Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuhusu Raisi Kitururu-:-)Duh!- IDI amINi!

>> Sunday, April 29, 2007

Samahani nakubaliana na Ndesanjo kwa hili!
Ndesanjo eeh!
Samahani, lakini ,!:-)
Niachie namba yako ya simu chobisi basi!
WENGINE.........................!
Ngojea Ndesanjo aseme kuhusu Idi Amini.......
ndesanjo has left a new comment on your post "Generali Idd Amini Dada akiongea, duh!":

Ingawa simuoni kama kiongozi wa kuigwa, Idd Amin Dada namvulia kofia. Huyu ni bwana ambaye kusoma na kuandika kulimpa tabu. Ila aliweza kutumia mbinu mbalimbali kuwahadaa Waingereza na baadaye Obote hadi akaja kuwa rais. Alikuwa na ndoto, akaifanyia kazi, akawa rais wa nchi akiwa hajui kiingereza au kiswahili sawasawa. Akiwa ni mbumbumbu. Kumbe umbumbu wa darasani sio kikwazo kwako kutimiza ndoto uliyonayo.

Waandishi waliowahi kumhoji wanasema kuwa maswali mengi makali waliyokuwa wamepanga kumuuliza au shutuma walizokuwa wamepanga kumpa zinatokomea wanapokaa naye chumba kimoja kumhoji. Wanasema alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kukufanya umwamini na kumhoji kirafiki.

Kuna mambo mengi alikuwa akifanya unajiuliza mbinu hizi alijifunzia wapi? Wakati viongozi wengi husoma vitabu na kuwa na washauri waliomaliza madarasa yote ili kupata mbinu za kutawala, Amin alikuwa akianzisha mbinu hizo mwenyewe bila kujifunza toka vitabuni.

Alikuwa na mbinu moja ya ajabu na kinyama aliyoitumia kwa watu aliokuwa ameamua wauawe. Kama mtu huyo ana jina au nafasi kubwa nchini, basi Amin alikuwa anaweza kumkaribisha ikulu ale chakula cha jioni na kunywa mvinyo. Wanapiga picha ambazo zinatolewa magazetini zikimuonyesha Amin na huyo mtu wakicheka kwa furaha na urafiki wa hali ya juu. Kisha baada ya siku tatu, idadi ya siku tunazoambiwa yesu alikufa, unasikia huyu jamaa katoweka. Baadaye unasikia amepatikana akiwa ameuawa baada ya kuteswa.

Urais katika mfumo wa kisiasa kama wa Uganda enzi za Amin sio kazi rahisi. Kuongoza nchi ya kidemokrasia ni kazi rahisi sana. Ila kuongoza nchi ya kidikteta, kujenga utamaduni wa ukimya na woga kwa wananchi wote, kuchunguza nani maadui zao na kuwaondoa duniani...aliwezaje kunyamazisha nchi nzima? Hofu. Alijua kuwa silaha kubwa kabisa dhidi ya mwanadamu ni hofu. Alijua binadamu wanapenda sana uhai. Binadamu wanaongopa, mara nyingi, jambo lolote ambalo linaweza kuhatarisha maisha yao. Amin alijua ukweli huu na akautimia ipasavyo.

Tuache hayo, hivi kuna mtu mwenye uhakika kuhusu Amin kuivamia Tanzania? Je ni kweli aliivamia Tanzania kisha sisi tukajibu au habari ya uvamizi huu ilizushwa kama propaganda ya kuhalalisha vita vya kumtoa madarakani kutokana na kuonekana kuwa tishio la usalama Afrika Mashariki?


Sasa mnambishia Ndesanjo?
Mimi nimekubali.
Namuacha huyu MuHaiti aishiye Ndesanjo na Mtanzania wajibanzako

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MTANZANIA. 7:01 pm  

Kitururu! Mimi nakubaliana na Ndesanjo kwamba uongozi ni karisima. Kwa maana hiyo kuwa na elimu sana haina maana ya kuwa kiongozi bora.

Nikiangalia ile video yake huwa nacheka sana. Kuna sehemu anasisitiza Uganda kutoa msaada wa chakula kwa Uingereza.

MTANZANIA. 8:37 pm  

Lkn pia nawe waweza kuwa Mh. Raisi Kitururu. Omba Mungu kura zitoshe!! hahahahaaaaaa

Simon Kitururu 11:33 am  

@Mtanzania:Unakumbuka msaada wake ulikuwa kwenye shilingi elfu fulani :-)Lakini ndio raisi pekee kutoka Afrika aliye taka kusaidia Uingezereza.Wengine wote wanaenda kuomba.
Kuhusu mimi kuwa raisi, nafikiri kura zitaanza kupotea wakistukia tu sichani nywele:-).

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP