Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama unanogewa na uchungu, CHUNGU ni TAMU!

>> Sunday, September 13, 2009

Kumbuka tu!

Kama sukari ni kipimo cha utamu, ....
.... basi wali si MTAMU.

Kama chai ni kipimo cha utamu,...
.... basi bia si TAMU.

Kama nyanya ni kipimo cha utamu,....
.... basi kitunguu si KITAMU.

Na kama pilipili ni kipimo cha kuwashwa na chakula kitamu,...
....basi KUJIKUNA wakati unawashwa KIPELE au UPUPU si kuwashwa na mkuno hata wa ukurutu ni kujisikia vizuri tu KWAKUWA UNA CHA KUKUNA na sio UTAMU.
Swali:
  • Ushagundua neno la kiswahili '''UTAMU'' halina maana usipo lipa hata ya ujinga maana?
  • AU unafikiri itakuwaje KACHUMBARI, UASHERATI na ASALI vyote vidaiwe ladha yake ni UTAMU?
  • Unajua kuelezea tofauti ya utamu wa kiporo cha ugali na utamu wa kiporo cha ukoko wa wali uliochacha pamoja na kujifanya kiswahili kinapanda?
  • Ushastukia kabla maumivu hayajazidi hata kukuna kidonda kiumacho kuna utamu?
  • Kwa hiyo si tunaweza kukubaliana maumivu ni aina ya utamu ?
  • Kwani unadhani kwa kuwa kuna chenza na chungwa KWA HIYO limao sio tamu?


NI HILO TU KIJEBA na ni wazo tu USITISHIKE na HII labda wala sio sayansi!

AU ngojea SHIHAN anyambulishe tena katika shairi-FLASHY WORDS


Au tu Paul Simon &Miriam Makeba walete kitu -Under African Skies

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Bennet 11:26 am  

Unaweza kumkimbiza kuku na kisha ukamkamata UTAMU

Simon Kitururu 12:20 pm  

@Bennet: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP