Ukiwa Uchochoroni!
>> Friday, April 20, 2007
Najua unakumbuka ukiwa uchochoroni nini kinatokeaaaaaa!
Duh!
Unaweza kubakwa.
Unaweza kubaka.
Lakini unaweza ukafanikisha mambo fulani fulani bila washikaji kustukia.
Umekumbuka eeeh?
Duh!
Nisikutishe kile kitu siri yako, hatukustukia !
Usiwe na shaka!
Lakini kabla sija sema sana......Magic System wako mawazoni.....
Duh!Lakini nimewakumbuka washikaji niliokuwa nao wiki jana.....
Sasaaaaaaaa.....
Mzee Ogola!
Labda ngojea aseme....
Kuhusu hiyo video hapo juu sisemi!Usiniulize!
Tuendelee......
Mzee Allen na Mimi
Mzee Allen na Martin
Mzee Allen ,Mimi na Martin
Au ngojea kidogo....
Okeiii nimestukia hicho!Ngojea nikutulize kidogo na Cheb Bilal hapa...
Basi tuendelee....
Mzee Johan
Mimi na Dj Ezza
Mheshimiwa Bonanza aka Cool Brother.
Kumbuka ni mimi tu naruhusiwa kumuita hivyo:-)
Asante kwa yote Bro!
Tukirudi Uchochoroni.....
Nisikufiche kuwa mara nyingi ni mimi muoga.
Lakini kwanini ni wewe unachagua kuogopa?
Ushastukia hakuna ajuaye unasilaha gani ndani ya koti?
Unajua hatujui nguvu za ile karate yako na u Bruce Lee wako ?
Samahani!
Lakini............najua....!
Ushawahi kuwa gizani, uchochoroni halafu ikawa ni wewe unaogopa.
Lakini najua ushawahi kwenda kujisaidia kichakani bila kujiuliza kuwa kuna nyoka wala sisimizi.Nakukubalia kuwa kichakani si uchochoroni.
Lakini.....?
Halafu ushajua kwenda haja hata kama ni muhimu kuna kastarehe kake?
AU UNABISHA?
Duh!
Sasa.......
Unafikiri kama wote tuko gizani, uchochoroni kwanini ni wewe unayeogopa?
Kwani unafikiri jambazi yeye anauhakika kwamba wewe.....
Duh!
Ngoja niache!Nisikuzingue!Kama huelewi nasema nini usiniulize:-)!
Ijumaa njema!
Nakuacha na TEEYAH akikupa couper decaler
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mzee Simon hayo ndio maisha ya majuu,hali ya hewa safi.
Mzee hongera kwa kutupa mambo ya huko.
Duh! nakumbuka zamani niliwahi kuishi sehemu fulani kwa hiyo nilipokwa narudi home lazima nipite kwenye kijichochoro,na pale jamaa walikuwa wanapigwa roba za mbao sana.
Wapiga roba walikuwa wanafahamika kila nikipita nilikuwa sikosi kuwapa sigara mbili tatu nikiwakuta kijiweni kwao.siku moja narudi usiku nikabanannishwa katika kichochoro jamaa wakanisachi lakini mmoja wao akanitambua wakaniomba msamaha sana.Wakanirudishia kila kitu changu.
Na kuanzia siku hiyo nikaishi kama mfalme hapo!
@Rasta:Kuhusu hayo mambo ya majuu, sinajibu.Lakini si ukweli kionekanacho ndio ukweli wenyewe.
@Mzee wa Makalio: Duh!Sina la kuesema!Asante kwa kunitembelea.
@Egdio: Kumbe wewe uko corrupt eeeeh!:-)Duh! Mpaka wajanja wakawa wanakuachia upite kichochoronni, wewe duh!Sisemi!:-)
Post a Comment