Maswala Ya kulamba Makamasi!
>> Wednesday, April 11, 2007
Mambo ya aibu na uchafu ni baadhi tu ya mambo yatawalayo mitazamo ya jamii .Ni jambo ambalo hutusababishia muelekeo wa matendo yetu na hata muonekano wetu.Inawezekana kabisa lile bugaluu na panki tulilonalo ni juhudi tu ya kujibanza kwenye jamii.
Lakini kuna maswala ya uchafu na aibu ambayo kwa mara nyingine watu huyaepuka hadharani tu . Ukiwaweka sehemu wakahisi hawaonekani basi mambo hutafsiriwa vingine.
Mimi si muhukumu mtu, nachojaribu kuuliza ni:
Je, ushawahi kujamba hadharani, watu wakasikia?.
Basi labda ulijikausha ukafikiri watu hawakukustukia.Lakini vilevile ukajua watazungumzia hilo baadaye.
Nafikiri hukufa kwa hilo. Naamini kuna mambo ni ya kibinadamu tu , huweza kutokea, lakini maisha yanaendelea hata baada ya kijambo tarumbeta. Lakini hebu mcheki Silvio Berlusconi akilamba kamasi kabla sijaendelea...
Sasa, ushawahi lamba makamasi kisirisiri?
Duh!Nimesahau kuwa wewe msafi. Lakini sinasikia unalamba na kunyonya sehemu-viungo vya kutolea haja ndogo , na mara kadhaa umefikiria kulamba sehemu ile nyingine.
Samahani tena!
Unajua nimechanganya watu!Nisamehe!
Lakini katika maswala ya uchafu watu wengi husahau chombo cha mabusu, yani mdomo yasadikika unavijemedari vihusianavyo na uchafu kuliko hata sehemu za haja ....
Duh!
Ushastukia kuwa mara nyingine common sense inatuchezea akili katika mahusiano yetu na uchafu?
Hivi ni tendo gani chafu kuliko yote ushalifanya?
- Ushawahi kushika mavi kwa kutaka kuyaangalia kwa karibu?
- Ushawahi kujikojolea?
- Wanaume: unakumbuka mara ya kwanza uliposhuhudia yale majimaji yenye mbegu ?
- Wanawake: Je unakumbuka , hasa kama utu uzima ulikukuta ukiwa hujajianda na mashabiki wawapo?
Twaweza kukubaliana kuwa tutake tusitakake kila siku tunachukua hatua kadhaa maishani.Kama tukohai matendo yatatendeka tutake au tutusitake.
Nisikufiche kuwa wengi wetu hupendelea matendo yetu yenye kutuletea sifa nzuri ndio yaonekane kwa watu. Matendo ambayo twahisi yatatuaibisha twayakwepa kwa kila njia.
Lakini..
Sisi kama binadamu lazima ubinadamu utatokea katika matendo yetu. Kuna mambo yatuleteayo sifa kwenye anga moja lakini yanatujengea maadui katika kambi nyingine.
Nachojiuliza ni jinsi tulivyoweza kutawaliwa na hulka hii ya kuonaaibu iwapo kunamapungufu katika matendo yetu. Inashangaza hata tuwezavyo kukwepa watu ambao twahisi hawatuletei sifa nzuri.
Nachojaribu kusema ni ni kwamba, sisi kama binadamu tutaendelea kufanya matendo kama binadamu. Tutajaribu kuwa malaika. Na ni vizuri kujaribu kuwa malaika. Lakini mapungufu tunayo.
Je umuhimu wa usafi tuuabuduo leo hii si zao la kuwepo kwa uchafu?
Hivi tunavyo jaribu sana kuwa wasafi ni kweli hatuutaki uchafu?Je , kuupiga vita uchafu si ni moja yashughuli tu ituwekayobize sisi kama binadamu?
Usitishike , nawaza tu!Ukweli ni kwamba baadhi ya mambo yapo tu hata tusipokumbushana. Lakini je ni vibaya kukumbushana? Sijui.Tuendelee kuupigavita uchafu. Lakini ushastukia kuna vile vimambo ni afadhali tu vifanyike kisirisiri ingawa hata ingawa tunajua vilivyotafsiriwa kuwa vinatia aibu mara nyingi ni mtazamo tu.
AU?
Namrudia Nina Simone akikuimbia Four Women
9 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Duh Berlusconi noma,kacheki huku na kule kama kuna mtu anamdeku akaona hakuna akalamba na kusukumizia na kikombe cha ghahawa.
Hivi kulamba makamasi ni kitendo cha aibu?
nasty
aliko
Greetings Mzee Simon,
katika blogu yako umeondoa ile blogu ya metz reflection mzee.
unawasiliana na Da Mija?
makamasi duu
Simon!
Ulishawahi kusikia msemo huu:-
"wameza kohozi na kutema mate".
Binadamu tuna hulka fulani kwamba kitokacho mwilini mwako si uchafu kulinganisha na kinachotoka ktk mwili wa mwingine. Labda hili ndo limesababisha jamaa akalila kamasi lake. (ref. clip)
Lkn suala la koni na chumvi duh! (kasheshe)
Kuna mdosi mmoja nimemuonyesha hii video,katapika chakula chote.Mpaka saa usiku naongea nae anasema kashindwa kula kila akimkumbuka mzee Berlusconi.
@Egdio:Si utani mambo ya Belu yaweza kumtapisha mtu. Lakini kama alivyosema Mtanzania, si watu humeza makohozi wakatema mate?
@Mtanzania: Watu humeza kohozi wakatema mate. Halafu katika kurizishana maswala ya koni na chumvi yanawakilishwa vyema tu. Na hivideo zetu za mitandaoni zinasaidia ufanikiwaji wake.Lakini katika hilo watu hawaiti uchafu , ni sehemu tu ya tendo.
@Al tunez: Karibu katika kublogi.Nimeonaumeanza pale kijiweni.Poa sana.
@Luihamu:Nilivyofanya ukarabati hapa bado sijarudisha links zote.Lakini ya Metty imerudi.Sijawasiliana na Damija.Labda yuko bize tu. Naamini tutamsikia hivi karibuni.
We Kitururu hujatulia kabisa. Yaani huoni aibu kuandika matusi humu bloguni mwako. Jaribu kutumia maneno yenye kupunguza makali.(tasfida). Hata wachangiaji wako utulivu hakuna. Sasa kulamba koni na chumvi ndo nini.
@Karikwaw:Nimekupata Mzee!Lakini hiyo koni na chumvi ilitumika ilikukata makali.Lakini labda chachu bado ipo.Samahani kwa lugha hiyo.
Post a Comment