Kuna mambo ambayo tunajitahidi sana kuyapinga kama binadamu. Lakini kuna mambo hayapingiki kama sisi ni binadamu. Au niseme.....
Lakini kuna kitu nashangaa baadhi ya watu wananitumia barua pepe kuwa niache kuweka. Mojawapo ni picha zangu na za rafiki zangu. Napenda kusema ni ukweli rafiki zangu kibao picha zao hazija tokea hapa. Na walio tokea ni rafiki zangu kibao pia ambao sijilaumu kwanini ni rafiki zangu ambao ukweli wananisaidia kujisikia naishi kisawasawa. Ee bwana eeh! Kama unajua maana ya blogu, basi niache nifanye nacho takakufanya na nachofanya. Duh! Tuishi basi! Kwa wale wanaodai nimezidisha labda niongezee na picha za leoleo. Lakini kwani ni nini nimezidisha? Kama tunapata choo basi siye mabigwa.AU?
Au labda...
Samahani lakini kwa kukataa kuacha kuweka mambo yangu au picha zangu. Au msikilizeBuju Bantonakisema Destiny
Ukiwa mgojwa huna ujanja.Dakitari akisema hunabudi kutii.Ubishe unalakubisha? Kweli usipoangalia unaweza kuamini kuwa mnyonge hana janja ya kusema hapana.
Duh!Au niseme.....
KUMTONGOZA MGONJWA! Mgonjwa si mali Hana kauli hata pale penye wali Na sina hata kaushauri Mambo yote ajua dakitari Yasemwa kauli zake si hatari Japo twajua hata kwa siri Si zote siku ye kachumbari
Lakini samahani! Nsikuweke mashakani Masharti kufuata kijiweni, so ndo maji wapata kisimani? Mwamini jiamini Je ni kweli huna jinsi? Jiamini muamini Je umelikwepa jinamizi?
Mwamini usimuamini Jaribu pata yako firigisi Na: Simon Kitururu Nakuacha na Manu Dibango basi akupe Afrika.....
Kuna mambo ambayo tamaduni nyingi zimekataa. Mojawapo ni hii ya ndugu kuingiliana kimwili au ku.........
Duh! Bado sielewi ni kitu gani kinafanya baadhi ya watu kumtamani dada au kaka yake kimapenzi. Lakini hiki kitu kipo.Wengine wanadai katika familia zinazolindwa sana. Nikimaanisha wazazi wakali, basi kuna baadhi inabidi wafanye kale kamchezo mumo kwa mumo.
Cha ajabu nasikia haka kamchezo ka kupata nyama ya hamu mumo kwa mumo si kuvunja sheria katika nchi nyingi. Halafu unajua tena enzi hizi za demokrasia wadau wa Ujerumani wanapigania haki ya kula mapochopocho ndani kwa ndani. Wasikilize basi dada na kaka hawa wakipigania haki yao ya mapenzi ya mumo kwa mumo...
Duh!Jamani haka kakitu mapenzi ni kagumu , lakini kweli ni kagumu mpaka hakapatikani nyumba ya jirani? Tupendane lakini.........!
Kuna watu wakikikutungia jina au hata wakitunga neno linashika. Kuna wengine hata wajaribu nini jina halishiki na wala kale kaneno watakako kukafanya maarufu watu wanakaacha kushoto.
Katika baadhi ya watu jina lao kama halishiki kama lilivyo basi watu hawachezi mbali na jina lake.Tukianzia na Amerigo Vespucci. Huyu jamaa kutokana na vyanzo vya habari vingi tu, ndio inasemekana aligundua Marekani na sio Christopher Columbus kama isemekanavyo. Inasemekana misafara ya kadhaa Mzee Chris alikuwa anaishia katika visiwa kadhaa kama West Indies nakadhalika. Lakini haya yote inategemea na vyanzo vya habari tofauti kuegemea sehemu tofauti. Tukirudi kwa Amerigo, huyu ndio inasemekana alichangia sana uchorwaji wa ramani ya marekani. Kwa kushirikiana na mchora ramani waenzi hizo maarufu aitwaye Martin Waldseemüller Huyu mchora ramani alipomaliza kuchora ramani ya dunia bara la Marekani akaliita America kwa kuhusisha bara hilo na stori za Amerigo na mtazamo wa Amerigo aliompa. Katika historia utakuta kunakipindi wachora ramani walitaka kubadili jina hilo kutokana na mashabiki wa Christopher Columbus kumpiga vita Amerigo kuwa muongo. Lakini wapi jina likan'gan'gania mpaka leo. Sitaki kuingia ndani katika swala hili la Christopher Columbus na Amerigo nani mkweli au muongo. Lakini nafikiri wote tutakubali kuwa wadau wa Christopher Columbus wamefanikiwa kumuekajina lake masikioni mwetu kuliko wadau wa Amerigo. Kuhusu kwanini likaitwa america na sio amerigo, kuna stori nyingi. Lakini iliyo shika ni kwamba mabara yote yalikuwa yanachukuliwa katika majina ya Kike. Africa, Europe....nk yote ni majina ya kike enzi hizo. Lakini....
Lakini poa tu ukimuita mtoto wako wakiume Africa. Sikuizi yote zembwela , ngoma ya ukae.
Afrika , hili jina kasheshe. Wengine wanadai hawa jamaa waitwao Afri kutoka Tunisia, kuwa wamechangia. Wengine wanadai limetokana na neno Aprica la kilatini nimaanishalo sehemu yenye jua. Wengine wamedai kuwa linatokana na neno la kigiriki Aphrike limaanishalo bila baridi.
Lakini unajuatena hakuna haja hapa yakuingia sana. Nachotakakusema kuna kamjamaafulani sina uhakika nani lakini nahisi ni kajamaa ka bara jingi kakasema na jina liwe Afrika. Na likawa.
Lakini....
Ziwa Victoria tumeenda mbele sendema kurudi nyuma sendema. Lakini pamoja na kujua jina lake la kweli, Watanzani wengi bado twaliita Victoria.
Dar-es-Salamu-Duh !Hivi Mzizima lilikuwa naubaya gani?
Na kadhalika kadhaa. Najua unajua majina kadhaa tuyatumiayo au
Usitishike.Labda jina ni jina tu. Au? Mimi mwenyewe nimefanikiwa kuitwa majina mengi. Nayameshika.Lakini chaajabu vikundi tofauti vyaniita jina tofauti. Hakuna noma lakini. Nimejaribu kutungia watu majina na yameshika. Lakini nawaonea wivu walio tungia mpaka barazima jina na lika shika.
Duh!Kumbe wivu mbaya eeh? Lakini si kweli kuwa kila wivu ni mbaya. Ukifanya vitu poa nivihusuduvyo sitakuloga napata nguvu tu ya kujaribu zaidi.
Sasa Baadaye basi! Ngoja nikuache na Sina Makosa na Soukous Stars
Napenda kukiri kuwa kuna watu wafanyavyo vitu vyao huwa hawanichoshi hata siku moja kuwa sikiliza au kuwaangalia. Lakini mara nyingi nashindwa kuacha kuzinguliwa na jinsi binadamu wanavyotengeneza vikorombezo mbalimbali vya aina mbalimbali kwa ajili tu ya kutaka kuwadaka binadamu wenzao kimawazo hata ki..... nakadhalika.
ukiangalia matambiko mbalimbali binadamu amfanyiayo Mungu wake hutaacha kuzinguka na madoido aonyeshayo. Wengine watalia huku wamenyosha mikono juu wengine watainama, wengine watalala juu ya misumari, ilimradi tu kumuonyesha Muumba au mauunguzaji jinsi gani wanamaanisha. Duh! Halafu hili swala la Mwenyezi Mungu watu wengi wanamuona kivyao!Halafu kila mmoja hakawi kuhisi mwenzie kapotea.Hapo ndio kasheshe.
Kinachoniacha hoi kingine ni jinsi binadamu akitaka kuonyesha madoido jinsi wachaguavyo mavazi yaendayo na madoido. Basi wengine watachagua kanzu, wengine vibwaya na vibuju , makofia makubwa kwa madogo na kadhalika kadhaa.
Ukweli ni kwamba hili swala la madoido nadhani mara nyingi tukubaliane tu halina mpango , lakini linaleta viutamu na vituko vyake ambavyo labda ni muhimu kwa sababu tumeamua tu kua ni muhimu .
Swali: Hivi duniani binadamu anajali vitu muhimu? Muhimu yako unaikumbuka?
Sasa.... Kwasababu tuko katika kipindi cha pasaka kwa wakrito na wakristu ngoja tuangali madoido katika kanisa la Holy Sepulchre
Hapa naona utaona jinsi madoido ya wanakanisa. Cha ajabu ni kwamba ingawa hapa ni miongoni mwa vipengele vya ardhi wakristo wavioanishavyo sana na yesu , huwa wanabwangana hapa kuhusu nani anamiliki kishkaji sehemu. Sasa hapo ndio madoido yanapo nishinda . Maana mpaka watu wanabwangana katika sehemu waziitazo takatifu. Duh! Lakini wengine wanaonyimwa kuonyeshwa madoido yao hapo wameamua kuhamia huku kwa Garden Tomb
Lakini achana na madoido ya dini zihusianishwazo na Mungu. Turudi katika uchawi.Wachawi kwa madoido huta waweza. Ila wachawi wakizungu huwa wananiacha hoi na madoido yao pia . Maana hawakawii kukuuzia DVD ujifunze nawe. Swali: Hivi kwanini wachawi wa Kiafrika wasirisiri sana? Hebu wajifunze kwa hawa hapa chini.....
Sasa kama kunamchawi yeyote atakaye tufanyebiashara yakuuleta uchawi huu karne hii tuwasiliane basi:-)
Lakini ushastukia wajanja wengi haswa hawa wanadini , wanasiasa, waigizaji na nasikia hata wachawi, ni wabunifu sana wa matumizi ya sauti. Wanajua jinsi ya kukutisha, kukufanya uwaamini, na hata....... Lakini wote mimi nawaamini kwa kuigiza.
Duh!Kabla sijaendelea ngoja nikuache na vuduMaana hii ya wadominika imeanza kuuzwa. Ya Benin na kwingineko sijasikia bado.
Sasa Tanzania vipi? Madoido ya nguvu za giza kuexport lini?Maana nasikia kuna wajanja wanatengeneza radi na kadhalika.Naamini zao la radi pekee linaweza kukomboa wengi hapa duniani kwa jinsi tesivyopendana,
Ee Bwana eeh !Kama msherehekeaji basi Pasaka njema!