Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Chakula cha Mawazo! -Yote Maisha?

>> Friday, July 13, 2007


Hivi kama unapata ulaji ,hata kwa kufanya mambo yakudhalilishayo , kuna noma?
Hebu mcheki huyu mkongo achongaye vinyago vya Tintin ingawa anaamini kuwa Tintin ilikuwa inadhalilisha Watu weusi.
Swali:
Si unakumbuka katika Tintin, Nyani na watu weusi walikuwa wanachorwa sawa?


Sasaa...
Unasemaje kuhusu hawa akina kaka ambao hawajulikani kama wasenge , wishio nakujulikana kama Ma -EUnuchs wa India?


Duh!
Basi bwana!
Pata sura za Waafrika wa Afrika.
AU?

Read more...

Maswala ya Kusubiri!

>> Wednesday, July 11, 2007

Kusubiri nishai!
Kwasababu , wakati unasubiri unajua au unahisi umsubirio anafanya mambo fulani ambayo kwako si muhimu au si... ambavyo ungetumia mda wako mchache. Ila pamoja nakua, kwako si muhimu kuna wengine ni muhimu mambo fulani.
Samahani kidogo....!


Sasa.......
mimi kama Katibu wa Jumuwata , ingawa siongei hapa ofishali, ni kwamba subirini kidogo.
JUMUWATA itakuwa baaabu kubwa, SUBIRI KIDOGO!
Ngojea nikwambie kwa sauti...


Ngojea kidooooogo kabla sija malizia..
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
James
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
James eeh!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Clemooo aka Clement aka Mtoto wa Nairobi.Tuko pamoja.
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!
Samahani!Namrudia King Sunny Ade

Read more...

Jamii Ina Tabia Mbaya.UKIFANIKIWA UTAsameHEWA!

>> Tuesday, July 10, 2007

Mbwa wee , Sura kama kinyesi!
Matusi ni kitu cha ajabu. Mara nyingi tusi likuuamalo, halina maana. Ukifikiria kidogo unaweza kujicheka kwa kuchukia.
Kabla sija sema...
Mpate Maxwell Vidima..

Jamii inatabia mbaya!
Katika jicho la jamii , ukiwa umefanikiwa, waweza kusamehewa hata yale unayostahili kulaumiwa.
DONDOO:
Unamkumbuka Mwalimu NYERERE?
Watatokea katika jamii ambao hata huwajui kukutetea , kama jichoni mwao unawakilisha mafanikio.

  • Pamoja na nia yako nzuri , ukifeli kufanikisha ambayo, ambacho, jamiii inayahusudu , kuyategemea kutoka kwako,......USISHANGAE KULAUMIWA hata kama HAYA KUHUSU!

DUH!
Usimaindi sana , niko mawazoni tu!

Ngojea niache baazi ya picha za wiki hii..
Lakini kabla ya picha ....!
Tulia kidogo na Kassav...

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Kukuruuuu Njiwa
Endeleza lakini!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
J.Karjalainen na...

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Eeh Bwana!

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mapenzi ya Somalia na Eritrea

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Sasaaaa
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Bup .Mzee wa Sauzi Sudan

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
David

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Bup na David

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
David eeh?

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Nikipigwa picha kwa simu

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Sasaaa...

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!

Samahani lakini!Kulikuwa na Mlonda Mlangoni lakini...
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Jukka eeh!Asante!


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Sasaaa!


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!
Sasa ngojea usikie nayemsikiliza sasa hivi wakati naandika.
Ni Mzee wa Tanzania , maarufu kwa jina la DULLY SYKES.

Ee bwana ee! Ni jina lake...
Msikilize basi ...



Mtimkubwa, Manento........, Nakumbuka!

Read more...

Ushawahi kutukanwa Tusi la Nguoni?


Kabla sija sema...
Mpate PHAROAHE MONCH

Mbwa wee !Sura kama kinyesi!...............

Na matusi mengine watukananayo, watutukanayo, tuwatukanayo jamaaa.....
Bado najiuliza kuwa, watukanwao wanajiuliza kuwa kwanini wanakasirika?
Kwa sababu...
najua maratisina tisa, tusi likuumalo halina uhusiano nawe
Swali:
Hivi ushatukana mara ngapi?
Ulifurahia tusi lako ehh?
Lili kuwa ninaleta maana?

Duh!
Ngojea niendelee kumuacha Pharoahe Monch

Read more...

Tarehe na imani za ajabu!

>> Saturday, July 07, 2007


Hivi Kalenda si ziko nyingi?
Lakini je ni ukweli kuwa kwa kalenda tuzifuatazo.Tarehe fulani zina mambo zaidi ya tarehe nyingine?

Lakini ......
Nafikiri una kumbuka kuwa hii kalenda tuifuatayo ni moja wapo tu ya kalenda nyingi duniani.

  • Si Unakumbuka kwa kiislamu huu sio mwaka 2007?
  • Si unakumbuka kwa kiIthiopia huu sio mwaka 2007
  • Si una kumbuka kwa........
DUH!
Tarehe hii ya 07.07.07 watu kibao wamejaribu kuoana, kutengeneza watoto, ku.....
Duh!
Lakinni mdau wangu Ronaldo , aka Mdau wa LONDON ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.
Namuacha na picha fulani......
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Kuwasili...
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Ronaldo ,Mzee wa London

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Ronaldo eeh!

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!

Samahani nilimisi pati fulani za chobisi.
Lakini ...

Tuko Pamoja!

Namuacha Steve Wonder aniwakilishe kukuambia Ronaldo!
Hapi Bethdei tu Yu!

Read more...

WaAfrika Wagombanapo kuhusu Mipaka ya Nchi Zao!

>> Friday, July 06, 2007

Inasikitisha kuwa sisi Waafrika bado tunagombana kuhusu mipaka ya nchi.

  • Hivi, si ni wakoloni walikaa pale Ujerumani wakagawana bara la Afrika?
  • Hivi si ni sisi Waafrika tunatakiwa kujua baada ya miaka yote hii , na busara zetu hizi, kuwa hawa jamaa waliotugawa kwa mipaka na tamaduni, na wanaoendelea kutugawa, kua wao wanaungana?Au zile EU na... bado hatuzielewi?

Samahani......

Ila Mimi kama Mtanzania, na marafiki wengi Wakenya kuliko Watanzania katika chobisi niliyopo.
Mimi kama Mtanzania na marafiki WaTanzania kama akina Ogola ambao wameishi Tanzania nakusoma Kenya kwasababu shule ya karibu ilikuwa Kenya.
Mimi kama .........
Duh!

Swali:
Hivi sisi kama Waafrika, mipaka ni kitu kitusumbuacho zaidi ya matatizo mengine mengi, ambayo ndio sura ya unyonge wa Muafrika mweusi?

Samahani, hebu msikilize huyu Mpiga Rege (Innocent Galinoma) Mtanzania ambaye baadhi ya watu wana msahau ingawa yuko katika anga tokea enzi zileeeeeeeeeeeee.....!




Sasaaa............
Mpaka leo .......
  • Tanzania na Malawi , wanagombania mpaka umepita wapi katika ziwa Nyasa(Malawi).
Hivi , Ziwa Nyasa limegawanyika katikati au lote liko Malawi?
  • Hivi , Wamasai na Waluo (Wajaluo)ni Wakenya na Watanzania ?Au kwasababu wako nchi zote , hawahitaji passport?
Hivi unajua kuwa Tanzania na Zambia ilikuwa katika vita ya Kidiplomasia hivi majuzi ,kwasababu inasemekana kuna Watanzania 22 wamejenga nyumba ndani ya mpaka wa Zambia?


Duh!
Samahani niko mawazoni tu!
Kabla sija kuacha, ngojea nikuache na picha zangu leo...
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Tulia basi na Sekouba Bambino

Read more...

Tamaduni za Uzinzi na EU!


Sisi wa Afrika na ....wale....
Si......

Tuna tamaduni ambazo mambo fulani ya maana......... ambayo tufundishanayo kuwa ni ya maaana..... na yajazayo Dunia...... si hatuyaongelei wala ku...au tu nayaongelea ingawa , tamaduni inakuwa mpaka....... ni wapi unatukana au wapi wewe ni mstaarabu unayejadili hoja ifundishayo au i.....?

Swali:
Hivi Ustaarabu ni nini?
Hivi matusi ni nini?

Najiuliza tu , au na wewe unajiuliza tu kuwa....................

  • Sisi WaAfrika na .... , si ndio mila zetu tunazitetea kila siku kuwa ndio zinazo tunza heshima?
  • Si ndio sisi tunadai au tuigao , wamagharibi( Waulaya, Marekani na....)kwa sababu mambo yao ndio tuonayo kuwa yameendelea?
Samahani lakini kama hunielewi !

Lakini ..............
Si binadamu wa kwanza aliyeanza kujifunza kufanya ya ubinadamu ,alitokea Afrika?

DUH..!
Samahani!

Dondooo:

Hivi unaweza kuamini kuwa sisi Waafrika, hata Wa........ , tumefikia kuamini kuwa maswala ya ngono , mapenzi, uzinzi , ni maswala ya sirisiri?
Si ndio maana tuna kufa ? Au?

Swali:
Hivi pamoja na utamaduni wetu wa kiafrika tuupendao, haya maswala kama ya ngono ya sababishayo tufe kwa UKIMWi , lakini yatupayo kale kastarehe ambako pia kampako mimba yule..................... , tukafumbie macho?

Usistuke !

Najiuliza tu!

Niko Mawazoni.

Hebu angalia Umoja wa Ulaya (EU)unavyotangaza jinsi gani maswala yao ya Movie za ulaya ni bomba.

Angalia lakini..........
Angalia tu kwanza kama umezidi miaka kumi na nane, halafu niambie!

Halafu jiulize kuwa hii kitu AU(African Union) ingetumia kutangaza maigizo (muvi aka kibira) za Afrika au Afrika mashariki kama hivi wafanyavyo wa Umoja wa Ulaya, Mheshimiwa wako(Mama na Baba na...) wangesemaje?
Tuko Pamoja
AU?

Read more...

Kifo na Biashara ya Majeneza!

>> Tuesday, July 03, 2007

Inasemekana kuwa kila janga kwa mmoja , hunufaisha wengine.
Ukitazama habari kuhusu Afrika , hukawiii kusikia jinsi vifo vinavyo tawala karibu vyombo vyote vya habari.

Kama hivi vyombo vya habari vinaaminika, basi haitashangaza jinsi biashara zihusianazo na vifo zinavyozidi kushamiri Afrika.

Hebu angalia wafanyabiashara wa majeneza wa kabila la Ga huko Ghana wanavyokutengenezea majeneza kutokana na hobi zako, ujuzi wako hata umaharufu wako.

Cheki mwenyewe baadhi ya majeneza hapa.
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Ukifa kama unapenda Coca cola utazikwa najeneza hili

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Baadhi tu ya majeneza kadhaa kutokana na ukumbukwavyo...

SAHARAN VIBE aliandika zaidi kuhusu hawa jamaa.

Lakini...
Inasemekana huko Malawi biashara ya majeneza ni ya upinzani sana. Na watengeza majeneza wamefikia kuwa na sifa ya kuwa wafanyabiashara wasiopenda mzaa kabisa. Ukitembelea duka la majeneza bila kuwa na nia ya kununua jeneza unaweza kushambuliwa hata kupigwa. Inasemekana wengi wa watengeneza majeneza huuzunika sana wakisikia kuwa makadirio ya watu kufa yanapungua.

Swali:
Ulikuwa unafikiri kila mtu anafurahi watu wasipo kufa kwa wingi?


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duka la Majeneza Malawi

Ila nacho wasifu wafanyabiashara wa Malawi ni kwamba biashara ya majeneza inapopungua ,huwa wanaanza kuuza fanicha nyingine.Naamini huu ubunifu wa kubadili bidhaa kutokana na uwepo wa mahitaji , inafaa kuigwa na wafanya biashara wengi Afrika.

Tatizo linalojitokeza tu, ni jinsi inavyojidhihirisha kuwa kuanzia wafanyabiashara wa majeneza mpaka serikali zetu Afrika ni ngumu sana kubunia nini kinakuja mbeleni.Mara nyingi soko tuna liingia bila yakujua hata kujiuliza kuwa , hivi kama leo ndizi zina hitajika kwa wingi ndio ina maana hata na kesho zitahitajika hivyo?Matokeo yake hatukawii kuzidisha tusivyohitaji na kupungukiwa na tunavyovihitaji.

Duh!

Biashara ya kifo haiishii hapo katika mifano hiyo miwili.

  • Chakusikitisha ni ukweli kuwa kifo kipo na baadhi wataendelea kuneemeka wakati wengine wakifa
  • Chakusikitisha ni kwamba kutokana na tamaduni , mara nyingi mtu akifa anaweza kugharimu waishio zaidi hata ya jinsi alivyo kuwa hai
Inasemekana asilimia kubwa ya tamaduni za Afrika zina mjengea mtu mazingira ambayo moja ya utu wake na umaana wake katika jamii unajengeka na jinsi atakavyozikwa au kuzika nduguze, umaarufu au sifa za wahudhuriao mazishi , gharama ya mazishi iangaliayo ni nini chakula, vinywaji nk watu walihudumiwa katika mazishi nk.
  • Chakusikitisha ni vigumu kwa watu kujitoa katika mfumo ambao mara nyingine huumiza waliohai na bila ya uhakika kuwa aliyefariki kuwa anafaidika na gharama waliohai walizoingia kufanikisha mazishi ya aliyefariki.
Najua si rahisi kukwepa maadili na tamaduni zetu!

Lakini .....!

Nashindwa kujizuia kugundua kuwa kumbe matatizo huzaa matatuzi.Na binadamu ahangaikiaye kutatua matatizo inasemekana hufanikiwa. Katika hoja ya hii, kifo huzalisha jinsi ya kuingiza pesa.

Sasa kama kifo kinasaidia baadhi ya wafanya biashara kuishi.
Umasikini uliotawala asilimia kubwa ya Waafrika unamfaidisha nani?

Au ndio hawa viongozi wetu nini?

Swali:
Hivi mimi na wewe tunafaidika na umasikini?
Au ndio tuseme umasikini hauna kauhaueni?

Usistuke niko Mawazoni tu!
Baadaye!
Nakuacha na James Brown

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP