Kuna watu nasikia wanajua kila kitu
>> Sunday, April 01, 2007
Maisha ni shule.Kila siku tunajifunza. Lakini kuna watu nasikia wanasema wanajua hata kama hawajui. Sasaaaa.....
ee bwana ye Luambo alikuwa anaongea hapo.
Nisikutishe !sikuelewa anasema nini.
Lakini kujua ni kitu kigumu. Nafikiri unafikiri unajua.
Lakini kuna kitu kama...ngojea niseme basi....
Sawa basi ngojea niache kusema. Msikilize basi Ninjaman
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Nina tatizo. Kama ushatembelea hapa siku kadhaa fulani . Utagundua rangi ya text imebadilika. Halafu sina muda sana wa kufikiria na kubadili hili tatizo. Nistue nifanye ninni basi kama unajua nini nifanye blogu ionekane sawa. Lakini endeleza basi. Au?
Simon ile simu imepatikana jipigie mshkaji anakusubiria.. Aliko
Simon,
Unachotakiwa kufanya ni ku-update template yako kutoka kwenye ile ya zamani kwenda mpya.Baada ya hapo utaweza kubadili kila kitu kuanzia background colours,text colors na font zake nk
Tatizo letu bin-adamu huwa hatupendi kuonekana hatujui. Ila ukweli unabaki palepale kwamba elimu ipo toka kuzaliwa mpaka siku ya kufa kwa mwana-adam. Hakuna anayejua kila kitu. Kwa maana hiyo ni vema mwana-adam akubali kuwa hiki sikijui. Nafikiri hii itakuwa ni njia muhimu ya kukijua.
Anyway! Franco alikua anaelezea mustakabali wa bendi yake baada ya kuondokewa na baadhi ya wanamuziki.
@Mtanzania: asante kwa tafsiri.
@Jeff : asante kwa dondoo. Najaribu bado kuifanyiakazi.
Post a Comment