiitacho cha bure ni sifuri?
- Thamani ya kitu ni nini na inatoka wapi?
SIkuKATAliI!
Lakini......
.... kuna watakao kubaliana na mimi kuwa , hakuna kitu cha bure, inategemea tu na vitu vyako unavithamanishaje.
Unaweza kujisahau na kufikiria hela ndio kipimo cha thamani ya chupi, wakati dagaa au bata waweza kuwa kipimo cha thamani ya mahari ya Simon katika kumposa Mwajuma .
Swali:
- Ingekuwa utumwa ni biashara bomba, unafikiri ungemdaka Kijeba mtaani leo,ungemuuza shilingi ngapi?
- Na bei ya yule Mwanadada macho ya gololi je?
Sasaaa....
Naamini thamani ya kitu inatofautiana kati ya mtu na mtu.
Inasemekana kwa Muisraeli mmoja, ni Wapalestina kadhaa wa kadhaa jichoni kwa baadhi ya Waisraeli fulani.
Labda Kikwete mmoja anaweza akawa akina mimi kadhaa vilevile jichoni kwa yule au yeye.
Na labda Kikwete kabla hajawa Nyerere alikuwa sawa tu na Mkapa au Ali Hassan Mwinyi kabla hawajawa Nyerere.
AU
INAWEZEKANA ukweli ni hakuna chenye thamani duniani kama jamii, wewe na mimi hatujakipa au kuamini kina thamani.
NA
Kijambo kinaweza kudhalilika kutokana na harufu , lakini jamii ikiamini harufu ya kijambo ina thamani kubwa , hutakawia kuona vichupa vya pafyumu za kijambo chenye mchanganyiko wa HILIKI au MAHARAGE, ni maarufu duka fulani pale nanihii.
Lakini,
...serikali ya TANZANIA au ya ..... inaheshimu na kuthamini raia wa nchi yake, wakati askari wake hawakawii kukupiga virungu ukidai kuheshimiwa kama raia wake.
AU labda ni kweli....
..Dhahabu,almasi, pesa , ndovu ....mpaka Bata wanathamanisha vitu fulani kama unataka kujua thamani ya kitumbua.
Lakini labda wewe unathamani kwangu kwa sababu hakuna mwingine kama wewe duniani.
Labda umuhimu wa kile kwako ndio una sababisha uone hiki kinathamani kwako.
Cha ajabu ni kwamba nionacho hakina thamani chaweza kuwa ndio kitu muhimu kuliko vyote kwako.
- Si unakumbuka kama uthaminivyo wazazi wako, wako wawauao wazazi wao ili wapate urithi?
- Si unakumbuka kucheua kudharauliwako sehemu nyingine, kuna maeneo kinatumika kutoa heshima kwa mpishi katika kuonyesha jamaa wameshiba?
- SI jangwa kama SAHARA tulipigalo vita kwa baadi ya makabila ya Waberiberi ndi mahali pazuri kuliko pote duniani?
Basi bwana Naaacha topiki hii Mkuu!
Nawaza tu hapa katika mtiririko fulani !
Nakuthamini lakini!
AU?
Kwani wewe au mimi unadhani ni shilingi au talanta ngapi?
...
Kila lakheri katika kuendeleza kuthaminisha vitu, watu au hata matako ya Ngedere!
TUKUMBUKE tu kuwa BURE pia ni thamani!
..........................................................................................................................................................................
Hebu kama una muda mcheki tena James Randi atukumbushe jinsi ya maajabu katika saikolojia ya sisi wenye kuamini na kusoma Nyota zetu Magazetini.
Mcheki akitazama Astrology
Ningependa kuwashukuru tena ndugu, marafiki na maadui!
Hasa marafiki hawa niliokutanao na kuwadaka muda wa karibuni kama watokeao na wasio tokea kwenye baadhi ya picha zangu zifuatazo:
EBWANA samahani nilizimika!Kwa waulizao , ni kweli nilianguka:-(
ASANTENI!
Hebu tumsikilize Aretha Franklin akithamanisha HESHIMA katika wimbo R.E.S.P.E.C.T
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment