Sijui kwanini
Nani na nani ana nini
haiepuki mimi na ninyi
Ya washawasha maini
Matajiri kwa masikini
roho ngumu kama nini
Lakini kwanini?
Ni nini kiini?
Wataka yote maini
Tugaiane kwa makini
Yatutosha wote hiyo nini
Sasa, nini?
Na:Simon Kitururu
--
© Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008
Back to TOP
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kuna washairi waliojifichaficha huku bloguni. Huwa wanajitokeza hapa na pale. Huko nyuma tulikuwa na magwiji wa ushairi ila wakatokomea. Haya, tuendeleze fani hii ya kucheza na lugha na maudhui.
@Ndesanjo:si utani. huwa kuna baadhi ya siku hujisikia kucheza na lugha.La kini ugwiji sijaufikia. Sijui kwanini sioni mashairi ya Mwandani siku hizi.Kwa sababu yeye kwa mtazamo wangu ni gwiji.
Ongera Kaka haina haja ya kuwa gwiji.. kwangu mimi shairi lako ni super tu.
Umesema sawa Simon. Mwandani gwiji. Mashairi yake niliyapenda zamani kabisa kabla hata blogu kuzaliwa.
Mwandani: tunakusihi...tupe aya.
Je aya hizi za mwanablogu wa Kenya umeziona? Wakenya hawajui Kiswahili? Tazama aya hizi uniambie:
http://serinaserina.wordpress.com/
@Halifa: asante kwa kunitembelea. Nashukuru kwa kunipa moyo katika anga ya ushairi.
@Ndesanjo: Nimecheki pale.Mara nyingi ni rahisi kwa Watanzania kudai kuwa Wakenya hawajui kiswahili. Nahisi hii ni sawa tu na Wakenya wapendavyo kudai Watanzania hawajui Kiingereza. Hili jambo ukiliamini utashangaa mwenyewe jinsi gani unavyoweza ukawa umekosea.
@Halifa:Tunasubiri blogu yako.
Post a Comment