........unaamsha huku Ukiamsha kule ......naanza kustukia maswala ya NINI na KWANINI.
NINI na kwanini, ni maswala ya kujiuliza tu.
NA.....
Nikianza kujiuliza , nitataka kupata majibu.
AU...
Bila shaka nitaanza kutafuta majibu.
Tatizo la majibu ni kwamba, hata MAJIBU ya UONGO ni MAJIBU kwa afikiriaye kapata jibu.
Kwa yoyote MJANJA, usicheze na ufikiriaye mjinga ambaye KASHATEKENYWA na KASTUKIA, na anatafuta MAJIBU kutokana na UJANJA wako.
Akipata jibu , laweza likawa si jibu ulilotegemea!
SI wanadai aliyelala USIMUAMSHE?
Naamini AFRIKA imeamka! Naamini mimi na wewe tuko macho , tumeamka , na tunatafuta jibu! AU? Swali:
Wewe na mimi tunatafuta jibu la swali gani?
Wewe , mimi na yule tunaweza kuwa na swali moja wakati mmoja?
Samahani kama nimekutekenya! Nawaza tu hapa katika mtiririko fulani! Kama hunielewi naongelea nini au hutekenyeki; ASANTE kwa ushirikiano!
Siku njema! ------------------------------------------------------------------------------------- Cheki kidogo mtu awezapo kubabaika akidhani jamii imemfumania..
AU nirudi tu katika Blues nikisaidiwa na JIMI HENDRIX katika kibao Hear My Train A Comin'
Kama mimi na wewe tushafundishwa maswala ya UMUHIMU wa BAJETI halafu tukachacha katikati ya mwezi, wakati mwanzo wa mwezi tulikuwa na pesa yakukupitisha mwezi mzima , kwa mtazamo mwingine , wewe na mie hatuna tofauti na aliyefundishwa UMUHIMU wa MISITU halafu akakata mti ,akifikiri atapanda mwingine baadaye kidogo kabla msitu haujaisha.
Tofauti ni kwamba ukichacha unaweza ukakopa au kuvizia misiba mpaka mwezi ukapita(si kwenye harusi ukizamia ni rahisi kustukiwa kuliko msibani?), na ukikata mti , kuotesha msitu mpya ni vigumu ,kutokana na muda au hata hali ya hewa iharibikayo au hali iuleteayo mizengweMTI KUKUA hasa pale UKUAPO wakati tunautolea macho kutokana na msitu kutokuwepo.
Sasaaaa....
Yule , yeye na mimi, tunaweza kukubali kuwa mtu na akili zake hawezi kuondoka tu nyumbani kwenda kujikatia miti bila sababu. Tunajua karibu watu bilioni tatu wanatumia kuni na mkaa ili kuhakikisha kisamvu au maharage yameiva.Kwa hiyo kila siku kuna watu bilioni tatu kinamna lazima wanyemele mti fulani uwe umekauka au la:-(
Halafu ,.... ....kwa wale ambao hawajawahi kukata mti , napenda kuwakumbusha kuwa kukata mti sio kazi rahisi sana, hasa ukikumbuka wakataji miti waliowengi duniani hawana vifaa virahisishavyo sana kazi hii ya kutengeneza jangwa ,zaidi ya shoka , panga au goti.
Basi labda .... ....kuna watakao sema kuwa kupanda mbegu ya mti au kupanda mti ni rahisi kuliko kukata mti na wakaanza kushangaa kwanini wakatao mti walio wengi hawapandi mti. Inawezekana ukafikiria hivyo kirahisi kama utasahau sifa ya binadamu ya kufikiria ya leo zaidi ya ya kesho au mtondogoo.
TATIZO hili la kufikiria kesho au kizazi kijacho linafundishika zaidi hasa pale binadamu anapokuwa na uhakika wa kwake binafsi kuhusu kesho au baadaye ataimuduje kitu ambacho ni kigumu kwa maskini .
Swali:
Kwani unafikiri ni kwanini raia wa nchi tajiri ni rahisi zaidi kufikiria maswala ya vizazi vijavyo kuliko masikini ambaye hata kila mtoto amzaaye anaamini amekuja na ridhiki yake?
Ukiwa na njaa leo huwa unakumbuka sana jinsi utakavyo kabili mambo ya mwaka kesho?
Ukiwa na njaa sana leo ni ndugu zako wangapi wasiohusiana na wewe kula leo wakujiao akilini pamoja na mapenzi yako kama nyonyo kwao?
Nachojaribu kusema hapa ukiachia miti na misitu ni kwamba, tabia ya binadamu umchekaye au umdharauyo inaweza ikawa sawa tu na yako wewe au mimi, ila labda mimi na wewe tunafanya makosa hayohayo katika kitu kingine ambacho hatukiangalii kwa mkao wa jicho tumchungulialo tumnyosheaye kidole. Ukifikiria sana kosa la mkata mti na kosa ufanyalo , vyote vyaweza kuzaa matunda sawasawa tu, kama vile jangwa .
Au labda... ....Kosa la bajeti au hata lile katika kucheza mchezo wa UASHERATI a.k.a MIKASI, wakati umedhamiria kustarehe halafu ukastukia unalia kwa kupata mzigo wa KUZAA au hata bahati ya KASWENDE usiyoitarajia , laweza kuwa kisaikolojia lina mizizi sawa na kosa la asiyejali akikata mti halafu analalamika akiona JANGWA.
SWALI:
Una uhakika ukikata mti utapanda miti?
Unakumbuka kama ukikata mti halafu ukapanda mti na sio miti labda unapiga makitaimu?
Naacha basi topiki! Labda hata mtiririko wa mawazo katika swala hili uko kushoto. Samahani! Si kujihami IMO? AU? Hebu tuangalie afanyacho BILL GATES siku ya MWISHO KAZINI au hata baada ya KUNG'ATUKA
AU tumsikilize tu Teddy Pendergrass aliyekuwa maarufu kwa kupiga SHOO kwa WANAWAKE pekee, atukumbushe STAREHE yaKUJUA UMPENDAYE ANAKUPENDA PIA:
Samahani,labda nikulete miaka ya karibu kidogo na ya miaka ya sasa kwa donell jones : anung'unikie maswala ya : U know what's up Read more...
Kama unaishi inamaana unathaminisha vitu. Kama unathaminisha vitu inawezekana unadharau kitu au kuna kitu unafikiri kinathamani zaidi ya kile , hiki au hata nywelenywele za kikwapa cha nanihiii.
Lakini ....
Labda thamani ni kama noti ya pesa ambayo ni karatasi tu, wengi mkiwa na machale nayo, inageuka kuwa kama pesa ya Zimbabwe mwaka 2008, ambayo hata uwe na noti ngapi, unawezapata tatizo lakukusaidia kununua vikusaidiavyo kukuwezesha kwenda choo.
Labda hata thamani hata ya maneno inafanya tuamini kuwa maneno fulani ni machafu na mengine ni ya kuimbia kwaya KANISANI au pale chini ya MBUYU.
AU
Labda kweli kuna uchafu na usafi, hasa kama kwako vipodozi ni usafi ingawa huvilambi, mate kwako ni uchafu ukitemewa lakini si ukipigwa busu, au ukioga unaamini ngozi ishakuwa safi kama tu uaminivyo ukipiga deki, sakafu ni safi.
Angalau bado inasemekana; HESHIMA ni kitu cha BURE.
NA....
Labda ni kweli kuna kitu umewahi kufanya kwa thamani iitwayo bure!
Lakini ni kweli inasemekana , .... kuna vitu baadhi ya watu wanaweza wakakiri kutoweza kuthaminisha, kama vile, mapenzi yao kwa wazazi , ndugu ,jamaa au limpezi nanihino. Swali:
Kitu cha bure ni nini?
Unafikiri thamani ya kitu ukiitacho cha bure ni sifuri?
Thamani ya kitu ni nini na inatoka wapi?
SIkuKATAliI! Lakini...... .... kuna watakao kubaliana na mimi kuwa , hakuna kitu cha bure, inategemea tu na vitu vyako unavithamanishaje.
Unaweza kujisahau na kufikiria hela ndio kipimo cha thamani ya chupi, wakati dagaa au bata waweza kuwa kipimo cha thamani ya mahari ya Simon katika kumposa Mwajuma. Swali:
Ingekuwa utumwa ni biashara bomba, unafikiri ungemdaka Kijeba mtaani leo,ungemuuza shilingi ngapi?
Na bei ya yule Mwanadada macho ya gololi je?
Sasaaa....
Naamini thamani ya kitu inatofautiana kati ya mtu na mtu. Inasemekana kwa Muisraeli mmoja, ni Wapalestina kadhaa wa kadhaa jichoni kwa baadhi ya Waisraeli fulani.
Labda Kikwete mmoja anaweza akawa akina mimi kadhaa vilevile jichoni kwa yule au yeye. Na labda Kikwete kabla hajawa Nyerere alikuwa sawa tu na Mkapa au Ali Hassan Mwinyi kabla hawajawa Nyerere.
AU
INAWEZEKANA ukweli ni hakuna chenye thamani duniani kama jamii, wewe na mimi hatujakipa au kuamini kina thamani.
NA
Kijambo kinaweza kudhalilika kutokana na harufu , lakini jamii ikiamini harufu ya kijambo ina thamani kubwa , hutakawia kuona vichupa vya pafyumu za kijambo chenye mchanganyiko wa HILIKI au MAHARAGE, ni maarufu duka fulani pale nanihii.
Lakini, ...serikali ya TANZANIA au ya ..... inaheshimu na kuthamini raia wa nchi yake, wakati askari wake hawakawii kukupiga virungu ukidai kuheshimiwa kama raia wake.
AU labda ni kweli....
..Dhahabu,almasi, pesa , ndovu ....mpaka Bata wanathamanisha vitu fulani kama unataka kujua thamani ya kitumbua.
Lakini labda wewe unathamani kwangu kwa sababu hakuna mwingine kama wewe duniani. Labda umuhimu wa kile kwako ndio una sababisha uone hiki kinathamani kwako.
Cha ajabu ni kwamba nionacho hakina thamani chaweza kuwa ndio kitu muhimu kuliko vyote kwako.
Si unakumbuka kama uthaminivyo wazazi wako, wako wawauao wazazi wao ili wapate urithi?
Si unakumbuka kucheua kudharauliwako sehemu nyingine, kuna maeneo kinatumika kutoa heshima kwa mpishi katika kuonyesha jamaa wameshiba?
SI jangwa kama SAHARA tulipigalo vita kwa baadi ya makabila ya Waberiberi ndi mahali pazuri kuliko pote duniani?
Basi bwana Naaacha topiki hii Mkuu! Nawaza tu hapa katika mtiririko fulani ! Nakuthamini lakini! AU? Kwani wewe au mimi unadhani ni shilingi au talanta ngapi? ... Kila lakheri katika kuendeleza kuthaminisha vitu, watu au hata matako ya Ngedere! TUKUMBUKE tu kuwa BURE pia ni thamani! .......................................................................................................................................................................... Hebu kama una muda mcheki tena James Randi atukumbushe jinsi ya maajabu katika saikolojia ya sisi wenye kuamini na kusoma Nyota zetu Magazetini. Mcheki akitazama Astrology
Ningependa kuwashukuru tena ndugu, marafiki na maadui! Hasa marafiki hawa niliokutanao na kuwadaka muda wa karibuni kama watokeao na wasio tokea kwenye baadhi ya picha zangu zifuatazo:
EBWANA samahani nilizimika!Kwa waulizao , ni kweli nilianguka:-(
Kuna mambo , ni staili yako ya kuyafikiria leo itofautishayo ULIVYOFIKiRI mwaka juzi! Kwa ujumla inawezekana kila siku tokea uzaliwe kuna mambo yajirudiayo ambayo siku nyingine eti utanikuta nimenuna kana kwamba ni jambo jipya!
Sasaaa..... Kutokana na taarifa bwelele kuhusu NANIHII zote watu wajuazo ,nikichezea moto nikaungua, na maswala ya ukicheza peku si lazima upate au umgawie mimba yule nanihii , SI ni jambo lijulikanalo na KWA HIYO nikipata UKIMWI au kwenda MOTONI au akipata mimba, pale nikifanikiwa kufa, si nisi- AUasi-shangae?
AU?
INAWEZEKANA tokea asubuhi mpaka jioni , ni chaguo lako tu la nini au nani UNATAKA kiuumize roho au kiangalie mnato katika makalio yako ili ustukie LEO ambacho KILIKUWEPO jana au walikuwepo tu tokea msimu wa UKWAJU.
Swali:
Unafikiri ni mangapi uyapitayo njiani bila kuyaona lakini unamstukia nanihii?
Samahani narudia mcheuo... Nahisi labda fikira zako za jana zinaweza kuwa ndio hizo hizo zikuzinguazo leo ila staili tu ndio ya leo inaweza ikatofautisha MAPENZI yako kwa NYERERE , KIGOLi au RAis MUGABE. Kwa mfano:
Kama una njaa leo , utafikiria kuhusu maswala ya kula kama juzi tu, labda staili ya kupata CHAKULA ndio itafanana na ya mtondogoo.
Kama wewe muhusika huna uhakika na wewe mwenyewe , watu wakicheka leo utahisi wana kucheka kama juzi tu ulivyofikiria.
Kama wewe mwanaumume , kuna kamuda kwa siku, fikira za UASHERATI ukiona au ukikosa nanihii zitakuja kama juzi tu , hasa kama mazingira ni ya kawaida na hufukuzwi na kicheche ndani ya muda .(Si ndio maana wenye busara wanashauri tuondokane na UKAPERA?)
Sasaa.... Ni mangapi umefikiria leo ni sawasawa na MWAKA JUZI?
Na ni kwanini leo au juzi ya wiki iliopita inawezekana ukawa unahisi UMEFIKIRIA ZAIDI na unakumbuka zaidi UBWABWA wakati jana katika yote uyakumbukayo ukipewa karatasi itachukua muda kuyaweka yote ndani ya kibwagizo?
Hivi si Ubongo wa binadamu unafanyiakazi mambo bilioni kwa sekunde?Sasa kwanini unakumbuka unachokumbuka na hukumbuki usichokumbuka?
DUH! NAWaZA tu hapa na NAACHA topiki! JUMA fulani NJEMA!
Inasemekana unazaliwa na machale! Kibaya wakistukia.
Inasemekana kitu kizuri hakihitaji kujitembeza iliutamani kukiiba. Hata hukohuko chini ya uvungu, waweza kukistukia kama wewe muinamaji au muinamishwaji.
SIKATAI! Labda ni kweli.
Lakini je ni kweli?
Wakoloni walipofika kututawala kuna waliostukia pipi na lawalawa nyama zao kuwa si bomba na kuna walozipenda kama KUBWA JINGA.Kuna waliofikiri wanakuwa wakarimu kwa wageni , wakati waliokuwa wanakarimiwa wakitafsiri ni UJINGA.
Kuna watu wakamuua YESU ingawa mpaka kesho ya mwaka fulani wapo watakaokiri YESU alikuwa anawafunza mazuri.
Kuna wanaona MFAlme MTUKUFU MUGABE anafanya mazuri kupigania kuikomboa nchi yake tukufu ya ZIMBABWE kutoka kwa wakoloni mwaka 2008 , wakati wengine wakimuona nikatili ingawa anabomba la mustachi kiduchu.
Lakini.....
HELLO TANZANIA !
MWALIMU Nyerere mzuri......
...... hivi mtoto azaliwaye leo, atakumbuka alifanya nini ikiwa wakirio kuwa alikuwa mwalimu wao hawakumbuki aliwafundisha nini?
RAIS Mwinyi mzuri..... ..... kwa aliyezaliwa miaka kadhaa iliyopita, anakumbuka aliruhusu nini kama hivi sasa mpaka UFISADI ruksa?
RAIS MKAPA mzuri... ......si tutakumbuka alijenga uwanja wa mpira kwa sababu sisi ni mashabiki wa mpira wa timu za UINGEREZA?
Rais KIKWETE mzuri.... ... si nasikia anasura nzuri ?
SASAAA....
Swali:
Hivi ni kweli kila mtu anatamani akumbukwe?
Labda ni kweli waliosema TENDA mema na usingoje shukurani walikuwa wana busara ya kustukia kuwa MAOVU yako+ kutenda VIBAYA ndio vyaweza kuamsha MORI wa UMATI wa kutoshukuru .
AU
Labda tutende mema na twende zetu msalani, na kama tutakumbukwa basi isiwe kwa sauti tuzitengenezazo msalani. Si nasikia tuko wengi hatupendi kuonekana tukitoka msalani tukihisi kuna sauti zimesikika katika kuku wengi?
Lakini... .....napenda jinsi TELEVISHENI a.k.a LUNINGA inavyo tusaidia kutukumbusha kitu kwa kututangazia matangazo yatukumbushayo ngwagulo au HATA NANIHII ni vizuri kwako kununua.SASA nasikia mpaka unaanza kununua mayayi ya kuku wakati mpango wako ulikuwa ni kula MAYAI ya BATA kama kawaida yako.
Nashukuru pia TELEVISHENI , magazeti NA bila kumsahau kipenzi wazamani REDIO vilivyotusaidia mpaka KUGUNDUA MSICHANA GANI NI MZURI kutokana na MASHINDANO ya UZURI ya MISS MBAGA MANKA. Labda sasa hata yule KIGOLI niliyekuwa nammezea mate, sitaki hata kuonekana naye tukifanya shopingi za mitumba.
CHAKUJIULIZA tu .....
....ni vibaya vingapi twafikiri ni vizuri kwasababu tumevisoma kwenyeKAMAsutra au tumeambiwa ni ujanja kula mshikaki?
Je kuna binadamu ambaye machale yake ni sahihi tu?
Lakini...
Naogopa wasomi! COMMON SENSE yao ina kuja na shule na uonapo banda yeye anaona gorofa.
Naogopa walioenda shule! Wanaweza wakafanya wanayofikiri waliyasoma shuleni hatakama hawakuelewa kitabu na mwalimu.
NAACHA hapa hii topiki nisije nikaanza kukuambia blogu yangu nzuri ,halafu ukaanza kuamini kuwa ni kweli ina ladha ya NYANYA MSHUMAA:-(
DUH! Nammisi kipenzi changu kingine katika BASS , Mwanadada MESHELL NDEGEOCELLO, msikilize kidogo kama FUNK inapanda akupe SLAP FUNK
Unaweza kumsikiliza Graham Norton kama hutatukanika kama maneno yanaweza kuwa si matusi kama yanaaminika kuwa si matusi(Usicheki kama matusi ni matusi kwako.Na unaweza usijifunze kitu katika kideohiki SAMAHANI!:-(
Usitishike MDAU! Nawaza tu ya KESHO, kwani sina uhakika na ya leo.
WEWE je? Kila laKHERi kwa leo yako ili ikusaidie kesho yako iwe KULIA zaidi ya KUSHOTO! HASA ikiwa fikira zako kuhusu kushoto ,ziko karibu na tafakari ya mchambia kono la shoto.
BASI Mkuu naacha topiki!
Tulia kidogo TAMANI KAONDO akukumbushe unaweza kuwa MPWEKE kesho.
AU kama MAJAZZ yanapanda, Mcheki kipenzi changu katika BASS na JAZZ kwa ujumla Mwanadada ESPERANZA SPALDING
TATIZO la kusifiwa ni jinsi utamu wa sifa uwezavyo kufanya ASIFIWAYE kuanza kusahau kuwa binadamu wote duniani kuna kitu washawahi kusifiwa hata kama ni sifa za jinsi wajuavyo kufunga breki ya baiskeli kwa KISIGINO.
Ni udhaifu tu usababishao KASTAREHE au KAUTAMU upatako UKISIFIWA. NA... .....ni vigumu kukutana na binadamu asiyependa kusifiwa.
Lakini..... ....INAWEZEKANA mimi na wewe ni wastaarabu ambao hatuwezi kukiri TUNAPENDA SIFA. Lakini..... ... INAWEZEKANA, anayedai hapendi sifa, hajastukia afurahiavyo sifa hata kama sifa yenyewe ni ya mashavu yake murua kama embe dodo. SWALI:
Hujawahi kufurahia ukisifiwa sifa za uongo?
Una uhakika sifa zako usifiwazo ni sifa?
Labda,.... ... chochote afanyacho binadamu ni sifa.
Si ulokole, wizi , ufisadi au hata MENO KAMA NGIRI vyote ni sifa vikiwekwa kwenye sentensi fulani?
Chakusikitisha ni kwamba unaweza kujikuta unalazimika kuishi kwa kujaribu kujilinganisha na sifa usifiwazo ambazo hauna.
SAMAHANI! Nawaza tu hapa!:-( Hebu tumsikilize I -WAYNE akikiri katika CAN'T SATISFY HER
au tuwasikilize tu Bascom X ft I Wayne, Richie Spice, Chuck Fender & Capleton Read more...
Tafsiri ya chochote kile yaweza kusababisha mtu awe kapata au kukosa. Ukifeli mtihani inaweza kuwa ndio somo kubwa kwako la kufaulu mtihani.
Tafsiri ya kuishi miaka mingi, inaweza kuwa ni jinsi tu ya binadamu achelewavyo kufa.
Kuna vitu kibao mtu huweza kusema ni muhimu sana maishani mwake hasa kutokana na ubahiri wake au ukarimu wake kwa binadamu mwingine au hata dunia.
Vitu kama familia, ndugu, marafiki austaili ya kumzimia MWenyezi MUNGU ,ni moja au mbili tu ya baadhi ya yale yawezayo kuwa karibu katika fikira ,ukimuuliza yule au yeye kuwa ni nini muhimu maishani mwake, ingawa inawezeka KWA KULA mlafi kasingiziwa.
Lakini..... ......INAWEZEKANA, maadui, kutofanikiwa au hata shetani atusaidiaye kukumbuka kuabudu Mungu , vyaweza kuwa na umuhimu katika dakika hizi tuishizo au tuziitazo kuwa tuko hai. Lakini..... ....INAWEZEKANA, naogopa kuamini kuwa kitu muhimu kwangu ni cha kijinga kwako.
Kumbuka tu, tafsiri yako ya kitu inaweza tu ndio ikawa imekufanya uwe na furaha au huzuni leo. SWALI:
Kwa tafsiri yako leo, wewe umefanikiwa au umeshindwa ?
Unafikiri tafsiri zako za maisha zinaathiriwa vipi na mtazamo wa jamii kwako?
Ushawahi kufikiria tofauti za mtazamo wako kuhusu wewe binafsi UKIWA CHOONI na UKIWA STESHENIya BASI zitofautianavyo?
NAWAZA TU hapa MDAU! SIKU njema!
Unaweza kumsikiliza kidogo Matthieu Ricard ajaribu kukupa mtazamo wake wa TABIA za kuwa na FURAHA
Au wacheki wapenzi wapendao kuishi uchi , wakisaidia kutukumbusha mapenzi ya binadamu kwa binadamu ya kibinadamu
Au msikilize tu ABETI MASIKINI kama mimi, akukumbushe kabla ya ndombolo ya SOLO