Uganda Histori Yajirudia/Wolfowitz naye adakwa
>> Friday, April 13, 2007
Mtu usipoangalia unaweza kuacha kufuatilia habari za dunia.Halafu si mchezo , ukizoea kuangali habari hukawii kudumaa kinamna. Kila siku utasikia huyu kafa wale wamelipuliwa , wale wanakufa njaa, mafuriko nk.Inasikitisha kuwa habari muhimu zimekuwa ni zile zenye maswala mabaya mabaya tu.Halafu naamini akili inazoe kuwa hizi ndio habari.
Ukitaka kujua kuwa hii tabia ya kwamba habari mbaya ndio habari nzuri imewaingia watu kisawasawa, tembelea blogu au tovuti zenye habari nzuri za watu au kitu. Hapo utakuta watoa maoni wanaanza kutoa maoni mabaya kuhusu huyo mtu au hicho kitu.Hivyo kuna watu tayari wasipopewa habari mbaya , wakichangia watatoa maoni mabaya.
Lakini kama kawaida hakuna haja ya kulichukulia hili swala kijuujuu. Labda mimi na wewe ni kweli hatudakwi tukizubalia habari mbaya.
Au?
Lakini umesikia Uganda Waasia wanabwengwa kisa mmoja wao mfanyabiashara ya sukari alitaka kukata msitu wa Mabira kwa ajili ya shamba? Inasemekana kulikuwa na watu kibao waliokuwa wanadai Waasia warudi kwao. Na hisi hii inanikumbusha Idi Amini.
Duh!La hasha!
Inanikumbusha Mchungaji Mtikila enzi zake alipoanzisha kampeni yake yakuwaita wahindi Magabachori.
Nilishuhudia mawe kadhaa yakiandama magari ya Wahindi na biashara zao Bongo.
Na umesikia Mzee Wolfowitz, raisi wa benki ya dunia ambaye anasifika kupiga vita rushwa katika benki hiyo, kadakwa akimpa uchochoro wakufikia juu kwenye mshahara mzuri mpenzi wake?
Duh!
Ngoja nifikirie habari nzuri ya kuandika!
Bingo!
Ni bomba sana kuwa mimi na wewe ni wazima!
Ijumaa njema!
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment