Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Karibu tena Chifu Nyerere!

>> Tuesday, April 17, 2007

Samahani nilikuwa na maanisha Chifu Mandla Mandela!

Nakubali kuwa Afrika Kusini si Tanzania. Na nakubali ukiwauliza watu wengi wanaweza kusema kuwa lilikuwa wazo zuri kuufuta uchifu Tanzania. Mtu anaweza kudai kuwa uchifu ulikuwa unagawa watu na maeneo katika hali ambayo ingehatarisha utaifa wa Tanzania.

Sasa hivi baada ya miaka siku kadhaa, nafikiri si vigumu kugundua tofauti ya Dar es Salaam na Mtwara. Nafikiri si siri kuwa ukubwa wa kipenyo kati ya tajiri na masikini unakua kila siku.

Ndioo..!

Naamini labda ukabila ulikatwa nguvu baada ya kuua uchifu,
Labda tulivyounganishwa chini ya kiongozi mmoja lilikuwa jambo zuri.
Sasa unafikiri tuko chini ya kiongozi mmoja nchini Tanzania?
Kama ni kiongozi mmoja , je mbona matabaka ambayo tulikuwa tumetafutia dawa kwa kuwa chini ya kiongozi mmoja yanakua?

Hivi unafikiri Kikwete ni kiongozi wa matajiri au masikini?
Utashangaa uchifu ukirudi Tanzania kama Ulivyorudi kwa mjukuu wa Nelson Mandela?

Usitishike, nawaza tu!

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MTANZANIA. 11:32 pm  

Simon!
Mawazo yako yanaoana na mawazo ya Mh. Mbunge mmoja ktk kikao cha bunge kilichopita. Alipendekeza serikali iangalie upya hili suala la wachifu.

Ebwana itakuwa balaa kama hiyo hali itarudi. Nasema hivyo kwa sababu huo mfumo una mapungufu yake. Kule kwetu bado kuna elements za watemi. Hizi familia bado zinaendeleza umwinyi/u-alwatan fulani. Sipingi hili jambo ila ikitokea linarudia TZ basi ni lazima sheria fulani zitungwe kuwapunguzia madaraka hawa machifu, watemi n.k

Simon Kitururu 6:22 am  

Niliandika hiki kihabari haraka haraka. Nilichotaka kusema ni kwamba mfumo tulionao sasa ingawa ni mzuri tumeshindwa kuutumia kuondoa matabaka. Kwa sasa unaongeza matabaka. Lakini mfumo huu mimi naukubali kuliko wa uchifu hasa kwa sababu unaondoa ulazima wa familia moja kutawala milele hata kama imepungukiwa uwezo.Siamini kuwa kwa sababu Nelson Mandela ni kiongozi mzuri basi hiyo inamaana na Mandla Mandela atakuwa kiongozi mzuri

Anonymous 6:32 pm  

Kama mfumo wa uchifu ulijenga matabaka ya kikabila, mfumo wa uongozi tulionao hivi sasa umejenga matabaka ya kimali, kinafasi, na kielimu. Tabaka la wasio nacho na wasio nacho. Umeleta makabila mawili: walionacho na wasionacho. Watawala na watawaliwa.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP