Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKIMCHUNGULIA akataye MITI katika Ule msitu pale MBELE kidogo ya NANIHII!

>> Thursday, July 03, 2008

Kama mimi na wewe tushafundishwa maswala ya UMUHIMU wa BAJETI halafu tukachacha katikati ya mwezi, wakati mwanzo wa mwezi tulikuwa na pesa yakukupitisha mwezi mzima , kwa mtazamo mwingine , wewe na mie hatuna tofauti na aliyefundishwa UMUHIMU wa MISITU halafu akakata mti ,akifikiri atapanda mwingine baadaye kidogo kabla msitu haujaisha.

Tofauti ni kwamba ukichacha unaweza ukakopa au kuvizia misiba mpaka mwezi ukapita(si kwenye harusi ukizamia ni rahisi kustukiwa kuliko msibani?), na ukikata mti , kuotesha msitu mpya ni vigumu ,kutokana na muda au hata hali ya hewa iharibikayo au hali iuleteayo mizengweMTI KUKUA hasa pale UKUAPO wakati tunautolea macho kutokana na msitu kutokuwepo.

Sasaaaa....

Yule , yeye na mimi, tunaweza kukubali kuwa mtu na akili zake hawezi kuondoka tu nyumbani kwenda kujikatia miti bila sababu. Tunajua karibu watu bilioni tatu wanatumia kuni na mkaa ili kuhakikisha kisamvu au maharage yameiva.Kwa hiyo kila siku kuna watu bilioni tatu kinamna lazima wanyemele mti fulani uwe umekauka au la:-(

Halafu ,....
....kwa wale ambao hawajawahi kukata mti , napenda kuwakumbusha kuwa kukata mti sio kazi rahisi sana, hasa ukikumbuka wakataji miti waliowengi duniani hawana vifaa virahisishavyo sana kazi hii ya kutengeneza jangwa ,zaidi ya shoka , panga au goti.

Basi labda ....
....kuna watakao sema kuwa kupanda mbegu ya mti au kupanda mti ni rahisi kuliko kukata mti na wakaanza kushangaa kwanini wakatao mti walio wengi hawapandi mti.
Inawezekana ukafikiria hivyo kirahisi kama utasahau sifa ya binadamu ya kufikiria ya leo zaidi ya ya kesho au mtondogoo.

TATIZO hili la kufikiria kesho au kizazi kijacho linafundishika zaidi hasa pale binadamu anapokuwa na uhakika wa kwake binafsi kuhusu kesho au baadaye ataimuduje kitu ambacho ni kigumu kwa maskini .

Swali:

  • Kwani unafikiri ni kwanini raia wa nchi tajiri ni rahisi zaidi kufikiria maswala ya vizazi vijavyo kuliko masikini ambaye hata kila mtoto amzaaye anaamini amekuja na ridhiki yake?
  • Ukiwa na njaa leo huwa unakumbuka sana jinsi utakavyo kabili mambo ya mwaka kesho?
  • Ukiwa na njaa sana leo ni ndugu zako wangapi wasiohusiana na wewe kula leo wakujiao akilini pamoja na mapenzi yako kama nyonyo kwao?

Nachojaribu kusema hapa ukiachia miti na misitu ni kwamba, tabia ya binadamu umchekaye au umdharauyo inaweza ikawa sawa tu na yako wewe au mimi, ila labda mimi na wewe tunafanya makosa hayohayo katika kitu kingine ambacho hatukiangalii kwa mkao wa jicho tumchungulialo tumnyosheaye kidole.
Ukifikiria sana kosa la mkata mti na kosa ufanyalo , vyote vyaweza kuzaa matunda sawasawa tu, kama vile jangwa .

Au labda...
....Kosa la bajeti au hata lile katika kucheza mchezo wa UASHERATI a.k.a MIKASI, wakati umedhamiria kustarehe halafu ukastukia unalia kwa kupata mzigo wa KUZAA au hata bahati ya KASWENDE usiyoitarajia , laweza kuwa kisaikolojia lina mizizi sawa na kosa la asiyejali akikata mti halafu analalamika akiona JANGWA.

SWALI:
  • Una uhakika ukikata mti utapanda miti?
  • Unakumbuka kama ukikata mti halafu ukapanda mti na sio miti labda unapiga makitaimu?

Naacha basi topiki!
Labda hata mtiririko wa mawazo katika swala hili uko kushoto.
Samahani! Si kujihami IMO?
AU?
Hebu tuangalie afanyacho BILL GATES siku ya MWISHO KAZINI au hata baada ya KUNG'ATUKA

AU tumsikilize tu Teddy Pendergrass aliyekuwa maarufu kwa kupiga SHOO kwa WANAWAKE pekee, atukumbushe STAREHE yaKUJUA UMPENDAYE ANAKUPENDA PIA:


Samahani,labda nikulete miaka ya karibu kidogo na ya miaka ya sasa kwa donell jones : anung'unikie maswala ya : U know what's up

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP