Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Msenge aongeleapo maswala ya Uke!

>> Thursday, April 19, 2007


Ilipotokea ile filamu ya Darwin's Nightmare, watu wengi walilalamika jinsi gani mtu kutoka sehemu nyingine kutengeneza filamu kama hii kuhusu Tanzania.Hata mimi kama binadamu ambaye sipendi kudhalilishwa ilinigusa kinamna, ila ikaanza kunifanya nijiulize sana maswali kibao.
Moja ya maswali yalikuwa....

  • Hivi kipofu kwa kua haoni , hawezi kuusimulia uzuri wa vionekanavyo?
  • Je, msenge hawezi kuwana kauli zenye kina kuhusu mahusiano ya mawanamke na mwanamume?
  • Hivi mtoto hawezi kuona jambo wakubwa waliotealo makengeza?
  • .............nk


Basi ngojea nikupe trailer ya Darwin kama umeisahau.......



Basi bwana.......!
Katika kujiuliza sana haya maswala nikaona kuwa mara nyingi sisi wabishi tu. Kipofu na aonaye wote tunamapungufu. Naamini kuwa tutake tusitake mara nyingine kipofu ndio aonaye kuliko mwenye macho. Inategemea tu nini mnalenga.Ingawa pia jambo hili si rahisi kufananisha, lakini mara nyingine mwenyeji huzoea jambo, muonekano , hata harufu ambazo ni mgeni huweza kustukia au kuona ni tatizo.
Unaweza kubisha lakini!Sikukatalii!
Lakini kabla sijaendelea ngoje nimuache Steve Wonder, miongoni mwa vipofu wawezao kukusimulia uzuri na upendezaji wakitu kuliko wengi sisi tuonao......


Sasa ...!
Swali:
Baada ya ile filamu ya Darwin's Nightmare unafikiri nini kimebdilika kuhusu swala aliloliongelea?Au ndo lishapita tena?


Haya basi nikipata muda nitaendelea kuongelea swala hili. Lakini nachotaka kukuambia ni kwamba usishangae Msenge akakufundisha maswala ya uke. Au unafikiri msagaji kwasababu ni msagaji hajui maswala ya uume?
Hebu nikuache na George Michael , msenge ambaye jicho lake kwenye baadhi ya lirics zake zaonyesha anaweza akafundisha maswala kadhaa ya jinsi ya kumuangalia msichana.....

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Bijoy 10:50 am  
This comment has been removed by a blog administrator.
Simon Kitururu 5:39 pm  

Thanx!U are welcome

Mikundu Matako Makalio Manundu 10:38 am  
This comment has been removed by a blog administrator.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP