Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Leo ni Siku Ya Malaria!

>> Wednesday, April 25, 2007


Huwa natishika sana kuiita siku moja kuwa ni ya kaugonjwa fulani.
Lakini kusema ukweli huu ugonjwa unatumaliza. Inasadikika watu milioni moja huondoka kutoka kijiwe hiki cha dunia, kila mwaka kwa ugonjwa huu.

Chakutisha nikwamba unazidi kuwa sugu kila siku!
Na kingine ni kwamba wataalamu hawachoki kutuhakikishia kuwa ugonjwa huu unakabilika!

Kinachotushinda nchi masikini ni pamoja na umaskini wetu .
Eti fedha ya hawa matajiri za kukabilia huu ugonjwa, ambayo baadhi ipo, bado ina masharti.Ukiwa hununui vyandarua ambavyo wanakubaliananavyo, madawa ambayo wanakubaliana nayo au hata kama huna mfumo wa kudhibiti ugonjwa huu wakubalianao nao , hupata hizi fedha.

Lakini.....!
Wenzetu nao walikua na ugonjwa huu!Lakini wao wakatumia DDT na madawa mengine ya sumu kuumaliza.Sisi lakini haturuhusiwi kutumia dawa hizi , kwasababu wanasema kuwa zinaharibu mazingira.
Siwabishii hilo!....

Siwabishii kuwa hazi haribu mazingira,...
lakini najiuliza kuwa kwanini wao mambo huyahalalisha na yanakua mabaya tu pale wengine wanapotaka kufanya kama wao?

Umestukia pia hata katika viwanda , nguvu za nyukilia, nk; kwao ni sawa lakini ukigusa mwingine Umoja wa Mataifa unaanza kukuwekea vikao kuwa mkorofi?

Labda ni kweli kuwa wao walitangulia mapema wakastukia madhara ndio maana hawataki na sisi kurudia makosa.
Lakini!....
Mbona wao wanajinoma? Sisi je?

Nakubali kuwa nia ya mbu jike ni kujitafutia damu ili kupata lishe bora kwa ajili ya taifa lake la kesho na sio kuwa mbeba malaria. Hivyo kama akikosekana mtu mwenye vijibaba vya Malaria basi akikuonja hana madhara.
Sasa kuhakikisha kuwa hakuna mtu mwenye vijibaba vya Malaria maeneo, hapo ndio kasheshe!Wenzetu kwakutumia sumu wakaweza.

Unakumbuka kuwa sehemu kama Florida , Marekani ni sehemu zenye mbu kuliko sehemu nyingi duniani?

Hivi kwa wale washabiki wautunzaji wa mazingira:...........
Hivi kunasiku kutakua na mradi wakutunza Mbu wasipotee duniani?

Duh!
Inasikitisha sana kuwa mapka kuna statistics zijulikanazo, zidaizo kuna mtoto anakufa na Malaria kila dakika tatu Afrika.

Tujaribu kufanya kila tuwezalo wajameni , kusaidia kufuta hili.Hata ikiwa ni kufukia vidimbwi uani kwetu au kutotunza lilekopo lakwendea msalani lisilotumika pale nje ya choo.
Basi ngoja niondoke zangu!
Lakini nakuacha na Amadou na Mariamwakikupa kile kibao Senegal Fast Food

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MTANZANIA. 5:42 pm  

Simon! Ngoja nikukumbushe baadhi ya nyingine. Kuna siku ya ukimwi, kifua kikuu, kifaduro,surua n.k Ila kwa RVF bado haijawa-specified!

Ni vema sikukuu hizi zikawa zinaadhimishwa kwa vitendo zaidi kuliko propaganda.

Lakini Simon! Umesheherekea Muungano vzr huko? Ingawa afya ya bwana Muungano Tanzania si njema sana ni vzr tusaidieni kimawazo namna ya kuiboresha afya yake. Nashukuru leo hata Maalim alifika kumuona bwana Muungano Tanzania.

Simon Kitururu 11:07 am  

Mzee Mtanzania bado sina nguvu ya kusaidia mgonjwa.Duh!Mimi Mbaya eeeh?:-)

Anonymous 4:00 pm  

Siku ya Malaria kusema kweli nimesikia kwako...wanaoishi kwenye sehemu za mbu wamesahau tulivyofunzwa shuleni??? fyeka nyasi na kadhalika...utafiti wa madawa haitoshi...wananchi nao wafanye lao!

Simon Kitururu 9:44 am  

@Serina:Kweli tupu usemayo!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP